Weekend Story! The Grass is always greener on the other side

The ones you love most hurt you most!

Kesho nakutwa narudiiii! Aiseeeee. Nimeamua nikirudi baas kazi ya punda basi, natafuta kazi halali kama kuchoma chips au kukaanga vitumbua ila upunda mimi baaas. Nimelichungulia kaburi live. Na kilichofanya nisife ni mambo ma 2, kwanza sijatubu bado, pili najua sisi mapunda tunaofia ugenini tunatupwa tu barabarani na kuzikwa na jiji. Nisingekubali shamba ninunue afu nisizikwe kwenye hilo shamba nibakie ku wa hunt wajukuu zangu wakinikera kama mzimu. Thubutuuuuu. Ill die another time, another day.

Nimestuka wahaniwekea bangili mwanawane, hio tayari kwenda central. Akaja Dr. nikamsomesha mimi nina hela nyingi sana tu, kwenye hii card ya bank, wewe nitibie taratibu, magonjwa yoote, nifanyie vipimo vyote kwa raha zako, sina haraka and most of all i can afford it

Basi polisi wakaja kunihoji, kuhusu cartel, organised drug deals. Mi nikasema siongei chochote bila Lawayer. Wakanilitea Lawyer ananishauri ni cut deal, nikubali charges wanipige mvua 15. Mjue mi sinaga akili nikaona nimuulize boss wangu. Nikawaza hii UK nikipiga namba ya boss au mtu yeyote kwenye oragnisation nitakuwa nishamchoma it will be stupid.

Nikampigia Ticha, cause i was sure she was clean. Nikaongea nae kwa mafumbo, nenda kwangu, vunja kitasa pale tulipotiana mara ya mwisho chini kuna diary, tafta namba ya yule mgeni mwambie mimi nimedakwaaa. Afu waha wavupumba wanamase nibakuli na kuwato lidi wapeni kamia miku na nota. Nijefanya? Zemuuli sibo nguwa nijefanye. Shoke kwalepe laje, nikijango sike indae kwa lapito.

Nikapelekwa jela, sasa jela ndo shambaaaa. Msione kwenye muvi mkajua jela ukiingia ndo unaliwa Tigo sijui nini sio kweli. Kwa wenzetu kuna sheria. Isitoshe mi Cartel, nimefika nikakuta wabongo kibaooo, wa kenya, wa rundi, wa zambia, Tukatambuana nikapewa ulinzi wa kutosha.

Mwanasheria anakuja mara moja moja sanaa, na namuona kabisaa yuko upande wa serikali. Hanitakii mema. Wale wanangu wakaniambia usi cut deal, ukikaa kimya unawaelekeza familia wanaenda kwa boss kuchukua pesa ya matumizi kama kawaida. Ukiongea kufungwa utafungwa, afu familia itateketea. Ila ukikaa kimya unakaa mda, ila kama likizo, familia wanapewa chochote kitu, isitoshe watalipwa hela yako ya awamu hii, na pia ukitoka unarudia kazini kama umri bado upo, kama umeisha utapewa kiinua mgongo.

Kiukweli bora ufungwe huku kuliko bongo. Huku kama niko likizo. Kazi ndogo ndogo tu kudeki vyoo sijui nini sio za mtoto wa kiume kulalamika. Misosi ya ukweliii, afu kila saa mnakula, gym kubwa, tv za kumwaga, kama niko likizo tu.

Isitoshe jioni ndo kikao cha dharura na wa Asia na Latin America kupeana connections za shamba. Wanakuomba wakueletee unga, malipo baada ya miezi 6. Bila kufingwa huwezi kuwa kingpin wa unga. Jinsi biashara ilivo the only place unapata intel ya kutosha kuhusu unga ni jela tu. Na unaaminika si umeshakutwa na mzoga, na umepewa mvua huwezi kuwa under cover.

Mpaka ma boss wa huko Asia wanawatuma watu wakajifungishe jela huko watafute wateja wa unga. Nikawa nachukua contact lengo nimpe boss Carleone, sababu tuna supplier mmoja tu, maybe tuwe na wengi, tuweke varieties za unga, tutofautishe grade. Haikuwa hasara kabisaaa.

