Wenye elimu ya dini nisaidieni: Ni ipi hekima iliyojificha katika mateso makali wayapatayo wanyama?

WhoWeBe

JF-Expert Member
Dec 18, 2022
2,301
4,243
Habarini!

Wenye ujuzi tupeane maarifa kidogo tafadhali.

Msingi wa swali langu unaegemea zaidi maisha ya wanyama hawa wala nyasi. Naona maisha yao yamejaa tabu na mateso na wasiwasi mtupu.

Wakikoswa kupigwa meno ya shingo na kunyonywa damu na simba au chui basi huishia kuliwa kwa kumegwa vipandevipande huku wakiwa hai na kujiona na mbwa mwitu, fisi n.k. Maumivu makali kiasi gani! Akili au uwezo wa maana wa kujitetea hata hawajapewa, unaona kabisa kuna sehemu kuna ambalo wangeweza kufanya kujiokoa na kukomesha uonevu lakini wapi. Mwenzao anachunwa ngozi hapa na fisi akiwa hai wao wapo pembeni wanaangalia tu. Angalau kidogo nyati wanajitahidi kupambana lakini bado sana, wazito na tegemeo lipo kwenye pembe tu ambazo simba na chui huwa wanazikwepa kiurahisi tu.

Unakuta mama twiga mtoto wake ameshambuliwa na chui au simba anajitahidi kumtetea lakini pekee anachoweza kufanya ni kumlambalamba tu huku akishindwa hata kumnyanyua (kutokana na kukosa maarifa) aondoke nae na kumshuhudia akifa kwa uchungu. Mateso ya kiasi gani ya kisaikolojia. Kuna wakati nashindwa kabisa kuangalia documentaries za wanyama.

Yapo mengi yanayowakuta, hapo sijazungumzia mateso kutoka kwa binadamu. Kule China samaki anakaangwa upande mmoja taratiibu bila kumuua na kuanza kumla upande huo huku akiwa hai, baadae (akiwa ameshateseka sana, bila shaka) ndo anakaangwa na upande mwingine na kufa kabisa. Jambo hili hufanyika kwa furaha kuu!

Hapa kwetu, kule umasaini kwa mfano, ng'ombe anaweza kuchomwa sijui kukatwa mshipa fulani na damu kutoka kwa wingi. Damu hiyo hukingwa na kunywewa. Maumivu anayapatayo ng'ombe huyu bila shaka unaweza kuyahisi. Sijazungumzia uchinjaji wa nguruwe ambapo anapigwa magongo ya kichwa kwanza na ule wa kisasa. Hatari tupu, wanyama wanaterezeshwa kwenye sakafu lainiii na kujichinja wenyewe katika kifaa kimoja kikali sana kilichowekwa hapo.

Ndege wanafungiwa kwenye matundu, hawana uhuru wa kujichanganya maisha yao yoote huku wengine wakifungiwa mazizini.

Swali langu, ni nini hekima ya Muumba iliyopo nyuma ya haya?

Swali la nyongeza; kuna hekima gani juu ya mfanano wa damu ya binadamu, wanyama na ndege? Mdada angalia anavyomkimbia mtu aliyejeruhiwa kidogo kwenye gari (hata kama ni kidole tu) kwa kuogopa damu, lakini ajabu mwangalie anavyokimbilia kumchaangachaanga ng'ombe au mbuzi mwenye damu yenye mfanano tu na ya binadamu.
 
Ndio maana jinsia ya ke inadai haki Sawa , haiwezekani ageuzwe geuzwe kama kitafunwa

Popo kanyea mbingu
Mende aliyekufa
Mbuzi kagoma kwenda
Mbwa mbishi
Fisi maji mjeuri
Kamburumundu
Sitaki nataka
Twende kibishi n.k

Ifike mda sasa wanyama nao wadai haki zao- asikari wa wanyama Pori mnaona kabsa Simba-Bob junior anapigwa mpaka anauliwa nyie mnawaachia tu watalii wachukue tu video na kutowafukuza simba wengine wasi tuondolee kivutio pedwa duniani.
 
Msingi wa swali lako una assume kwamba kuna muumba aliyepanga na kuumba

Msingi huu ni potofu. Hakuna muumba huyo.

Ukiondoa uwepo wa muumba huyo, mabaya haya yote yanayowakuta wanyama hayataleta contradiction yoyote.

Contradiction inakuja ukikubali muumba huyo yupo.

Hili suala linaonesha muumba huyo hayupo.
 
Ndo maana mungu ameumba moto na pepo kwa ajili binaadamu, na tutaulizwa akili, hekima na utashi tuliopewa tumeutumiaje kutawala dunia na vilivyomo.

