Western Propaganda Turns Mugabe into a Tyrant


Mpango Wa Kumtoa Mugabe Ni Wa Blair Na Bush...then Nia Yao Nini?
Kuna Anayejua Kuwa Bush Ana Uhusiano Wa Damu Na Familia Ya Kifalme Ya Uingereza?
Kwanini Cia Walimwua Lumumba Na Nkrumah!?
Je..ni Haki Wakimwua Mugabe?
Je..tuwasaidie Kufanya Hivyo?
 
Nia Yangu Ni Kuufanya Mjadala Huu Uwe Fair Na Kuelimishana Badala Ya Propaganda!
 
Na Kama Ni Waafrika Wangekuwa Wameporwa Ardhi Na Kwenda Kulalamika Kwa Malikia Wa Uingereza..then..KICHAKA Agewasaidia?
MALKIA ALITOLEWA ZIMBABWE NA NANI?
JE..BADO ANAIPENDA ARDHI YA ZIMBABWE AMA SASA ANAWAPENDA RAIA WAKE?
NA KAMA ANAWAPENDA WAZIMBABWE...KWANINI ALIWAUA WAKATI WAKIDAI HAKI,USAWA NA UHURU?
NAULIZA TENA...AFRIKA NI HURU?
 

Mkandara,

Hebu kwanza tujadiliane tuone hiki kichwa cha habari tulicho nacho sasa. Western propaganda turns Mugabe into a Tyrant. A Tyrant is by definition any person in a position of authority who exercises power oppressively or despotically.

Who is Mugabe oppressing - is it the western media or the citizens of Zimbabwe.

Who are dying in Zimbabwe - are they the so called westerners or the helpless peoples of Zimbabwe.

Who are being rendered homeless now in their own country - are they the British, Americans etc - or the sons and daughters of Zimbabwe.

Who are going hungry in Zimbabwe - are they some beings from space or the innocent children of mother Africa.

The naked truth is that the people of Zimbabwe are ready for change and Mugabe is standing in their way. People like Mugabe will come and go BUT Zimbabwe will live on....

For some of us who witnessed UDI in Northern Rhodesia and saw the fall of Ian Smith and have some memories of the power struggle for leadership in independent Zimbabwe, Mugabe is turning into a despicable old man who by msemo wa Mwalimu "aogopwe kama ukoma".

Mwenzio akinyolewa na wewe anza kutia maji. Could we in Tanzania be heading the same way? This is a question we should all be asking ourselves.
 
Wazungu Wanaipenda Zimbabwe?
What About Africa?
Wanaipenda Ardhi Ama Watu?
Afrika Ni Tajiri Kuliko Bara Lolote...vipi Kuhusu Watu Wake?
Wana Chakula?
Pa Kulala Je?
Uhuru?
Haki?
Maendeleo?
Elimu?
 
Jokakuu,
Kumbuka maelezo yangu ya awali kwamba Uchumi wa nchi nzima ya Ziimbabwe ulishikwa na wazungu ambao kama sisi wana uchungu pindi mzungu mwenzie anapoonewa. leo hii hatukubali kinachotokea Zimbabwe kwa sababu hawa wananchi ni ndugu zetu na hata kama asingekuwa Mugabe angekuwa mzungu bado lawama zetu zingeendela kusikika kwa sababu hawa ni ndugu zetu..Wazungu ni binadamu na wana feelings hizi kama sisi. Hivyo wanalindana kama tunavyolindana sisi na ikibidi kutuumiza watafanya..
Kuna ukweli kuwa Mugabe ana support kubwa ya vijana ambao ndio wamesoma na wengi wao hawakupitia mapambano ya Uhuru kisha ajira zao zinategemea mzungu aliyewekesha nchini humo. None of these people anahitaji ardhi hiyo isipokuwa ajira yake. na haiwezi kupatikana kama ardhi ya mzungu aliyedhulumiwa haitarudi.
Pili nimesema Mugabe ali overlokk ama hakutegemea kile kilichomkuta kiuchumi, pili ardhi ile yenye rutba ni ya kutengenezwa kuotesha mazao fulani na inahitajika mbolea na baadhi ya mbegu zipate kumea. Hivi vitu vyote vinakuwa imported na kama umefuatilia sasa hivi India ina tatizo kubwa la ukulima wa Mpunga kutokana na ukosefu wa mbolea tu. Wanakadiria mavuno yatakuwa chini almost asilimia 50 ya mategemeo kama wangekuwa na mbolea ya kutosha. hii ni ktk mwaka mmoja tu sasa fikiri nchi ktk miaka 8...
Kumbuka wakati wa Nyerere sisi tulifikia mahala hata dawa ya mswaki tulikuwa hatuna.. acha hizo foleni za sukari na unga.. yet tulikuwa nyuma ya mwalimu kama vichaa vile kwa sababu tuliona kuwa kutaifisha mali za wageni kilikuwa kitendo halali kabisa! bahati nzuri sisi tulikuwa na mahala pa kugeuza jahazi letu bila masharti magumu kama ya Mugabe. Mugabe hawezi kugeuka jiwe na amekusudia...

