Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro inakufa

Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro inakufa

Nilijua ni kweli ila kwa Mada hizo, mtoa mada hapa anachuki au analishwa matango pori na watu wahuko ikuinii.. 🤣
 
Nimewahi kuitembelea wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro nilichokiona huko kinatisha, Rombo ni wilaya ambayo iko nyuma sana kimaendeleo na watu wake hawana habari yoyote ya maendeleo zaidi ya kunywa pombe!

Pombe, pombe, pombe hakuna cha mzee au mtoto hata mwanafunzi! Shule zinakosa wanafunzi kiasi cha kufikia kuunganisha shule au madarasa! Rombo hakuna makaburi! Utashangaa kuona mafuvu ya watu kwenye migomba! Ni kitu cha kawaida sana.

Nirudi kwenye ulevi, pombe nyingi za chupa zinazotengenezwa majumbani huuzwa shilingi mia tano tu na ni kali sana! Wazee kwa watoto wanazinywa sana kuanzia asubuhi mpaka usiku hakuna kufanyakazi na watu wazima wanaume nao majukumu ya kuendeleza kizazi kinawapiga chenga kiasi cha kuwafanya wake zao watafute mamluki wa kutekeleza jukumu ya kuendeleza kizazi.

Serikali iwasaidiaje, serikali iwaelimishe madhara ya pombe pamoja na kidhibiti viwanda bubu vya pombe. Nini mbadala wa pombe, serikali iwafundishe kilimo cha miparachichi ya muda mfupi tofauti na waliyonayo, ardhi ya Rombo ni nzuri kwa miparachichi.

Watalimaje, iwaweke kwenye vikundi vidogo vidogo ambavyo vitakuwa rahisi kudhibitiwa.

Ninaamini wazazi wanaume wakidhibitiwa kwenye ulevi watoto ni wazi hawatafurukuta watarudi shule.

Serikali ione kinachoendelea Rombo ambacho kimeanza kuiambukiza Marangu ni janga la taifa.
naona umekuja kishari shari....ngoja nipunzike kwanza..maana nimechafuka nyongo 🙂 🙂
 
hamna wilaya katika mkoa wa kilimanjaro isokuwa na janga la ulevi....na inaonekana wazi wewe ni mpita njia ....so asha shobo fanya yaliyokupeleka na urudishe makongoro kwenu kusikokuwa na wanywaji wa pombe
 
Ndugu wanaweka mafuvu ya ndugu zao nyumbani kwenye migomba yao. Warombo makaburi hawayajali wala hawayatilii maanani, unaweza ukasimama chini ya mti akaja mtu kukiambia imesimama juu ya kaburi, miti ndiyo alama ya makaburi.
yani wewe ndo unaonekana hauelewi kitu kabisa...kama hauna info piga kimya tu..
 
Baada ya Mods kushindwa kuihamishia Post hii kwenda kwenye siasa, naona Post imepoteza lengo kwa walengwa hivyo nafikiria kuifuta.
Post yako ina ukweli kidogo sana. Rombo nilikuwepo mwaka huu kikazi. Ukifananisha Rombo na wilaya nyingine za Tanzania, Rombo ina maendeleo makubwa. Jambo lililo na ukweli kwenye post yako ni moja tu: kuna baadhi ya wakazi wamejiingiza kwenye unywaji wa pombe kupitiliza. Wanywaji wabobezi ni wachache ukilinganisha na wasiokunywa kupitiliza. Mambo mengine kama huduma za afya, benki, shule, usafiri, maduka nk Rombo ni moja ya wilaya zenye viwango vya juu kwa wilaya za Tanzania ambazo hazipo mijini.
 
asante kwa kuliona hilo...naunga na wewe maanake mimi ni mzaliwa wa kule...pombe imekuwa kero lakini kwenye maendeleo wilaya ipo vizuri ukilinganisha na wilaya nyingine ndani ya TZ
 
Ingia tu ata gugo sarch tarakea ressot au ata snow cape afu ndo uendelee kupiga mdomo
Ndo hapa?
250px-Rombo_mjini_2006.jpg
 
Unachosema ni kweli ila kwa hali ya hewa na rutuba iliyoko haistahili kuwa hivyo, fananisha na jirani yao Marangu uone tofauti iliyopo japo nayo siku hizi vijana wamejiingiza kwenye ulevi hawataki kazi.
Mkoa wa kilimanjaro kwa ujumla imekumwa na wimbi la hili tatizo la unywaji wa pombe uliopitiliza ....nadhani hii inatokana na swala la kudorora uchumi na ukosefu wa ajira kwa vijana wengi....
 
wanaume wa Dar tu majangaa...itakuwa wa huko mikoani
 
Mkoa wa kilimanjaro kwa ujumla imekumwa na wimbi la hili tatizo la unywaji wa pombe uliopitiliza ....nadhani hii inatokana na swala la kudorora uchumi na ukosefu wa ajira kwa vijana wengi....
images (3).jpeg
images (2).jpeg
images (1).jpeg
download (1).jpeg
download.jpeg
download (3).jpeg
 
maeneo ya himo hayo...swala la kushuka kwa kazi za tours nalo limechangia kukosa hata zile kazi za kupandisha watalii mlimani....CORONA Kweli imetuweza..
Kweli we ni sifuri kwaio io gorofa ya maulidi na hio hotel ya resot zipo himo!
 
Kweli we ni sifuri kwaio io gorofa ya maulidi na hio hotel ya resot zipo himo!
sasa zihaka zote hizo zinatoka wapi...kunakibaya kipi nimekisema hapo ...kuwa mstaarabu !!!!
 
sasa tushike lipi jamani?!!!!!

juzi nimeona makala maalumu kupitia ITV, aisee kuna walevi huko si mchezo!
 
Back
Top Bottom