Una kasoro kama walizo nazo wanadamu wengine including hao wanaume. Kwa hiyo uko perfect. hao wanaume leo ukiwaambia wakuorodheshee madhaifu yako wataishia kukuchanganya maana kila mmoja atakupa orodha tofauti. tabia hiyo hiyo inaweza kukinzana au kuvutana na nyingine. Badala ya kusikitika kuwa unawatoa watu kwenye ukapuku halafu wanakuacha pata faraja kuwa wewe si box tupu. Una kitu ndani yako kikubwa tu ila unakitumia kusiko. Shukuru umejua.
Huu wakati wa huzuni ulio nao ni mzuri sana. Nimeupenda. Ndo wakati wa kupona. Sasa retreat and connect to your inner self. Uko mbali na nafsi na roho yako. Kaa mwenyewe, jitafute, jichambue, jitambue. Kwa lugha rahisi jiunganishe na Mungu wako aliyeko ndani yako, siyo wa kanisani. Ukishaimarisha uhusiano na wewe mwenyewe sasa unaweza kuanza kutafuta mkaka kichwa kikiwa kimetulia maana utakua tayari una amani moyoni na unajua unatafuta nini kwa mwanaume. Utakua umeshajua kwa nini unaishi na mwanaume gani ataendana na maisha unayotaka. Sasa hivi unajihisi mpungufu na unafikiri mwanaume ndo atakukamilisha matokeo yake unaishia kuumia.
Kuna watu wamekwambia sasa hivi achana na mapenzi jishughulishe na masomo, biashara, kuboresha taaluma, hobi, kuhudumia jamii, kufufua mahusiano na ndugu na marafiki n.k. Nami nasema hivyo hivyo. Lakini hivi vitu huwezi kuvifanya kwa ukamilifu kama hujatulia na kujitafuta na kujenga mahusiano ya karibu na wewe mwenyewe. Kuna wakati tunakuwa busy sana na mambo ya wenzetu kama kushauri na kusaidia wapenzi tunasahau kushughulika na sisi wenyewe. Unakua busy na boyfriend, unamsindikiza kwenye mpira, au akienda kwenye mpira wewe unanuna unaamua kulala. Kwa nini? Kwa sababu huna uhusiano na wewe mwenyewe kwa hiyo hata hobi zako huzijui unasindikiza za wenzio au kukereka nazo. Huna lengo kwenye maisha. Unasaidia wenzio kufikia malengo yao. Siku ukiachwa unaishia tu kulialia na kujilaumu na hata kulala ndani maka mzima hujui uanzie wapi kwa sababu hujui unaenda wapi wala kwa nini upo. Unasubiri mtu anayeenda kwenye safari yake aende na wewe. Unamsaidia mizigo akishafika, anakuacha. Anakuja mwingine anakukuta unalialia pale, kwa kuwa hukuwa na safari yako unaenda naye. Anafika, anakuacha. Hivyo hivyo.... Mwishowe unajikuta umeachwa mahali hata hujui ni wapi hata kurudi huwezi na hakuna tena mtu anayefika huko. Hapo sasa ndo inaitwa kutia akili. Huelewi uelekee wapi. Unajikuta umefika mpaka JF kuuliza njia. Ujitegemee mpaka utoke. Ndo uanze safari yako mwenyewe na akitokea mtu anataka mwende wote lazima utamuuliza anaenda wapi. Akikwambia "popote tu" au "twende tutajua huko huko mbele" unajua hili famba hili. Unatupa huko unaendelea mbele, wala hata moyo haukuumi. Unaendelea, ukikutana na anayejua anakoenda kama mnaenda kumoja, hewala unashukuru. Kama anakwenda kwingine na wewe kwingine lakini mkaamua ku-compromise kidogo ili kila mmoja afike haya... Ukikosa kabisa pia unashukuru, ukimpata baadae akaondoka unashukuru. Safari lazima iendelee. Samahani kwa kuandika sana. Nilikuwa sijui kama najua kuandika mpaka nilipoachwa. 😀😀😀 Uwe na amani. Maisha ni mtihani. Mtihani mgumu ni ule wa kukutoa ngazi moja kwenda nyingine ya juu zaidi. TULIA