Wito kwa Serikali, TANROADS: Tunahitaji mkakati wa kupanua kipande cha barabara Mlima Kitonga, Iringa

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,826
9,533
Kwa miaka mingi sasa eneo hili limekuwa eneo korofi kwa kusababisha ajali nyingi sana kila uchao. Kwa wanaotumia barabara ya TANZAM ni nadra sana upite KITONGA usikutane na ajali hasa ya magari makubwa..

Ajali nyingi kwenye kipanda-njia hiki ni za Malori na Mabasi kwa sababu zifuatazo:-

1. Barabara ni nyembamba sana kiasi kwamba hairuhusu mpishano na smooth riding;

2. Barabara ina KONA NYINGI tena ni SHARP CORNERS ambazo zinalazimisha MANY BLIND SPOTS zinazoeleweka kuwa hatari katika uendeshaji vyombo vya moto;

3. Uoto jirani na njia unazuia clear passage;

4. Kingo za barabara hii ni dhaifu kiasi kwamba haziwezeshi kukinga athari za failures kv brake failures kwa malori hasa na magari mengine like BUSES

5. Kipande hiki hakina alama muhimu za tahadhari ndani ya kipande cha barabara with exception kwa alama za mwanzo wa barabara.

NINI KIFANYIKE:

  1. Barabara hii IPANULIWE kwa kiwango cha kuwezesha LORIES NA BUSES kuwa na their own climbing lane
  2. Alama za tahadhari ziwekwe
  3. Kingo za barabara ziwekwe; tena zile thabiti kabisa "strong parapet walls"
  4. Iwekwe barabara ya zege nzito na iwe smooth siyo kama ilivyo sasa iko stressed kiasi kwamba inaongeza hofu kwa drivers
  5. Iwekewe vidhibiti mwendo kv matuta yasiyoudhi ambayo hayatakuwa chanzo kingine cha ajali
  6. Liwe ni eneo la tahadhari kubwa na ikiwezekana pawekwe Cameras kwa ajili ya kumonita mwendo hasa wa regional buses ambazo zimekuwa chanzo cha ajali nyingi
  7. Ifanyike tathmini ya ajali kwenye barabara ya TANZAM hasa kipande hiki naamini utafiti utabainisha kuwa KITONGA ni tatizo kubwa kwenye ajali na hapa malori mengi ya mizigo ya nchi jirani yanaanguka na kuwasababishia hawa wateja wetu hasara...hii inapunguza trust wasije kutuhama
  8. Drainage system iwe improved ili kudhibiti maji yatokayo mlimani kwenda bondeni...hali ilivyo sasa hakuna mifereji ya maana no wonder maji yanasababisha athari kwa kuharibu barabara kuna mwaka fulani maji yalikuwa yanatembea juu ya barabara ya KITONGA kama mto hivi...you can prove kwamba kuna failure kwenye designs za drainage systems kwenye kipande hiki.
  9. Hebu someni dodoso hili hasa ndugu zangu hapo TANROADS naamini mtapata tirio la pa kuanzia DESIGNING HILL ROADS_THE ENGINEERING COMMUNITY
  10. Tuchukulie SUALA hili kwa uzito WATUNGA SERA, WAFANYA MAAMUZI, SERIKALI, TANROADS, POLISI FORCE, WADAU WA MAENDELEO MHESHIMIWA RAIS JMT na WANANCHI maisha mengi ambayo ni nguvu kazi ya taifa inapotelea hapa KITONGA pia rasilimali na mitaji inapotelea hapa...Kwa kuanza Polisi IRINGA watoe takwimu za ajali hapo KITONGA mtathibitisha hili.
PICHA: Baadhi ya Picha zikionesha ajali mbalimbali zilizowahi kutokea KITONGA CLIMBING Road.

kitonga ingnine.jpg

kitonga.jpg

sugu.jpg

fdd.jpg
 
Pale kitonga ni hatari sana mara ya mwisho kupitia njia hyo ilikuwa 2016 mwshoni, but panatakiwa papanuliwe tena kwa kiwango chenye ubora wa hali ya juu. Ila asante kwa picha mtoa mada😁
 
Back
Top Bottom