Wezi wamenitenda vibaya, Msaada

Wezi wamenitenda vibaya, Msaada

Habari za Asubuhi wadau,

Juzi jumamosi maeneo ya Tabata Liwiti, majira ya saa kumi alfajiri nimestuka kuona mlango wa chumbani kwangu upo wazi, niaamka fasta, kufika sebuleni nikakuta milango ipo wazi, nikatoka nje fasta nikaona pochi ya honey imetupwa, geti lipo wazi, nikatoka speed nje nikawaona vibaka wanakimbia na pikipiki huku wamekumbatia TV Singsung Inch 42, nikawakimbiza bila mafanikio.

Hawa jamaa waliingiaje ndani? Ndio swali ninalojiuliza mpaka sasa, maana hakuna mlango uliovunjwa wala kitasa cha mlango.

Walichukua TV, wakachukua wallet yenye kilo 6, na kilo 6 ingine ilikuwa mezani (nilikuwa niende site kuwalipa mafundi hivyo nilidroo pesa kiasi bank), simu aina ya Blackberry i10, wakanywa na Heinken 1 kwenye friji na maji ya baridi (manina zao).

Hasira zinanipanda kila nikifikiria walivyomkuta honey kalala naked, bora mm nilikuwa na bukta. Nimejaribu kuwasiliana na jamaa zangu ambao nao wamewahi kupatwa na dhahama kama hii wanasema jamaa wanatumia ushirikina.

Popote mtakaposikia mtu anauza TV, tafadhali mdau wangu, uje inbox fasta unistue...!

Natangaza rasmi, Kuanzia leo popote nitakapokuta mwizi/kibaka anapigwa, lazima nimmalizie.

Hao ni vibaka wa hapo hapo Tabata tu chunguza pale balakuda au magengeni
 
pole sana mkuu kwa matatzo bt jarbu kufanya utafiti kwa watu na majirani zako wa karbu ujue nani kakuchomeshA maana hao jamaa hawabahatishi wakijA lazma wakuparasite vya kutoshA.
 
Habari za Asubuhi wadau,

Juzi jumamosi maeneo ya Tabata Liwiti, majira ya saa kumi alfajiri nimestuka kuona mlango wa chumbani kwangu upo wazi, niaamka fasta, kufika sebuleni nikakuta milango ipo wazi, nikatoka nje fasta nikaona pochi ya honey imetupwa, geti lipo wazi, nikatoka speed nje nikawaona vibaka wanakimbia na pikipiki huku wamekumbatia TV Singsung Inch 42, nikawakimbiza bila mafanikio.

Hawa jamaa waliingiaje ndani? Ndio swali ninalojiuliza mpaka sasa, maana hakuna mlango uliovunjwa wala kitasa cha mlango.

Walichukua TV, wakachukua wallet yenye kilo 6, na kilo 6 ingine ilikuwa mezani (nilikuwa niende site kuwalipa mafundi hivyo nilidroo pesa kiasi bank), simu aina ya Blackberry i10, wakanywa na Heinken 1 kwenye friji na maji ya baridi (manina zao).

Hasira zinanipanda kila nikifikiria walivyomkuta honey kalala naked, bora mm nilikuwa na bukta. Nimejaribu kuwasiliana na jamaa zangu ambao nao wamewahi kupatwa na dhahama kama hii wanasema jamaa wanatumia ushirikina.

Popote mtakaposikia mtu anauza TV, tafadhali mdau wangu, uje inbox fasta unistue...!

Natangaza rasmi, Kuanzia leo popote nitakapokuta mwizi/kibaka anapigwa, lazima nimmalizie.
Kwa ushaur SHUKA pale barakuda bondeni mtafute jamaa anaitwa Selaa yuko pale uwanjani ongea naye VIZURI atakutajia vijana wezi.. AU pale pale tanesco Kwa nje Kuna jamaa dalali mchunguze kimya kimya yeye Ana jua genge LA waizi WA huo mtindo mitaa Yao ni hapa chini msimbazi. Nshasikia kisanga cha hivo hivo aliibiwa hivo mdada WA kenya nyuma kidogo ya Benki ya crdb.. Ila fanya uchunguz kwanza usiwafuate direct chimbo Lao lingine waizi WA hivyo ni hapo viwanja vya sigara wajinga Sana watoto WA tabata pole Sana
Hao ni vibaka wa hapo hapo Tabata tu chunguza pale balakuda au magengeni
 
Wakati mwingine wezi wanafaidi sana! Kumpembua mtu aliyelala uchi yataka moyo! Waweza sahau kuiba.
 
Huku kwetu mbezi luis ndio mtindo kwa sasa...tarehe 6 na 20 ya mwezi huu walivamia kwa majirani zangu wawili wakaiba tv,ving'amuzi,deck,mitungi ya gesi,mchele,sukari nk...sasa usiku wa kuamkia jana wamekuja kwangu wakavunja mlango wa stoo ila hawakuchukua kitu chochote maana huwa tunahifadhi mkaa na kuni tu..sasa najiuliza nitawadhibiti vp kabla hawajaja kuvunja ndani kwangu kbs???maana najua watarudi na siku hizi wanavunja hata madirisha.
 
Huko nako unaenda kupigwa tena. bora ufanye mengine achana na ushirikina mkuu.
 
Pole sana ndugu yangu kwa tukio la kuhuzunisha.
Kwa sasa tuliza akili wezi huwa hawatoki mbali. Kama hawakufahamu basi wamepata msaada kwa anayekufahamu.
Badala ya kufikiria wezi fikiria watu waliowapa msaada na taarifa wezi juu ya pesa ulizotoa benkiNimeshiriki kwenye upelelezi wa kesi nyingi za wizi hasa za majumbani na zote zinafanana kwenye jambo moja tu; unaibiwa na anayekufahamu au aliyepata taarifa zako kutoka kwa mtu anayekufahamu.
Upo sahihi Kabisa na km na house girl au boy aanze nao... Pole sana Kaka
 
Huku kwetu mbezi luis ndio mtindo kwa sasa...tarehe 6 na 20 ya mwezi huu walivamia kwa majirani zangu wawili wakaiba tv,ving'amuzi,deck,mitungi ya gesi,mchele,sukari nk...sasa usiku wa kuamkia jana wamekuja kwangu wakavunja mlango wa stoo ila hawakuchukua kitu chochote maana huwa tunahifadhi mkaa na kuni tu..sasa najiuliza nitawadhibiti vp kabla hawajaja kuvunja ndani kwangu kbs???maana najua watarudi na siku hizi wanavunja hata madirisha.
Anzisheni sungu-sungu haraka iwezekanavyo
 
Km unafahamu IMEI ya simu yako hiyo, ripoti polish, pia wasiliana na TCRA fasta
 
Bongo DarSlum.

Pole sana Mkuu. Tafuta 'fundi' wa ukweli uwaroge hao washenzi.

-Kaveli-
 
Mkuu naomba kuuliza,milango yako unafunga na ufunguo wa aina gani? Kama ni zile vitasa vya kunyonga,huwa ukifunga unachomoa ufunguo kwa ndani?

Kama jibu ni kwamba huchomoi,basi vile vitasa havikubali kuingiza ufunguo mwingine wakati kuna ufunguo kwa ndani!

Au labda walikupumbaza ukalala bila kufunga mlango!
 
Hivi Wewe sio lucas urasa? maana miandiko na na eneo la tukio ni mulemule.

Anza upelelezi na honey wako..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom