Our time is now!
Nimeenda Indonesia kule kukaa bond kwa wasiwasi hivi kumuamini gani mwanamke hata kama unamtaniaaa? Sio kwa kujiweka rehani. Kule mi nikawa nakula na kunyaaa tu kwa raha zangu. Siku wanapakia mzigo sikuaminiiii. Wahindi nyokoooooo. Wana tamaa ya pesa mpaka basi. Sijawahi kuona wahindi jeuri kama wale. Mpaka nikaanza kutubu najua unga ule mwingi sanaaa, Naola atashindwa kuuzungusha na kuulipa. Isitoshe hana experience kabisaa juu ya hii biashara. Nikawa najua ikiisha miezi 6 wananiuaaa.
Nimekaa pale kwa mashakaaa, naona issue nzima zinazofanyikaa. Wale tuliokuwa nao bond ndugu zao wakapewa unga afu hawajarudi kuleta pesa wanauawa kizembe na kufukuiwa kama mizoga tu. Daaah! Nikasema nikipona hii sirudiii kuiweka roho yangu kwenye mikono ya mwanamke. Sirudiii. Kwanza nilikubalije kubalije. Kmanina afu mwanamke ajitie kuja kunizuluuu sijui nitamfanyaje. Sijuiiii.
Nimekaa miezi mi 3 tu, nikaja kufatwa haya nenda, deni lako lote lilishalipwa. Jana wamefanya transfer. Nikastukaaaa. Sijaamini kama nimetoka rehani. Wakaniambia nijiandae, wakanifunga macho mpaka airport. Nimefika airport nikapanda ndege mpaka bongo. Walinitauarishia kila kitu. Narudiii sasa wear house nakuta full shangwe, full kazi kwa kaziiii.
Nikaenda kwanza kupumzikaa. Nijitafakari nakuwaje Alcapone kwanza. Nimefika nategemea nikute nyumba imejaa cash, mahela kila mahala. Sijakuta hata mia. Nikampigia Naila, rudi nyumbani kwanza tuongeee. Akaja, nikambana hela zangu ziko wapi? Akashanga hela gani? Nikamwambia za unga? Ziko wapi. Sifanyi lolote mpaka niione hela.
Akadai hela zipo, kazihifadhi. Nikakomaa wapi, inatakiwa nikazione. Kama vipi kila mtu ahifadhi hela zake kivyake, mambo ya kuwekeana hela ndo mwanzo wa kuuwana.Pesa ikishakuwa nyinhi unaona mwenzio anakubana duniani. Akakubali. Tukaenda alikoficha hizo hela, tukahesabu na kugawana pasu kwa pasu. Ikakubaliwa mauzo yakija ikatolewa hela ya mzigo, hela za wafanyakazi, faida tunagawana hapo hapo kila mtu akafe na yake mbele. Ukawa ndo utaratibu.
Naila akanionya tu nispeleke hela bank maana wataanza kunifatilia afu ishu itakuwa hamnaaa. Nikamwambia ushawahi kusikia mimi nina account bank? Akasema sawa. Wanawake sio watu wa kuwaamini sanaa. Ni watu wa kuishi nao kwa akili kubwa sanaa.
Nikaanza kazi kila mtu ananiheshimu. Hata wale washkaji wa zamani nao wananijia kwa adabu, chezea boss mwenye watu wangu. Alcapone. Na urahisi tulioupata ni kwamba Godfather hakuwa na mziho, tukachukua masoko yake na punda wake tukajisevia. Kiukweli soko la Godfather lilikuwa si la kitoto. The market was built over 10 years.
Siku ya siku nimekaa mwanangu Ommy akaja maskani, akaishia getini maana huu utawala mwingine na yeye bado yupo kwa Leila, akaniulizia. Nikaamua tu nikamsikize. Ila kiukweli kitendo chao cha kuona kuliko wafanye kazi na mimi bora wasifanye kiliniumaaa sanaa. Sanaaaa. Wale vijana wenzangu nilitegemea support yao sanaaa. Na kisa cha kenda kumsikiliza nilitegemea angeniambia amekuja kujiunga.
