Binafsi sijaona hoja yenye kulihusisha shirika la wamisionari wabenediktini hawa katika mauaji hayo, kwani kama kuonekana sahihi za baadhi yao kwenye mikataba au shughuli mbalimbali ni wengi sana na ni mashirika mengi na watu binafsi walifanya kazi kama hizo na Hayati Mwaikusa. Je hao wote wahisiwe kuhusika na kifo hicho eti kwa vile walisiana kikazi katika uhai wake basi ndio walitoa uhai wake?
Nisingependa mhariri wa gazeti achukue habari za vijiweni na kuifanya habari kuu kwenye gazeti lake isiyo kuwa na utafiti wala vielelezo vya kuridhisha umma kwa shirika kama hili limehusika kukodi wauaji.
Jambo moja hili si shirika la Tanzania, ni la kimataifa, maana yake hali inaweza kuchukuliwa kimataifa kwa vile wakuu wa shirika hilo si raia wa Tanzania, bali ni wa nchi ya kigeni. Ndio maana kuna umihimu Gazeti lithibitishe tuhuma hizo au la likanushe kwa uzito ule ule, vinginevyo lifungiwe kwa uzushi.
Labda Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea Mhashamu Norbert Mtega atatoa kauli. Vinginevyo Mkuu wa shirika lao Abbot Jeremy toka St Otilien Ujeruman atoe ufafanuzi wa kuhisika shirika lake katika mauaji haya.