Wezi wamenitenda vibaya, Msaada

Wezi wamenitenda vibaya, Msaada

Wezi wenginr huvizia ile asbh mkifungua mlango kwenda toilet (kwa wenye vyoo vya nje) wao wanaingia wanajificha mvunguni mkirudi wanawachora tu mpk mnaenda kulala wakijua ile saa 9 wao ndio wanaanza shughuli zao. Hatarr sana. Utakuta mlilala nao humo ndani. Pole sana
 
Wezi washenzi sana mie alhamis wamefungua gari wameiba vifaa vya gari vilikua kwa buti na aliekua anajua vilipo ni Fundi tu basi cjui kawacholesha wenzake au kaja mwenyewe tabu tupu
 
blackberry mpaka dec zinakua sio issue...hakuna whatsapp or whatsoever...
 
wezi n watu wapuuz sana alafu vitu wamavyoiba wanaenda kuuza kwa bei ya mchicha
 
inasemekana njia sahihi ya kujifungia ndani.. ni kufunga kwa komeo kwa ndani.... hapo mtu hata aje na funguo malaya gani hawezi kuufungua yeye akiwa nje..
Hasara yake ni pale unapopata ajali ya moto kutokana na tatizo la umeme, walioko nje watakapotaka kutoa msaada itawawia vigumu sana kufungua mlango.
 
pole mkuu...nenda katoe taarifa kituo kilichopo karibu yako.
 
Pole mkuu. Ila nimecheka sana eti wakanywa heinken na maji baridi!!
Hawa wezi noma
 
Sasa hivi ni nani ananunua mali za wizi maana yule anayesadikiwa ndio hivyo tena katobolewa Macho
 
Habari za Asubuhi wadau,

Juzi jumamosi maeneo ya Tabata Liwiti, majira ya saa kumi alfajiri nimestuka kuona mlango wa chumbani kwangu upo wazi, niaamka fasta, kufika sebuleni nikakuta milango ipo wazi, nikatoka nje fasta nikaona pochi ya honey imetupwa, geti lipo wazi, nikatoka speed nje nikawaona vibaka wanakimbia na pikipiki huku wamekumbatia TV Singsung Inch 42, nikawakimbiza bila mafanikio.

Hawa jamaa waliingiaje ndani? Ndio swali ninalojiuliza mpaka sasa, maana hakuna mlango uliovunjwa wala kitasa cha mlango.

Walichukua TV, wakachukua wallet yenye kilo 6, na kilo 6 ingine ilikuwa mezani (nilikuwa niende site kuwalipa mafundi hivyo nilidroo pesa kiasi bank), simu aina ya Blackberry i10, wakanywa na Heinken 1 kwenye friji na maji ya baridi (manina zao).

Hasira zinanipanda kila nikifikiria walivyomkuta honey kalala naked, bora mm nilikuwa na bukta. Nimejaribu kuwasiliana na jamaa zangu ambao nao wamewahi kupatwa na dhahama kama hii wanasema jamaa wanatumia ushirikina.

Popote mtakaposikia mtu anauza TV, tafadhali mdau wangu, uje inbox fasta unistue...!

Natangaza rasmi, Kuanzia leo popote nitakapokuta mwizi/kibaka anapigwa, lazima nimmalizie.
Pole sana mkuu hayo maeneo ndo zao walishamsafisha mshikaji akiwa kalala na mkewe ndani. Walikupilizia dawa kwanza ndo wakaanza ujuzi wao wa kutegua vitasa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom