Wito: "wanaoua Albino na wenyewe muwaue!" - Pinda

nimesikiliza BBC hata hivyo na wao wameweka kipande kidogo sana na wala hakikaribiani na hiyo nukuu ya Mwananchi. Naamini kuwa hotuba nzima si rahisi kupatikana.

Nadhani baada ya kushtukia PM amechemsha, huo mkanda umeshageuka dili. Kuna jamaa wa PM anarekodi kila kitu ila kwa hii soo lazima atasita. Hata ikipatikana hotuba yake rasmi, hayo maneno aliyasema impromptu na kesho mwandishi wake wa habari atakanusha kuwa PM alinukuliwa vibaya.
 
Na Victor Kinambile, Tabora
KATIKA hali ya isiyo ya kawaida, Waziri Mkuu Mizengo Pinda jana aliwaambia wananchi kuwa wanaoua watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) pamoja na vikongwe nao hawana budi kuuawa kwa kuwa wakisubiri mahakama kuwahukumu, watakuwa wanakosea.

Kweli Tanzania tumejaliwa viongozi wanaokurupuka na kutoa kauli bila kutathmini athari ya kauli zao. Itakuwa vizuri ukitoa ruhusa kwa wananchi wachukue sheria mikononi na kuwaua mafisadi ambao wanakwamisha maendeleo ya nchi yetu kwa sababu mahakamani kumejaa usanii tu.
 
Kweli Tanzania tumejaliwa viongozi wanaokurupuka na kutoa kauli bila kutathmini athari ya kauli zao. Itakuwa vizuri ukitoa ruhusa kwa wananchi wachukue sheria mikononi na kuwaua mafisadi ambao wanakwamisha maendeleo ya nchi yetu kwa sababu mahakamani kumejaa usanii tu.


Lakini mimi namuunga mkono pinda, kwa sababu mtu gani mwenye akili atataka kumuua mtoto mdogo tena ki ukatili namna hiyo. We have to be considerate

Au lazima tuwe like US Blogger Dr. Shayo? ndo tusijulikane kwamba tumetamka kitu fulani?
 
Imefika wakati auwaye kwa upanga naye auwawe kwa upanga ... kama tatizo ni kutamkwa na Waziri Mkuu ... basi mshaurini awaombe radhi wale mlioguswa na kusikitishwa na kauli hii, lakini sisi wengine hizi kazi tulishazianza siku nyingi .. tukianza na majambazi sugu ambao walimekuwa wakitusumbua sana vijijini kwetu na hasa kuvamia wavuvi na kuwazamisha ziwani kabla ya kuwanyang'anya vifaa vyao vya uvuvi.

Asikwambie mtu bwana ... siku likikukuta ndipo utajua ukatili wa hawa wauaji ...

Sasa hivi wala hatuhitaji jeshi la polisi wala nini ... sungusungu yetu inatosha ... serikali inalijua hilo. Mafanikio ni makubwa sana, maana hawa wakipelekwa mahakamani wanatetewa kisheria na mwisho wanarudi vijijini na kuendelea kututishia usalama wetu ...

Pinda akiwa serikali za mitaa alifika na kupewa taarifa hizi za mafanikio ya sungusungu na nina imani kwa siri moyoni mwake alisema: "Safi sana". Sasa naona ameamua iwe official ...na uwe mkakati wa kitaifa ... na kwa composition ya sungusungu ni vigumu sana kumuonea mtu ... hawa jamaa wanafanya uchuguzi kuliko hata polisi; na wanawafahamu majambazi na wauaji wote na washirika wao.

Na nimefurahishwa na kupigwa marufuku kwa waganga wote wa jadi ...
 
Kwa mahali nchi yetu ilipofika, a serious dictator guided by the best interests of the country at heart, MAY be the best way to go!.... Haki za wahalifu zitafuata tukishakaa sawa.
 
mimi nadhani ni kweli viongozi wamechoka, na kuchoka huko ni kwa sababu ya kuwa na uhakika na maisha yao as wanajua mwananchi wa kawaida hawezi kuwatoa.

He just show us that viongozi wote wameshachoka kufuata utawala wa sheria "innocent until proven guilt"

watanzania naomba tuwapumzishe watakufa hawa wazee "uongozi wote tumeshachoka"
 
Kama kweli Pinda katoa kauli hiyo ya kuruhusu watu kuua, ANA HOJA YA KUJIBU MBELE YA WATANZANIA NA MBELE YA MUNGU.
 
Mhhhhhhhh mkulu Mwanakijiji ukiipata tuweke hapa nisi ugaibuni tuisikie laivu.

