Why watu wenye mafanikio wamesoma kayumba? Samatta, Diamond, Doctors, Engineers, President etc

Kwanza tukubaliane international schools ni zipi hapa bongo maana naona wengine wanataja tusiime kama international, seriously? Tukiongelea international tuwaongelee akina IST, DIA, BRAEBURN, MIS, ISM, HOPAC and the like...Tusiime sijui St.Marys ni kayumba zilizochangamka

Sent using Jamii Forums mobile app
jamaniii umenichekesha sana, eti kayumba zilizochangamka
 
mtoa mada wewe umesoma wapi? Kayumba au international schools?
Kama jibu ni kayumba, je? mafanikio yako unayalinganisha na ya nani hapo sammata? au diamond?
 
Elimu bora ipo INTERNATIONAL SCHOOL huku kwingne sijui st kayumba na private school za kawaida hamna kitu.
Tofauti ya private school za kawaida kama st Mary's ni lugha na mazingira ya kaujifunzia ni rafiki. Ila mambo wanayo soma ni yale yale ya kukalilisha ili wafaulu. Tofauti na International school wao mtoto anasoma kitu kinacho endana na wakati.

Sema wengi tuliosoma kayumba mafanikio yetu huwa yapo kwa kile Mungu alichotupatia kipaji, karama, nk
 
Nmesoma comments zote kwa umakini mkubwa.
Ni kweli kwamba asilimia kubwa ya watanzania hatumudu kulipa ada kwa hizo shule. Angalia tunavyosumbuana tu na mikopo ya Loan Board, ndo maana hata Rais aligoma lockdown ya corona kwa kuzingatia hali zetu za maisha.
Kuhusu hizi shule za international nafikiri zinatuzidi kwenye mazingira ya shule na msimamizi ila walimu ni wa kawaida sana. Ndg yangu alishashafundisha IST miaka ilopita.
Tukubali tu ukweli kuwa hizi shule ni kwa ajili ya royal families. Tofauti za kimaisha ni kawaida tu maana hata huko Ulaya na Marekani maskini wapo. Leo hii mimi mwalimu nalipwa say laki 4 kwa mwezi siwezi kumsomesha mtoto shule km hiyo hata km natamani, hesabu haziruhusu. La muhimu tupambane kutafuta maisha mazuri ila kwa njia halali.
Ila pia hao wstu walosoma hizo IST wamekuwa na mchango gani kwa nchi yetu? Mbona tupo vilevile? Hatua gani sisi km nchi au jamii tumepiga kwa kuwa na hao watu?
Ebu tuendelee kujifukiza buana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona umekuja kubishana bila sababu huku uzi wangu umeuelewa naongelea tusiime na shule za english medium za kati.. nitajie mtu mmoja aliesoma IST kisha chuo akasoma udsm.. ama ameajiriwa na serikali kama doctor, engineer ama fani yoyote ? Mtaje mmoja tu...
Tusiime ni Kayumba inayotumia Lugha ya Kiingereza.International ni IST,Aga Khan,ISM hao ndo international
 
Jikite kwenye mada mkuu, acha kujadili watu.

Suala lako Ni kusomesha Mtoto wako PRIVATE SCHOOL vs GOVERNMENT SCHOOL.

Sasa unapoambiwa habari za IST, ukaanza kutoa povu.

Wakati nayo pia Ni private school.

TUNABAKI TUNAKUSHANGAA.

Sent using Jamii Forums mobile app
Jamaa kasema Eti Kayumba vs International unamtajia IST anaanza kubisha.Kasahau Kuwa Tusiime sio International ila ni Kayumba ambayo ni English Medium
 
Umaskini tu,
ILA kiukweli elimu Bora Inapatkana INTERNATIONAL SCHOOLS.

Tanzania tuna uhaba sana wa ajira,

Ila Ni ngumu sana kukutana na bahasha ya kijana alietoka TANGANYIKA INTERNATIONAL SCHOOL akiomba ajira mitaani.

Pia, Ni ngumu kuskia graduate wa TANGANYIKA kaajiliwa ktk utumishi wa Umma.
Hasa hizi kada za chini chini Kama ualimu,nursing, n.k

Jiulize wakimalizaga wanaenda wapi?

Na hizi shule Kila mwaka zipo, na zinatoa wanafunzi wengi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa ndipo penye swali kwanza. Hebu tupe uelewa kidogo huwa wanafanya kazi wapi. C kwamba kutokana na wazazi wao kuweza kuwasomesha shule za gharama hvyo huwa kiukweli wako vzuri kifedha kwa hyo hata hao watoto wakimaliza ajira ikawa ishu wanakuwa shaped na utajiri wa wazazi so ni vigumu kuona msoto wao?
 
Mkuu watu wenye mafanikio unaowasema wewe ni wenye miaka 40+. Sasa ukikutana na mtu wa namna hii akikupa historia ya elimu yake sana sana shule za private zilikuwa za seminary. Shule za private zimeanza kuja miaka ya 2000. Na zilikuja kama mbadala wa upungufu wa shule Tz. Shule za serikali zilikuwa chache sana. Wanafunzi wachache sana waliweza kufaulu na kuendelea na shule.

Wale waliokuwa na wazazi wenye kipato cha juu, waliweza kwenda shule za private. Huzi shule wanafunzi walionekana kama failures.

Shukrani ziende kwa mkapa na JK kwa kuleta shule za kata. Shule zikajengwa kila kata. Wanafunzi hata wasiojua kusoma na kuandika wakaweza nao kufaulu na kuendelea na shule katika hizi shule za serikali.

Wazazi sasa wakaanza kuogopa shule za serikali sababu ufaulu ni mdogo ingawa zinabebwa na serikali. Wazazi wakaanza kukimbiza watoto wao private. Shule za private zikawa nyingi na adda zikawa za kawaida.

Wanafunzi shule za private wakaanza kufaulu zaidi ya shule za serikali. Sasa mambo yamebadilika. Wamafunzi wa private wanaonesha kuwa na uwezo mkubwa kuliko shule za serikali.

Effect ya hii kitu utaanza kuiona miaka 20 ikayo. Maana wanafunzi waliosoma private ndyo wataonekana kuwa na mafanikio kuliko wa serikali wanaomaliza secondary hawajui hata kuandika.
 
Habari wadau..

Mbona watu wengi wenye mafanikio wamesoma kayumba?

Hizi shule za kizungu zinakosea nini kuandaa watoto ?

Nimepima sector zote.. kuanzia michezo, business, politics, music, engineering naona kayumba wanaongoza...

Nawaza tu hizi shule za mtoto kubeba begi kubwa na kuchukuliwa na school bus saa 12 asubuh na kurudi saa 10 jioni au saa 12 jioni. Zinaweza kweli kumuandaa samatta au mchezaji hata wa yanga na simba mbeleni

Nawaza diamond wa mbeleni anaweza toka hizi shule kweli

Nawaza magufuli wa mbeleni anaweza toka hizi shule kweli?

Nawaza mwanangu nimpeleke goverment school kisha niwape walimu hela za tution shuleni kwake.. na kisha ada ambayo ningelipa tusiime nijikaze na kujitahidi kumjengea kila mwaka chumba kimoja...

Target kila mwaka chumba kimoja... ili nikishindwa maisha wapate hata pa kupangisha kama nikiondoka duniani...kuliko kupeleka ada shule ambazo imetokea corona ya miezi miwili tu zinanyanyasa walimu. Shule haziruhusu talent zinakomaa na mtoto siku nzima anashinda darasani hapati hata muda wa kucheza
Ugumu wa maisha huleta maarifa kwa anae jitambua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom