Mambo ya kumuaminisha mwenza/mpenzio unapendeka ukiwa umetoka kusamehewa

mmmuhumba

JF-Expert Member
Nov 8, 2017
491
476
1. Kumpa uhuru wa kuwasiliana nawe.
Wengi wapenzi upima na kuyafurahia upya mahusiano yao kwa kuona nafasi aliyonayo kimawasiliano na mpenzie au mwenza waliotoka kukosana na kuombana msamaha.

Ikiwa bado suala la mawasiliano ni la kutafuta kwa tochi, mambo kama lawana, kuonesha dharau na kutujali ujengeka kwa mwenzio aliyekuwa radhi kusamehe. Ni bora akipiga simu wakati wowote upokee/ sms jibu na kama unafahamu ugumu wa mawasiliano kwako, basi muweke wazi apate kutambua asiwaza mabaya.

2. Mheshimishe
Kumheshimisha ni kumpa hadhi, kumtambulisha, kumtambua, kumuweka wazi panapo stahili na kuwa na sauti ya wapenzi wenye afya katika maamuzi yenu, kwenye mabishano yenu na kuwa na staha na mapungufu yenu.

Ikiwa umesamehewa halafu unamtenga, unashindwa kumuita mpenzi, unashindwa kumuweka wazi kwa ndugu na watu wako wa karibu kama mwenza au mpenzi, unatengeneza tatizo.

3. Mjulie hali mara kwa mara na mtakie mema.
Mpe muda wako wa kumtambua hali yake, mahitaji yake, afya yake na ahisi yuko na mtu ampendaye badala ya kumpa upweke angali anaye mpenzi.
Siyo poa kuwa na mpenzi lakini ukatawaliwa na hali ya upweke na hata kuona huna haja ya kuwa na uliyenaye.

4. Mtimizie mahitaji yake ya kimazingira na ya kihisia.
Kusamehewa uambatana na kubeba majukumu yako sawia, usiwe ni mtu wa kukumbushwa na kubembelezwa.

Unapaswa kujiongeza mwenyewe kujua wapi unaweza timiza kimazingira na kihisia. Msamaha huwa mwepesi sana pale mpenzi anapoona anatimiziwa mahitaji yake kimazingira na kihisia bila kuomba.

5. Onyesha kujitoa kwake kimawazo, kinguvu na kimali.
Unaposamehewa ni lazima uonyeshe upo kimalengo na siyo mguu ndani na mguu nje. Unapoonyesha kujitoa kimawazo, kinguvu na kimali ni wazi uaminisha, wewe na yeye mko sawa na mna safiri gari moja la maisha na mapenzi.

6. Mpe wivu.
Kwa kupendeza, kuzungumzia mahaba, cheza na hisia zake kwa kumnogesha, cheza na jinsia yako, fanya kilicho cha maana au yaliyo ya maana iwe kiuchumi au kihisia.
Unapompa wivu kwa kujiwekea mazingira ya kuonyesha wewe ni bora kwamba uliteleza tu, inafanya akupe thamani, akutunze na uone anajitahidi/amejitahidi kukubadilisha.

7. Acha wasiwasi jiamini.
Kwa lolote unalokuwa unafanya ukiwa naye jiamini kama mtu ambaye hakuna baya lilitokea kati yenu, wenza ama wapenzi, mmoja anapokosa kujiamini uzalishaji mashaka kwa mwenziye. Mashaka yako uonyesha umuamini au haujiamini kwa uamuzi huo.

8. Jitenge na jipe likizo na hulka zako fulani.
Baadhi ya hulka za mtu huweza leta majungu, fitina, kukuangaza utazamike vingine japo haipo hivyo. Huwa ni ngumu kufuta hulka yako ila ni rahisi kuanzisha hulka mpya na kuiacha ya zamani.
Kama unataka mabadiliko ya mahusiano yako ni bora ukajitoa kuepuka kuonekana ni yule yule au ubebeki.

9. Punguza kumchunga mwenziyo.
Unapokuwa umesamehewa na muda mfupi unaonyesha kumfuatilia sana mpenzi au mwenza wako, huwa ni kuonyesha nawe unamtafutia kosa au una mtafuta ubaya.
Lakini uonyesha pia una tafuta kisasi katika hili lilopita kati yenu.
Wapo watu ukosea na wakasamehewa, lakini wapo tayari kuwatengenezea wenzao makosa tu ili tu nao waonekane ni wakosefu na wao wameweza kuwasamehe.

10. Uwe na kumbukumbu.
Epuka kurudia vitu, kukaa mazingira, kuwa na watu wale wale, kufanya yale yale, kufunga mdomo, kujizuia na kuwa staha na shida zako.
Kukumbuka ahadi zako na uwezo wako wa kutimiza ahadi ulizohaidi wakati unaomba msamaha.
#Na mmmuhumba
#imarika
View attachment 2737139
textgram_1690030103.jpg
 
Ebu ngoja kwanza....
Hivi hayamaoni yako yanafaa kwenye muvi ama huku kwenye mahusiano yetu na akina chiku..??
 
Ebu ngoja kwanza....
Hivi hayamaoni yako yanafaa kwenye muvi ama huku kwenye mahusiano yetu na akina chiku..??
jambo la msingi umeelewa na unapaswa kutambua muvi ni kuigiza, hiki ni kipaji cha kila binadamu tofauti ni weledi tu na mkazo ukidhamiria.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom