Weekend Story! The Grass is always greener on the other side

Weekend Story! The Grass is always greener on the other side

Hahahahaaaaa! Ifikapo leo mchana kama bado hujachagua tema baaaasi utapoteza haki yako ya kuchagua team.
lara ni ngumu kuchagua team,kila mtu kajihami na bomu la nuclear,Siza kampata mwl na inaonyesha teacher yuko vizuri kwenye medani za chini kwa chini na kule Leyla ana bigboss dah!

Wacha niendelee kumpa credit Siza[emoji123]
 
The art of keeping Men!

Hivi ushawahi kuwa unaishi maisha ya kusubiriaaa? Umechokaaaa, umechokaaaa huna dira wala direction, huna ambition huna lolote. You are just sitting waiting in vain, kitokeee kitu, kitu chochote kitakacho badili maisha yako. That was me not so long ago. I was waiting day by day, year by year and nothing happened. Then Ceasar happened! I wam going to do whatever it takes to keep this life. I am never going back to the waiting zone again.

Nimejitahidi yaani nimejitahidi kutokaaaa sio kwa jitihada za dunia hii, ila nimefeli. Nikaona sina nyotaaa. Nafanya kazi sanaaa, najitumaaa sanaa, na fight sanaaa, ila mwisho wa siku najikuta natumia msuli wa tembo matokeo ya sisimizi. Nikaonaaaa mimi sina nyotaaaa.

Nikawa nikipata wanaume nakiweka juhudi kidogoo tu, yaani kidogo, hata nikitoa wazo tu, anafanikiwa sio kidogo. Nikisema nifanye mwenyewe nachinaaa, nachinaaaaa. Nimejitahidi ila ndo iko hivo. Akija mtu Naila hivi na hivi nikaweka mawazo kidogo basi ndo mafaniki one way!

Tatizo likawa nakuwa na mwanaume FREE P, nampa mtaji na mawazo, anakuja kufanikiwa ki nyoko nyokooo mpaka inakuwa aibuuu. Wakifanikiwa tu wana nisahau kabisaaa kabisaaa. Wanachukua wanawake wengineee. Na mimi nimechoka mwenzenu hizi mambo za kutumika kama daraja. Ila akili za mtu za mtu tu, wakifeli basi wanataka kurudi na mimi sitaki tenaaaa.

Siza kaenda huko sijui imekuwajeee, karudi kama mtu tofautiiii.Nikajuaaa tu, yani nikajua kwamba huko alikokwenda kuna kitu kikubwa tu hataki kukisemaaa. Think of it, mtu katoka hapa anajua kabisaa Godfather sio mtu mzuriii, na bado kanipigaaa mtu nilie mlipia bail na kumtoa gerezani.

Ghafla anarudi all committed and ready to take action mda wowote. Ile sema suuuuu. Nikaona kaivaa. Sasa kama nilivosema nimechoka kuwa daraja. Nimechokaaa. Nikamwambia kama unataka tushirikiane kimaisha fanya ufanyavo NDOA baba, ndoaaa. Akasema niko tayari. Sasa alivoisema ile kirahisi rahisi nikajua ofisini huko kuna jambo limetokea. Mpaka kakubali ndo nikapata hamu ya kujua nini kimetokea cha kumnyongonyeza Siza.

Nikawaambia sasa wasiliana na shamba, uone kama mzigo unakuja au vipi. Akawasiliana nao, kwamba mzigo unakuwaje. Wakataka profile yake, network yake, connect yake ya zamani of which katika hivo hana lolote. Nikaona ngoma nzito. Nikamwambia pose kama umetumwa na Godfather. Tutumie kila kitu cha Godfather, tukadanganya afya ya Godfather ni mbaya sanaa. Wa kufa leo kesho, ndo maana Siza akiwa kama right hand wa Godfather, anaanda mazingira ya kuwa Godfather hana uhakika kama source ya zamani ya Godfather watampokea yeye au vipi but he is so so ambitious he is not taking any chances, anaongea nao, wakikubaliana Godfather anakufa na source yake.

Wakawa interested sanaaa. Maana kuwa impress tukawapa business plan ya Godfather. Not exact ila Siza alikuwa anajua mambo mengi. Wakasema tunatawajibu. Baadae wakasema wako interested sana sanaa, anakuja mtoto wa huyo baba kuhakikisha Godfather is at dying point kwa macho yake mwenyewe na kuhakiki sturcture na kutest capacity ya network ya Godfather on the ground. Kujua how powerful wapooo.

Siza akaanza kupakiniki, akaona mbona dili limekuwa dirisha. Anasema ooh bora nikamuombe msamaha Godfather hivo hivo tuyamalize nirudi kuwa punda. Stupi.d a.ss negro. Mi nikamwambia kubaliii, kwanza tutajua la kufanya baadae. Analalamika mwanamke unaniponza wewe. Akakubaliii.

