Wezi wamenitenda vibaya, Msaada

Wezi wamenitenda vibaya, Msaada

Mkuu pole sana!siku moja nlisikiliza kipindi cha clouds fm,kuna kibaka alikua anaelezea anasema usiku huwa wanapita kukagua milango kama imefungwa!na wanakutaga mingi ne imesahaulika!tangia siku hiyo nlifuga mbwa!pole kaka tafuta mbwa kiboko ya vibaka

Ni kweli kabisa kwangu mara kama tatu hivi nakuta mlango wa mbele haujafungwa kabisa, hivyo nimeweka alarm kila siku saa 4 lazima nikague milango mimi mwenyewe. KITUO
 
Fundi wajenzi wanatabia ya kugonga funguo kwenye sabuni wanaenda kuchonga kopi rait;
Hela lazima ulale nayo beneti heri ukose tendo la ndoa hela ilale kwenye bukta;
Hata Mimi nimejiuliza hela IPO sitting room wewe upo chumbani halafu umejiamini .


Hela unakua nayo muda wote tena ikiwa ndani hata ulinzi unaongezeka
 
Mkuu fatilia watu wanao kuja kuja nyumbani kwako mara kwa mara - na watu wame washauriwa kwamba vitu expensive msiwe mnaweka/display kwenye sebure viwekeni kwenye family room, kwenye ukumbi weka ki TV cha gharama ndogo na vitu vingine kama hivyo ambavyo si attractive kwa potential thieves.

Sasa suala lako tukija specifically mafundi wano kujengea nyumba au fundi mkuu wao kama ana kawaida ya kuja kuja nyumbani kwako - je, ni watu wangapi walijua siku hiyo ungetoa hela Benki za kuwalipa mafundi?
 
Pole sn mkuu. Naona una hasira. Ndio maisha na mitihani yake.
Mimi tangia jirani yangu aibiwe kwa kuchaniwa dirisha na kuibiwa pochi yenye hela na vitu vya dhahabu. Nikilala naweka hela kwenye drawer la kabati.
 
Habari za Asubuhi wadau,

Juzi jumamosi maeneo ya Tabata Liwiti, majira ya saa kumi alfajiri nimestuka kuona mlango wa chumbani kwangu upo wazi, niaamka fasta, kufika sebuleni nikakuta milango ipo wazi, nikatoka nje fasta nikaona pochi ya honey imetupwa, geti lipo wazi, nikatoka speed nje nikawaona vibaka wanakimbia na pikipiki huku wamekumbatia TV Singsung Inch 42, nikawakimbiza bila mafanikio.

Hawa jamaa waliingiaje ndani? Ndio swali ninalojiuliza mpaka sasa, maana hakuna mlango uliovunjwa wala kitasa cha mlango.

Walichukua TV, wakachukua wallet yenye kilo 6, na kilo 6 ingine ilikuwa mezani (nilikuwa niende site kuwalipa mafundi hivyo nilidroo pesa kiasi bank), simu aina ya Blackberry i10, wakanywa na Heinken 1 kwenye friji na maji ya baridi (manina zao).

Hasira zinanipanda kila nikifikiria walivyomkuta honey kalala naked, bora mm nilikuwa na bukta. Nimejaribu kuwasiliana na jamaa zangu ambao nao wamewahi kupatwa na dhahama kama hii wanasema jamaa wanatumia ushirikina.

Popote mtakaposikia mtu anauza TV, tafadhali mdau wangu, uje inbox fasta unistue...!

Natangaza rasmi, Kuanzia leo popote nitakapokuta mwizi/kibaka anapigwa, lazima nimmalizie.
Heinken yako ya kuzimulia nayo wakanywa duh!
 
Wewe huo mchezo umechezwa ndani ya familia yako
Kwanini wasije siku zote waje siku ambayo unahela.

Sio kila kitu ushirikina,hapo ndio mnapopotezwa akilia.
Hii ni inside jobuuu,umepigwa kwa kuchongeshwa
 
USHAURI WA BURE! MSITHUBUTU KUWEKA MAKUFURI YA KUNING'INIA NDANI USIKU UKIWA UMELALA NI HATARI ZAIDI MOTO UNAPOTOKEA NI NGUMU KUFUNGUA ....TAFTENI MBADALA IKIWEMO KUJIRINDA NA KUWEKA VITASA ORIGINAL ....VIKINEVYO NI HATARI
 
Tabata kwa wizi si jambo la kuuliza wala kushangaa,

Tena hizo TVs ndio wanazipenda kweli yani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom