Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro inakufa

Kuna maendeleo
ahsante!

nilihisi kitu kama hicho. nimesoma kwenye hiyo post kuna sehemu inasema ardhi nzuri inayofaa kwa kilimo cha maparachichi. nikakumbuka jinsi maparachichi yalivyo na hela, pia nikakumbuka nilivyofika mpaka tandahimba ndani kabisa na kukutana na vijana wa kilimanjaro wakitafuta ridhiki nikabaki najiuliza inawezaje wakimbie kwao na kuja mbali kote huku ilihali ardhi yao iko vizuri tu?!
 
Watu wachache ndio wanafanya paonekane pabaya
 
Labda huijui Rombo.Tuulize sisi tuliozaliwa na kukulia rombo.

Eti rombo hakuna makaburi,huu ni utoposhaji wa kiwango cha juu mno.

Kama hawafanyi kazi,hizo hela za kunywa pombe wanapata wapi?
 
Hili kwakweli naamini amekoleza chumvi. Ni kawaida watu kuponda pasio kwao na huku kwao kukiwa hohehahe hadi aibu.
Ataje kwao mtoa post ili tupathaminishe.
 
Ukisema Rombo haijaendelea, si kweli hukufanya tathmini ya kutosha. Hebu angalia idadi ya wasomi na matajiri wa Rombo. Angalia magari ya mkoani yanavyopiga toot Rombo, ina maana kuna mzunguko mzuri wa pesa. Ni baadhi tu ya wachache ambao watakomeshwa. Watapewa elimu ili wajitambue.
 
Nilijua ni kweli ila kwa Mada hizo, mtoa mada hapa anachuki au analishwa matango pori na watu wahuko ikuinii.. 🤣
Kwahiyo haukubali kwamba Rombo kuna ulevi wa kutisha! Mbona hata huyo uliyemnukuu anakubali kwamba kuna ulevi mkubwa, hiki nilichoandika hakina tofauti na kilichotangazwa na ITV jana usiku. Tatizo huwa hamuelewi mada inazungumzia nini, mada haihusu maghorofa wala maduka, inahusu ulevi wa kupindukia.
 
Tatizo baadhi ya wanaochangia mada ni wale wasiofuatilia vipindi vya habari kwenye TV, wanashindwa kuona kuwa kunawachangiaji wengine wameona kwenye TV hili tatizo la ulevi, lakini pia hata bungeni limewahi kufikishwa zaidi mara moja, ukweli utabaki kuwa Rombo kuna ulevi wa kupindukia. Anayetaka kuongelea mabasi aongelee japo halihusiani na ulevi.
Soma #64
 
Kwahiyo haukubali kwamba Rombo kuna ulevi wa kutisha! Mbona hata huyo uliyemnukuu anakubali kwamba kuna ulevi mkubwa, hiki nilichoandika hakina tofauti na kilichotangazwa na ITV jana usiku. Tatizo huwa hamuelewi mada inazungumzia nini, mada haihusu maghorofa wala maduka, inahusu ulevi wa kupindukia.
Ulevi wakupindukia ni dalili ya kuwa na akili ya kutafuta, kila mlevi anajua kuchakarika ajue wapi anapata ya kunywa bohora kesho yake, hongera wana Rombo kwa kuongezq mapato ya serikali na kuwezesha wilaya nyingine kupata huduma muhimu kwa kunywa pombe
 
Hawanywi hizo za tozo, wao wanaviwanda vyao chupa sh500/= ni kali kuliko hiyo ya sh2,000/=.
 
Nashangaa sana watu kujadili kwamba wana-rombo hawataki kazi,hili suala la kutotaka kazi siyo kwa wanarombo tu bali ni suala la watanzania wengi!!
 
Mkoa wa kilimanjaro kwa ujumla imekumwa na wimbi la hili tatizo la unywaji wa pombe uliopitiliza ....nadhani hii inatokana na swala la kudorora uchumi na ukosefu wa ajira kwa vijana wengi....
Hilo litakuwa kweli, watu wa kutengeneza ajira Kilimanjaro wapo mikoa mingine. Ardhi ya kilimo hakuna, mtu anaamua kupiga tu pombe.
 
Nashangaa sana watu kujadili kwamba wana-rombo hawataki kazi,hili suala la kutotaka kazi siyo kwa wanarombo tu bali ni suala la watanzania wengi!!
Mada inahusu ulevi wa kupindukia kiasi cha wanawake kulalamika na kukiri wanakwenda Kenya kujikimu haja zao, wanaobisha waendelee tu kubisha.
 
Hawanywi hizo za tozo, wao wanaviwanda vyao chupa sh500/= ni kali kuliko hiyo ya sh2,000/=.
Unaiona 500 ndogo ? Toka asubuhi sijaiokota mahali, respect hustle za watu wewe wao kulewa inakuwasha wapi, mume wako Mworombo kakunyima matumizi au?
 
Baada ya kunikashifu moyo wako umefurahi! Wenzako tunajadili ili tupate suluhisho wewe suluhisho lako ni matusi, asante.
 
Watu wachache ndio wanafanya paonekane pabaya
Unaweza ukasema wachache ila ukienda huko utakuta vijana na wanafunzi wamejikita kwenye ulevi wa kupindukia. Haijawahi kutokea uwepo wa utalii wa ulevi! Rombo upo! Wanywaji wanaotaka pombe zenye viwango vya juu vya ulevi na zenye bei nafuu sana, hivyo wanywaji hutoka Kenya kwenda kunywa Rombo na kurudi kwao.
 
tazama hapa Ripoti maalumu ITV kuhusu unywaji pombe ulio kithiri uko wilayani Rombo

Hao wanaobisha wanazo simujanja ila wanashindwa kuingia kwenye app. ya ITV ambako wangejionea hali halisi badala ya kubisha tu.
 
Back
Top Bottom