Mchongoma,
Hii mkuu yote ni sera ambayo haizungumzii kwa kina nani atapewa ardhi hiyo..Na kama lugha yenyewe inasema watapewa wale wenye vibali halali vya kuhodhi ardhi ni wazungu na pia ukitazama wale wenye uwezo wa kulima bila shakla ni Wazungu hivyo anapozungumzia sehemu kuwapa wananchi wenye kutaka kulima hizo sehemu nyingene, wana maana gani ikiwa hawa wazungu wana hati za kumiliki ardhi ile yenye rutuba ambayo asilimia 70 ya ardhi yote ya n Zimbabwe..
Kitu kimoja tu aseme mweusi atapewa sehemu gani kwa sababu hakuna mweusi mwenye hati halali kutokana na ukoloni ulokuwepo toka wakati wa Ian Smith. Mimi nachotaka ni maewlezo ya kuvunja hoja ya ISO kuwa MDC haiwezi kurudisha ardhi zile kwa wazungu isipokuwa watagawana na wananchi ambao kutokana na sheria za zamani walikosa hati za kumiliki ardhi zile. na hatuwezi kutokubali ukweli kwamba Wazimbabwe walikosa ardhi zile kutokana na sheria ya mkoloni pamoja na kwamba nchi ilikuwa yao. Wapi ktk sera za MDC inasema waafrika watapewa ardhi!... kwa sababu swala hili suluhu yake ni kati ya wazungu Makaburu na waafrika weusi.. Taja kiunagaubaga nafasi ya mtu mweusi kwani kisheria mtu mweusi hana kitu hadi sasa hivi.
Na hakuna sheria yoyote ya hati ya ardhi iliyotangulia ama kuja wakati wa mkoloni ama wa Mugabe kabla ya mwaka 2000. je, ni sheria gani MDC watatumia sheria gani ikiwa mnapinga mgao wa Mugabe na hati zao hazitatambulika! - Ati Kuunda kamati! sii uongo mweupe huu!

Mag3,
Mimi nimekwenda deep zaidi ya kichwa cha habari tu. Nimesoma yaliyoandikwa ndani ambayo sii mageni kwetu na wapo kama Mugabe kibao..Nitarudia kusema maneno ya FMES, usafi huanzia nyumbani na sijawasikia wakisema kitu pamoja na kelele zote za wana JF..
 
Nani anayefikiri kuwa Mkololoni aliondoka ZIMBABWE KWA KUPENDA?
JE...SERA ZA MZUNGU KABLA YA KUTOLEWA RHODESIA KWA DAMU ZIMEBADILIKA?
JE..TUMSIKILIZE NANI?
KUNA KITU MUGABE AMEONA?
JE WAZUNGU BADO WANAPENDA ZIMABABWE IWE HURU?



