Preta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 24,320
- 18,875
dadeki........hili zege limetulia.......hapa utie ile pilipili ya bar........
dadeki........hili zege limetulia.......hapa utie ile pilipili ya bar........
Ha ha ha ha, si kweli bana
Mnatuonea tu
wanayakanda baada ya kutoa mikono huku, lazima u-enjoy tu
![]()
Vyakula vingi vyenye asili ya mimea hutokana na TUNDA...
Mathalani,
Vyakula vyote asili ya mkunde kunde (maharage, choroko, kunde n.k)
Vyakula vyote vyenye asili ya nafaka (mahindi, uwele n.k)
Sasa iweje sababu ya kutopenda NDIZI iwe ni kwa kuwa lenyewe ni TUNDA...sidhani kama hiyo ni sababu ya msingi!
CC: Kongosho
Aisee, umenikunaje
Mie niliogopa kusema, hata mie tofauti kabisa na huu msosi, huwa nakula kuonja tu
Ila kama ni kulala siwezi, lazima nitaamka kula
Mkuu ndizi ni zaidi ya tunda. Personally nikila ndizi mbivu au mbichi sioni kama vile nakula tunda. Suala kama ndizi ni tunda tuu au ni zaidi ya tunda limeshafika mpaka mahakamani.
Tafuta na uisome kesi moja mashuhuri sana ya United Brands vs European Commission. United Brands walikuwa ni major suppliers wa ndizi kwenye Umoja wa Ulaya. Walikuwa wana-import ndizi mbichi na mbivu.
Kwenye kesi hiyo, mahakama ilikuwa inaamua, pamoja na mambo mengine, soko la ndizi (relevant product market) in the context of competition law.
United Brands walidai kuwa soko la ndizi limejikita tuu kwenye matunda. European Commission wakadai kuwa ndizi ni zaidi ya tunda na kwamba the relevant product market siyo matunda bali ni ndizi.
Mahakama iliamua kuwa soko la ndizi ni tofauti na soka la matunda. Mahakama ilisema zao la ndizi lina special attributes kama mwonekano, taste, ulaini na kutokuwa na mbegu.
Mahakama iliongeza kuwa zao la ndizi ni muhimu sana kwa watu kama watoto, wazee na wagonjwa. Zaidi ndizi hazizalishiwi kwa msimu kama matunda ambayo yanapanda na kushuka bei kulingana na msimu wao.
Hii kesi inaonyesha tofauti kubwa iliyopo kati ya ndizi na matunda. I am sure hata wataalamu wa afya na lishe (achilia mbali Wahaya na Wachaga) watakuambia kuwa ndizi ni zaidi ya tunda. Usitake kuniambia hii ni miti ya matunda.
![]()
Ndizi ni tunda, hayo yote ni visingizo tu vya kutafuta soko. There's no country in Europe which has ndizi as their staple food, haya makampuni ya usafirishaji yanapeleka ndizi na some tropical fruits there kwa ajili ya foreigners waliopo kule. Yes, katika usafirishaji lazima zipelekwe ndizi mbichi kwa sababu given proper time zitaiva na kuuzika kirahisi kuliko kupelea zilizoiva kabisa. Kaka zangu wanafanya hii kazi ya kuuza matunda nje ya nchi na ndizi ikiwa ni moja ya hayo matunda. Hakuna mjadala hapa, ndizi si chakula ni tunda.
Kama hupendi ndizi as staple food basi usile, na usilete kisingizio kuwa in Europe hawali kama chakula, kwanza ni nchi ngapi huko Europe wanazalisha ndizi?
Nenda Bukoba au Moshi ndio utajua kwa nini watu wameamua kuzipika, kula kama tunda na wengine kutengeneza pombe.... usikaririshwe na wazungu!
Unamaanisha kama hii P?
![]()
Duniani kote ndizi ni tunda linaloliwa pale linapoiva. Kuna baadhi ya makabila wamefanya kuwa chakula cha asili ila hiki kitu ni tunda uwa linaliwa pale linapoiva au kuchoma kula na nyama as a snack NOT mlo big.
hii ni ipi hii......?.....nikilewa naweza kula........?