Siku ya simu Ticha akaniambia ashapata visa anakuja kunitoa. Kapata ya mualiko wa Kanisa, yeye ni Pentecoste, so mchungaji kamfanyia mpango kanisa limemualika na sababu ni Ticha haijazingua. Kaja kuniona na mwanasheria. Msitake kujua ili cost bei gani. Mwana sheria nimemueleza akasema kesi hamna. Nikipanda tu mahakamani natembea. Nikajua ananipa moyo.

Kweli siku ya kwanza kupanda mahakamani kamaliza mchezo. Ilikuwa unlwaful arrest. Dr alibanwa na kiapo cha patient n dr privacy. Sababu nilimwambia mwenywe nina madawa, kujiokoa. Ingekuwa nimeanguka akajua yeye ningekula mvua za kutosha. Sikuamini kabisaaa.

Mda wote najua Ticha katumwa na Godfather na mpunga wote umetoka kwa Godfather. Tushamalizana na lawyer, kila kitu. Passport ishapigwa figisu kwamba mimi UK kuinhia ni mwikoooo. Tuko kwenye ndege, i am so exited kukutana na boss, nikampe ma connection niliopata, na mawazo kibao ya kuboresha biashara.

Nikamwambia Ticha navomjua Godfather atakuwa anatungoja airport. Mi Godfather mtu wangu kinomaaa nomaaaa. Akasema Godfather kiukweli mi niliwasiliana nae, kama ulivoniambia, nikamuuliza ufanyaje, akasema you should cut the deal, take the plea ufungwe masikaa 15. Nikaongea nae sanaa, akasema that is the best option. Nikamwambia kwanini tusifanye trial, inaweza kutokea loop hole, it is worth a trial, akagoma. Kiukweli mimi kama mimi nimejipa ruhusa ya kufanya trial. Godfather anajua you took the plea deal.

Nikastukaaa. Nikammind kwanini hakunipa msimamo wa Godfather? Kwanini alichukua maamuzi muhimu ya maisha yangu on my behalf. Wanawake ni nyokooooo. Unadiriki kwenda kinyume na Godfather bila wasiwasi kabisaaa. Does she have any idea what she has done? Nili mmind si kidogo.

In defence analalamika tu, kama hio ndo shukrani yako poa tu. Fadhila mfadhili mbuzi utamnywa mchuziii, binadamu wana maudhi. Do you have any idea niliko pata hizo hela za kuku bail out na kumlipa Lawyer. I got you the best lawyer possible and guess what? He is facking expensive. Nimeuza shamba la urithi mbarali, nimewadhulumu wadogo zangu haki yao, urithi wa baba yao, nimeuza nyumba 2 za urthi, just to get you facking outside and all you care is what your facking Godfather said. Do you have any idea ndugu zangu wakijua nilichowafanyia wadogo zangu watachonifanya? Fack you.

Na mimi nampa, i am cartel, i am insured, all you had to do is tell Godfather, and tell him right. Ume mmis inform purposely, i know Godfather, i have know him for years. Beach. Na yeye anakuja juu! Who gave shit that you will rote in prison? Me! Who put their life saving to save your stupi.d ass? Me! Who bailed you out? Me again! Right now i am your Godfather and you should be thankful!

Safari ilikuwa ndefu sanaaa, sanaaa. Maelewano hakuna kabisaa kabisaaa. Tumefika bongo nikamwambia ITS OVER! Kila mtu achukue ustaarabu wake. Akaniambia "Usinitanieeeeeee! Utanioaaaa, na utanioaa kanisani mbele za watu. Do you have any facking idea what i have done? Ni hivi as of nauza zile mali za urithi zangu na wadogo zangu, kuokoa korodani zako, i made a choice, kati ya ukoo wangu na wewe. Sasa sina ukoo as of now, sina ndugu, sina familia. We ndo ndugu yangu, wewe ndo ukoo wangu, wewe ndo familia yangu. Ukinizingua Godfather wont have to kill you, ill do him that favor. Kaa ukijua wea re too deep baby haina kuachana.

Na aliongea amenikazia jicho, hapepesi kope, there was no fear in her whatsoever. Yaaani! Mpaka nikawa mdogo kama piriton na kuamua maybe ill stick with her a little longer, atanichoka mwenyeweeee. Ataondoka bila kuaga. Yeye si jeuri subiriiii.

