Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,883
- 6,884
Kweli Tanzania hatutaendelea, watawa wanafanya njama za kuua kwa ajili ya pesa eti unawaita wahuni.
Ama kweli Tanzania italiwa kwelikweli, maana maliasili zinaondoka bado tunawatetea wahalifu.
Hiyo skandali ni kweli kabisa na shirika ndio lililokuwa linamiliki mgodi, hapa hakuna kumunya munya. Kwenye hili hakuna siri. Juu ya mauaji ya Prof sijui.
Subirini CHADEMA washinde migodi yote itamilikiwa na Shirika wakisaidiwa na Ujerumani. Hapa ndio mwisho wa Tanzania.
Are you sure what you talking about? Hayati Mwaikusa alifanya mashauri mengi kwenye makampuni mengi ya kitaifa na kimataifa, binafsi na ya kiserikali, jumuiya mbalimbali nk, iweje wadonoe kapunje haka na kutogusa sehemu ambazo zinaweza kuashiria uwezekano huu?
Unamfahamu Rt Rev. Abbot Lambert Dorr OSB wa Abatia Peramihi, wilaya ya Songea vijijini katika Mkoa Ruvuma ambaye alikuwa anaongoza Abatia hiyo ya wamisionari wabenediktini ambayo makao yake makuu yako St. Otilien nchini Ujerumani na makao makuu ya confoederation yakiwa Rome wanakoendesha Chuo cha St Anselm ambao kinatoa mafunzo ya shahada za Liturgia ya kanisa, Mkuu wa hapo St Anselmo akiwa ni Victor Damez aliyekuwa Mkuu wa St Otilian?
Huo uchafu wa mgodi ni nini ukilinganisha na makubwa yalifanywa miaka nenda rudi kujenga mashule, hospitali, zahanati, vituo vya afya, na mengineyo, ni mgodi gani waliouendesha kupata pesa za kujenga hayo kama si misaada ya waumini na serikali ya Ujerumani na Uswiss kufadhili hayo yote?
Unafahamu umri wa hawa wazungu wa Ujerumani? Kama nilivyokuambia sasa hivi ni wazee ambao hata kukumbuka maua kuyamwagilia uani pao hawana, halafu wahangaikie migoni ya uswahilini? Zaidi kibaya eti kupanga na kumwuka Maikusa? Kama hatua zikichukuliwa na wahusika kulishinikiza gazeti lithibitishe publication nakuhakikishia itaumbuka.
Mhariri mkuu wa gazeti hilo anatakiwa kutafakari vya kutosha kuhusu upotoshaji huo, wasionewe wanyonge kwa vile hawana uwezo wa kujenga hoja za kujitetea.