Kila kitu kina roho na kina uungu ndani yake

2 of Amerikaz most wanted

JF-Expert Member
Jan 13, 2023
1,328
3,692
Huko nyuma nilishaelezea nadharia kuhusu Mungu kwamba Neno hilo ni kiiwakilishi cha NGUVU KUU iliyopo kila mahali (Omnipresent) kwa wakati mmoja (Omnipotent) na ya kwamba kila kinachoonekana na kisichoonekana vyote vimebeba NGUVU KUU kwa levels tofauti tofauti.

NGUVU KUU (THE SUPER CONSCIOUS ENERGY) ni nishati ambayo kila kitu kimetokana nayo.

Nyote mnafahamu kuwa "energy can neither be created nor destroyed, but can be transformed into another form"

Ndio maana watu wa dini wanaiita SUPER CONSCIOUS ENERGY, Mungu; kwa sababu ya kutokuwa na mwanzo wala mwisho na kuwa ndani ya kila kitu na kuwepo kila mahali.

Yenyewe inachofanya ni kujibadili badili katika maumbo na hali tofauti tofauti.

Kwa Kanuni ya polarity, energy ina direction mbili za transformation (mabadiliko)
✍🏻Mabadiliko yaliyosababisha consciousness na
✍🏻 Mabadiliko yaliyosababisha matter.

Matter ni maada (kitu chochote chenye uzito na kinachochukua nafasi, hiyo ni Physics form one)

Consciousness tunaweza ita ile hali ya asili ya kitu; yaani kitu kimejikuta kipo hivyo kilivyo na hakijui kwa nini kipo hivyo!

Kwa lugha nyepesi tuseme consciousness ni ufahamu, may be; hivyo maada na ufahamu vyote ni energy, si ndio?

Vyote ni product of energy katika law of polarity; upande huu kuna matter na ule kuna consciousness; vyote viwili vinategemeana na vyote vina- react!

🗣️Sasa basi Kuna Kingdom 4 za asili au tuseme za uumbaji:

1. Mineral Kingdom

2. Plant Kingdom

3. Animal Kingdom

4. Human Kingdom

👉Consciousness inapoingia kwenye minerals, kwenye 'mawe' inachofanya ni kuifanya ardhi na vyote vilivyomo (minerals nk) kuwa na hali fulani ya ufahamu, wenyewe mnaita 'roho' ni sawa Kwa sababu roho pia ni energy Katika sayansi Yani Roho ktk dini... Hivyo tunakubaliana sasa kwamba energy in the form of consciousness ikiwa ndani ya jiwe/ mineral/ udongo, inaachilia uhai ndani yake; ni jiwe lakini ni 'Living Stone' ambalo lina uhai/ roho ndani yake.

Hii level ya uhai tunasema ni kwenye dimensions za chini kabisa, kwa sababu jiwe halina brain/ubongo kuweza kuchanganua mambo, lakini ndani yake kuna uhai (cosmic sub consciousness)

👉Baada ya hapo ule ufahamu(consciousness) unaingia kwenye hatua ya pili ya Plant Kingdom na kuji-store(kujiweka) mle, ndio maana tunasema mimea na miti ya kila aina inasikia na kuelewa kila kitu ingawa haiwezi kusema kwa sauti kama wanyama na watu lakini ina roho ndani yake (collective sub consciousness)
Yaani ufahamu wa mimea ni zaidi ya ufahamu wa mawe; mimea ina ufahau flani/ some intelligence kuliko mawe!

👉Baada ya muda fulani ile consciousness inapoendelea ku- develop inaingia kwenye level ya 3, kwenye animal Kingdom. Wanyama wa aina mbalimbali wana roho au ufahamu mkubwa kuliko mimea na mawe... Huu ufahamu unaitwa Sub conscious... Yaani unaweza kuongea na wanyama kwa ishara wakakuelewa kwa urahisi zaidi kuliko miti na mawe. Hao wanyama pamoja na kuwa kwenye sub consciousness level, bado wanatofautiana ufahamu kwenye hiyo level.

