Tarehe 27/4/2001, Raisi Benjamin William Mkapa alimteua Bwana John Tendwa kuwa Msajili mpya wa Vyama vya Siasa akichukua nafasi ya George Christopher Liundi ambaye muda wake ulimalizika.
Kabla ya hapo John Tendwa alikuwa wapi na alikuwa anafanya nini - wana JF mpo? - msaada unatakiwa kwani giza lililotanda kuhusu historia yake linaleta wasi wasi.
Je ni Mtanzania? Alizaliwa wapi? Alisomea wapi?
Again tunarudi kule kule, ndio maana tulimwambia MKJJ kuhusiana na upinzani bungeni kujengwa, hilo litawezesha kubadili taratibu nyingi za ki kiritimba....Tatizo Tanzania wateule wa rais hawapitishwi na Bunge ndiyo maana wengine hata u-research hautagundua chochote kuhusu CV zao na ni kwanini wamechaguliwa kuongoza kitengo au ofisi husika.
Ilitakiwa rasi akifanya uteuzi mzito kama hii ya msajili wa vyama vya siasa basi jina lipelekwe Bungeni na rais mwenyewe au kupitia waliopo chini yake wa-make case ya kwa nini rais kamchagua mtu fulani kwa ajili ya nafasi fulani. Raisi akishatoa maelezo yake (preferably kwa maandishi) kamati husika ijadili uwezo wa mtu huyo kupewa nafasi hiyo. Baada ya hapo mteuliwa mwenyewe apewe nafasi ya kujieleza mbele ya kamati ya Bunge au Bunge lenyewe ni kwa sababu gani anaona ana uwezo wa kuongoza ofisi husika. Kinacho fuata hapo ni mteuliwa kupigiwa kura na Bunge.
Tukifuata utaratibu wa wateule mbali mbali kupitishwa na Bunge basi hatutakuwa na shida ya kuchunguza bila mafanikio mtu katokea wapi. Kupitia utaratibu wa mtu kupitishwa na Bunge, kupitia yeye mwenyewe na aliyemteua wataelezea wasifu wake na kwa nini anafaa. Tusipofanya hivi watu watashika nafasi mbalimbali muhimu bila hata kujua wanatokea wapi.
Kama wanasiasa wanajieleza kwa wananchi ni kwa nini wanafaa (iwe wanadanganya au la) kwa nini na viongozi wengine muhimu wa kuteuliwa wasipitie process hiyo hiyo?
Kuna vitu vingi vidogovidogo tunaweza kufanya ambavyo vitasaidia kuepuka maswali madogo madogo ambayo wala hayakutakiwa kuwa tatizo. Majawabu rahisi yapo kwa matatizo ambayo tunayaona makubwa. Tunahitaji tu kufikiri kidogo na kutunga sheria practical badala ya sheria zisizo na faida zozote kwa taifa.
Again tunarudi kule kule, ndio maana tulimwambia MKJJ kuhusiana na upinzani bungeni kujengwa, hilo litawezesha kubadili taratibu nyingi za ki kiritimba....
Kuing'oa ccm kwanza then all is possible, ukpo MKJJ?
Lakini hili swala ni la Watanzania wote si MKJJ tu. MKJJ hawezi kuleta mabadiliko Bungeni na wala pekee hata kuwa factor ya kuing'oa CCM. This call should be to all Tanzanians.
Kama kuna wadau wanaweza kunisaidia (naamini itawasaidia wengine) kuweza kumjua vema ni nani, ametoka wapi, na hapa alipo tutarajie wapi ataelekea... (I doubt anaweza kuingia kwenye siasa na akawa upande wa chama 'flani').
Mkuu, kwa uhakika kabisa huyu Bwana ni mpare. Kuna mdogo wake wa kuzaliwa tumbo nafahamiana naye. Ni mpare wa kutokea Same. Ila CV yake kwa kweli sina, labda nijaribu kumdodosa huyu jamaa. Na kwa bahati mbaya huyu bwana mdogo na kaka yake hawaivi kabisa.John tendwa mi nimewahi kusikia ni mhehe,halafu nikasikia ni mngoni.......
John tendwa mi nimewahi kusikia ni mhehe,halafu nikasikia ni mngoni.......
HApA NDIO UMUHIMU WA SAUTI YA UMEME, FMEs' aka MZEE WA NYETI UNAPOONEKANA, HII KITU INGESHUSHWA SASA HIVI, MKUU YUKO WAPI SIKU HIZI