Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,897
- 941
LUDEWA TUNASEMA ASANTE MHE. RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
Wilaya ya Ludewa tunamshukuru Rais wa Jamhuri wa Muugano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hasani kwa kuipatia fedha Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Milioni 977,600,000/= chini ya mradi wa Boost katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023.
Wilaya ya Ludewa imepokea fedha hizo na zimeelekea moja kwa moja kwenye maeneo ya miradi husika kama ifuatavyo:
1. Kata ya Mavanga imepokea fedha ya kujenga shule ya msingi mpya eneo la Ruhuhu Darajani kiasi cha jumla ya shilingi milioni 347,500,000/=. Aidha shule ya msingi Mbugani imepokea kiasi cha jumla ya shilingi 81,000,000/= kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa na matundu 3 ya choo.
2. Kata ya Ludewa imepokea fedha ya kujenga madarasa 2 ya elimu ya awali katika shule ya msingi Ludewa Mjini kiasi cha jumla ya shilingi 69,100,000/=
3. Kata ya Milo imepokea fedha ya kujenga madarasa 3 na matundu 3 ya choo katika shule ya msingi Mapogoro kiasi cha jumla ya shilingi 81,000,000/=
4. Kata ya Ludende imepokea fedha ya kujenga madarasa 3 na matundu 3 ya choo katika shule ya msingi Maholong’wa kiasi cha jumla ya shilingi 81,000,000/=
5. Kata ya Mlangali imepokea fedha ya kujenga madarasa 4 na matundu 3 ya choo katika shule ya msingi Mlangali kiasi cha jumla ya shilingi 106,000,000/=
6. Kata ya Mundindi imepokea fedha ya kujenga darasa 1 na matundu 3 ya choo katika shule ya msingi ya elimu maalumu Mundindi kiasi cha jumla ya shilingi 31,000,000/=
7. Kata ya Lupingu imepokea fedha kiasi cha jumla ya shilingi 181,000,000/= kwaajili ya ujenzi wa madarasa 3, ujenzi wa matundu 3 ya choo na nyumba mbili za walimu katika Shule ya Msingi ya Nindi
Aidha, Tunaishukuru Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha kwaajili ya kuboresha elimu ya Kidato cha Tano na Sita Wilayani Ludewa kwa kuongeza idadi ya Wanafunzi kwenye Shule ya Sekondari Mundindi Iliyopo Tarafa ya Liganga, Kata ya Mundindi
Tumepewa Mchanganuo wa miundombinu kama ifuatavyo; Madarasa 9, Mabweni 4, na Matundu ya vyoo 14 yenye Jumla ya Shilingi Milioni 773,000,000/= ambapo Muda wa Ujenzi ni Siku 90 tu.
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya tunaendelea kusimama thabiti na wananchi wa Kata ya Mundindi kwa usimamizi na kutoa ushirikiano wote ili miradi hiyo ikamilike ndani ya muda uliopangwa na kuleta tija iliyokusudiwa na kuonesha thamani ya fedha.
Ludewa Yetu, Maendeleo Yetu.