KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 19,765
- 39,524
Naona umeninukuu vibaya ila nimeona ulichoandika kuhusu wale birthers.
Hapo kuna tofauti kidogo.
Hao birthers sikuwahi kuwasikia hata siku moja wakidai wanacho cheti cha kuzaliwa cha Obama ambacho kinaonyesha alizaliwa Kakamega au kwingineko huko Kenya.
Au waliwahi kudai hivyo?
Licha ya hivyo, unajua ilimchukua muda gani Obama kukionyesha cheti chake?
Mimi pia nataka kuviona hivyo vyeti vya Makonda.
Kama yeye mwenyewe hataki kutuonyesha, na madhali kama Gwajima anasema yeye anavyo ofisini kwake.
Kwa nini sasa Gwajima asituonyeshe tu yeye mwenyewe kuliko kumsubiri Makonda?
Hawezi kufanya hizo kwa sababu hana hicho alichodai kuwa anacho........
Ni utapeli mwingine kutoka kwa watu wenye ushawishi mkubwa kwenye jamii ya watu waliochagua kuwa watumwa wa mihemko yao.....!!