Kufika ananiambia mambo ya kipuuzi. Eti mwanangu Juma amemuona mienendo yake sio mizuri kabisaa. Kaacha shule. Ada imekosekana, mimi hawanipati kwa hio nafanyaje. Khaaaaaa! Nikamwambia Ommy yule sio mtoto wangu, achana nao na mama yake watajijua wenyewe. Mi mda wa kumsomesha sijui kufanya nini sinaaa. Na kama kwa ishu za kipuuzi kama hizi usije.
I thought after getting a lot of money ill be happy! I wasnt. Nilikuwa nipo kama sipo. Honestly i missed my old life. I was stuck with Naila ambae simpendiii hata kidogoo. Yupo obssesed kutafuta mtoto. Ashanifumania mara 10 na zaidi ila ana deal tu na huyo mwanamke and i get to walk free. Haniulizi wala hasemi chochote. Nikawa nahisi atakuja kuniua usingizini.
Unga una helaaaa, unga una helaaaa. Nimeshika helaaaa. Nimeshika helaaaaa. Nikaamua kunua boti basi yuuu. Sio boti ya uvuvi, boti ya kula bata yatch. Nikajiunga na Daresalaam Yatch Club, nika mingle na matajiri kila weekend. The good life.
Nikaamua kujiunga na golf club, sina sehemu ya kupotezea mda. Nashinda nakunywa na kucheza golf tu. Nifanyaje sasa. Warembo ndo niliwatombaaaa mpaka nikawa sitaki tena K. Nilikinaiii. Ni kitendo cha ku handpick tu, nataka mwanamke flani, namwambia kuwadi wangu, namkita hotelini, kila kitu kuwadiii kamalizaaa.
Nikaona wanawake wa bongo hawana ladha tena nikaamua kwenda latin america, nako nikachokaaa, nikaenda kwa wahindi wakanishinda hawana makalio na ndo uhonjwa wangu. Nikaamua kwenda rwanda na burundi ujirani mwema. Mwisho nikawa sitaki tena wanawake. Nikasema nijaribu wanaume. Wakanishinda. Muonekano tu nilishibaaa. Dumee dumee hata lijilegezee na kujipodoa vipi bado dume tuu.
Nikasema sasa niamie kwenye chabo ya kisasa. Chabo ya kisasa unawalipa tu watu, wakifanya unaangalia tu kupata zile stimu. Unaweza walipa wakafanya kwa group sex au wawili, shetani langu litakavo nituma siku hio. Nikijisikia naniunga humo humo kwenye hio group. Balaa juu ya laana. Cha ajabu ukiwa huna pesa unatamani wanawake mpaka wabaya, hata sabuni tu inakutosha ila ukiwa na pesa utapiga hata chabo ila stimu hazipandiii.
Nikanunua nyumba, ambayo ndo ikawa kama base yangu ya kufichia pesa humo. Nyu,ba nikawa aniheshimu sanaa, nashinda kwa heshima na adabu. Hata mzigo pia ulikuwa unakaa humo kwa mda. Kila ukija hukosi stock ya maana ya mzigo. Afu nikawa na appartment ambayo tulikaa na Naila. Haya mambo yangu baadhi Naila alikua anayajuaaa baadhi alojitahidi kutonifatilia.
She tried really hard to make us work. Mpaka akakubali 3 some, sema haya mambo kama huwezi huwezi tu. Anakubalia ila sasa mara aanze kulia kabla ya mtanange. Hayaweziii haya mambo ya kifirauniii. Nikaja kumjua kwamba legevu sana kwenye hii sekta. Akisema sijui nini namkatalia no.
My sex life was deteriorating afu sijui kwanini. Au naanza kuwa shoga? Dalili mbona kama sizielewi. Nikaamua ku research. Nikagundua nina dalili zote za kuwa hanisi. Tobaaaaa. Nikawaza maybe i should get new addiction. Fetish habbits. Wapi!
Akaja mtu pale kazini kunistua huenda wananifanyia mambo ya kiswahili. Nitembeee. Hakisema nani. Nikaamua kutembea. Mtaalamu wa 1 akasema kweli kuna mwanamke ananifanyia mambo niwe hanisi. Nikajua tu Leila. Mwanamke mbaya yuleeee. Loooh! Kaona pesa ninayo kaamua kunikamata kwenye engine. Wataalamu wa 4 wote jibu hilo hilo nafanyiwa mandingo ndingo niwe hanisiiii. Nilikunywa dawa za wataalamu wa 5 tofauti. Kidogo nikawa fitiiii. Hamu ikarudiiii, na urijaliii wangu ukarudiii. Asite mtoto mzuri lazima nimuimbishe na nimle.
Daaaaaah! Niliwawahi walikuwa washanipotezaaa kabisaa. Kiukweli nikahis hata Godfather wakati tuko nae hakuwa muhuni muhuni kabisaa. Nikahisi watu watakuwa washamtengenezaaa. Maana hakuwa mtu wa wanawake. Mpaka tukawa tunamtilia shakaaa. Na hakuwa mtu wa wanaume either. Tukasema labda mdau wa CHAPUTA ila hatukupata uhakika. Usikute wanawake washafanya yao.
In 2 years mambo yalikuwa baaam, baaam. Ngoma inogileeee. Leila akaja kuniambia kuna mtu alitaka kumuua Godfather nikajua tu ni Naila. Sikumwambia Leila ila nilinua. Nikamuweka kikao cha dhararura, kwanini atake kufanya huo ukatili.
Katika utetezi wale akasema Godfather anaweza kupona kwa nguvu za Mungu, we should tie that loose end before its too late. He is done, he wont be comming back any time soon. Nikajua hajawa comvised and she will try it again. Nikaamua kumwambia " Baby tumetoka mbali sanaaa, sanaa, sasa ukimtoa Godfather kwenye picha ujue Leila atakuwa Free, and loose. And i cant gurantee what i will do next akiwa free. Si plan ila shetani anaweza kunipitia. As long as Godfather yupo, Leila is off my limits. Dont you want that baby?"
Akakaaa tu kimya, nikajua somo limemuingia sawa. Hatothubutuuu. Not that i lied ila kiukweli i couldnt guranteee. Wazo la ku get rid of Naila and Godfather just like the old days tubakie mimi na Leila tu kwenye picha lilikuwa linakatiza katiza kichwani mwangu mara nyingi tu. Only i didnt have balls to make it a reality. Ila Leila design angejiongeza kidogo tu kwenye uelekeo huo, design kama sielewi msimamo wangu ungekuwa vipi. Pamoja na kiwa kazaa mapacha tena nisingejali.
Then Leila had a come back! Mwanamke nyokooo yule. Who on earth alitegemea atapata connect. Ilileta taharuki kubwaaa sanaa kwenye organisation yangu. Kwanza kabisaa mapunda wakaleta undumila kiwili kutaka kurudi kule kwa Leila, maana kwanza walibaki wachache akabadilisha structure nzima ya ufanyaji kazi.
Structure yake ilikuwa nusra nusra ile almanusra itutoe kwenye biashara. Inaonesha ile miaka mi 2 aliokiwa bench alikuwa akiusoma mchezoo kwa makini kabisaaa. Na alileta mapinduzi makubwaa sanaa. Hakuna alie amini kama mwanamke anaweza kufanya mapinduzi yale. Watu wakadai Godfather lapona ndo anaendesha kampuni, sio akili za mwanamke.
Tofauti na mimi na Godfather ambao tuliamini lazima ku oprate from base hapa bongo 100%. Na structure zote zilanzia hapa kama HQ. Afu tunauza substance moja tu. Supplier mmoja,Na soko hilo hilo miaka yote. We were more of a logistic organization, kama ma transporter tu. Focus yetu ilikuwa ku move substance.
Leila was something else. Kwanza ana supplier wa 3, wana m supply grade 3 tofauti, ana masoko tofauti kutegemeana na product. Akawa mtu wa kwanza kui brand product yake kwa kuweka rangi pink. Unga mwingi ni mweupe, na umezoeleka ni mweupe. Mwanamke mwanamke rangi zote kachagua pink, ambao jina la kitaaa ulikuwa unaitwa Pink sugar una grade 1 mpaka 3. Aliuza sanaaa sanaa. Maana wateja wanakomaa wanataka pink sugar. Supplier wetu akashindwa kuweka rangi bila kushusha ubora. Akawa mpaka anatafutwa na wateja Pink sugar hio. Tamaaa tamaa zake akaleta rangi 3. Aliona neno grade linampunguzia wateja. Akaja na pink sugar kama ilivokua, color me purple ambao ilikuwa ndo grade 2 ya zamani , yellow instincts ambayo ndo grade 3 na aka launch product mpya haijapata kuwa demanded inaitwa Black Magic.
