AFRICON 2027 inakuja na neema ya ujenzi wa barabara 4 ,kuanzia mbagala - chamazi- chanika

PureView zeiss

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
9,099
29,888
Ni neema juu ya neema Kwa Sisi wakazi wa maeneo haya ya mbagala,chamazi,msongola,kitonga Hadi chanika baada serikali kutaka kuanza ujenzi ramsi wa barabara 4 ( 2 lanes)..
Toka mwezi uliopita TANROAD wamepigwa alama ya X nyumba zote zilizopo kwenye hifadhi ya barabara pamoja na notes ya siku 14 ya ubomoaji... Maandalizi haya ya AFRICON ambayo yanafadhiliwa na chama cha Mpira barani Africa CAF Kwa kutoa pesa Kwa nchi inayoandaa michuano husika Kwaajili ya miundombinu ya barabara na viwanja hatimae imetuangukia na sisi tunaoishi huku.

Uwanja wa Azam chamazi complex utatumika na kwenye mashindano ya 2027 kama kiwanja ramsi cha mazoezi na kambi ya timu mbili za mashindano Kwa muktadha huu hii barabara yetu itakuwa busy sana hasa kwa washabiki watakao shuka na ndege kuelekea Gongolamboto-chanika-mvuti-kitonga Hadi chamazi uwanjani

Wale mafala ambao HAPA MJINI WAMEKUJA tunawaambia kilasiku kuwa hapa DAR kila sehemu ina umuhimu wake na hakuna ushuwani wala uswahilini Bali sehemu zote zinafanana Tu
 
Back
Top Bottom