Salamu ya Shikamoo ni ya kitumwa

foroy

Senior Member
May 2, 2018
186
288
Hivi bado kuna haja ya kuendelea kuitumia hii salamu katika zama zetu hizi? Kwa lipi hasa?

Katika misingi ya salamu zote kwa lugha zote duniani hakuna kitu chenye mfanano na "shikamoo".

Ili kujua kama shikamoo sio salamu ya kukumbatia, tuanze kwa kujua maana ya salamu na dhima yake.

Salamu ni tamko la awali watu wanapokutana kwa mara ya kwanza baada ya kupita kitambo fulani bila kuonana, mathalani baada ya kuamka, kabla ya kuanza safari au kazi na hata baada ya hayo.

Salamu hutoa muunganiko kati ya mtu na mtu, au mtu na watu, kabla ya kuanza siku, kazi, ibada, au shughuli ya aina yoyote inayowaunganisha pamoja kwa wakati huo. Kimsingi dhima ya salamu ni kujuliana hali na kutakiana heri.

Kwa upande mwingine, salamu ni lango. Linaweza kuwa lango la baraka na heri au lango la nuksi na laana. Kwa hivyo, salamu ni lango la mtu kumpokea mtu mwingine kabla ya kufanya jambo lolote. Ni sahihi pia kusema kwamba salamu imebeba pia roho ya mtu. Dhamira mbaya au hai huanzia kwenye salamu.

Wachawi na washirikina hutumia salamu pia kama nyenzo ya kupenyeza sihiri na ulozi kwa waliowakusudia. Ndiyo maana baadhi ya watu hukataa kuitikia salamu za wanaowahisi kuwa wabaya wao, kwa imani kama hizi. Na si tu kupokea salamu, bali hata kutoa salamu. Katika ulimwengu usionekana kuna watu wana uwezo wa kupokonya baraka na nyota yako kupitia salamu yako kwake, au yake kwako.

Kama huamini hayo, kasome kitabu cha Luka 1: 28-29, Mariam alipotembelewa na Malaika Gabriel; alikuja na salamu iliyomshangaza mpaka akahoji, salamu hii ni salamu ya aina gani? Mariam alitaka kujua kama ilikuwa ya heri au ya shari. Mpaka Gabriel alipomhakikishia kuwa ilikuwa ya heri, ndipo akaipokea kwa mikono miwili.

Lakini pia katika Luka 10:4, Yesu akiwa anawaagiza wanafunzi kwenda kuhubiri injili mahala fulani, aliwapa onyo zito wale mitume, "njiani msimwamkie mtu yeyote...." Umeona? Kwanini? Salamu ni lango la uharibifu pia. Kuna watu ukisalimiana nao tu, mambo yako yanaharibika.

Hii ni mifano michache inayodhihirisha kuwa salamu ina nguvu ya kujenga au kubomoa, kuleta wepesi au uzito kwenye mwenendo mzima wa maisha ya kila siku ya watu.

Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokuja na salamu ya, Nawasalimu katika jina la Muungano wa Tanzania, Kazi iendelee...nilimwelewa mno na kumuunga mkono. Natamani sana kuona anaigeukia na hii salamu inayoendeleza utukufu wa colonial after effect na mental slavery ya siku nyingi.

Shikamoo ilitoka wapi? Historia yake sote tunaijua. Iliasisiwa katika kipindi cha utwana wa biashara ya utumwa na utumwa wenyewe. Wale mabwana waliojivika ubwana mkubwa walikuwa wakisalimiwa na watumwa kwa mtindo wa kuinama na kuwashika miguu yao na hata kuibusu; "niko chini ya miguu yako."
Ni ishara ya juu ya ku-surrender, kwamba lolote bwana mkubwa atakalosema au kuamua juu yako, ni hewala!

