Nimekujibu, tatizo hata ninapokujibu hulitambui jibu.
Mtu akisema hana tatizo na kunywa maji, ana tatizo na kunywa maji machafu kwani yatamletea ugonjwa, mtu huyo kakataa kunywa maji?
Sina tatizo na imani, naona tatizo imani potofu inapohubiriwa kama imani sahihi.
Mtu akisema kwamba katika Euclidean geometry pembetatu ni duara, hapo nitaona tatizo.
That's a contradiction
Mtu akisema kuna Mungu muweza yote, mwenye ujuzi wote na upendo wote ambaye kaumba ulimwengu huu unaoruhusu matetemeko na vimbunga nitaona tatizo hapo.That's a contradiction.
Mtu akisema jua litachomoza kesho ni imani pia, lakini sina tatizo na imani hiyo, hata mimi ninayo pia, ni imani isiyo na contradiction.
Mtu akiniambia kuna teknolojia ya kutuma ujumbe kwenye mtandao wa Jamiiforums halafu ujumbe huo ukamfikia mtu mwingine atakayetembelea Jamiiforums, na kama servers zipo online na ujumbe umekuwa posted atauona, sina hakika kama servers zitakuwa online baada ya mimi kuandika haya, lakini naandika na kuamini zitakuwa online na wewe utasoma.
Ukichunguza utakuta sina tatizo na imani. Mimi mwenyewe kupost messages hapa JF natumia imani.
Nina tatizo na imani potofu isiyo na mantiki ambayo inasemwa kwamba ni imani sahihi.