Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro inakufa

Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro inakufa

Nimewahi kuitembelea wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro nilichokiona huko kinatisha, Rombo ni wilaya ambayo iko nyuma sana kimaendeleo na watu wake hawana habari yoyote ya maendeleo zaidi ya kunywa pombe!

Pombe, pombe, pombe hakuna cha mzee au mtoto hata mwanafunzi! Shule zinakosa wanafunzi kiasi cha kufikia kuunganisha shule au madarasa! Rombo hakuna makaburi! Utashangaa kuona mafuvu ya watu kwenye migomba! Ni kitu cha kawaida sana.

Nirudi kwenye ulevi, pombe nyingi za chupa zinazotengenezwa majumbani huuzwa shilingi mia tano tu na ni kali sana! Wazee kwa watoto wanazinywa sana kuanzia asubuhi mpaka usiku hakuna kufanyakazi na watu wazima wanaume nao majukumu ya kuendeleza kizazi kinawapiga chenga kiasi cha kuwafanya wake zao watafute mamluki wa kutekeleza jukumu ya kuendeleza kizazi.

Serikali iwasaidiaje, serikali iwaelimishe madhara ya pombe pamoja na kidhibiti viwanda bubu vya pombe. Nini mbadala wa pombe, serikali iwafundishe kilimo cha miparachichi ya muda mfupi tofauti na waliyonayo, ardhi ya Rombo ni nzuri kwa miparachichi.

Watalimaje, iwaweke kwenye vikundi vidogo vidogo ambavyo vitakuwa rahisi kudhibitiwa.

Ninaamini wazazi wanaume wakidhibitiwa kwenye ulevi watoto ni wazi hawatafurukuta watarudi shule.

Serikali ione kinachoendelea Rombo ambacho kimeanza kuiambukiza Marangu ni janga la taifa.
Kumbe kuna wachagga wa hovyo hovyo na wala hamsemi.. nyie watu mna siri sana.
 
Post yako ina ukweli kidogo sana. Rombo nilikuwepo mwaka huu kikazi. Ukifananisha Rombo na wilaya nyingine za Tanzania, Rombo ina maendeleo makubwa. Jambo lililo na ukweli kwenye post yako ni moja tu: kuna baadhi ya wakazi wamejiingiza kwenye unywaji wa pombe kupitiliza. Wanywaji wabobezi ni wachache ukilinganisha na wasiokunywa kupitiliza. Mambo mengine kama huduma za afya, benki, shule, usafiri, maduka nk Rombo ni moja ya wilaya zenye viwango vya juu kwa wilaya za Tanzania ambazo hazipo mijini.
Haujaambiwa ulinganishe Rombo na Wilaya nyingine, kwanini unakuwa na kichwa kigumu kiasi hicho ?
 
..Basil Mramba asilaumiwe hapa.

..alijitahidi Rombo wakajenga shule za sekondari kila kata.

..waliobaki waendeleze na kuboresha mazuri aliyoyaacha.

NB:

..kuna majimbo hapa Tz yangetamani kuwa na mbunge mchapakazi kama Basil Pesambili Mramba.
Wamuache kabisa mwana kiaranu wetu[emoji4]
 
Nilijua ni kweli ila kwa Mada hizo, mtoa mada hapa anachuki au analishwa matango pori na watu wahuko ikuinii.. [emoji1787]
Hahaha mbona ikuini imejengeka wewe. Wacha mambo hizo bana
 
Viongozi wa dini wameshindwa, wakezao wameamua kuwafungia mageti! Kwa sababu ya uwezo mdogo na watoto hawaendi shule nao wameungana na baba zao kwenye pombe, wanawake ndio wamebaki wakiangalia nyumba. Rombo ina nyumba nyingi sana za mabanzi ya magogo na tofauti utaiona ukiimaliza Marangu, sasa humo kwenye hizo nyumba za mabanzi ndimo pombe hunyweka.
Tusimlaumu mbunge ngoma inayochezwa huko haiwezi, Selasini alishindwa japo alilalamika mpaka bungeni, Mramba yeye hakuwa na taimu na warombo wenzake, yeye alikuwa bize kudokoa nyanya kwenye bustani ya babu.
Suluhisho ni serikali iwakusanye vijana kwenye vikundi vidogo vidogo iwaanzishie mashamba ya miti ya miparachichi ya muda mfupi, taratibu watazoea kuyatunza kuliko mashamba ya mahindi na maharage.
[emoji23][emoji23] what a liar. Eti watoto wanafungiwa ndani. Wewe ni mmarangu kama sikosei. Kwanini uziite mabanzi badala ya mbao. Unajua kwanini wanajenga kwa kutumia mbao ama unanena tu? Unajua kwanini most of houses nyingi ni za mbao? Na unajua gharama zake? Ama kwakua hapo Rongai upatilanaji wa mbao ni mkubwa na rahisi ndo maana unachukulia poa hup ujenzi?

Nyumba za mbao ni nzuri na bora hasa mazingira ya baridi. Marangu mna nini nyie zaidi ya kujisifia wakati hamna kitu Mnakisifia shule ambayo kila mtu anapeleka mtoto wake shule siku hizi? Mmeishia kudanga tu Rombo. Nyodo tu.

Most of vijana hawako Rombo wako mbali kutafuta. Kama vijana hawapo unategemea vipi kupata vizazi vipya? Mbona hili jambo ni la muda sana mpaka shule zingine huko keni mfano walizifunga kabisa? Mbona ni kawaida sana huko uchagani boma mona unakuta miji hata mutano ila hakuna hata mtu zaidi ya wafanyakazi ama bibi na babu? Sasa kwanini idadi isiwe ndogo kanisani, hospitali na hata shule?

Funny enough wako wanaoshangaa mtu kutoka Rombo kwenda sehemu ya mbali kutafuta riziki ili hali na yeue amekuja rombo kutokea kwao kutafuta riziki? Unapoongelea Rombo unaongelea wafanya biashara. Ni mpumbavu mmoja atashangaa eti mtu kwenda mazingira mengine kuwekeza. Ama ni shule tatizo kichwani? Mbona hamshangai dangote kuja kuwekeza tz?
 
Kwenye uzi wako umeanza kwa kusema Rombo ipo nyuma sana kimaendeleo,sasa watu tunaoijua Rombo tunakwambia huu ni uongo..labda ungetuambia iko nyuma sana nyuma ya wilaya zipi hizo??..

Uzi umekaa kichukichuki na sio kweli kumulika unywaji pombe uliokithiri.
[emoji23][emoji23][emoji23] ujue nimeshangaa sana. Anadai kuna.mafuvu migombani[emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119]

Anaongelea mambo ya mbuoni ambayo yalikuaga miaka hiyo uchaggani almost kote ambapo walishaacha muda snaa ile hata hatujazaliwa. Yaani post yake ya chuki sana. Nakuambia kama jamaa si mmarangu basi tena
 
Hahaha mbona ikuini imejengeka wewe. Wacha mambo hizo bana
Mada imejikita kwenye ulevi wakupindukia inaolalamikiwa pia na wake zao, ilianza kama mzaha miakaminne iliyopita wanawake wa Rombo walipofunguka hadharani na kusema watawanyima unyumba waume zao kwa sababu ya ulevi.
 
Huu wote ni uongo mtupu.. maana kama ni ulevi, vijiji vyote Tanzania vinakunywa Pombe. Hivi kuna mahali watu wanapiga pombe kama mkoa wa Kagera?
 
Huu wote ni uongo mtupu.. maana kama ni ulevi, vijiji vyote Tanzania vinakunywa Pombe. Hivi kuna mahali watu wanapiga pombe kama mkoa wa Kagera?
Mbona wanawake wa Kagera hawalalamiki, je, nako kumejaa viwanda bubu vya kutengeneza pombe za kwenye chupa?
 
Rombo iko nyuma sana kimaendeleo??Hivi kuna watu wamejenga kwao kama Warombo?..Kwa standard yetu duni ya Tz,Rombo iko vizuri.

Umeme upo long time tu huko..hata barabara nyingi zinapitika fresh..watu wamejenga pia sana.

Hii Tanzania yetu duni ni Wilaya chache tu ambazo zitalingana na Rombo kwa unafuu..(tukitoa wilaya lizilobeba mji wa Mkoa)

Pombe ni kweli zinanyweka vibaya mno..serikali iingilie hizi pombe kali za bei rahisi rahisi zidhibitiwe.
Binafsi nimekuelewa sana hapa mkuu.
Nadhani wanaokejeli Rombo bila shaka wanaitazama based on other Wilaya za Kilimanjaro.
But kiukweli Rombo haina hali mbaya kiasi kama hichi watu naona wanaitazama.
 
Fine, mimi mjinga lakini si mlevi. Ninaongelea walevi wa Rombo ambao mimi ninawajua na nimekunywa nao pombe. Mimi ninaohusiano kuanzia Marangu mpaka Tarakea, hapo katikati ziko familia nne zinazonihusu sana pamoja na ujinga wangu. Hivi kilichotangazwa jana usiku saa mbili kuhusu walevi wa Rombo na hatua zilizochukuliwa ziliandaliwa na chuki ya CNN! Hizo ni siasa za kisoshalisti ambazo zimepitwa na wakati. Watangazaji unaosema wanaichikia Rombo bahati mbaya ni wachaga! Lakini hao wake zenu huenda na wako yumo mbona ndio waliokwenda kulalamika kwenye vyombo vya habari! Mbona jirani zenu wamarangu wanasema sana kwa ulevi wenu kiasi cha kutelekeza familia.
Mjadala huu nimeuleta ili werevu wauone na kutoa msaada wa kukukwamua wewe na walevi wenzako ili nguvu zirudi na kizazi kirudi, wenzenu wa Tanga waliokolewa kutoka kwenye madawa ya kulevya kwa kuwekewa Sober Houses.
Sijui utanitukana tena kuwa mjinga au utaleta jipya toka Kenya.
Hii taarifa iliketwa na Mwandishi wa Marangu usisahau hili na pia siasa zilikua nyingi. Na ni nani anakidanganya uchaggani kungine hakuna ulevi?
 
Mada imejikita kwenye ulevi wakupindukia inaolalamikiwa pia na wake zao, ilianza kama mzaha miakaminne iliyopita wanawake wa Rombo walipofunguka hadharani na kusema watawanyima unyumba waume zao kwa sababu ya ulevi.
Ukweli ni kwamba, ulevi upo, na sivyo unavyokuzwa kisiasa. Ni idadi ya wangapi hao wanaokunywa kiasi hicho? Mnaongea na sisi wenyeji ama hao ITV walioamua kujitafutia mileage za kisiasa? Unakumbuka tena kipindi kile cha HUU NI UKIMWI ROMBO cha Betty mkwassa ndo akajipatia na vyeo? Is it true iko vile? Ni familia moja iliyoathirika na ni family kabisa. Lakini ilikua generalised as ni Rombo yote. Kwanini? Naongea hili kwakua naijua hiyo familia kindakikindaki. Yaani at times mtu akitaka njia ya kutoma anatafuta jambo tu apate njia. Akaacha enda makete huko ila akavamia familia ya mtengie. Familia ambayo wanaishi maisha yao tu. Hawalali hata kwa njaa.

Sameways na hili la ulevi. Rombo hakuna watu, hakuna watu nakueleza. Na waliopo majority hawanywi kama inavyokuzwa. Wanaokunywa ni wachache sana.

Pia unapaswa kujua kwamba pombe hasa bia kwa kenya ni ghali sana. Hivyi jionj wao huvuka boda hasa hapo Tarakea na kuja kunywa bia zetu na kisha kurudi kenya.

Mbona unadanganya kuhusu mafuvu? Hizi ni tamaduni zilikuwepo uchagani kote labda utoe machame tu ambapo kuna sehem panaitwa mbuoni ndipo walikua wakipeleka hapo mabaki ya miili? Na hii tamaduni mbona imekufa miaka mingi sana? Kwanini unatia sana chumvi?

Kuhusu kusema rombo haina maendeleo umewahi tembelea mbona muongo sana wewe jamaa? Ama kwakua tuko humbled hatujibrag? Mushazoea wanaojibrag? Acha uongo.
 
Hii taarifa iliketwa na Mwandishi wa Marangu usisahau hili na pia siasa zilikua nyingi. Na ni nani anakidanganya uchaggani kungine hakuna ulevi?
Nimesema janga la ulevi limeanza kuiambukiza Marangu kuanzia Mwika mpaka Marangu Mtoni vijana wameanza ila wao bado wana banana tu hawana brandi nyingi kama Rombo kwani viwanda bubu bado.
Mbona Tanga ilipokabiliwa na tatizo la vijana ulevi wa mihadarati wake kwa waume walilipokea na hivi sasa limekuwa dogo kumebakiwa na watoto wa ibilisi.
 