Nafahamu fika, kwasasa hakuna anayeitumia shikamoo katika muktadha wa kuwa chini ya miguu ya mtu, la hasha. Lakini ukweli ni kuwa salamu hiyo ingali inatutesa; kwa kujua au kutokujua. Na pengine moja ya sababu zisizoonekana za watoto wengi kuwa chini ya utegemezi wa wazazi au walezi wao mpaka wanapatwa na mvi, ni hiyo salamu. Na pengine kama taifa, tunaendelea kuwa chini ya miguu yao kiuchumi, kimaarifa, na hata kiutamaduni kwa sababu ya nguvu ya hii salamu, shikamoo. (A little bit joking but it's alarming)

Bila kupepesa macho, Shikamoo ni salamu ya kitumwa na haina maana. Nakupa mifano;

Katika salamu zote duniani, ni shikamoo ndiyo salamu inayoweza kumuumiza mtu kichwa kabla ya kuitoa. Yaani badala ya kumsalimu binadamu mwenzako kwa roho safi, unaanza kujipa kazi ya kukadiria umri wake. Hivi huyu mtu ni mkubwa au mdogo? Amenizidi sana au tunalingana? Nimwamkie au nimwambie 'za saa hizi'? Salamu inayoanza kukutesa kabla ya kuitoa ni ithibati ya utumwa kama sio uchizi.

Ni shikamoo pekee inayosababisha tuogope kusalimia baadhi ya watu "Haujambo!" Leo hii ukimwambia mtu anayeamini kuwa mkubwa kiumri zaidi yako, 'haujambo?' atakujia juu na maneno ya laana utatupiwa! Unaniambia mimi haujambo? Huna adabu...umekuwa eh?

Lakini haujambo si ndiyo how are you? Si ndiyo Como esta? Si ndiyo comment ca? Shida nini? Kwa hiyo haujambo anatakiwa kuambiwa nani? Kuna utumwa zaidi ya huu? Yaani salamu itumike kukupandisha chati, uonekane mkubwa kuliko yeye au wao! Ndiyo kazi ya salamu hiyo? Si ndio utwana wenyewe huu?

Ni shikamoo pekee, salamu inayoweza kukufedhehesha kama ukiitoa kimakosa. Salamu inaanzaje kukufedhesha? Niliwahi kumwamkia mama mmoja, shikamoo; nikamuona anaangua bonge la kicheko. We Foroy, umesahau tulisoma darasa moja shule ya msingi? Godamn!! Nikaanza kujikuna kichwa kwa fadhaa! Fadhaa ya nini kwenye salamu?

Kuanzia hapo, nikasema ntapunguza kuamkia watu hovyo hovyo. Kumbe najitengenezea mazingira ya kufedheheka kwa mara ya pili.

Safari hii akaja dada fulani nyumbani, nikiwa na shangazi yangu. Sikumwamkia huyo dada. Baadaye shangazi akamtambulisha huyo dada, umemuona Foroy alivyokuwa? Umemtambua? Yule mama ndiyo kuachama kwa mshangao huku akinitupia jicho la pembeni....Kale ka-Foro tulikuwa tunakabeba mgongoni mpaka kanatukojolea?! We Foro hujambo? Mbona hujaniamkia? Ndiyo umekuwa hivi!!

Niliitoa shikamoo kwa mateso huku jasho likinitoka. Nauliza tena, kuna utumwa mkubwa kuliko huu? Ya nini mateso makali haya? Kisa ni shikamoo? Hii ni pure psychological slavery!

Na ukitaka kuamini hilo, fanya utafiti huu. Waswahili wenzetu wenye asili ya kiarabu wengi wao hawatumii sana hii salamu. Salamu rasmi na yenye mantiki ni Salam Aleykum; amani iwe kwenu. Hii ni salamu safi na halali kabisa. Salamu yenye mantiki. Hata Bwana Yesu alikuwa akiitumia mara zote. Wala si salamu ya kiislamu pekee kama wengi wanavyodhani.

Mtoto wa kiarabu hata kama yupo darasa la pili, hawezi kukwambia shikamoo, atakwambia Salam aleykum. Nina experience na hili, na nimelifanyia utafiti wa kutosha. Na wala sina shida na hilo. Ni halali kabisa.
Wao wenye kujua chimbuko la lugha ya kiswahili ambayo ndani yake kiarabu kina mchango mkubwa, hawaitumii shikamoo, sisi tumeikumbatia. Dubai, Saudia mpaka Yemen, kote huko huwezi kukutana na shikamoo, na bado tunaambiwa ni neno la kiarabu.

Waama! Tuna kipaji kikubwa cha kukumbatia mambo yasiyo na maana!

