Kwanza napenda kusema kuwa,wakati najihusisha na masuala ya mahusiano sijawahi kucheat,so sikuwahi kujua sababu ya kufanya hivyo,kiumri nina miaka 3....So that nimeona mengi mpaka mimeamua kuuliza hapa jamvini leo,nimeshashuhudia na watu wakilalamika wengine mpaka wamejiua wengine wapo gerezani wengine maisha yakipata dhroruba(mimi pia nipo kwenye kundi hili thats why sitaki ndoa wala mahusiano ya kimapenzi)wengine wana vilema n.k kwa sababu ya cheating!Hivi wakati unafanya hayo unakuwa unawaza nini?Je ni kisasi,au ni kutokuridhishwa kimapenzi,fedha au ni nini?Nauliza coz malalamiko ya jambo hili na athari zake ni kubwa katika jamii yetu,hebu mnaocheat au mliofanya jambo hili mtuambie sababu japokua mpaka leo sijaona sababu ya msingi ya kufanya jambo hilo,pia mtakua mmewasaidia wale walioko kwenye uhusiano au wanaotaka kuanzisha mahusiano!Maana kama unataka kuondoa tatizo tafuta chanzo cha tatizo!
Loh sasa wewe naona unataka kuturudisha kule kule. But ni kweli kuwa ukitaka kutatua tatizo ni vema kujua chanzo cha tatizo hilo. Najua ninawezakwenda tofauti na wengi but kwa mimi na mtazamo wangu nina haya ya kusema
1. Kwa cheaters ambao wana mahusiano halali i.e. Mume wa mtu na mke wa mtu : Hawa ni tamaa tu na kusema ukwelii wanawakosea sana wenzi wao wa halali!. Kusolve hili ni kujaribu kukidhiana haja za miili, akili na hisia zetu tuwapo na wenzi wetu na pia kuendelea kuomba hofu ya MUNGU itawale.
2. Kwa wale Mke wa Mtu na Serengeti boy - Tamaa na maadili mabovu (ya mama kutaka kutoka nje na mtoto/ mvulana n.e. ) nayo ni aibu na makosa kwa mume wa Mmama. Sina uhakika ila ninaamini pia kuwa kwa kijana wa aina hii anajitwika laana na mikosi tu,
3. Mue wa mtu na binti wa rika dogo lets say mwanafunzi au mfanyakazi but bado ni binti- Ukosefu wa maadili kwa wote mbaba na binti, na kuliondioa ni kuendelea kupreach na kupreach kwa mabinti zetu tuwafungue wajitambue.
4. Mume wa mtu na mdada ambaye ni aged na single/ widow/separated/divorced and the alike............Hapa ninashikwa na kigugumizi kwa sababu kuu moja
- Mwanamke wa aina hii, let say ashafikia 35 and above, alishakata tamaa ya kuolewa (wether aliharibu huko nyuma kwa makusudi au mfumo tu wa maisha ulimfanya akawa hapo alipo mf. masomo kwanza akasahau kuwa vyote vyaenda kwa pamoja, au hajabahatika tu kumpata mkweli wa kumwoa kifupi hana stable relationship. Ina maana at her age, kumpata tena mwanaume (wa age yake and above ambaye yuko single ni ngumu, ambaye amedivorce, ameseparate au ni widower, inakuwa ni ngumu kwa kuwa (ni fikra yangu pia)
- Ni wababa wachache wanaoweza kukaa muda mrefu baada ya either kudivorce, separate au kufiwa na mke bila kuoa mwingine! (So possibility ya mdada huyu kujipatia inakuwa ndogo kulinganisha na wanawake wa aina yao
Sasa ili tutatue tatizo la hawa kucheat na watu wa watu, tunawapa mbinu gani za kukabiliana na 'hali ya ubinadamu'? kama kweli tunasema binadamu hawezikaa muda mrefu pasipo ku-do. Ili asitoke na an occupied man au serengeti boy?
Eh sijui kama nimeeleweka maana na hii Ballantine kichwani!