Mkuu Mushi - Huyu mkoloni unayemsema ni yui hasa maana serikali ya kikoloni ya Rhodesia waliendelea kuishi Zimbabwe hata baada ya uhuru, including Iain Smith the then president. Kama waliondoka kwa kupenda au si kupenda is just simple hawakupenda

Swali lako la pili limekaa zaidi kichochezi maana hiyo inayoitwa sera ya Mzungu ni ipi? Unajua most of us Africans bado tunaishi kwenye dunia ya kufikirika eti kwamba kuna club flani ya wazungu (Well Joji kichaka na wenzake) wapo wanapanga mikakati ya kumkandamiza au kmwibia mtu mweusi hii ni dhana potofu na it was like tht miaka hiyo ya 50 na 60. Sera za nchi za magharibi (Sio wazungu kama ulivyosema) ziko more bitter kwa middle east kuliko Africa. Kumbuka Iain Smith wakati ule alikuwa amepigwa full sanctions kwa kujitangazia uhuru wa Zimbabwe chini ya UDI na hivyo alikuwa haripoti Uingereza wala hakuwa controlled na taifa lolote la magharibi. Baada ya uhuru serkali ya Rhodesia was gone and is gone for good. Hkukuwa na sera ya mzungu wala ya Rhodesia.

Swala la kwamba tumsikilize nani???? Hii siyo mchezo wa kuigiza it is happening, real and people are in for it unachotakiwa kufanya ni kujifunza kutofautisha facts na opinions and then judge from there.

Mugabe hajaona chochote, in a perspective ya swali lako. Mugabe kama unaijua vizuei historia ya Zim alikuwa ni strong ally wa UK and US. nI mpaka pale hali yake ya kisiasa ilpotishwa na Morgan Tsvagirai in 1999 ndipo alipobadilika na kuifikisha nchi hapa ilipo. Tsvangirai si wa kwanza alikuwepo Ndabaningi Sthole, Abel Muzorewa, Edgar Tekere lakini Morgan na MDC yake ndio hasa imekuwa strong. Hayo maswala ya empowerment 100% yalishindikana vp in the 80's na 90's???

Wazungu unaosema wanapenda Zimbabwe iwe huru ni wa wapi, wazimbabwe au waingereza na ni uhuru upi huo???? Kumbuka kuwa Zimbabwe ni huru na ni uhuru huo umewezesha hata hao mainvestor kuiamini nchi na kuwekeza. It is far much better mfano kuwekeza South Afrika sasa kuliko enzi zile za apartheid. Kwa hiyo moja kwa moja suala la wazungu kupenda Zimbabwe kuwa huru liko wazi na if u think otherwise U are free to do so.

Mkuu jmushi bahati mbaya sina muda lakini otherwise tungeongea mengi kuhusu Zim maana I have lived there and I do spend about 40 days per year there. Mugabe is a TYRANT and will be remembered that way thru history.
 
Wakuu kama mkinipa majibu..THEN NA MIMI NITAJIANDIKISHA KWENDA KUMTOA MUGABE MADARAKANI KWA KUMSAIDIA MKOLONI AMBAYE NI MUGABE HUYO HUYO ALIMWONDOA!
KUNA ANAYEJUA WHATS NEO COLONIALISM?
 

Mkutano wa BERLIN 1885-1888 ULIKUWA WA NINI?
MIPAKA YA AFRIKA NANI ALIWEKA?
KWANINI?
MAPIGANO YA WENYEWE KWA WENYEWE YA AFRIKA NANI ANA YA FACILITATE?
WHO SHAPED AFRICA?
 
SADDAM HUSSEIN ALIYEFANYA Mauwaji ya KIMBARI...NANI ALIMTUMA?
NANI ALIMPA silaha?
nani kamtuma TSIVANGIRAI?
 
Mwalimu aliwaamisha kwanguvu wanakijiji chini ya sera za UJAMAA...WENGINE WALIUWAWA...JE..WHAS HE A TYRANT?
 
walimu wangu mara zote wamekuwa wakichukia majibu yangu mafupi......! lakini mimi mwenyewe nina imani katika majbu yangu (direct to the point & no porojo) sasa kuhusu maswali ambayo Comrade Mushi1 ameuliza majibu yake ni rahisi sana.....!
THOSE COLOURLESS (whites) HAVE NOTHING GOOD ABOUT AFRICA......!
MUGABE ALICHOFANYA NI KU-BRING INTO ZERO MAAMUZI YA MKUTANO WA BERLIN 1884/5....( area for.... area for..... area for..... etc).
THE TRUE SON OF AFRICA amechukua kilichokuwa chao (toka kwa magabacholi) na kuwapa watu wake.....! hilo nalo kosa.......!? MBONA WAO WALIGAWANA AFRICA NASI TULIKUWA KIMYA KAMA MANG'OMBE YANAYOPELEKWA MNADANI.....!
LEO HII MUGABE AME-ACT ACCORDINGLY tunalaumu na kumgeuka kama ilivyokuwa kwenye kita bu kimoja cha fasihi okwonkwo alipomuua mtumishi wa wazungu wenzake wakamgeuka.....! let this not happen to MUGABE
 
