Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro inakufa

Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro inakufa

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
23,961
Reaction score
29,338
Nimewahi kuitembelea wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro nilichokiona huko kinatisha, Rombo ni wilaya ambayo iko nyuma sana kimaendeleo na watu wake hawana habari yoyote ya maendeleo zaidi ya kunywa pombe!

Pombe, pombe, pombe hakuna cha mzee au mtoto hata mwanafunzi! Shule zinakosa wanafunzi kiasi cha kufikia kuunganisha shule au madarasa! Rombo hakuna makaburi! Utashangaa kuona mafuvu ya watu kwenye migomba! Ni kitu cha kawaida sana.

Nirudi kwenye ulevi, pombe nyingi za chupa zinazotengenezwa majumbani huuzwa shilingi mia tano tu na ni kali sana! Wazee kwa watoto wanazinywa sana kuanzia asubuhi mpaka usiku hakuna kufanyakazi na watu wazima wanaume nao majukumu ya kuendeleza kizazi kinawapiga chenga kiasi cha kuwafanya wake zao watafute mamluki wa kutekeleza jukumu ya kuendeleza kizazi.

Serikali iwasaidiaje, serikali iwaelimishe madhara ya pombe pamoja na kidhibiti viwanda bubu vya pombe. Nini mbadala wa pombe, serikali iwafundishe kilimo cha miparachichi ya muda mfupi tofauti na waliyonayo, ardhi ya Rombo ni nzuri kwa miparachichi.

Watalimaje, iwaweke kwenye vikundi vidogo vidogo ambavyo vitakuwa rahisi kudhibitiwa.

Ninaamini wazazi wanaume wakidhibitiwa kwenye ulevi watoto ni wazi hawatafurukuta watarudi shule.

Serikali ione kinachoendelea Rombo ambacho kimeanza kuiambukiza Marangu ni janga la taifa.
 
Nimewahi kuitembelea wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro nilichokiona huko kinatisha, Rombo ni wilaya ambayo iko nyuma sana kimaendeleo na watu wake hawana habari yoyote ya maendeleo zaidi ya kunywa pombe! Pombe, pombe, pombe hakuna cha mzee au mtoto hata mwanafunzi! Shule zinakosa wanafunzi kiasi cha kufikia kuunganisha shule au madarasa! Rombo hakuna makaburi! Utashangaa kuona mafuvu ya watu kwenye migomba! Ni kitu cha kawaida sana.

Nirudi kwenye ulevi, pombe nyingi za chupa zinazotengenezwa majumbani huuzwa shilingi mia tano tu na ni kali sana! Wazee kwa watoto wanazinywa sana kuanzia asubuhi mpaka usiku hakuna kufanyakazi na watu wazima wanaume nao majukumu ya kuendeleza kizazi kinawapiga chenga kiasi cha kuwafanya wake zao watafute mamluki wa kutekeleza jukumu ya kuendeleza kizazi.

Serikali iwasaidiaje, serikali iwaelimishe madhara ya pombe pamoja na kidhibiti viwanda bubu vya pombe. Nini mbadala wa pombe, serikali iwafundishe kilimo cha miparachichi ya muda mfupi tofauti na waliyonayo, ardhi ya Rombo ni nzuri kwa miparachichi. Watalimaje, iwaweke kwenye vikundi vidogo vidogo ambavyo vitakuwa rahisi kudhibitiwa.
Ninaamini wazazi wanaume wakidhibitiwa kwenye ulevi watoto ni wazi hawatafurukuta watarudi shule.
Serikali ione kinachoendelea Rombo ambacho kimeanza kuiambukiza Marangu ni janga la taifa.
Duuh! Hivi huku ndiyo nyumbani kwa yule waziri wa fedha aliyefukuzwa kazi na kuhukumiwa kwenda jela? Pia akiwa katika kiti cha enzi alituambia tule majani ili ndege ya Mkapa inunuliwe!
 
Ulevi hata aliyekuwa mbunge Selasini aliwahi kuliongelea bingeni ikiwa ni pamoja ya malalamiko toka kwa viongozi wa dini.

..mbunge na viongozi wengine wenyeji wa Rombo wanapaswa kubeba suala hilo.

..DC, DAS, na viongozi wengine wa serikali, hawawezi kuwa na uchungu na watu huko Rombo.

..Mshahara wa DC wa Rombo upo palepale bila kujali madhara wanayoyapata Warombo.
 
Duuh! Hivi huku ndiyo nyumbani kwa yule waziri wa fedha aliyefukuzwa kazi na kuhukumiwa kwenda jela? Pia akiwa katika kiti cha enzi alituambia tule majani ili ndege ya Mkapa inunuliwe!

..Basil Mramba asilaumiwe hapa.

..alijitahidi Rombo wakajenga shule za sekondari kila kata.

..waliobaki waendeleze na kuboresha mazuri aliyoyaacha.

NB:

..kuna majimbo hapa Tz yangetamani kuwa na mbunge mchapakazi kama Basil Pesambili Mramba.
 
Hilo la mafuvu kukutwa kwenye migomba ni kweli au chumvi tu ndugu yangu!
Ndugu wanaweka mafuvu ya ndugu zao nyumbani kwenye migomba yao. Warombo makaburi hawayajali wala hawayatilii maanani, unaweza ukasimama chini ya mti akaja mtu kukiambia imesimama juu ya kaburi, miti ndiyo alama ya makaburi.
 
Back
Top Bottom