Binafsi nimekuelewa sana hapa mkuu.
Nadhani wanaokejeli Rombo bila shaka wanaitazama based on other Wilaya za Kilimanjaro.
But kiukweli Rombo haina hali mbaya kiasi kama hichi watu naona wanaitazama.
Rombo tena ya sasa ni matata kuliko hata hizo wilaya zingine za kilimanjaro. Niamini mimi. Ni vile huwa hawana makelele.
 
Nimesema janga la ulevi limeanza kuiambukiza Marangu kuanzia Mwika mpaka Marangu Mtoni vijana wameanza ila wao bado wana banana tu hawana brandi nyingi kama Rombo kwani viwanda bubu bado.
Mbona Tanga ilipokabiliwa na tatizo la vijana ulevi wa mihadarati wake kwa waume walilipokea na hivi sasa limekuwa dogo kumebakiwa na watoto wa ibilisi.
Wewe mmarangu tulia. Mukipataga pa kuhemea ndo kama hivi chuki. Tutakua hatuoi dada zenu tena wanaodangadanga. Ulevi uko kila mahali. Ni vile kila mtu anatafuta mada yake apate pa kutokea.

Huoni kama kuna viwanda vingi watu ni wachapakazi kwakua rasilimali zake zinapatikana kwa urahisi kwa maana hiyo serikali ilitakiwa sasa iweke mazingira bora katika hii kitu ili ziboreshwe? Nyie marangu zaidi ya utalii kuna nini kingine?

Sisi kuna viwanda vya mbao, kuna utalii via rongai route na lake chala etc, kuna kilimo cha nyanya, vitungui, ndizo, viazi mbiringo vya west, border ya kenya, route kamili za mabasi etc. Bado vijaana wana ujasiri wa kutoka nke ya wilaya na mkoa na hata nje ya nchi kama nairobi etc kusaka noti. Nyie lazi yenu ipi kama si vijana wa kiume kuolewa ulaya? Hio habari mmeibeba sana
 
Huko Ndiyo Wanawake Walikuwa Wanakwenda Kenya Kupata Wanaume
 
Ukweli ni kwamba, ulevi upo, na sivyo unavyokuzwa kisiasa. Ni idadi ya wangapi hao wanaokunywa kiasi hicho? Mnaongea na sisi wenyeji ama hao ITV walioamua kujitafutia mileage za kisiasa? Unakumbuka tena kipindi kile cha HUU NI UKIMWI ROMBO cha Betty mkwassa ndo akajipatia na vyeo? Is it true iko vile? Ni familia moja iliyoathirika na ni family kabisa. Lakini ilikua generalised as ni Rombo yote. Kwanini? Naongea hili kwakua naijua hiyo familia kindakikindaki. Yaani at times mtu akitaka njia ya kutoma anatafuta jambo tu apate njia. Akaacha enda makete huko ila akavamia familia ya mtengie. Familia ambayo wanaishi maisha yao tu. Hawalali hata kwa njaa.

Sameways na hili la ulevi. Rombo hakuna watu, hakuna watu nakueleza. Na waliopo majority hawanywi kama inavyokuzwa. Wanaokunywa ni wachache sana.

Pia unapaswa kujua kwamba pombe hasa bia kwa kenya ni ghali sana. Hivyi jionj wao huvuka boda hasa hapo Tarakea na kuja kunywa bia zetu na kisha kurudi kenya.

Mbona unadanganya kuhusu mafuvu? Hizi ni tamaduni zilikuwepo uchagani kote labda utoe machame tu ambapo kuna sehem panaitwa mbuoni ndipo walikua wakipeleka hapo mabaki ya miili? Na hii tamaduni mbona imekufa miaka mingi sana? Kwanini unatia sana chumvi?

Kuhusu kusema rombo haina maendeleo umewahi tembelea mbona muongo sana wewe jamaa? Ama kwakua tuko humbled hatujibrag? Mushazoea wanaojibrag? Acha uongo.
Acha mengine tatizo la ulevi waulize wanawake wa Rombo wanaohangaika na maisha kila kukicha mikungu ya ndizi na maparachichi kichwani kupeleka sokoni, sijui kama nao ni wanasiasa.
Unajua Rombo ina brandi nyingi za pombe za chupa toka viwanda bubu.
 
Back
Top Bottom