Wito rasmi kwa Marekani(USA)na Jumuiya ya Ulaya (EU): Hii ndo namna pekee mnaweza kutusaidia Watanzania dhidi ya Utawala mbovu wa CCM.

Wito rasmi kwa Marekani(USA)na Jumuiya ya Ulaya (EU): Hii ndo namna pekee mnaweza kutusaidia Watanzania dhidi ya Utawala mbovu wa CCM.

Lord Denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
23,494
Reaction score
57,869
Nawaandikia Marekani, Umoja wa Ulaya, Uingereza na Canada.

Kama sehemu ya mamilioni ya Watanzania tunaodhulumiwa haki zetu za Utawala huu mbovu wa CCM napenda kwanza kuwashukuru sana Marekani na Nchi zote za Jumuiya ya Ulaya na Mataifa mengine ya Magharibi kama Uingereza na Canada kwa namna mnavyooneshwa kuguswa sana na maisha ya Watanzania hasa tunavyoteswa na kunyanyaswa na huu utawala huu dhalimu wa CCM.

Tunapenda pia kuwashukuru kwa namna kwa nyakati tofauti mmetoa matamko mbalimbali ya kuguswa hasa na namna Ccm na utawala wao wanavyodhulumu haki zetu ikiwemo haki za kuabudu, kuishi, kuchagua viongozi tunaowataka na kufanya shughuli zetu bila bughuza zozote zile.

Tunawashukuru pia kwa vikwazo mbalimbali mlivyoweka. Ingawa kwa namna moja au nyingine vinatuathiri hadi sisi ila tunaelewa hii ni njia ya awali mnayoitumiaga kuwaonesha watawala madhalimu kuwa hamridhiki na matendo yao hivyo kuwataka wabadilike. Ukweli ni kwamba vikwazo hivi ni na muhimu maana utawala wa ccm na vyombo vyao vya ulinzi vimeua ndugu zetu zaidi ya elfu 10 kwenye maandamano ya kupinga Uchaguzi Mkuu mwaka jana.

Leo napenda kuwasilisha kwenu maombi yetu Watanzania kuomba msaada wenu kwetu ili tuweze kuondokana na hili jinamizi CCM ambalo kwa sasa linaona raha kututeka, kutuua, kutulawiti na kutufungulia kesi za uongo ili tu kutufanya Wananchi tusizungumze kwa namna wanavyotutawala kwa nguvu, kufisadi kodi zetu na kuenda kinyume na matakwa yetu sisi Wananchi.

Pamoja na hatua zote mlizochukua dhidi ya Utawala wa CCM na Serikali yao, tunaomba kuwaambia kuwa bado mna nafasi ya kuchukua hatua ambazo sio tu zitahakikisha CCM haipo bali Taifa hili linabadilika kweli na kuwa Taifa la Haki ambalo Wananchi wanaishi kwa furaha, amani, utulivu na wanashiriki vizuri shughuli za maendeleo na kufaidika kweli. Hatua ambazo zitahakikisha pia maslahi ya nchi zenu yanalindwa kweli na hayaingiliwi na Mataifa ya kidhalimu kama Iran, China, Urusi na Korea Kaskazini ambao hawa ni washirika wa kudumu wa CCM.

Jambo kuu mnalopaswa kulitambua ni kwamba Watanzania tunapenda sana kushirikiana na nyie kiuchumi kuliko kushirikiana na Mataifa ya China, Urusi na Korea ya Kaskazini kwa sababu mataifa haya hayawezi kuwakemea CCM kwa namna wanavyodhulumu haki zetu.

Hivyo tunaomba, ili kuhakikisha jinamizi la CCM linatutoka Watanzania muhakikishe yafuatayo yanafanyika.

1. Kuitaka Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ( ICC), kuanzisha uchunguzi rasmi na kutoa hati ya kukamatwa na kushtakiwa kwa Mwenyekiti wa ccm, Bi Samia Suluhu Hassan , IGP Wambura, DGIS Mombo, CDF Mkunda, CP Awadhi, SACP Mafwele, SACP Muliro, RPC, RSO wa Mikoa ya Geita, Mwanza, Arusha, Mbeya, Songwe, Ruvuma na Dodoma kwa uhalifu dhidi ya binadamu na mauaji ya Watanzania zaidi ya elfu kumi kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka jana. Jambo hili ndilo litakuwa the turning point kwa Taifa la Tanzania maana litafanya Viongozi wengine wote wajao kuepuka kutenda ukatili na mauaji kwa Watanzania katika siku zijazo.

2. Tusaidieni pia kutoa hati za kukamatwa kwa watu wa karibu wa Rais Samia hasa mshauri wake Kheri, mtoto wake Abdul, mkwe wake Mchengerwa, Paul Makonda na Waziri Salum aliyekuwa Katibu wake katika Mahakama ya ICC au Mahakama zenu kwa makosa dhidi ya Binadamu . Hawa wamehusika sana kuratibu na kutoa amri za kutekwa, kuuwawa na kupotezwa kwa watu mbalimbali akiwemo Humphrey Polepole, Mdude Nyangali, Ali Kibao, Deus Soka na wengineo wengi.

Mambo haya mawili sio tu yatasababisha Tanzania inangozwa na mifumo imara ya haki na misingi ya utawala bora, bali yatahakikisha pia maslahi yenu ya kiuchumi yanakuwa imara na salama kwa faida ya Watanzania na nyie pia. Mambo haya mailing yatafanya watawala waliopo waendeshe mchakatk huru wa Katiba Mpya utakaohakikisha tunapata Katiba bora iliyo imara ambayo itasimika mifumo huru iliyo imara itakayohakikisha inafanya kazi kwa maslahi ya Wananchi na sio maslahi ya ccm na vikundi vya watu wachche wahuni na wauaji. Kupitia hilo tutapata Tume Huru kweli ya Uchaguzi itakayofanya kazi kwa kuangalia matakwa ya wananchi na kuyaheshimu na sio ccm.

Mwisho napenda kuwashukuru tena kwa namna mnavyolisaidia hili Taifa. Msichoke kutupambania Watanzania dhidi ya hawa wauaji CCM na Serikali yao kama mlivyopambana na utawala wa makabulu wa Afrika Kusini hadi kuufanya waondoke madarakani.


Mungu awabariki sana.
 
Naunga mkono hoja zako,lakini haya mataifa uliyoyataja yanafanya kazi kwa mtindo huu au kuna namna nyingine umewasilosha hoja hizi?
 
Cc. British High Commission Tanzania
US Embassy Tanzania
EU High Commission Tanzania
Canada High Commission Tanzania
 
Back
Top Bottom