So, hustle ili uwe mtawala, na utakapo wasulubu hao wanyama uwasukubu kwa utaratibu ili ukiulizwa useme, ulikuwa mtu mwema mpaka wanyama uliwatendea wema
 
Ni watu wachache wanakuwa na fikra za kujali wanyama ni hasa wale walioendelea au kustarabika. Nilipokuwa mdogo kiumri chini ya miaka 25 nilikuwa sioni shida sana kuangalia nguruwe, ng’ombe na mbuzi wakichinjwa wengine kwa kukata shingo na wengine kwa kupigwa shoka kichwani. Leo ufahamu wangu hunisuta kushuhudia hayo.

Niseme tu kuwa wanyama hao wanateseka lakini hata hivyo Mungu Muumba kawaondolea ufahamu mkubwa na wa ndani wa mambo na hisia zao si kali na za kudumu kama za binadamu. Ukweli ni kwamba binadamu ndio kiumbe mwenye kuteseka zaidi ya viumbe wengine wote. Binadamu huteseka kisaikolojia/kihisia na pia kimwili kwani mwili wake ni sensitive zaidi.

Kumbuka pia mateso ya wanyama hao ni ya muda mfupi tu, mara nyingi sio zaidi ya robo saa. Fikra za mwanadamu zinakuza mambo lakini Aliyeumba yote anajua kuwa ni ya kuvumilika na ya mpito tu.

Damu inahusishwa na uhai na kweli ni kitu cha thamani sana, kiimani, kibiologia na kihisia. Wekundu wake hutokana na chembe chembe ziitwazo haemoglobin ambazo kazi yake ni kufyonza oxygen na kuipeleka sehemu husika za mwili.

Mwanadamu ana uwezo wa kuchagua kuona ulimwengu jinsi apendavyo. Akili yake huhalalisha mambo kulingana na mahitaji yake. Wapo wanadamu wanakula wanadamu wenzao kama kuku na hawaoni shida. Sitaki sana kusema yanayotokea katika ulimwengu wa giza, ni makubwa! Ila kuwa na amani, yote yanapita na kusahaulika.
 
Tuiache nature ifanye kazi yake kubalance maisha ya viumbe hai na vinavyowazunguka...sometime nature is very brutal....
 
Cha ajabu wanoliwa Mungu aliwapa uwezo wa kujizalisha zaidi mfano swala ni wengi zaidi mbugani ila simba ni wachache, nafikir Kila kiumbe kinapitia mauti na mauti ni mauti hata hao wanowararua wengine nao huraruliwa na wengine au wenzao.

Viombu tunakulana ili tuendelee kuwa hai yaani uhai ndio unalisha uhai, kama tukila mawe hakika viombe wote tutapotea.
 
Mfano Simba kumrarua swala na kumla, ni utaratibu wa Muumba wa kumpatia Simba chakula chake. Simba hana kosa, anatafuta chakula alichoandaliwa na Muumba.
Mungu si ana huruma iliyotukuka?

Sasa anaruhusu vipi kiumbe alichokiumba kwa upendo mkubwa kiraruliwe?

Au hana huruma?
 
Habarini!

Wenye ujuzi tupeane maarifa kidogo tafadhali.

Msingi wa swali langu unaegemea zaidi maisha ya wanyama hawa wala nyasi. Naona maisha yao yamejaa tabu na mateso na wasiwasi mtupu.

Wakikoswa kupigwa meno ya shingo na kunyonywa damu na simba au chui basi huishia kuliwa kwa kumegwa vipandevipande huku wakiwa hai na kujiona na mbwa mwitu, fisi n.k. Maumivu makali kiasi gani! Akili au uwezo wa maana wa kujitetea hata hawajapewa, unaona kabisa kuna sehemu kuna ambalo wangeweza kufanya kujiokoa na kukomesha uonevu lakini wapi. Mwenzao anachunwa ngozi hapa na fisi akiwa hai wao wapo pembeni wanaangalia tu. Angalau kidogo nyati wanajitahidi kupambana lakini bado sana, wazito na tegemeo lipo kwenye pembe tu ambazo simba na chui huwa wanazikwepa kiurahisi tu.

Unakuta mama twiga mtoto wake ameshambuliwa na chui au simba anajitahidi kumtetea lakini pekee anachoweza kufanya ni kumlambalamba tu huku akishindwa hata kumnyanyua (kutokana na kukosa maarifa) aondoke nae na kumshuhudia akifa kwa uchungu. Mateso ya kiasi gani ya kisaikolojia. Kuna wakati nashindwa kabisa kuangalia documentaries za wanyama.

