Wilaya ya Mbarali imekuwa ikitoza ushuru wakulima bila kuwatengenezea barabara

Mpap Ndabhit

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
237
239
Moja Kwa Moja kwenye mada; niwapongeze wilaya ya Mbeya vijijini waliohusika na ujenzi wa Barabara ya Inyala -Malamba kupitia hospitali ya wilaya iliyopo Inyala Hadi stesheni ya Tazara Kijiji Cha Malamba.

Barabara hii haijawahi kutengenezwa toka mwaka 1970 wakati wa ujenzi wa reli. Barabara hii ni njia ya mkato inayotemegewa sana kupitisha mazao ya wakulima hususani, mahindi, maharage na mpunga kutoka mashambani.

Licha ya umuhimu wake Halmashauri ya Mbarali imeitekeleza Barabara Kwa miaka mingi Kwa kuinyima bajeti ya matengenezo. Wananchi wanalazimika kusafiri Kwa mzunguko umbali wa karibu kilometa 100 wakati Barabara ya mkato IPO na haizidi kilometa 10.

Sasa halmashauri ya wilaya ya Mbeya vijijini wametuletea hospitali ya wilaya jirani inayotegemewa na vijiji vya Malamba, machimbo, Ruiwa, mahango, motomoto lakini wanavijiji watalamizika kusafiri umbali karibu kilometa 100 Badala ya kilometa 10 kupata huduma hospitalini ikiwa Barabara ya mkato itajengwa.

Kama Haitoshi Mbeya vijijini wamejenga Barabara umbali wa kilometa 7 Ili kuunganisha na hivyo vijiji vya Mbarali lakini mpaka Sasa hainekani jitihada yoyote kuumaliza kipande hicho upande wa Mbarali. Wilaya ya Mbarali wamekuwa wakitoza ushuru wakulima bila kuwatengenezea hiyo barabara.

My take: Mnaotegemea kupewa kura kwenye uchaguzi msiende Kuomba kura huko maana wamewachoka na ahadi zenu. Wananchi wanaomba wajulikane wapo wilaya ya Mbeya vijijini badala Mbarali.
 
Back
Top Bottom