Hii black magic hakuwa na supplier alikuwa ana i manufacture hapa hapa. Ule unga anaoletewa ana u process zaidi kuwa Black Magic. Na sokoni hakuna mtu aliekuwa nao. Yaani ulikuwa hela hela ya maan. Mpaka Naila alikaa nae mezani kama vi atu supply black magic kwa bei ya jumla akagomaaa.
Watu wakawa wanadai black magic anachanganya unga aina zote 3. Tukajaribu kuoda unga kwake tokea china, tukachanganya haikuwa. Kukawa na habari nyingi ana changany hiki na hiki na kile, mtaalamu akipika hamna kitu.
Pia akaanzisha territory, na ana apoint territory managers ambao hawagusi bongo wanakaa huko huko nchi za mbele. Kazi yao ni kutafuta masoko mapya, ku establish distribution systems, ku study demand, na kuresearch market, kusoma competition. Ilimsaidia sanaa kupunguza causalities na lost goods. Mpaka kwa zile product 3 akawa na demand kubwa kiasi ni vigumu kwake kuja kuship toka huku. Ikawa more profitable kwa supplie wake ku ship kwenye territory directly. Alifanya kazi mjinga yule mwanamke.
To keep up competition tukawa tuna mcopy. Ila cha kucopy hakina ubora. Tukakata bei, ili tuweze ku retain wateja, ilikula kwenye faida yetu. Tukapandisha comission kwa mapunda ili wapige kazi. Akaja na mbinu mpya ya kutumia mapunda wa kike, hawa wasichana wazuriii waliofeli maisha anawapa hio dili, ikaonekana sucess rate yao iko juu sanaa kupita wanaume. Tukai adopt na sisi. Ilitufaa sanaaa.
Ila sokoni ikawa Leila ambae walimpachika majina ya Mama au Bi mkubwa, ndo anaongoza wengine wanafata. Kwa miaka mi 3 tumeenda nae jino kwa jino. Wakipata hela hivi, kesho na sisi tunaanzisha kama wao. Nchi huru hii jamani.
Pesa haitoshiiii. Haitoshiiii. Haitoshiiii. Kila ukipata ndo kama unaanza leo kupata. Ukienda mahotel ya world standards unaona wewe mtu mdogo sanaa. Hivo hivo unavunja safe kujitutumua. Mpaka inafikia kipindi unajiuliza hivi sh ngapi inatosha? Labda ni kuridhika tu. Maana unaenda The Ritz ku book, wanakwambia kumejaaa. Na hela sio ya kitoto pale. Unakaa waiting list hata mwaka mzima. Ukienda kila unachojaribu unaona kama umevamia kina kirefu. Ila inakupa challange ya kukomaa zaidi.
Siku hio nimechill maskani naangalia online world most expensive restaurants nifanye booking, maybe niende over the weekends kwa ajili ya kujipumzishaaa na kula dinner. At this stage mdau nilikuwa naweza kuamka na kwenda Dubai kupunga upepo nikarudi, pesa ipoooo. Tatizo nini? Akaja mtu mbio mbio nikawa nimejiweka kwa tahadhariii. Akasema Godfather kaponaaa.
Nikamuuliza eeeeeh? Akasema Godfather kaponaaa ndo habari iliopo mjini. Jana kaenda ofisini kwake. Mzimaaa, mzimaaaa. Kama sio yeye alielala miaka mi 5. Akili zake nzima kabisaaa. Na ni yeye yule yule. Wamethibitisha watu zaidi ya wa 5.
Nikapagawa kabisaa, na kumkumbuka Naila alisema ile ni loose end. Anaendelea kuniambia ila kuna fukuto kubwa sanaa, kubwa kuliko maelezo kati ya Godfather na Leila na Wafanyakazi. Yani usipime mambo vuluuu vuluuu. Godfather kaweka stop order ya operations zote. Kimenukaaa sio kidogooo.
Nikampigia Naila, simuuu ikaitaa we haijapokelewa. Mpaka usiki hajarudi na simu haijokelewa. Na siki 2 nilikuwa nimesafiri nimerudi siku hio hio so hatujaonana bado afu napewa taarifa kwamba kubwa la maadui ndo limerudi mzigoni.
INAENDELEA USIKU HUUU HUU.