Yapo mengi yanayowakuta, hapo sijazungumzia mateso kutoka kwa binadamu. Kule China samaki anakaangwa upande mmoja taratiibu bila kumuua na kuanza kumla upande huo huku akiwa hai, baadae (akiwa ameshateseka sana, bila shaka) ndo anakaangwa na upande mwingine na kufa kabisa. Jambo hili hufanyika kwa furaha kuu!

Hapa kwetu, kule umasaini kwa mfano, ng'ombe anaweza kuchomwa sijui kukatwa mshipa fulani na damu kutoka kwa wingi. Damu hiyo hukingwa na kunywewa. Maumivu anayapatayo ng'ombe huyu bila shaka unaweza kuyahisi. Sijazungumzia uchinjaji wa nguruwe ambapo anapigwa magongo ya kichwa kwanza na ule wa kisasa. Hatari tupu, wanyama wanaterezeshwa kwenye sakafu lainiii na kujichinja wenyewe katika kifaa kimoja kikali sana kilichowekwa hapo.

Ndege wanafungiwa kwenye matundu, hawana uhuru wa kujichanganya maisha yao yoote huku wengine wakifungiwa mazizini.

Swali langu, ni nini hekima ya Muumba iliyopo nyuma ya haya?

Swali la nyongeza; kuna hekima gani juu ya mfanano wa damu ya binadamu, wanyama na ndege? Mdada angalia anavyomkimbia mtu aliyejeruhiwa kidogo kwenye gari (hata kama ni kidole tu) kwa kuogopa damu, lakini ajabu mwangalie anavyokimbilia kumchaangachaanga ng'ombe au mbuzi mwenye damu yenye mfanano tu na ya binadamu.
Umeuliza maswali mazuri sana na hawa wachangiaji wamejiongelesha tu hawajatoa majibu....mi mwenyewe sina jibu.

Siku moja mida kama saa5 usiku nipo zangu home kwa nje nachati, (sisi ni wafugaji) nikasikia sauti ya kondoo akilia kwa uchungu. Kwenda kuangalia nikakuta anazaa, nilijisikia vibaya sana kwa sauti ile ya uchungu...nikajiwazia, kwa nini Mungu kaweka uchungu wa kuzaa hadi kwa wanyama wakati tunasoma maandiko yake aliwapa uchungu huo wanadamu kwa kutokumtii, iweje adhabu hiyo iende hadi kwa viumbe ambavyo havikufanya kosa!
 
Just live your life ili upate furaha
Na ukitaka kufa kwa stress na majonzi ishi maisha ya viumbe wengine.
 
Ni watu wachache wanakuwa na fikra za kujali wanyama ni hasa wale walioendelea au kustarabika. Nilipokuwa mdogo kiumri chini ya miaka 25 nilikuwa sioni shida sana kuangalia nguruwe, ng’ombe na mbuzi wakichinjwa wengine kwa kukata shingo na wengine kwa kupigwa shoka kichwani. Leo ufahamu wangu hunisuta kushuhudia hayo.

Niseme tu kuwa wanyama hao wanateseka lakini hata hivyo Mungu Muumba kawaondolea ufahamu mkubwa na wa ndani wa mambo na hisia zao si kali na za kudumu kama za binadamu. Ukweli ni kwamba binadamu ndio kiumbe mwenye kuteseka zaidi ya viumbe wengine wote. Binadamu huteseka kisaikolojia/kihisia na pia kimwili kwani mwili wake ni sensitive zaidi.

Kumbuka pia mateso ya wanyama hao ni ya muda mfupi tu, mara nyingi sio zaidi ya robo saa. Fikra za mwanadamu zinakuza mambo lakini Aliyeumba yote anajua kuwa ni ya kuvumilika na ya mpito tu.

Damu inahusishwa na uhai na kweli ni kitu cha thamani sana, kiimani, kibiologia na kihisia. Wekundu wake hutokana na chembe chembe ziitwazo haemoglobin ambazo kazi yake ni kufyonza oxygen na kuipeleka sehemu husika za mwili.

Mwanadamu ana uwezo wa kuchagua kuona ulimwengu jinsi apendavyo. Akili yake huhalalisha mambo kulingana na mahitaji yake. Wapo wanadamu wanakula wanadamu wenzao kama kuku na hawaoni shida. Sitaki sana kusema yanayotokea katika ulimwengu wa giza, ni makubwa! Ila kuwa na amani, yote yanapita na kusahaulika.
Nahisi Nina mengi sana ya kujifunza kutoka kwako. Hekima hii ni kutoka kitabuni au ni kichwani TU ??.
 
Iyo ni nature ilivyo na hakiwezi badilika kitu
Hata sisi binadamu tuna tawalana mwenye nguvu anamtawala asiye na nguvu
 
Back
Top Bottom