Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro inakufa

Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro inakufa

Nimeona makala ya ITV kuhusu unywaji wa hii pombe majuzi jumatano. Inasikitisha hii hali aisee.
 
Huyo mbunge walipitishwa na mwendazake,hajui hata shida za Wana Rombo.
Viongozi wa dini wameshindwa, wakezao wameamua kuwafungia mageti! Kwa sababu ya uwezo mdogo na watoto hawaendi shule nao wameungana na baba zao kwenye pombe, wanawake ndio wamebaki wakiangalia nyumba. Rombo ina nyumba nyingi sana za mabanzi ya magogo na tofauti utaiona ukiimaliza Marangu, sasa humo kwenye hizo nyumba za mabanzi ndimo pombe hunyweka.
Tusimlaumu mbunge ngoma inayochezwa huko haiwezi, Selasini alishindwa japo alilalamika mpaka bungeni, Mramba yeye hakuwa na taimu na warombo wenzake, yeye alikuwa bize kudokoa nyanya kwenye bustani ya babu.
Suluhisho ni serikali iwakusanye vijana kwenye vikundi vidogo vidogo iwaanzishie mashamba ya miti ya miparachichi ya muda mfupi, taratibu watazoea kuyatunza kuliko mashamba ya mahindi na maharage.
 
Nimewahi kuitembelea wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro nilichokiona huko kinatisha, Rombo ni wilaya ambayo iko nyuma sana kimaendeleo na watu wake hawana habari yoyote ya maendeleo zaidi ya kunywa pombe!

Pombe, pombe, pombe hakuna cha mzee au mtoto hata mwanafunzi! Shule zinakosa wanafunzi kiasi cha kufikia kuunganisha shule au madarasa! Rombo hakuna makaburi! Utashangaa kuona mafuvu ya watu kwenye migomba! Ni kitu cha kawaida sana.

Nirudi kwenye ulevi, pombe nyingi za chupa zinazotengenezwa majumbani huuzwa shilingi mia tano tu na ni kali sana! Wazee kwa watoto wanazinywa sana kuanzia asubuhi mpaka usiku hakuna kufanyakazi na watu wazima wanaume nao majukumu ya kuendeleza kizazi kinawapiga chenga kiasi cha kuwafanya wake zao watafute mamluki wa kutekeleza jukumu ya kuendeleza kizazi.

Serikali iwasaidiaje, serikali iwaelimishe madhara ya pombe pamoja na kidhibiti viwanda bubu vya pombe. Nini mbadala wa pombe, serikali iwafundishe kilimo cha miparachichi ya muda mfupi tofauti na waliyonayo, ardhi ya Rombo ni nzuri kwa miparachichi.

Watalimaje, iwaweke kwenye vikundi vidogo vidogo ambavyo vitakuwa rahisi kudhibitiwa.

Ninaamini wazazi wanaume wakidhibitiwa kwenye ulevi watoto ni wazi hawatafurukuta watarudi shule.

Serikali ione kinachoendelea Rombo ambacho kimeanza kuiambukiza Marangu ni janga la taifa.
Nilitaka niseme nemo ila nimeamua kuacha moyoni.Naomba kuijua wilaya yenu ili tuilinganishe na Rombo.Maana naongelea Rombo kwa kuishi ina maendeleo Sana ukilinganisha na wilaya nyingi Tz na pili Warombo kwa asili ni wachapakazi Sana na hawana majivuno.
 
Nilitaka niseme nemo ila nimeamua kuacha moyoni.Naomba kuijua wilaya yenu ili tuilinganishe na Rombo.Maana naongelea Rombo kwa kuishi ina maendeleo Sana ukilinganisha na wilaya nyingi Tz na pili Warombo kwa asili ni wachapakazi Sana na hawana majivuno.
Hoja yako ni nini, hoja iliyopo hapa ni ulevi uliopindukia, hakuna maendeleo ya ulevi duniani. Naona tatizo lako ni kiswahili.
 
Soma vizuri hoja imejikita kwenye nini, wewe unaishi Dar haujui hali insyoendelea Rombo, ukiona wake wanasema wanalazimika kwenda Kenya kujikimu haja ya baba na mama ujue hali si hali tena. Wewe umejikita kwenye mabasi na maghorofa!
Thank you elvischirwa nimeona hiyo report. Aisee thanks Khali sio Kama nilivyoiacha miaka Ile nachumbia kule. The situation is pathetic. Serikali ifanye kitu.
 