👉Energy ikitoka hapo inakwenda kwenye level of consciousness ambayo ni kwa human Kingdom!, Hapa ndipo unakutana na watu ulimwenguni mfano binadamu hapa duniani

Hiyo ni energy evolution, from lowest level to the highest!

Binadamu ndiye kiumbe pekee chenye uwezo wa ku-access sub consciousness na super consciousness chenyewe kikiwa kwenye consciousness level.

Binadamu anaweza kuchukua nguvu (energies/ power/ upako) kutoka kwenye first level of consciousness mpaka kwenye highest level of consciousness!

Maana yake ni mtu peke yake kati ya kingdoms zote NNE ndiye mwenye ubongo unaoweza ku- access hizo energies zote.

Mtu anaweza kuamua kitu chochote kiwe Mungu kwake na kikawa... Akiamua jiwe liwe Mungu wake na lifanye Miujiza inakuwa. Akiamua mti fulani awe Mungu wake au akaamua Ng'ombe, Mbuzi, Chui, Nyoka, Samaki nk awe Mungu wake inakuwa Kwa sababu ya mfumo wake WA UFAHAMU ni mkubwa kupitia ubongo ambao una NGUVU/ energies za kutosha za Asili ya uumbaji iliyosababisha kila kitu kuwepo.

Mtu akiamua Mungu wa Israeli, Yesu au Maria awe Mungu wake inakuwa. Akiamua Allah awe Mungu wake au Muhammad awe mtume wake inakuwa; brain au moyo ukiamua chochote kiwe na nguvu inakuwa!

Ndio maana kwenye dini zote na imani zote duniani kila moja hudai ndiyo sahihi na iliyo bora zaidi kuliko zingine. Ndiyo tabia ya dini kwa sababu mtu anaona kila akiomba kwa Jina la Mungu wake anapata majibu!
Kwa watu waliokwishavuka levels za mambo ya dini kwao kila kitu ni sawa tu maana hakuna binadamu aliye bora zaidi ya mwingine mbele za NGUVU KUU!

Nafikiri mmekiona, kwamba kuna energy na kuna matter Yani Kuna energy(Roho) na mada/matter(vitu vya kimwili upo hapo?)

Energy/roho inapenya kwenye matter na kuifanya iwe kiumbe hai (dormant au active living being) hivyo Roho/nishati/energy ikitoka kinakufa Au tuseme roho ya Mungu imo ndani ya kila kitu!!! Nataka tuelewe kipengele hicho kabla hatujaendelea.

Ni binadamu pekee mwenye uwezo wa kufanya mabadiliko yoyote duniani kwa sababu ya Consciousness level of energy aliyo nayo. Mawe (minerals), miti (plants) na wanyama (animals) ni falme ambazo licha ya kwamba zina consciousness, lakini natives wake hawawezi kufanya mabadiliko yoyote kwa sababu hawana brain na hata wanyama wenye brain, bado brain yao haiwezi kuwaruhusu kuwaza, kutafakari na kupambanua mambo. Ni binadamu peke yake kutoka human kingdom mwenye complex brain anayeweza ku- access energies from cosmic sub consciousness level hadi cosmic super consciousness level.

Levels of energy kutoka ya 1 hadi ya 4 zinafikiwa naturally /kiasili by evolution of consciousness; lakini levels ya 5 hadi ya 7 zinafikiwa kupitia meditation/tahamuli/tarajudi

Ni high, higher na highest spiritual levels of energy.

Level ya 5 inaitwa Super Consciousness level, ya 6 inaitwa Collective Super Consciousness na ya 7 ni Super Cosmic consciousness!

