What is your favorite food?

What is your favorite food?

Mmh, inawezekana kuna wanaokuwa na mchanga. Ila sijakutana nao. Ngoja niombe ruhusa kwa Pa2 siku nikipika dagaa nikualike. Dagaa is delicious asikuambie mtu!

Sawa tu we omba ruhusa I will appreciate it, ila nitakuja na P..... wangu huko. Tulete kinywaji gani ili tushushie hizo miba na michanga?
 
Hiki chakula sidhani kama ipo siku nitakuja kukipenda. Yaani kufanya tunda kuwa chakula, hiyo hapana.

Mkuu ndizi ni zaidi ya tunda. Personally nikila ndizi mbivu au mbichi sioni kama vile nakula tunda. Suala kama ndizi ni tunda tuu au ni zaidi ya tunda limeshafika mpaka mahakamani.

Tafuta na uisome kesi moja mashuhuri sana ya United Brands vs European Commission. United Brands walikuwa ni major suppliers wa ndizi kwenye Umoja wa Ulaya. Walikuwa wana-import ndizi mbichi na mbivu.

Kwenye kesi hiyo, mahakama ilikuwa inaamua, pamoja na mambo mengine, soko la ndizi (relevant product market) in the context of competition law.

United Brands walidai kuwa soko la ndizi limejikita tuu kwenye matunda. European Commission wakadai kuwa ndizi ni zaidi ya tunda na kwamba the relevant product market siyo matunda bali ni ndizi.

Mahakama iliamua kuwa soko la ndizi ni tofauti na soka la matunda. Mahakama ilisema zao la ndizi lina special attributes kama mwonekano, taste, ulaini na kutokuwa na mbegu.

Mahakama iliongeza kuwa zao la ndizi ni muhimu sana kwa watu kama watoto, wazee na wagonjwa. Zaidi ndizi hazizalishiwi kwa msimu kama matunda ambayo yanapanda na kushuka bei kulingana na msimu wao.

Hii kesi inaonyesha tofauti kubwa iliyopo kati ya ndizi na matunda. I am sure hata wataalamu wa afya na lishe (achilia mbali Wahaya na Wachaga) watakuambia kuwa ndizi ni zaidi ya tunda. Usitake kuniambia hii ni miti ya matunda.

DSC05989.JPG
 
Dah mkuu ila kisamvu kura process mpaka utwangwe au kusagwa,ila sijui kikwenu mnapika mazima mazima?

Kutwanga siyo ishu mkuu,nenda pale makumbusho opposite na millenium towers agiza ugali kisamvu usikilizie balaa lake
 
full udenda, post imenikumbusha mblai sana hii, na mimi nitaleta yangu
 
Namsaidia mamsapu kuboresha biashara yake...huku dogo akifuatilia kwa makini...

Watu8 wewe mbaya! Yaani umemuomba Bi Mkubwa akae nyuma wewe upige picha kwenye ofisi yake! Siyo vizuri japo umependeza.
 
Wali mweupe na seafood
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1371107236021.jpg
    uploadfromtaptalk1371107236021.jpg
    96.2 KB · Views: 67
Back
Top Bottom