Why me? Kila mahusiano napitia magumu

Why me? Kila mahusiano napitia magumu

hujasema udhaifu wako ila lzm utakuwepo tu either ni cool sn yaan umekaa kaa tu km upo haupo hapo mtu ana lose interest au unakaba sn humpi mtu mda wa kupumua. una bana mno mtu anahisi hana uhuru.yan lzm unakitu unachofanya ambcho wanaume hawapendi...kwa mfano mimi mwanamk ambye hawezi kusema hiki sipendi,kile napenda,jana uliniudhi siwez kua nae uwaga na lose interested faster sio tabia mbya sn ila inanifanya ni lose interest sasa wewe unakatabia kadogo sn tu ambako kana madhara makubwa sn kwenye psychologia ya mwanaume hlf umesema unapata wa chini unawapandisha ww,nina mshikaji wangu ambye demu ake kwao wapo vzr ila shida sasa nkama sasa yeye ndo kawa mwanaume yan full kumpa hela na kumpangia masharti,men hatupendi hizo jamaa kila siku ansema huyu demu ntamuacha tu lkn nimalize pia km unaile tabia yenu ya kupenda msipopendwa na kujikodoa kodo na kujipitisha pitisha uache
 
Una tatizo....unayapa mahusiano too much attention
jaribu ku have fun kidogo
akija mtu hata unamkubali mchukulie kawaida
usi invest a lot hayo mahusiano
nenda taratibu tu......

wanasema love comes when you are not looking for it...
I like ur advice!!
 
Sometimes uwe unajaribu na maombi aiseee.

Isije kuwa wajanja wa dunia hii washakuona una nyota nzuri wakawa washafanya yao.

Vifungo vipo , tena vibaya sana.

Kuna mchezo siku hizi wa kuchafua uso wa mtu, omba hio isiwe ndio uliyofanyiwa.

Omba sana Mungu aiseee, kama huwezi tafuta mtu akusaidie katika hilo.
Nikweli, maombi muhimu
 
Amini Mungu, ipo siku atakupa. Kwa mawazo ya kibinadamu unawezafikiri kwamba una tatizo lakini huwezi jua mpango wa Mungu huenda ndo anakuepusha na yatakayotokea mbele, amini Mungu na siku zote yeye ni mwaminifu, atatengeneza njia pasipo na njia.
 
Utakuwa una matatizo sehemu, jichunguze vizuri
Na inaweza kuwa hana tatizo lolote ni vile tu Mungu hajampa mwenza wake awe na subira tu asilazimishe kabla mungu hajatoa kibali
 
Habari za jumapili,

Kwa mara ya kwanza najitokeza kuomba ushauri kwa hichi kinachonisumbua kila siku, jinsia yangu mimi ni ke, lakini katika haya maisha ya mahusiano nimekua nikipitia magumu hadi najihisi labda mimi niko tofauti...

Nimejaribu kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi lakini hakuna hata uhusiano mmoja ambao unanileta positive impacts ingawa kila mwanaume ninaekutana nae hua anaonyesha kuvutiwa na mimi in all aspects (kitabia, upole, heshima) na mambo mengine, but at the end of the day naishia kuumia...

Na kwa bahati mbaya zaidi wote kimaisha wanakua wako chini lakini huwa najitahidi kutoa support hadi mtu anafikia mafanikio, ila akishafanikiwa kama ni gari atapanda mwingine na mimi naishia kuachwa...

Na ikitokea nimempata ambaye yuko well organized anakuwa anaonyesha hana imani na anahisi nimempenda sababu ya vitu ingawa sio kweli kabisa najikuta naishia tu kuumia na kitu kingine kinachoniumiza zaidi wakishaachana na mimi baada ya mda wanaanza kunisumbua na kudai I was a right person na hii hutokea kwa wote...Hichi kitu kinaniumiza, mbaya zaidi hata kama mtu kaoa still anakuwa maswala yake ya maisha atahitaji mimi nimshauri...