Super Cosmic consciousness level ni level ya juu kabisa ambayo mtu yeyote anayeifikia huitwa Mungu! Ni level ambayo mtu huonekana wa ajabu
Mungu ni nadharia kwamba kuna kiumbe kwenye anga za mbali sana (juu mbinguni) ambacho kinaratibu maisha ya binadamu, ulimwengu wote na viumbe vyote vilivyomo; ndio maana Paulo mtume, kama Mwanafalsafa mashuhuri wa kale anaandika kwenye nyaraka zake kuwa "kuna miungu wengi sana duniani na mbinguni" (1Cor. 8:5)
KILA kinachotajwa na kuabudiwa kama Mungu kina hisia ambazo basically ni sifa na tabia za kibinadamu kama hasira, wivu, furaha, kisasi, huzuni, ubaguzi nk.
Je, Mungu unayemuabudu wewe hana hizo sifa za kibinadamu?

Aidha, kila Mungu anayo historia yake ya ni lini alijitambulisha kwa watu wa jamii yake; hivyo kutudhihirishia kuwa anao mwanzo wake na mwisho wake pia.

Neno Mungu huwa na nguvu mahali palipo na binadamu; ukimwondoa binadamu automatically Mungu naye 'kwishnei ' lakini INFINITY ADJUSTER, NGUVU KUU ILIYOASISI VYOTE YENYEWE HAINA MWANZO WALA MWISHO, IPO TU IKIENDELEA KUJIBADILI BADILI KADIRI ITAKAVYO!

NGUVU KUU ikifanya transformation ya kuama kutoka kwenye Sayari ya Dunia, automatically kila kitu kitatoweka ndani ya sekunde tu

Kwenye highest level of energy hakuna lisilowezekana endapo mwanadamu ataweza ku- access hizo energies kwa namna yoyote iwe kwa meditation, kwa maombi, kwa kufunga, kwa matambiko nk.

Kila binadamu huzaliwa akiwa kwenye Fourth level of consciousness(level ya 4 au chini)lakini uwa anahisi kwamba kuna higher power kumzidi, yaani huwa ana- feel like kuna mwenye nguvu zaidi yake ndiyo maana hakuna binadamu anayefundishwa Kuabudu, hujikuta anaabudu chochote automaticall kwa sababu ya influence ya NGUVU KUU. Wale wenye dini wanajikita kwenye dini zao na wasio na dini wanakuwa na namna ya kujaribu kuzifikia/ kuzi- access nguvu KUU zaidi yao!

Mtu anayeishia kutumia level yake ya 4 aliyojikuta anayo alipoanza kujitambua huwa anaishia kwenye maangaiko yasiyo na matokeo ndio maana asili mia kubwa ya wanadamu wote duniani wanakimbizana na masuala ya dini, uganga na namna nyingine nyingine ili mradi waende levels zaidi za kiroho!
Hata wale wanaoitwa 'unbelievers - wasioamini kama atheists, nao kuna namna wanaamini juu ya uwepo wa something stronger, smarter and wiser than them

Ni ukweli usiopingika kuwa mtu anayejikita kwenye maombi au kwenye ushirikina, maisha yake hayawezi kuwa sawa na mtu asiyejishughulisha kabisa na mambo hayo. Ni wazi mtu aliyezama in deep kwenye mambo ya dini na mchawi au mbobezi wa matambiko na ushirikina, si watu wa kawaida kama walivyo hawa walioridhika na hii level of consciousness!

Lakini, hata hivyo ni muhimu mtu anayetaka kukua katika nguvu/ upako/ neema/ uwezo mkuu wa kiroho, ahakikishe anafanya meditation kwa bidii na kufuata Kanuni zake huku akisaka maarifa mbalimbali ya kiroho na kuyafanyia kazi.

Kufanya hivi kutafungua nguvu za level ya 5 ambazo sio automatic bali ni dormant; zinahitaji kufuatwa kwenye realm yake kwa Kanuni zake.

