Nimewahi kuitembelea wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro nilichokiona huko kinatisha, Rombo ni wilaya ambayo iko nyuma sana kimaendeleo na watu wake hawana habari yoyote ya maendeleo zaidi ya kunywa pombe!
Pombe, pombe, pombe hakuna cha mzee au mtoto hata mwanafunzi! Shule zinakosa wanafunzi kiasi cha kufikia kuunganisha shule au madarasa! Rombo hakuna makaburi! Utashangaa kuona mafuvu ya watu kwenye migomba! Ni kitu cha kawaida sana.
Nirudi kwenye ulevi, pombe nyingi za chupa zinazotengenezwa majumbani huuzwa shilingi mia tano tu na ni kali sana! Wazee kwa watoto wanazinywa sana kuanzia asubuhi mpaka usiku hakuna kufanyakazi na watu wazima wanaume nao majukumu ya kuendeleza kizazi kinawapiga chenga kiasi cha kuwafanya wake zao watafute mamluki wa kutekeleza jukumu ya kuendeleza kizazi.
Serikali iwasaidiaje, serikali iwaelimishe madhara ya pombe pamoja na kidhibiti viwanda bubu vya pombe. Nini mbadala wa pombe, serikali iwafundishe kilimo cha miparachichi ya muda mfupi tofauti na waliyonayo, ardhi ya Rombo ni nzuri kwa miparachichi.
Watalimaje, iwaweke kwenye vikundi vidogo vidogo ambavyo vitakuwa rahisi kudhibitiwa.
Ninaamini wazazi wanaume wakidhibitiwa kwenye ulevi watoto ni wazi hawatafurukuta watarudi shule.
Serikali ione kinachoendelea Rombo ambacho kimeanza kuiambukiza Marangu ni janga la taifa.