Habari za jumapili! Kwa mara ya kwanza najitokeza kuomba ushauri kwa hichi kinachonisumbua kila siku....
Jinsia yangu mm ni ke, lakini ktk haya maisha ya mahusiano nmekua nikipitia magumu hadi najihisi labda mm niko tofauti......
Nmejaribu kua kwenye mahusiano ya kimapenzi lkn hakuna ata uhusiano mmoja ambao unanileta positive impacts ingawa kila mwanaume nnae kutana nae hua anaonyesha kuvutiwa na mm in all aspects(kitabia, upole, heshima) na mambo mengine, but at the end of the day naishia kuumia.
Na kwa bahati mbaya zaidi wote kimaisha wanakua wako chini lkn hua najitahidi kutoa support hadi mtu anafikia mafanikio, ila akishafanikiwa kama ni gari atapanda mwingine na mm naishia kuachwa..... Na ikitokea nmempata ambaye yuko well organized anakua anaonyesha hana imani na anahisi nmempenda sababu ya vitu ingawa sio kweli kabsaa najikuta naishia tu kuumia...
Na kitu kingine kinachoniumiza zaidi wakishaachana na mm baada ya mda wanaanza kunisumbua na kudai I was a right person na hii hutokea kwa wote..... Hichi kitu kinaniumiza, mbaya zaidi ata kama mtu kaoa still anakua maswala yake ya maisha atahitaji mm ni mshauri...
Naumia sana ndugu zangu natoa machozi kila siku, Natamani ifike siku Mungu anione na mm nmpate atakae tambua nafasi yangu.... Kuna mda natamani nizae tu mtoto nisahau habari za ndoa lakini naona ntakua naidanganya nafsi yangu kuishi maisha ambayo sikuwahi yawaza....
Naamini humu kuna wetu wengi wenye busara watanisaidia kiushauri nn cha kufanya, naogopa sana kukata tamaa lkn najiona ndiko nnakoelekea...
Kama nitakua nmeandika vibaya am sorry...
Karibuni!!