Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro inakufa

Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro inakufa

inaonyesha hujawahi hata kufika Rombo.
Rombo ni moja ya wilaya zilizoendelea sana.
 
Ndugu wanaweka mafuvu ya ndugu zao nyumbani kwenye migomba yao. Warombo makaburi hawayajali wala hawayatilii maanani, unaweza ukasimama chini ya mti akaja mtu kukiambia imesimama juu ya kaburi, miti ndiyo alama ya makaburi.
huu uongo unakusaidia nini?
stupid
 
hayo ni maoni yako...na unaonekana hauna busara..wilaya ya rombo mbunge na madiwani wengi walitoka CCM...so jifikirie tena
Baada ya jiwe kuiba viti vyote bila kujali wananchi wamemchagua nani kuwa kiongozi wao.
 
ahsante!

nilihisi kitu kama hicho. nimesoma kwenye hiyo post kuna sehemu inasema ardhi nzuri inayofaa kwa kilimo cha maparachichi. nikakumbuka jinsi maparachichi yalivyo na hela, pia nikakumbuka nilivyofika mpaka tandahimba ndani kabisa na kukutana na vijana wa kilimanjaro wakitafuta ridhiki nikabaki najiuliza inawezaje wakimbie kwao na kuja mbali kote huku ilihali ardhi yao iko vizuri tu?!
Ardhi imejaa ile. Kwa wastani familia moja miliki kama heka moja au pungufu. Hapo hata uweke miparachichi haifiki miche 100.
 
Ardhi imejaa ile. Kwa wastani familia mojamiliki chini ya heka moja. Hapo hata uweke miparachichi haifiki miche 100.
Huyu anaona kwamba yeye na ITV ndio wanaijua ROMBO kuliko sisi wazawa, inabidi tumuambie asante kwa kuitangaza Rombo japo kwa mabaya ila wazawa tunaijua vizuri
 
Nimewahi kuitembelea wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro nilichokiona huko kinatisha, Rombo ni wilaya ambayo iko nyuma sana kimaendeleo na watu wake hawana habari yoyote ya maendeleo zaidi ya kunywa pombe!

Pombe, pombe, pombe hakuna cha mzee au mtoto hata mwanafunzi! Shule zinakosa wanafunzi kiasi cha kufikia kuunganisha shule au madarasa! Rombo hakuna makaburi! Utashangaa kuona mafuvu ya watu kwenye migomba! Ni kitu cha kawaida sana.

Nirudi kwenye ulevi, pombe nyingi za chupa zinazotengenezwa majumbani huuzwa shilingi mia tano tu na ni kali sana! Wazee kwa watoto wanazinywa sana kuanzia asubuhi mpaka usiku hakuna kufanyakazi na watu wazima wanaume nao majukumu ya kuendeleza kizazi kinawapiga chenga kiasi cha kuwafanya wake zao watafute mamluki wa kutekeleza jukumu ya kuendeleza kizazi.

Serikali iwasaidiaje, serikali iwaelimishe madhara ya pombe pamoja na kidhibiti viwanda bubu vya pombe. Nini mbadala wa pombe, serikali iwafundishe kilimo cha miparachichi ya muda mfupi tofauti na waliyonayo, ardhi ya Rombo ni nzuri kwa miparachichi.

Watalimaje, iwaweke kwenye vikundi vidogo vidogo ambavyo vitakuwa rahisi kudhibitiwa.

Ninaamini wazazi wanaume wakidhibitiwa kwenye ulevi watoto ni wazi hawatafurukuta watarudi shule.

Serikali ione kinachoendelea Rombo ambacho kimeanza kuiambukiza Marangu ni janga la taifa.
Wewe ni mtu unahusda tu na kiroho cha kwa nini.

Ulichokiona Rombo ni watu wanakunywa tu pombe?

Kwa nini usishangae kwamba Rombo hakuna tena nyumba za tope?

Hakuna tena nyumba za Nyasi?

Kwanini usione ajabu watu wanahamasisha ujenzi wa Vyoo vya maji?