Ukifika kwenye level ya 5 (level of Super Consciousness) utaanza kujihisi nguvu zisizo za kawaida... Utaanza kuona vile wengine hawaoni na kusikia wasiyosikia wengine... Utaanza kufanya Miujiza ya kila aina kwenye maisha yako!

Watu walioitwa Manabii hapo zamani ni watu ambao waliingia kwenye hii level of energy wakiwa bado duniani! Japokuwa hapa manabii wa kikushi wanafichwa na kubuni manabii wa uongo wa NGOZI NYEUPE kupitia dini zao za kimapokeo

Hata sasa wapo watu wanaofanya mambo yasiyo ya kawaida. Wanaweza kukwambia matatizo yako bila kuambiwa na mtu. Wanaweza kusema chochote kikatokea. Wanaweza kumgusa mgonjwa akapona. Wanaweza kubuni vitu visivyo vya kawaida kwa sababu wanakuwa na uwezo wa ku- access ulimwengu wa nguvu kuu!

Wakiendelea kwenye hii levels wakazoeleka, wanaweza kuamua kwenda level nyingine ambayo ni ya 6 (kwenye collective Super Consciousness)

Huku ndio mtu anakuwa haangaiki tena kutafuta heshima, sifa, fedha, cheo, kula na kunywa nk..
Ni level ambayo mtu anakuwa contented!
Hakuna cha kukupelekesha, kila kitu kwako ni kawaida... Mwema na mwovu wote kwako ni kawaida... Maskini na tajiri wote wanakuwa ni kawaida kwako... Vitu vyote vinakuwa kawaida. Hata kuonea wanyama kunaondoka kabisa ndani yako, huwezi kukutana na nyoka njiani ukamuua wala huwezi kufurahia kula nyama ambayo imetokana na kiumbe mwenye hisia ambaye hupata maumivu makali kama binadamu wakati anapochinjwa! hapa ndiko Kuna HOJA ya kutokula nyama kwa Imani ya Kirastafar japokuwa sio marastar wapo ktk level hiyo Ila nikwakuwa pia nyama za buchani hutiwa dawa zinazoathiri Tezi penuel , jicho3

Sasa Ukitoka hiyo level unakwenda level ya juu kabisa ambayo maisha yanapoteza maana kabisa. Kufa na kuishi vyote ni yale yale...
Shauku ya kila kitu inatoweka kabisa. Unakosa hamu ya kila kitu duniani hata chakula, sex, marafiki nk vyote vinakosa maana kwako... Unabaki kutamani kuishi kwenye maeneo ya utulivu ukiwa peke yako hata kula unasahau... Unakuwa ushahama duniani huku bado unaishi duniani!
Hii ni highest level of consciousness (super Cosmic consciousness)

Unaweza kuishi hata na wanyama wasikudhuru. Mbu hata hawawezi kukugusa. Unakuwa pure energy, pure spirit; kwako lije jema sawa, baya sawa... Emotions zinakufa kabisa. Hapa ndo tunasema wewe ni Mungu kwenye mwili wa damu na nyama, ukiuvua mwili huu ni MOJA KWA MOJA kwenye highest realm (wengine wanaita Mbingu ya 7) Katika freemasonry hii Ni nyuzi/degree ya 33 ya ukuhani.

Unakwenda kuishi na Roho takatifu zisizo na waa wala mapungufu kabisa!!!
Unakwenda kupumzika kwani unakuwa huna unfinished business yoyote duniani... Unakuwa umemaliza kiila kitu. Unakwenda kukaa kama pure energy/ spirit kwenye highest level of consciousness na hapa hutozaliwa Tena ktk ulimwengu wa 3D utavuka kuingia ktk 5D,6D-12D.

🔴Imetayalishwa na kuandikwa na Naligia Mninoi.
 
Acha fix mkuu, Mbu hawakung'ati?
Labda ujipake dawa ya kufukuza mbu!
 
Back
Top Bottom