TARURA na Mbunge wa Kibamba, barabara ya Kibamba-Hondogo-Kidimu ni mbovu sana. Tutengenezeeni

sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
3,022
5,254
Hali ni mbaya sana kwa barabara ya Kibamba kwenda Hondogo kata ya Kibamba wilaya ya Ubungo. Hatuoni viongozi wakichukua hatua kurekebisha, si TARURA, si diwani, mbunge wa kuchaguliwa wala mbunge wa viti maalum wamefanya hata ziara kuangalia au hata kuagiza magreda kuja kutengeneza barabara.

Barabara haina mitaro, mvua zimeichimba katikati na kusababisha mifereji iliyojikatizia barabarani kuweka mashimo makubwa, na hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa pikipiki (bodaboda) ambazo ndio usafiri rasmi huku maana hakuna daladala zinazokuja. Kuna wakazi wengi sana Hondogo na pia kuna viongozi wengi wanaishi huku lakini hakuna msaada wowote wanaotoa na wala wingi wa wakazi haujaliwi ndio maana mpaka leo hakuna ruti ya daladala kwenda Mbezi au Hata Kibamba Njiapanda, ni mwendo wa bodaboda tu kwa umbali wa kilometa karibu 7.

Mbunge wa Kibamba, Mhe. Issa Mtemvu kata ya Kibamba ndipo makazi yako yalipo ajabu hatuoni ukipambana tupate barabara ya lami, sijui kwa kuwa wewe gari lako ni la juu hivyo halipati shida kwa barabara hizi. Diwani Kilango tunasikia amehama kata anaishi nje ya kibamba, labda ndio sababu ya kutowajali wapiga kura wake.

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo. Mhe. Hashim Komba tunaomba uingilie kati mtutengenezee barabara. Wewe ulipita wiki mbili zilizopita ulipokwenda kukagua eneo la kujenga chuo cha VETA pale Shule ya msingi Kibwegere, ulijionea ubovu wa barabara, tusaidieni.

Tunajua tunastahili kupata barabara ya lami au zege kama zilizojengwa kwa Musuguli kwenda Malamba mawili, au Kimara Korogwe kwenda Kilungure na maji chumvi lakini sio mbaya mkileta hata greda lichonge na vifusi vimwagwe kuimarisha barabara, kipindi hiki cha mvua zipitike vizuri.

Changamoto kubwa ni kuongezeka kwa Nauli za bodaboda maana vyombo vinaharibika kupiga piga mashimo ukizingatia kuwa tumezoeana kupanda mishkaki ili kupunguza gharama maana hali ni tight.

Yaani Kutoka Hondogo kwenda Mbezi na kurudi mtu unatumia Tshs. 4000 mpaka elfu 5 na ni umbali wa km 15 tu huku mtu anayetoka Mbagala kuja Mbezi akitumia Tshs. 1700 tu kwenda na kurudi. Pale Kibamba Njiapanda kuna karibu bodaboda 500 zinazokwenda Hondogo, Kibwegere na Kidimu, ushahidi kuwa wakazi huko ni wengi sana.

Tafadhali tuoneeni huruma, tutengenezeeni barua ili gharama za usafiri zipungue na hata mabasi/daladala huenda yatakuja. Huku kuna zahanati, kuna shule 2 za msingi, shule 2 za sekondari (za serikali) na sasa mtajenga chuo cha VETA kwa Wilaya ya Ubungo, hii miundombinu inahitaji barabara bora.
 
Mkuu na mimi naongezea kero yangu,

Barabara ya kutoka Magufuli stand kupitia M/magoe kuelekea M/pande mpaka bunju B yenye ukubwa wa 25KM, ni mbovu sana kiasi kwamba daldala na Bus zinazoenda kaskazini zimeisusia zinapitia njia ya goba-madale

Just imagine Gari inayotoka Mbezi mwisho stand kwenda bunju inapitia njia ya Goba ,wakati kuna short cut ya kufika Bunju B just 25Km ,ila serikali yetu imekaa kimya tuu hakuna plan ya kuwekwa lami kwa siku za hivi karibuni

Wakazi wa M/magoe, Msumi na msakuzi wanaelewa changamoto wanayokumbana nao kila siku

Asante
 
Niliona mahali wanasema mwaka wa fedha 2024/25 mradi wa DMDP utajenga kilometa 36 kwa kiwango cha lami kwa wilaya ya Ubungo.

BARABARA ZA MITAA ZITAKAZOJENGWA NA DMDP

Kwa wilaya ya Ubungo, jumla ya kilomita 36.11 zitajengwa kwenye maeneo zaidi ya 20 kwa umbali tofauti.

Katika maeneo yote barabara ndefu zaidi ni kilomita 9.83 ya Msumi, na Goba Wakorea kilomita 7.76, huku barabara fupi ni ile ya kilomita 0.28 ya Tiptop na barabara ya Shule.

Nyingine ni Hondogo Shija (4.16), Makoka (4.04), Posta Matembe (0.82), Sheikh Bofu (1.13), Msikitini (0.37), Sinza KKKT (0.27), Segesera (0.77), Lion (0.84), Juma Ikangaa (0.97), Mbegani (0.28), Namnani (0.66), Chimwaga (0.34) na Mikindani (0.45)

Zimo barabara za Ubungo NHC (0.6), Midizini (0.99) na Binti Kayenga (1.27). Jumla ni kilomita 36.11.
 
Back
Top Bottom