Kimsingi najaribu kuona uhalali wa adhabu ya kifo. Hivyo wanaharakati wanaopinga adhabu ya kifo Tanzania nadhani wanaweza pata somo hapa juu ya chanzo cha adhabu kama hizi.
 
wewe uliaka wanaoua albino wabaki kwasababu gani? si na wao wauawe? unatetea mauaji ya albino ehee, wewe ungekuwa albino hapo ungeona how moto na shida yenyewe ilivyo. watu mnaongea tu kwasababu ninyi hamuwindwi, mngekuwa nyie ndo albino, nakwambia mngetamani hata kujilipua. mimi naona kama ndo hivyo, adhabu ya kifo iwe kunyogwa au kupigwa na wananchi, no pia tu. poa mzee pinda kama utakuwa ulisema hivyo. ninyi wateja wa viungo vya albino ndo muanze kumsakama baba wa watu sasa.
 
Lakini mimi namuunga mkono pinda, kwa sababu mtu gani mwenye akili atataka kumuua mtoto mdogo tena ki ukatili namna hiyo...

...Imefika wakati auwaye kwa upanga naye auwawe kwa upanga ...

.... Haki za wahalifu zitafuata tukishakaa sawa.

...safi sana, ila tahadhari; hii ina apply kwa MUUAJI ATAYEONEKANA tu ...i.e caught red handed na shoka/panga lake na mkono wa albino...

Revenge has no more quenching effect on emotions, than salt water has on thirst.

Mmejuaje ni mhalifu?

Tutajuaje umemuona? We Mbu ndo kabisa unalikoroga, umetetea kisasi halafu hapo hapo unatoa ki-kauli mbiu kinachopinga kisasi.

Mwataka mambo hamtayaweza.


25swat.600.jpg
 
mhhhhhhhh mkulu mwanakijiji ukiipata tuweke hapa nisi ugaibuni tuisikie laivu.

Kimsingi najaribu kuona uhalali wa adhabu ya kifo. Hivyo wanaharakati wanaopinga adhabu ya kifo tanzania nadhani wanaweza pata somo hapa juu ya chanzo cha adhabu kama hizi.

kamwe hamna kitu kama hicho...never ever......
 
Mzee Mwanakijiji,

KWa taarifa nilizo nazo ni kuwa Mwananchi na TAnzania Daima walimnukuu vibaya Waziri Mkuu,I mean wameelewa vibaya kauli aliyosema nakwa maana nyingine walikimblia kusema jambo la kufikirika kwanza.

Waziri mkuu alisema kuwa ili kukomesha mauaji ya Malbino unaweza tumia sheria Mkononi bila kusubiri mahakama.Sheria mknoni siyo kuua mtu ila hata kumkamata mtu ni kujichukulia sheria mkononi.

Naungana na maneno ya Mkapa aliyowahi kuyasema siku moja,Tanzania ya sasa imejaa watu wanopenda siasa za chuki,wanaweza eneza jambo fulani ili mtu flani achukiwe na Jamii hata akiwa ni mwema.

Na siku zote nimekuwa nikionya kuhusiana na Hili.Mwanakijiji na wewe unatak kukubali kutumika kwa hili kama mtaji?Na hii ndiyo sababu kubwa ya Watanzania kutochagua wapinzani hata kama CCM imewachosha..

Habari hiyo ukiipata kwa pesa nyingi itakusaidia nini?Una lengo gani?na kwa faida ya nani mpaka utumie pesa nyingi kuiasi hicho?ina mana Huwa unanunu Habari?
 
Kwa siku kadhaa sasa hivi kile ambacho alisema Waziri Mkuu kuhusu wauaji wa Albino kinabakia kuwa siri kubwa. Kumekuwa na jitihada za makusudi kabisa kuficha alichosema Waziri Mkuu.

Jana katika taarifa ya habari ya saa mbili (za usiku) TBC ilizungumzia jinsi NCCR ilivyotoa tamko la kulaani mauaji ya Albino. Wao wakaongezea na kusema kuwa Waziri Mkuu alisema kuwa wale wanaohusika na mauaji ya Albino "washughulikiwe kwa mujibu wa sheria".

Nimepata nafasi ya kuzungumza na watu wengi weekend hii kupata hasa alichosema Waziri Mkuu karibu wote wanazungumzia kile "alichomaanisha". Nimegundua hakuna anayesema hasa kile "alichosema".

