We umeniambia kuwa kwa sababu siwezi kuthibitisha kitu ninachokiamini hivyo naamini kitu chenye contradiction.
Au sikukuelewa vizuri?
Hapana.
Hujanielewa kama kawaida yako.
Nimekwambia unaamini kitu ambacho huwezi kukithibitisha na chenye contradiction.
Hivi ni vitu viwili tofauti.
Sina tatizo sana na mtu anayeamini kitu ambacho hawezi kukithibitisha. Kimsingi vitu vyote ambavyo tunakubali vitatokea katika muda ujao ni vitu tunavyoamini bila kuwa na uwezo wa kuvithibitisha. Muda ndio unatusaidia kuthibitisha. Hivyo mimi ninapoamini jua litachomoza kesho naamini kitu ambacho leo siwezi kukithibitisha. Nitaweza kukithibitisha kesho.
Hilo sina tatizo nalo. Hata mimi kuna vitu ambavyo naamini ambavyo siwezi kuvithibitisha kama hilo la jua kuchomoza kesho.
Lakini hilo halina contradiction. Mtu akisema "naamini jua litachomoza kesho" hakuna contradiction yoyote katika imani hiyo. In fact imani hiyo ina msingi mzuri tu katika rekodi ya jua kuchomoza kila siku bila kushindwa kuchomoza hata siku moja katika maisha yake yote huyu mtu.
Ila mtu anaposema "naamini kuna Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote ambaye alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kutokea, lakini hakuumba ulimwengu huo akaumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea" habari hii ina contradiction.
Contradiction ni mambo mawili yanayojipinga.
Kusema "naamini jua litachomoza kesho" hakuna mambo mawili yanayojipinga.
Kusema "naamini kuna Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote aliyekuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani lakini kaumba ulimwengu huu ambao mabaya yanawezekana" kuna contradiction.
Upande mmoja Mungu ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote wa kuumba dunia ambayo mabaya hayawezekani, upande wa pili Mungu huyu anaamua kuumba dunia ambayo mabaya yanawezekana. Kwa nini? Mungu anajipinga mwenyewe huyu.
Kama ana uwezo wote na upendo wote, kwa nini hajaumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
Alitaka kuumba ulimwengu huo lakini akashindwa tu?
Kama alitaka na akashindwa tu, ni kweli ana uwezo wote?
Ama aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani ila hakutaka tu?
Kama aliweza na hakutaka tu, je ni kweli ana upendo wote?
Je ni kweli Mungu huyu yupo au ni hadithi za watu tu?
Unaweza kuthibitisha yupo na kuondoa contradiction hii?