Au hujawahi kutembea kwenye Wilaya za nchi hii au umevimbiwa tu maharage ukajiandikia kishabiki.

Kahifunze Rombo wale watu wanachapa kazi acha kabisa.
 
Unaweza ukasema wachache ila ukienda huko utakuta vijana na wanafunzi wamejikita kwenye ulevi wa kupindukia. Haijawahi kutokea uwepo wa utalii wa ulevi! Rombo upo! Wanywaji wanaotaka pombe zenye viwango vya juu vya ulevi na zenye bei nafuu sana, hivyo wanywaji hutoka Kenya kwenda kunywa Rombo na kurudi kwao.
Nitakuja nipatembelee soon
 
Wewe ni mtu unahusda tu na kiroho cha kwa nini.

Ulichokiona Rombo ni watu wanakunywa tu pombe?

Kwa nini usishangae kwamba Rombo hakuna tena nyumba za tope?

Hakuna tena nyumba za Nyasi?

Kwanini usione ajabu watu wanahamasisha ujenzi wa Vyoo vya maji?

Au hujawahi kutembea kwenye Wilaya za nchi hii au umevimbiwa tu maharage ukajiandikia kishabiki.

Kahifunze Rombo wale watu wanachapa kazi acha kabisa.
Ingia Facebook tafuta ITV Ripoti Maalum 1st September 2021 saa 3:30 usiku, naona tutamaliza ubishi huko.
Kinachozungumzwa hapa si maghorofa ni ulevi uliopindukia wa hizi pombe za chupa za kijani unazoziona kwenye picha hii. Pombe hizi zinatengenezwa majumbani na bei ni kati ya sh.400 na 500 kwa chupa.

239732907_373687784404560_6739017304008787912_n.jpg
 
Mnao nishutumu mngeanza na wanawake wa Rombo wanaolalamika kuwa ulevi wenu umeharibu ndoa zenu kwa kushindwa kuwatimizia haja zao za baba na mama, siyo mabasi na maghorofa.
 
Mmesema Rombo hakuna maendeleo. Maendeleo gani mnauazungumzia? Unaweza kuilinganisha Rombo na Jimbo la ndugai ambako hata maji ya kutawadha Ni changamoto?
 
Kuna kipindi Cha ripoti maalumu Cha ITV wiki kadhaa zilizopita walionyesha hali ilivyo huko Rombo kama ni kweli walichoonyesha ndiyo hali halisi ilivyo basi Kuna haja ya kuchukua hatua kwa maslahi mapana ya wananchi wa Rombo na Taifa kwa ujumla.
 
Mmesema Rombo hakuna maendeleo. Maendeleo gani mnauazungumzia? Unaweza kuilinganisha Rombo na Jimbo la ndugai ambako hata maji ya kutawadha Ni changamoto?
Soma vizuri hoja imejikita kwenye nini, wewe unaishi Dar haujui hali insyoendelea Rombo, ukiona wake wanasema wanalazimika kwenda Kenya kujikimu haja ya baba na mama ujue hali si hali tena. Wewe umejikita kwenye mabasi na maghorofa!
 
Kuna kipindi Cha ripoti maalumu Cha ITV wiki kadhaa zilizopita walionyesha hali ilivyo huko Rombo kama ni kweli walichoonyesha ndiyo hali halisi ilivyo basi Kuna haja ya kuchukua hatua kwa maslahi mapana ya wananchi wa Rombo na Taifa kwa ujumla.
Ile ilikuwa sehemu ya kwanza, sehemu ya pili ilikuwa tarehe 1 mwezi wa 9 / 2021 saa 3:30 usiku, huko ndiko balaa kabisa utakuta wakenya wanaokuja Rombo utalii wa kunywa pombe za bei nafuu na akina mama walioyelekezwa huku waume zao wakidai hawana hamu nao zaidi ya pombe!
Ingia Facebook ITV Ripoti Maalum 01/09 2021 3:30 usiku.
 
Back
Top Bottom