Je ni kweli Waziri Mkuu alitoa kauli hizi kama zilivyonukuliwa na Mwananchi?:

a. Mkimuona mtu akamkata mwingine shingo naye muueni kwani sasa viongozi wote tumechoka... no more, I can`t tolerate anymore (imetosha, siwezi kuvumilia tena

na hii hapa kuhusu UVCCM kushiriki katika kukomesha mauaji ya albino, labda kwa kuangalia (a) hapo juu.

b. Umoja wa vijana mna jeshi zuri ambalo naamini mkiamua mnaweza kutokomeza mauaji ya wazee wetu pmoja na ndugu zetu maalbino na kazi hiyo nawaagiza muanze leo msisubri auawe mwingine tena

Naamini hakuna "maelezo" au "taarifa kwa vyombo vya habari" ambayo inajibu swali la nini hasa Waziri Mkuu alisema.

Kuna njia moja tu ya kuamua kwa haki kauli ya Waziri Mkuu ilikuwa ni ipi hasa maana uwezekano kuwa Waziri Mkuu wetu akizungumza kwa niaba ya "viongozi wote" na kwa jina la serikali kwamba amewaambia watu wa kijijini kuwa wanaweza kuua with impunity inatisha. Hofu yangu siyo kwa wasomi wa kisheria na watu ambao wanaweza kuelewa "alichomaanisha" bali wale watu ambao walikuwa wanamsikiliza walisikia nini hasa.

Sisi wengine wanaweza kutuzuga kuwa alimaanisha nini lakini wale Sungusungu, na wanakijiji kule Shinyanga walivyomsikia watakuwa na utata wowote wa kuelewa alichomaanisha?
 
Yaani hadi namuonea huruma Pinda jamani labda alikuwa haaminishi hivyo labda ...ila na yeye anatakiwa kukanusha au kubadili usemi wake.....jamani siasa kazi sana hasa ukiwa na jazba jukwaani.
 
Napenda kuwasilisha mada hii hapa jamii Forums baada ya siku za hivi karibuni mheshimiwa Pinda kutoa kauli ya kwamba yeyote yule atakayemuua ama kuhisiwa kumuua Albino auwawe hapo mara moja ni kauli ambayo inasikitisha sana

tunaelewa kilio kinachoendelea nchini hivi sasa kuhusiana na mauaji ya albino ila njia iliyotolewa na Pinda siyo sahihi hata kidogo.

Haki za binadamu zitavunjwa na kitachotokea ni vurugu tupu.

Katiba ya tanzania section 14 inatamka wazi kuhusiana na right to life na kumlinda kila raia.

katiba katika section 13 inasema 'the civic rights,duties and intrests of every person and community shall be protected and determined by the courts of law or other state agencies established by the law.

Pinda anaendelea kusema kwamba jeshi la uvccm litumike sasa katiba imesema wazi kuhusiana na armed forces.

kuna suala kubwa sana la kujadili kuhusiana na kauli ya pinda ya collective punishment.

Pinda anapaswa asimame na kurekebisha kauli kaye otherwise tunarudi kwenye state of nature.
 
Mzee wangu Mwanakijiji, ili kujua hasaa kilichosemwa ni kupata tape (ambayohaijahaririwa). Ni vigumu kujibiwa na mtu yeyote kwa ushahihi kwani spining imekuwa kubwa mno hasa kwa kumlinda Mheshimiwa. Nimesikiliza bbc/swahili ya leo asubuhi, amehojiwa Mwandishi/Msemaji wa Waziri Mkuu juu ya kauli haswa iliyosemwa na Mhe. Pinda. Mwandishi ameshindwa kabisa kueleza chochote zaidi ya kusema kila mtu anaweza kutafsiri anavyoelewa. That means, Mhe. alitamka maneno 'tata' yanayoweza kutumiwa vibaya na sungusungu, green guards au mtu mwingine yeyote.
 
bila kumtetea Pinda alitoa kauli ya jino kwa jino isiyojali utawala wa sheria... "unamkuta mtu na mkono wa albino unategemea nini kama siyo na yeye auliwe?" nimejaribu kumnukuuu
 
Mimi nilisikia sehemu ndogo tu ya aliyokuwa anasema. Ni kweli pengine kauli aliyoitoa ni kama vile inasupport 'sheria mkononi'. Hata hivyo nadhani critics wake wanajaribu kuyatoa manano yake kwenye context ili kummaliza kisiasa.

Pinda katika kukemea mauwaji ya albino na kuonesha possible immediate conseqences za kuua albino alitoa mfano akijaribu kujiweka katika nafasi ya kama mmoja wa wanakijiji.

Sina uwezo wa kukumbuka neno kwa neno (inawezekana nimepunguza au kuongeza) lakini ile context yake ilikuwa kama hivi:

"Umeua albino, kukata viungo vyake na nakukimbia navyo. Tunakufukuza na kukukamata, je tukupeleke polisi tusubili uhukumiwe na mahakama? Hatutaweza kusubiri, tutakuuwa tu!"
 
Back
Top Bottom