Maria Roza
JF-Expert Member
- Apr 1, 2009
- 6,797
- 1,567
Wivu ni kidonda ukishiriki utakondaa
kuna wimbo tulivyokuwa watoto tulikuwa tunaimba :lol::lol::lol::lol:
kuna wimbo tulivyokuwa watoto tulikuwa tunaimba :lol::lol::lol::lol:
Wivu ni kidonda ukishiriki utakondaa
kuna wimbo tulivyokuwa watoto tulikuwa tunaimba :lol::lol::lol::lol:
Mimi naona siku zote WIVU sio mzuri.. Unaweza chukiwa bure, eti kwa saabu umemshinda rafiki yako class! au umependeza siku ya sikukuu, au kwenu kuna video (Enzi za Mwalimu)
Uchakachuaji wa thread bila hata kuchangia hautakiwi!
Hehehe unadhani wataacha kufurahia?Imagine wa2 wa3 wenye chuki na mtu mmoja au kundi la watu..kusikia kila mmoja akiongelea vibaya kuhusu wanaemchukia itafanya siku yao nzuriLizzy,
Mtu wa namna hiyo ni looser...Ameshakubali kwaba hawezi kufanya lolote la maana na kwa hiyo anaishia kucheza na mdomo..umbeya mtupu. Shida yetu Watanzania ni kwamba kuna watu wanapenda hizo hadithi za kishenzi na ndio maana watu wanaosema hovyo namna hiyo wanayo hadhira ya kutosha!
Kumbe ehh?Haya umesamehewa ila usiendekeze wivu!
USIENDEKEZE yani usikuendeshe...uendeshe wewe!
Hehehe unadhani wataacha kufurahia?Imagine wa2 wa3 wenye chuki na mtu mmoja au kundi la watu..kusikia kila mmoja akiongelea vibaya kuhusu wanaemchukia itafanya siku yao nzuri
tulipishana tena aisee. Spanish lady miss wewe. Hajambo tatizo kaugonjwa ka kukumiss. Lol!Mambo my spanish lady leo tumekutana, u mzima ?
WIVU!!
Wivu uko kila mahali...kwenye mapenzi...kati ya marafiki...kati ya wafanyakazi na wanafunzi wenza...ndugu na hata maadui.
''Wivu ni kidonda ukizidisha utakonda.'' Ndivyo tulivyokua tukiambiana wakati tunakua...na huo ndio ukweli wenyewe.Maana kama vitu vingine vingi wivu ni mzuri ila ukizidi kipimo unageuka sumu.
Kwenye mapenzi: Wivu kati ya wawili ndani ya mahusiano unaweza kua kirutubisho au chachu ya mapenzi.Ukionyesha kwa kiasi utamfanya mwenzi wako ahisi kwamba unampenda na kumjali...sisemi kwamba ni kitu pekee kinachofanya hivyo bali ni kichocheo kizuri iwapo hakitazidishwa na kusababisha kero.Wivu unapozidi unaonyesha mapungufu yako kanakwamba hujiamini kitu ambacho kinaweza kupelekea mwenzako nae ahisi kwamba HUMUAMINI.
Kati ya wanafunzi/wafanyakazi: Unapomuonea wivu mwenzako kwa maendeleo yako ikiwa utaupangilia vizuri itakusukuma wewe kujitahidi kufika alipo yeye au hata zaidi.Ila ukikosea tu ukazidisha kiasi itasababisha chuki dhidi ya mwenzako huyo.Na kama mnavyojua chuki ni sumu.....sumu inayomuumiza aliyenayo na sio anayepelekewa hiyo chuki.Ukiwa na chuki utaishia kuchukia maendeleo ya mwenzako badala ya kujiboresha wewe hivyo hautafaidika.
Wivu kati ya ndugu na marafiki: Kwanza jiulize kwanini umuonee wivu ndugu au rafiki yako??Kwanini usifurahie mafanikio yake huku ukijaribu kufikia pale alipo yeye???Katika watu ambao unatakiwa ujitahidi kutowaonea wivu ni ndugu au rafiki wa karibu....maana ukizidi unaweza kuzaa chuki.Ikiwa unawaonea utumie kama msukumo wa kuelekea kwenye ubora badala ya kuonyesha udhaifu wako na kupelekea kumchukia mwenzako kwa kua na kitu ambacho huna.
Wivu dhidi ya adui: Jua kabisa kama humpendi mtu tayari kitendo cha kumuonea wivu kitakuumiza zaidi wewe binafsi zaidi ya kukusaidia.Japo ukiweza kuuendesha wivu wako badala ya wivu kukuendesha unaweza ukafaidika!
Kwahiyo wivu ni mzuri maana huleta maendeleo na hudumisha mapenzi pale unapotumiwa vizuri.....ila wivu huo huo huweza kugeuka kero au kuzaa chuki ambayo matokeo yake yaweza kua ufitini..umbea..kutojiridhisha/kutojitosheleza...na hata kufikia hatua ya kuumizana.
Hivyo basi....usiache kumuonyesha mpenzi wako wivu angalau kidogo wala usiache kuwa na wivu wa maendeleo....hayo mengine achana nayo maana maisha mafupi haya usitumie muda wako kuchukia na kuharibu....utumie kukunufaisha wewe na uwapendao.
Nawatakia jumatatu na wiki njema kwa ujumla.
Last edited by Lizzy; Today at 01:35 AM. Reason: napendezesha!
Sijui nina wivu ngoja nikajicheki kwenye kioo vizuri leo.
ukiona una kama vinywele nywele juu ya macho yako yote mawili ujue hiyo ni dalili ya wivu.