Hii mada imefika hadi ukurasa wa 80+ bila ya kupatikana majibu ya kutosha.
Ukweli ni kwamba hata nyie wenyewe hamna uhakika ama hamjui kama kweli Mungu yupo.
Mkijitafakari wenyewe kwa utulivu binafsi halafu mchunguze ni nini hasa mnachokiabudu, mtagundua kuna maswali mengi yanayoibuka na pengine kuwaacha njia panda.
Waliomuumba Mungu kwenye mawazo yao walishajifia zamani wamewarithisha watu hii dhana ya Mungu na kuieneza kwa watu.
Mungu + dini ni tamaduni za watu, ni kama mababu wa Afrika walivyokuwa na dhana potofu kuwa miti, miamba, ama milima ndiyo Mungu.Waliiabudu na kuitolea sadaka, waliitukuwa pamoja na mizimu ya watangulizi wao.
Vivyo hivyo kwa Miungu ya kwenye Bibilia, ni utamaduni wa waisrael(kama zilivyo tamaduni za makabila ya Afrika), wana mizimu yao kama kina Abraham, Isaka, na Yakobo.Ni watu waliokufa zamani lakini mizimu yao inatukuzwa kwenye makabila yao na kuenezwa nje ya makabila yao.
Kinachofanya hizi mila za wayahudi(dini) kuendelea kuwepo na kuenezwa ni ubabe na dharau kwa mila nyingine.Walizieneza hadi Ulaya kisha Afrika.Waliozipinga waliteswa sana na wengine waliuawa.
Dini na Mungu ni tamaduni za watu, hata sisi tulikuwa na za kwetu lakini kutokana na udhaifu wa mababu zetu, tamaduni zetu ziliuawa na kuwa replaced na hizi za wageni ambazo waafrika wanazienzi na kuziendeleza hadi leo kama Mnachokifanya hapa Jukwaani.