Naumia sana ndugu zangu natoa machozi kila siku, natamani ifike siku Mungu anione na mimi nimpate atakae tambua nafasi yangu kuna mda natamani nizae tu mtoto nisahau habari za ndoa lakini naona nitakuwa naidanganya nafsi yangu kuishi maisha ambayo sikuwahi yawaza...

Naamini humu kuna wetu wengi wenye busara watanisaidia kiushauri nini cha kufanya, naogopa sana kukata tamaa lakini najiona ndiko ninakoelekea...

Kama nitakua nmeandika vibaya am sorry...

Karibuni!
Ujue siku ukijitambua hayata kupata tena, usiwe na haraka na mapenzi mtu wa ukweli ukutani naye kwa kujirahisisha kwake!

Shida yako ni moja tu, hujiamini unashusha kwa wanaume usijidai wala usijirahisishe be determined utapata mtu wa maana.
 
Hata mm mwanzoni nilidhani hivyo lkn nnejitahidi kwa kila namna ndugu yangu
Amini kuwa hauna mapungufu shost kinachotakiwa ni kumuomba Mungu pekee ndo anakujua na anaijua kesho yako kuliko unavyofikiria. Muda ukifika atakupa wako ambaye hautojutia maishani na utajidharau kwa yaliyopita ya nyuma
 
Touching. .... ila ningekushauri kuwa labda ungeanza kujitathimini hasa kwa vile vitu ambavyo hao wenza wako huwa wanavilalamikia kutoka kwako, na hasa mnapokuwa na kutokuelewana. Inaweza ikawa njia nzuri ya kuanzia.
Ni kwamba bado tu kopo halijapata mfuniko wake bana mbona wenye mapungufu weeengi wanaolewa na kuoa? Awe na subira ipo siku iliyopangwa na Mungu wetu
 
Habari za jumapili,

Kwa mara ya kwanza najitokeza kuomba ushauri kwa hichi kinachonisumbua kila siku, jinsia yangu mimi ni ke, lakini katika haya maisha ya mahusiano nimekua nikipitia magumu hadi najihisi labda mimi niko tofauti...

Nimejaribu kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi lakini hakuna hata uhusiano mmoja ambao unanileta positive impacts ingawa kila mwanaume ninaekutana nae hua anaonyesha kuvutiwa na mimi in all aspects (kitabia, upole, heshima) na mambo mengine, but at the end of the day naishia kuumia...

Na kwa bahati mbaya zaidi wote kimaisha wanakua wako chini lakini huwa najitahidi kutoa support hadi mtu anafikia mafanikio, ila akishafanikiwa kama ni gari atapanda mwingine na mimi naishia kuachwa...

Na ikitokea nimempata ambaye yuko well organized anakuwa anaonyesha hana imani na anahisi nimempenda sababu ya vitu ingawa sio kweli kabisa najikuta naishia tu kuumia na kitu kingine kinachoniumiza zaidi wakishaachana na mimi baada ya mda wanaanza kunisumbua na kudai I was a right person na hii hutokea kwa wote...Hichi kitu kinaniumiza, mbaya zaidi hata kama mtu kaoa still anakuwa maswala yake ya maisha atahitaji mimi nimshauri...

Naumia sana ndugu zangu natoa machozi kila siku, natamani ifike siku Mungu anione na mimi nimpate atakae tambua nafasi yangu kuna mda natamani nizae tu mtoto nisahau habari za ndoa lakini naona nitakuwa naidanganya nafsi yangu kuishi maisha ambayo sikuwahi yawaza...

Naamini humu kuna wetu wengi wenye busara watanisaidia kiushauri nini cha kufanya, naogopa sana kukata tamaa lakini najiona ndiko ninakoelekea...

Kama nitakua nmeandika vibaya am sorry...

Karibuni!
Tafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na Haki yake, na hayo mengine yote mtazidishiwa
PIA
Mtwikeni yeye fadhaha zenu zote, maana Yeye ni Mtulivu na Mnyenyekevu, atawakweza kwa wakati wake
PIA
Bwana asipoujenga mji waujengao wafanya kazi Bure
 
Back
Top Bottom