Katika lugha zote duniani, hata za makabila yetu salamu haitenganishi wala kubagua umri wa mtu. Salamu inapaswa kuunganisha watu. Sio kutisha watu na kuwapa kibarua cha kukadiria umri za watu. Kikubwa ni heshima na namna ya kuitoa. Vinginevyo, salamu ina kazi moja tu, ya kujuliana hali na kutakiana heri. Kuendelea kutumia shikamoo ni kukuendelea kukumbatia na kuenzi utumwa. Kimsingi ni salamu inayopaswa kuwekwa kwenye makumbusho ya taifa.

NAMAZILIA...

Wakati fulani nikawa nimepanga nyumba fulani, na jirani yangu alikuwa kijana mmoja tuliyekuwa tukiheshimiana sana. Ingawa alikuwa na mke na watoto wawili, bado mimi nilikuwa mkubwa kwake kiumri pamoja na kuishi kibachela. Na hatukuacha kuheshimiana.

Siku moja, kijana huyo akatembelewa na mama yake mzazi. Kwa umri wangu na kukadiria umri wa mama yake, sikuona kama nilikuwa na sababu ya kumpa shikamoo. Nikawa namsalimu kwa adabu kabisa, lakini kwa salamu za kawaida mbali na shikamoo.

Kumbe kijana akaonea namkosea adabu mzazi wake. Na sijui kama walijadiliana na mama yake au la! Lakini inaonesha siku hiyo alininywea pombe na kuamua kuja kunichana, kwanini namchukulia poa Bi mkubwa wake? Kwanini simwamkii kama wapangaji wengine? Nilisononeka kwa kweli, lakini sikumuacha na ujinga wake.

Nikamuuliza kistaarabu, mama yake ana miaka mingapi? Akanijibu 54. Na yeye? Akanambia alikuwa na miaka 32. Nikamfahamisha kuwa mimi nilikuwa na miaka 45... miaka 13 pungufu yake. Nikataka kujua, kwanini mimi alikuwa haniamkii shikamoo? Akaacha mdomo wazi.

Nikaenda mbali kwa kumjuza kuwa dada yangu wa kwanza ana miaka 62 na huwa tunasalimiana kikawaida bila kuingiza shikamoo. Kwa hivyo hata mama yake ni kama dada yangu!
Aliondoka akiwa anasonya, na tangu siku ile hakunichangamkia tena!

Japo nilimpuuza na kumhurumia lakini nilijiuliza sana, huu utumwa wa salamu ya shikamoo utaendelea kututesa na kuharibu ujamaa wetu hadi lini? Je, sio muhimu sasa tukaamua kuachana na zama za shikamoo ya nipo chini ya miguu yako? Natamani kiongozi mkuu atoe tamko!

Kuna kila sababu ya kureview upya hii salamu. Tusije tukawa kwenye kifungo cha kukiri utumwa bila kujitambua. Shime sasa!

#Mentalslavery

Sent from my Infinix X697 using JamiiForums mobile app
 
Hii salam hata mimi sijawahi kuielewa. Naona haijakaa kabisa katika mazingira ya usawa. Nadhani tungetafuta salam sahihi ya kusalimiana kwa makundi yote katika jamii.

Hakuna kitu kinakera kama kile cha kumsalimia mtu shikamoo, halafu baadaye unakuja kugundua kumbe umezidi umri!!!
 
Mbona umejieleza sana 😁

Kuna baadhi ya maneno ya Kiarabu yalijichomeka kwenye Lugha ya Kiswahili baada ya ujio wa wakoloni wa kiarabu.

Kuingia kwa maneno hayo haimaanishi tena kuwa yanaendelea kuwa kiarabu na kutafuta maana yake usilitafute kutoka kwenye asili yake Bali libaki la kiswahili hivyo hivyo ndio maana Mwarabu hawezi kuongea kiswahili mpaka ajifunze.

Kwa minajili hiyo, neno shikamoo kama lilivyo kwenye kiswahili kwa Sasa hivi ndio salamu Bora ya heshima ya kiswahili kumsalimia mtu aliyekuzidi umri. Na tusitafute tena maana ya kiarabu ya neno hilo Bali litafsiriwe maana mpya kwa kiswahili ili kulipa hadhi maana haliwezi tena kutoka kwenye lugha.
 
Back
Top Bottom