Wakasema ndani ya mwezi huyo mtoto anakuja. Nikamwambia nenda kule kazini kamwage sumuuuu, kwanza Godfather hana utu kwanini alifanya jaribio la kukua na pili kutaka ufungwe. Kama kakufanyia wewe atawafanyia na wao. Akaenda kumwaga sumu kule, hakupata watu. Na sababu kubwa ni kuwa godfather ni mtu mwemaa, mtu safiii, mtu wa uwazi. Mission ikawa impossible. Sinza anazidi kukonda na kulaumu, i told you so. We cant pull this.

Nikawaambia waite kikao, mi nitaongeaaa. Akasema hadhani kama watakjua. Nikamwambia nipe namba zao wote. Nawaita mimi. Akanipa list. Nikampigia mmoja mtu mzima babuuu. Babu akanipa mapyaaaa. Akanichana mama we hujuiiii, huyu Siza na Godfather wanagombea mwanamke, malaya malaya tu, si mganga wake nani, kawalisha nyama za mata.ko hawasikiii hawaoniii. Mama utajiumizaaaa. Mimi kama mimi mama siwezi ku risk maisha yangu na kipato changu kuunga mkono ugomvi wa kumgombea malaya.

Nikauliza malaya anaitwa nani? Akasema malaya anaitwa Leila. Roho ikafanyaaa paaah! Nikaona kama sielewei kama Leila kampa Godfather? Holly Cow! Mwanamke ana ki smart kikubwaa mngese yuleee. Ndo maana kamuchia siza kiroho safi kumbe ameenda kula Jackpot! Mamima kweli kweli. Nikajisikia vibaya sanaaa. Mi nahangaika na fight kuufufua mzoga Siza, afu yeye anatanua na Godfather na Siza is doing evrthing we are doing just to get back on her. Nilivunjika moyo sanaaaa. Nikamuaga tu babuuu.

Anasisitiza mama achana nao, fanya maisha yako. Hao washarogwa na kupewa limbwata hawaponi leo au keshooo. Watakusumbua tuuuuu. Mi nakwambia pale kwa siza hamnaa mwanaume mwanangu hamnaaaa, yule muhuni tu wa mjini. Nikafanya tu kukata simu.

Nikaenda baharini kuangalia bahari kama masaa 5 nawaza tu, na kuwazua nalijamba vipi hili shuzi. Nikaamua sasa cha kufanya ni kusimamia show mwenyewe. Mimi ni mwalimu, mimi na akiliiii. Mimi nawafundisha watu wanafanikiwaaa. Mimi ni nina akili kuliko navojizania. Nikapaata wazooo.

Nikaona nikiwaunganisha umoja ni nguvu, watu wengi bendera fata upepo, wakiona wengi wamekubali watakubalii, wakiona wengi wamekataaa watakaaa, dawa ni kumfata mmoja mmoja na kuongea na face to face mimi na siza na huyo muhusika. Atoe msimamo wake hapo yeye kama yeye haina kujifikiri. Watakaojiunga mwanzo watakuwa wakubwa na kupewa nafasi kubwa katika utawala mpya. Atakae kataa basi wasilaumu Siza aliwaacha kwenye utawala wake kawapa fair shot wamefanya maamuzi binafsi not to take it.

Sikutaka mizigoo, plan ilikuwa we work smart, we dont work hard. Tunachukua watu wachache wa msingi na muhimuuuu afu baaaas! Nikamwambia Siza toa list ya watu wale viungo. Tunaanza wakubwa na wadogo viongozi au hata kama sio viongozi wanajielewa wako smart. Akanipa na namba ya simu. Nawapigia simu Siza anaumwa snaaa, hataki watu wajue njoo wewe peke yako, Godfather akijua tunajua ni wewe ndo umeuza CD maana hatujamwambia yoyote.

Nikakaa na kumkamata Siza, anielekeze plan la Godfather mwanzo mwishooo, detailed. How it works A to Z. Bila kuruka details. Distribution plan, marketing plan, production, supply na kila kitu. Nikatulia na lile plan siku 5. Nikiangalia leak ziko wapi, udhaifu uko wapi. Though godfather was smart and all still he was not God

Wakija nawaonesha skype video call, recorded tulivoongea na ma boss wa Indonesiaaa. Kuna mambo makubwa yanakujaaaa. Makubwa sanaaaa. Makubwa sanaaaa! Itanyesha mvuaaa ya unga. Bomba kubwa sanaa la product, superior linakujaaa. Boss anakuja mwezi ujao na anataka kujua who is who is out. Sasa mda ndo huu. Siza anaingilia, na details connection kaipata jela, na wakati umefika, umri umefika wa Godfather kuwa na competitor. Kufuatia urafiki wao yey siza anampa chance, ila the issue is aseme kwa wakati huo huo anasimamia wapi. Na issue haijaliki ikiliki ni yeye ndo kalikisha.

Tumeongea nao, katika msafara wa mamba kenge hawakosekank. Tukapata watu wa 5 out of 50. Siza akazidi kufaaa, japo kweli wa 5 ni wachache ila mimi walinipa moyo. We are going somewhere. Siza anakufa moyoo hawa wote wa 5 ni viraka tuuu, hawana maana yoyote, hawako skilled ni mzigo tu kwa Godfather. Nikamwambia tulia.

Nikawaambia kuonesha commitment wakamuage Godfather live, live kwamba wanaacha waankuja kwa siza. Wakifanikisha ndo itakuwa deal. Out of 5, wakaweza wa 2. Nadhani mnajua by this time Siza yupo ICU. Kati ya skills na loyalty i always chhose loyalty. Nikajiapiza hawa viraka nitawapika watapikika mpaka watakapo onesha uwezo wao.

Siza akawa ashakata tamaa, kila mtu akawa anamuhurumiaa, anamuona kama kashikwa wazimu. Kila mtu anasema siza baaas tena. Anajiaibishaaa kabisaaa. Mda wa yule boss unakaribia kuja, na huku we are not making any progress.

Siza ashakata tamaa, na wale watu wa 2 nilitegemea wajute ila wala, wana moyo kuliko Sizaaa. Nikaona hapa hamna jinsi the heavens ruled in Godfathers favor. Ila sikupata shida sanaa, maana matokeo ya hivo nimeyazoeaaaa. Kilichonipa nguvu ni kwamba pamoja na yote Godfather nae binadamuuu tu, so lazima ana limitation zake.

Nikarudi kilingeniii. Kwenye ulozi, uchawii, gagulaaa. Kwa nilivomsoma Godfather mzunguu atakuwa hafanyi mambo yetu ya kiswahili halogiii. Nilikuwa nishapanikiii hatariii. Naenda kwa wataalamu ziadi ya 10. Namloga mtu mmoja tu Godfather. Nishapagawaaaa. Namloga afeeee. Maana bila kufaaa tusingeenda kokote. Mizizi yake mikubwa sanaa. Hapo najipa moyo waganga 10 wote wamshindwe yeye nani. Nimerogaa kwa fujoo fujooo. Hata kama ana roho 9, waganga 10 wanamtoshaaa.

Zikabakia wiki 2 yule boss aje bongo, Godfather mzimaaaa. Nikajua nimeliwaaa. Nikakata tamaa kabisaaa. Siku hio nasema kesho narudi kufundisha game over, napigiwa simu Godfather kaanguka Stroke. Ame paralyse upande mzima. Yupo mahututiiiii. Nikasema naam. Nikashindwa hata kurudi kushukuru maana sijii mganga gani kanirogea viziriiii.

Jioni hio hio simu zikaanza za watu ku decamp. In 2 days robo tatu ya watu kule kwa Godfather washa decamp. Kama kawaida nikasema sheria ya kudecamp hata kama Godfather yuko hospital wamataarifu kiwa wame decamp, iwe kwa sms, au wakamface hospital na waje na proof. Wengi walitumia njia ua sms. Watu kwa kufuata upepo. Ila wacahache wakabakia kwa Godfather.

Tukawa full mass nondo. Boss katua bongo. Ayaaaaaa! Kumuona bongo kazi ikawa imeishaaa. Kaongea na timu nzima, kwamba yeye na baba mtu sio wanataka tu kufungua bomba la product, wanataka kunyesha mvuaaa, tena gharikaaa ya ungaaaa. Watu woyoooooo. Utajiri umegika mlangoniiii. Watu wakaona ama kweli Mungu anawapenda, Godfather kapigwa stroke, huku connect mpya inaanza. Mambo bumper to bumper, Godfather to godfather jr.

Siza hapo yeye ndo anjifanya Man of the moment. Akaanza kabisa ku behave kama Carleone, mtu mwenye watu wake, boss la boss, Al capone. Mi niko pembeni tu, unnoticed. Yule mu indonesia akafatilia akasema kweli mtandao wetu mkubwa na mzitooo sanaaa. In the next 30 days watafungua bomba, na product itaanza kufika. Ila anataka mtu wa kuwekwa bond.

Kuwekwa bond interms unga ukiuzwa wasipolipa anachinjwa na consequences zingine. Nikamwambia Siza kakae bond wewe niachie show mimi, nimsambaratishe Godfather. Nipe mwezi tu, sihitaji miezi 6, tunalipa pesa zooote. Unarudi kama Alcapone. Siza akakubali kuondoka na wale wa Indonesia kwa ahadi ndani ya 30 days wanadondosha products.

Mi nikabaki kufanya maandalizi makubwa, kutengeneza masoko, kiparade ,mapundaaa. Kila kitu kilikuwa pakeeee. Na hivi nilikuwa na wa taalamu wa godfather haikuwa kazi. Maisha rahisi sanaa, have balls, take the lead and everything will fall in its place. Nangoja simu moja tu kuwa godfather kafa. Hata asipokufa kibiashara keshakufaaaaa.

ITAENDELEA USIKU SAA 4.
 
Naila mchawi mbwa kabisa[emoji19] [emoji19] ... Team Siza tunakisongeshaa[emoji23] [emoji23] [emoji23] .


Usitukane wakunga na uzazi ungalipo. Au kwa lugha nyepesi usitukane mamba kabla haujavuka mto!
 
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo. Au kwa lugha nyepesi usitukane mamba kabla haujavuka mto!

We mbona nahisi ni team Godfather wa chini chini. Hahahaaaa! Jitokezeee tu hadharani
 
Back
Top Bottom