Hoja yako ni nini, hoja iliyopo hapa ni ulevi uliopindukia, hakuna maendeleo ya ulevi duniani. Naona tatizo lako ni kiswahili.
Kwenye uzi wako umeanza kwa kusema Rombo ipo nyuma sana kimaendeleo,sasa watu tunaoijua Rombo tunakwambia huu ni uongo..labda ungetuambia iko nyuma sana nyuma ya wilaya zipi hizo??..

Uzi umekaa kichukichuki na sio kweli kumulika unywaji pombe uliokithiri.
 
..Basil Mramba asilaumiwe hapa.

..alijitahidi Rombo wakajenga shule za sekondari kila kata.

..waliobaki waendeleze na kuboresha mazuri aliyoyaacha.

NB:

..kuna majimbo hapa Tz yangetamani kuwa na mbunge mchapakazi kama Basil Pesambili Mramba.
Mramba alipeleka lami mpaka tarakea, ameacha legacy kubwa sana
 
Kwenye uzi wako umeanza kwa kusema Rombo ipo nyuma sana kimaendeleo,sasa watu tunaoijua Rombo tunakwambia huu ni uongo..labda ungetuambia iko nyuma sana nyuma ya wilaya zipi hizo??..

Uzi umekaa kichukichuki na sio kweli kumulika unywaji pombe uliokithiri.
Maendeleo unayoyajua wewe ni yapi, kununua vitu Kenya na kujauza Rombo! Kusafirisha bidhaa za Kenya kwa bodaboda maporini! Nimekuambia ingia Facebook ITV Ripoti Maalum 01/09/2021 3:30 usiku utakuta majibu yote, na hiki nilichokiandika siyo kipya kimekwisha semwa bungeni na aliyewahi kuwa mbunge wenu, wake zenu wanalalamika, walimu wanalalamika na viongozi wa dini wanalalamika, ila wewe uko Sinza unatetea! Mimi nimekwenda mbali zaidi kutoa ushauri wa kuwasaidia wahusika kutoka kwenye ulevi wasaidiwe kwenye kilimo cha miparachichi ya muda mfupi badala ya hiyo iliyoko huko labda na aina mpya ya migomba.
Naona wewe unaridhika kuharibikiwa vijana walioko huko na kama haujui janga hilo limeanza kuingia Marangu kuanzia Mwika mpaka Marangu Mtoni.
Endelea kutokubaliana na mimi ila tafuta ITV mtandaoni uone nini kinachoendelea Rombo, achana na mabasi na maghorofa, hayo ukisha yajenga hayazai kitu.
 
Miaka fulani wamama walisema hao wanaume nguvu zimepungua shauri ya pombe.

Rombo kama Bazir hakuwasaidia kimaendeleo ndo basi, wageukie kwa Uhuru
 
Du! Mkuu siku ukiyakuta yapige picha upost hapa na unitag. Mimi naona hayo ni moja ya maajabu juu ya hii sayari Dunia.
Jamaa sijui anazungumzia Rombo ya wapi
Mimi nimetokea Rombo, kati ya watu wanaochukulia suala la msiba na kuzika serious basi ni Rombo,

watu wanatoka mikoa ya mbali sana kwenda kuzika ndugu yao Rombo

Sasa hili la mafuvu sijui kaliona wapi
 
Ingia Facebook tafuta ITV Ripoti Maalum 1st September 2021 saa 3:30 usiku, naona tutamaliza ubishi huko.
Kinachozungumzwa hapa si maghorofa ni ulevi uliopindukia wa hizi pombe za chupa za kijani unazoziona kwenye picha hii. Pombe hizi zinatengenezwa majumbani na bei ni kati ya sh.400 na 500 kwa chupa.

View attachment 1923222
Hiyo ripoti ya ITV kaijibu waziri na mbunge wa Rombo

 
..mbunge na viongozi wengine wenyeji wa Rombo wanapaswa kubeba suala hilo.

..DC, DAS, na viongozi wengine wa serikali, hawawezi kuwa na uchungu na watu huko Rombo.

..Mshahara wa DC wa Rombo upo palepale bila kujali madhara wanayoyapata Warombo.
Yani pombe wanywe wananchi afu DC akatwe mshahara au unatakaje?.
 
Jamaa sijui anazungumzia Rombo ya wapi
Mimi nimetokea Rombo, kati ya watu wanaochukulia suala la msiba na kuzika serious basi ni Rombo,

watu wanatoka mikoa ya mbali sana kwenda kuzika ndugu yao Rombo

Sasa hili la mafuvu sijui kaliona wapi
Hii pia imewahi kutoka siku nyingi kwenye TV, mabaki hufukuliwa baada miaka na huwekwa kwenye migomba kama sehemu ya mila, kwani wamasai zamani walikuaje.
 
Back
Top Bottom