Nyambala,
Mkuu amini unachoamini wewe lakini mimi nawafahamu wazungu..naishi nao na nimekaa mkao wa kunyolewa longtime.. wao ndio vinyozi huwezi kudai utajinyoa mwenyewe, haya ndio ya Mugabe! NATO, G8, UN, IMF, Bank ya dunia na kadhalika ni vyombo vyao na vinatawala dunia..

Ian Smith alipigwa vita baada ya kujitangazia Uhuru dhidi ya serikali ya Malkia.. haikuwa kwa sababu ya mtu mweusi...
 

Maths anaonekana ni MJESHI?
NANI MTAMPELEKA ZIMBABWE AKAFE KWASABABU YA KICHAKA?
 
Maths anaonekana ni MJESHI?
NANI MTAMPELEKA ZIMBABWE AKAFE KWASABABU YA KICHAKA?
i am a SCOUT.......! boy scout trained by late Maneno Marite & late Lwago....... I am a scout who went 'that' BAHATI CAMP at which it was of lucky to reach live & get out safely.....!
It is SCOUT that taught me the spirit of PATRIOTISM.....!
it is SCOUT that shaped me at giving priorities.... 1.GOD 2. TAIFA LANGU 3. PEOPLE

TUPELEKE WATOTO WETU SCOUT WAKAWE SHAPED....!
 

Mahesabu...You are the TRUE son OF AFRIKA...Pia...Ni wazi wewe ni MTU WA MUNGU!
HUO UTATU WAKO WA GOD,TAIFA LAKO,NA THE PEOPLE...NI UTATU WA UTAKATIFU WA HAKI,USAWA NA UHURU
 

Inaelekea kuwa Zimbabwe wana tatizo la Uongozi.

Kuna rafiki yangu mmoja anaitwa Professor Mutambara, tulishirikiana naye sana mwishoni mwa miaka ya tisini katika mambo mbalimbali ya kitaaluma. Jamaa huyu naye nilimuona bomu sana lakini baadaye nikasikia kuwa na yeye ni kiongozi mmojawapo wa chama cha upinzani huko Zimbabwe. Ingawa alikuwa kifaru sana shuleni kiasi kuwa alipata Masters na Ph.D pale Oxford kwa muda wa miaka mitatu na nusu tu, people skills zake zilikuwa sifuri kabisa kiasi kuwa kwa maoni yangu nilimuona hafai kuongoza hata kikundi cha watu wanne tu. Kila wakati anataka watu wajue kuwa yeye ni msomi sana, hata kama yuko katika kundi la wasomi wenzie.

Dr. Simba Makoni naye ana matatizo yake mengi sana ya kiongozi ingawa naye ameenda shule nzito sana ya Chemistry. Huyu Makoni amehusika sana na kuanguka kwa uchumi wa Zimbabwe wakati akiwa Waziri wa Fedha. Kuna mwingine Professor Jonathan Moyo naye ameenda shule nzito sana lakini alipopewa uwaziri wa habari na Mzee Mugabe, jamaa akawa dikteta mkubwa sana kwa kufungia magazeti na vyombo vingine vya habari.

The list goes on.
 

...Mkuu Mkandara, kwa uelewa wangu 'mdogo' naamini MDC watajiingiza mtegoni kusema waafrika, wazungu, wahindi etc watagawiwa vipi ardhi, ...itakuwa ni sawa wamejiingiza kwenye mtego wa Discrimination na Rascism. Bado nataka kuamini MDC inazungumzia haki za wazimbabwe wote bila kujali dini, rangi , itikadi, ukabila nk...



...Hata kama MDC nyuma ya pazia hoja yao ni kutaifisha hayo mashamba, lakini kwenye karatasi ya sera zao angalau wametamka ardhi ni haki kwa wazimbabwe wote bila kujali 'ubaguzi', or am missing something?
 
Kama MUGABE NI DIKTETA..WHAT ABOUT MWALIMU?
TALKING ABOUT UHURU WA HABARI?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…