Imezoeleka sana kusikia kauli
kama "naweza nikacheat halafu bado nampenda mke/mpenzi wangu".Kauli
kama hizi nashindwa kuzielewa kabisa.Either,wanaosema hivyo hawajui
maana ya kupenda ama wanapotosha maana ya upendo ili kutafuta
kuhalalisha wanachofanya.Nijuavyo mimi upendo ni hali ya juu zaidi ya
utambuzi,utu na ufahamu.Nijuavyo mimi,Upendo unapokuwepo kunakua na
viashiria,viashiria hivyo ni UTU,HESHIMA,USAWA,HEKIMA,UFAHAMU n.k.Tukija
kwenye suala la ndoa.Ili ndoa isimame inahitaji vitu
vitatu,Ngono,Mapenzi na Upendo,lakini kati ya vyote hivyo UPENDO ndicho
kilicho kikuu.Kwa tafsiri yangu ya upendo ni vigumu sana ukamfanyia
matendo hasi unaempenda,kwa kuwa utamheshimu na utajiheshimu pia na
zaidi utakua na utu na usawa.Kucheat kwa mfano ni kinyume cha kumheshimu
mkeo/mumeo,lakini ni kinyume cha kujiheshimu kwa kuwa kuwaonesha
wanawake/wanaume mwili wako hovyo ni kujidhalilisha.Kucheat pia ni
kinyume cha utu kwa kuwa kufanya ngono hovyo sio utu ni unyama,yaani
hiyo ni sifa ya wanyama.Kwa maana hiyo ni vigumu na haiwezekani ucheat
halafu uwe unampenda mkeo/mumeo.Ukisema unampenda basi either hujui
maana ya upendo au kama unajua unajaribu kuhalalisha uovu wako.Sasa huu
ni msimamo wangu na mtazamo wangu,lakini haimaanishi niko sahihi,hebu
wewe ulietofauti nami niambie mawazo yako,ni kweli unaweza kuitoa HAKI
ya mwenza wako halafu ukawa UNAMPENDA??