Nikaingia kwenye tax, nae akaingia. Ni mwendo wa kimya kimya mpaka home. Mwanamke jasiri huyuuu, anaweza kukuua usingizini. Tumefika kapika, tukala. Hamuwezi amini usiku ananishika shikaaaanataka mchezooo. Na mimi mchezo sitakiii. Yaani simpendagi na makila kitu ndo simpendi zaidiii.

Niliwaa,bia machizi narudi mpaka mda huo Godfather hajanitafuta. Lazima kachukia kwamba sikumfata maelekezo, nimefanya nilichotaka. Kama vipi nalalaje inabidi niende kwa Godfather usiku huu huu. Maana akijua nimefika na nimelala itakuwa dharau kubwa sanaa. Hata kama kachukia nikimpa niliojifunza kule yatakuwa safiii.

Nikaamka usiku huo huooo. Godfather analala mchana, usiku ndo mda wa kazi, kwetu sisi. Naila ananiuliza unavaa unaenda wapi? Nikamuuliza umenioa sasa hivi? Akajishusha nauliza kwa upendo, unaweza kukutwa na matatizo, polisi watanihoji nae ishi na wewe. Nikamjibu tu kwa Godfather. Akuliza kufanya nini? Sikujibuuu. Nikawa natafuta shati. Akaniuliza hio tatoo yako nimeangalia vizuri mbona ni namba ya simu. Demu smart huyu mpaka kero. Nikamwambia kwa hio?

Akauliza umepata connect unaipeleka kwa Godfather? Hutoki humu ndani labda uniueee. Myoni nawaza tu anaki beep kifo, your wish is my command. Nitakupiga leooo mpaka utafurahi. Nikavaa shati, nataka kutoka akaziba mlango. "Sikia Siza, dont be stupid, bila mimi your life was over, lets work together, i know umepata connect ya shamba, lets build the biggest connect in Africa amd ran Godfather out of business. Lets become Godfather and mother. Me and you! Me and you baby!

Nilichekaaa tu. Nikamuuliza kabla ya kuwaza kuwa Godfather, anza kujaribu luwa pusher tu ili ujue unaongea nini. Dont get ideas baby, ideas will kill you eyes wide open. Pisha niende kwa Godfather, dont you worry, God father mtu safiii sanaa, he will reward me kwa hii connection and couple of other ideas. Maybe nitakuwa subsidiary au distro, who knows. Aya wewe lala kesho ukafundishe wanafunzi wako.

Akadinda malangoniii, yuko serious nisitokeee. Kmaninaaa. Nilimpa ngumi moja ya tumbo. Akakaza. "If you have to go to Godfather you have to kill me first, i wont let you throw your life away. " Nikaanza kumpa kichapo, bumper to bumper, kofi to kofi konde kwa konde, nakoz tu nakoz. Akaanguka kisalimu amri. Nikapitaaa king kong, Iddi amin dadar, singa singa gabar singh, kubwa la maadui.

Nikamtext Godfather page nzima, najielezea tu why hatujafata alivoagiza, ila nina new intel that will change the business, new ideas, new techniques, new connect. Kama vipi tukutane in person nitampa hayo yoteee bila wasiwasi. Akajibu niende ofisini kwake. Masaki huko. Usiku huo huo.

Nimefika ofisini nikamkuta na watu wa 2. Mmoja tulikuwa nae kwenye chips na Leila mwingine punda mzeee, mtu mzima wa siku nyingi anaitwa Babuuu. Mtu mzima miaka 60 ila ndo machenii, hereni, ijana kama ndo anauanza leo. Milegezooo. Hivo yaani. Wakafurahi kweli kunionaaaa.

Nikaingia ofisini. Na bashasha. Godfather, akawa kapose tu. Ila nili note haniangalii machoni wakati sio kawaida yake. Nikamsalimia, na kumuomba radhi kuwa ticha ndo alikiuka muongozo wake wala si mimi na sikujua kabisaaa. Akasema haina neno, its better i am back. Nikataka kustick to business nianze kumwaga data. Akasema kuna mazungumzo kabla ya hilo. Nikawa yu free.

