Wenye nyumba kuweni waelewa

Wenye nyumba kuweni waelewa

habari zenu,

wenye nyumba zenu mliopangisha na mpo humu, hebu kuweni waelewa muda mwingine jamani..

mtu anakulipa kodi siku zote on time bila maneno wala kelele, amekwama mwezi mmoja anaomba umvumlie hutaki kuelewa khaa.

hakuna mtu anapenda kudaiwa kila mpangaji anajua wajibu wake wa kulipa kodi ila kuna muda mipango sio matumizi muwe mnaelewa..

maisha hayapo hivyo jamani kuna kupata kuna kukosa mtu akikwama muwe mnawaskiliza..

wapangaji nao ni watu wanapaswa kusilizwa sio kuwanyanyasa…

msinichambe..
Wenye nyumba tu waelewa sana,tatizo ni kwamba baadhi yetu hadi tujenge tunakopa bank,Vicoba,kausha damu hadi tepesha shavu ndo nyumba ikamilike.Marejesho yanatakiwa kwa wakati na wao hawapokei maneno eti nimekwama.Wapangaji kuweni waelewa jamani.
 
Usiombe kupanga nyumba za wamama wa mjini wanaotegemea kodi kutatua matatizo yao utajuta,atakusumbua huyo kila akiwa na shida,na hapo kodi ushampa kamalizia kwenye starehe huko
 
Utahamishwa tu. Kuna kikundi hicho mbagala huko kazi yake kushughulika na wapangaji wakakorofi tu. Hao wanafatana na wewe kila unapokwenda bila wewe kuelewa, ukitowa pesa tu wanakukaba wanachukuwa kwa nguvu wanakwambia, ahsante, hii kodi unayodaiwa. Sasa nenda kashitaki kuwa umeshalipa kodi. Na risiti wanakupa.

Hao hata panya rodi wana afadhali.

Labda haupo Dar wewe.
Duh mbna hatari hao

Kama hawata nidhuruu Basi wachukue tu
 
Katika Kosa Nililowahi Kufanya Ni Kuzoeana na Wapangaji Kupitiliza Mwisho Mnakuwa kama Ndugu Hapo Kaa Ukijua Kodi Utapewa kwa Danadana Sana Tho Kuna Wengine Wapo Poa Sana
 
habari zenu,

wenye nyumba zenu mliopangisha na mpo humu, hebu kuweni waelewa muda mwingine jamani..

mtu anakulipa kodi siku zote on time bila maneno wala kelele, amekwama mwezi mmoja anaomba umvumlie hutaki kuelewa khaa.

hakuna mtu anapenda kudaiwa kila mpangaji anajua wajibu wake wa kulipa kodi ila kuna muda mipango sio matumizi muwe mnaelewa..

maisha hayapo hivyo jamani kuna kupata kuna kukosa mtu akikwama muwe mnawaskiliza..

wapangaji nao ni watu wanapaswa kusilizwa sio kuwanyanyasa…

msinichambe..
Wenye nyumba wote wa jf wamekusikia. Tatizo ni kwamba inawezekana mwenyenyumba wako hayumo humu. Delivery Report: Unsuccessful/not sent
 
"'ulivyokuwa Unapanda juu ya meza kidimbwi na kitambaa cheupe Ile Xmas nlikuwa nakuchora tu,na Kwa taarifa yako ww ndie unachelewesha ada za watoto na unajua shule jumatatu,jipange" Mimi mwenye nyumba wako.

heeeeee
 
Unakuta mwenye nyumba hana kazi nyingine amestafu labda, nyumba ndio kila kitu kwake. Kumchelewesha kulipa kunamfanya muda mwingine alale na njaa maana matumaini yote alishaweka kwako na hukumpa taarifa mapema kwamba mambo hayapo vizuri. Au ukute na yeye alikopa huko akawaambia nachukua kodi tarehe fulani.

Binafsi nimepanga na nimepangisha, naelewa adha ya pande zote yaani mpangaji na mpangishaji.

shida hazitoi taarifa

ila mi taarifa nilimpa mapema
 
Back
Top Bottom