Akaniambia bwana kuna mwamke nataka nimuoe, niko nae sahiviii. Naishi nae. Kipindi haupo dogo mambo mengi yamebadilika. Nikafurahiiii kiroho safiii. Aaaah boss kubwa, finally umepata mwanamke maana kwako wanawake wote hawana thamani. Finally. I cant wait to meet shemela wetu.

Akasema mwanamke mwenyewe unaweza kuwa unamjua sijui. Roho ikafanya paaah, isije kuwa nishammega maana mimi siaminiki aminiki. Nikajikaza, hapana siwezi kiwa namfahamu, boss nilivotulia hiviii nitakuwa simfahamuuu tu, mtu mzima kama wewe? Akasema hapana, jankii tu, afu siniite mtu mzima nashevia panga mimi useme mtu mzima? Hahaahaaaaaa! Tukacheka sanaaaa.

Toka nije ndo akaniangalia machoni. Mwanamke mwenyewe unamfahamu ni Leila. Nikajikuta nimeulizaaa Eeeeeeeeh? Akarudia ni Leila. Mi nimeona sababu mmeshindwana na wewe ulimuacha nikaoan why not nisiwe nae, its not like unatoka nae or something. Nikawa kama akili imepumbaaa kidogooo. Natikisa tu kichwa kukubaliana nae. Then it struck me, huyu bwege alijaribu kuniuaaa, akajaribu kunifungaa sababu tu ya mwanamke. Mazafakaaa! Damn!

Nikamtega, lakini boss Ex are off limits, sema nini mimi yule hatujamalizana, nilimpa likizooo, isitoshe nishakwambia mi nampendaaa. Anakuja na hoja "Sizaaa, sizaaa, Leila hawezi kukupenda tenaaa, ushampiga nusu umuue, umemnyanyasa sana hawezi kutoka na wewe tena. Isitoshe wewe bado kijana, you still have a chance kupata mke. Mi mtu mzima. We Leila niachie.

Nikajikuta nasema sio fair boss, sio fair kabisaaa. Anakuja na ooh naelewa kuki compesate chukia subsidiary ya mozambique. Nikasema Sitakiii! Akapnda dau subsidiary 2. Nikamwambia boss i trusted you with my life boss! Why? But why? Ulipanga kuniuaaa, ukapanga kunifungaaa jela. But why? What did i ever wronged you to deserve this? Why? Na mwanangu je nae unamchukua? Akasema Siza you know Leila will never let you near the baby! Ill raise her well! Treat her like my own. Nikaona yota nyota.

Nilienda na gari ila nilirudi kwa miguuu. Nimetoka nawaambia wale boss sio mtu, wakauliza kwa nini nikawaambia. Wakagawanyika. Yule msela akawa upande wangu, akaniambia Siza utachoamua tuko nyuma yako, sio utu, sio fresh. Yule babu akasema yey yuko upande wa boss kubwa. Sio kwamba anakubaliana na alichofanya ila umri umeenda, anangoja tu kustaaff.

Nimerudi ndani, namkuta Naila anajikandaa. Jicho limevimba hatariii. Kumbe nilimpigaa sanaa. Nikakaa kitako na kumuita Naila! Akaitika beeee! Nikamwambia Let us be God Mother and Godfather. Nifanye nini, hata ukisema nile mavi nakulaaa. We have to run Godfather bankrupt and out of businesss.

Akastukaaa! Akauliza why change of heart? Nikamwambia tu alijaribu kuniuaaa na kunifungaaaa. Siwezi kumsamehe. Naila akasema anataka garanteee maaana hio safari ndefu sanaa. Asije achwa njiani. Anataka guaranteee. Nikamuuliza guarantee gani anayotaka. Akasema anataka NDOA.

ITAENDELEA KESHO.
 
Whaaaat! Naila pentekoste.....nimecheka Sana hii kipande. Siza alivyovurugwa akikataa ndoa basi tena. Ticha kajitoa wote ili Siza asipotee, Ni upendo wa namna gani huu? Episode imeishia patamu
 
Hahaa kama naona jicho litakavyo mtoka leila akimuona siza...ila mliochagua team mmna moyo sana hii jamba jamba siitaki kwakwel
 
Back
Top Bottom