Endings and New Begginings!
Mama Kijacho nikiwa nimechokaaa kabisaa, mwezi wa 7 jamani ndo maana mtoto anauma jamani, safari sio fupiii. Sio kwamba nazaa kwa kupendaaa, imenibidiiii. Nimekunywa mpaka dawa za kutoa mimba hii mimba imegomaaa. Kwa jinsi mimba ilivokuwa na roho ngumu sikuwa na shaka ni mimba ya Siza. Mimba ina roho ngumu kama mwenye mimba.
Nikapokea simu niliokuwa naisubiria kwa hamu kubwa. "Hallo! Ashafariki huyo mwana haramu?" Nikasikia not quite! Kuna good news na bad news. Which one should i start?" Nikamwambia anza na "Bad news" Akasema HAJAFA. Roho ikafanya paaaaaah! Nikahisi kama uchungu unanianza. Nikamuuliza good news je? Akasema kete zile kama ulivotaka Leila zilifungwa loose, absolutaley loosely na zimepasukaaa, basi tu ana roho 9 kama paka. Nasikia amejiwahisha hospital mwenyewe ndo kilichomuokoa. Ila Polisi wamemdaka na kwa UK hatoki leo wala kesho. Kwa volume ile ya drugs atakula ndoo hata 20 mpaka 25. Akitoka Leila una 50 au 55 years nini kimebakia.
Nikahisi uchungu umenizidiaaaa. Nikamwambia nakupigiaaaaa. Nikamuita Mama nasikia uchungu huku. Mama yuko acha kujilegeza uchungu gani miezi 7. Namwambia Mama mi nazaa huku. Akaja mbio. Kunipeleka hospital, nikazaa kweli kabla ya wakati. Mtoto Premature wa kike. Mzimaa kabisaaa. Alichelewa kulia nikaanza kupata shaka ila alilia.
Nesi akataka kunipa, hongeraaa, umejifungua mtoto wa kike. Nikafunga macho! Nikamwambia muweke huko. Akashangaa sema sababu nawalipa hela ndefu na niliwaambia wanichane operation wamenizalisha kawaida wasinitubue zaidi nitakua silipiii kabisaaa bili.
Sikutaka kumuangalia mtoto kwa sababu kubwa 2. Kwanza ni toto la Siza, pili nimetoka kufanya jaribio la kumuua baba mtu, na nitafanya tena jingine siku si nyingi, 3 sikuridhia tu kumzaa huyu mtoto, nikajua nikimuona tu nitamchukiaaa. Nikakaa kimyaaaa.
Akaja Vicky, Mungu mkubwaaa umejifungua prematureee, ila salamaaaa. Nikajua hajaambiwa umafia wangu. Nikasema eeh Mungu mkubwa. Bwana weeeeeeee. Ukafika mda wa kuletewa mtoto, na mimi simtaki, kumbe Vicky kamwambia nesi mlete. Yaani inhekuwa sina maumivu ya kuzaa pasinge tosha. Namwambia Vicky sitakiii mtoto kumuonaaa. Vicky anamletaaaa. Mzuriii mrembooo, jamanii, mama hakutakiii.
Nimevimba kama chatuuuu. Vicky ananiuliza sasa atapataje joto la mzazi, huyu njiti, lazima apate joto lako. Nikamuuliza wanaozaa na kufariki watoto wao wanapata majoto ya nani? Sikuwa na nia kabisaa ya kumuona mtoto. Vicky akamleta akaniwekea. Kanaliaaa, nikakaangalia, my heart melted! Kaduchuuuu kama kipanyaaa. My heart melted. The nikaamua i will always take care of it. Sitompaaa mtu mtoto wangu. She was mine and mine only. So inocent, maskini hatokua na baba, ila mimi natoshaaa.
Vicky ananigombeza tembeaaa, sitakiii, mama mwenyewe alitukana matusi yote ila kwa Vicky nilitembeaaa. Nikaka hospital sababu mtoto premature wamuangalie kwa ulinzi zaidi. Basi mama anasema ujue ulivongangania kuzaa na operation nilijua unatoa Tigo, kweli vile mwanangu, niliumia sanaaa, kwanini ufanye michezooo hiooo. Umezaa kawaida sasa nimejihakikishia hutoi Tigo. Mxiuuuuuuuuuu! Wa mama sa zingine hamnaaa hamnaaaa.
Mwenzenu kwanza sikuwaambia nimepata bwana mpyaaaa! Bwana mwenyewe mzungu, sio mzungu hawa ngozi nyeupeee nooo, mambo yake. Black ila amekaaa sana nje. Sio bwana tayari ila soon atakuwa bwana. Ama kweli kama una nyota ya mabwana una nyota tuuu.
Huyu bwana mwenzenu kutaka kumuua Siza, na yeye si alitaka kuniuaaa? Nikaelekezwa packer hawa watu wanaopaki hizo kete. Hela imenitokaaaa. Hela imenitokaaa. Nikaongea nae yule Packer amfungie loose kete Siza ili zipasuke afe, nisihisiwe mimi hata kidogo na nilipanga iwe siri yangu. Mpaka naenda nayo kabirini. Sasa tatizo ni akataka million 50 kwa hio, mimi nina million 30. Afu hapo mimba kubwa 6 months nisingeweza hata kumpa papa. Nikaongea nae weee. Akakataa kata kata. Nikaondokaaa.
Nimefika akanipigia simu kwamba kesho niende tena tukaongeee. Kesho nimeenda nikawakuta wa 2 na mwenzie. Basi walivoniona nakuja na tumbo langua wakaongea kama walikubaliana yule mwenzie ndo aongee peke yake huyu mpya sasa.
Akaniuliza kwanini unataka kumuua Siza? Nikajibu na yeye alitaka kuniuaaaa! Akaniuliza kwani wewe Mama Juma? Nikasema hapana mi Leila. Akasemaa aaaaahhhhh! Alizungumzia siku kwamba alikupiga sanaa akawa anahisi utaenda polisi. Akauliza still kwanini na wewe usimtafutie watu wakampiga na kumteka na yeye kulipa kisasi but Kifo come on! Nikamwambia mtoto, sitaki mwanangu awe na part ya kudeal na monster kama yule. Sitakiii. I want him dead as DEAD. After all sio bure naweka 30 million cash.
Akaniambia yeye anaitwa Carleone, ni packer pia, mwenzie alimwambia kuwa kainawa kazi yangu ila yeye yuko tayari kuifanya. Ila hataki pesa. Hata 100. Niakstukaaa nikajua atanifanya punda sio bureee. Niakmuuliza unataka nini? Akasema hapendi wanawake wanyanyasike, mama yake kanyanyaswa sanaa so he do Siza for me for free. Mmmmmmmhhhhhh! Ila nikizaa mtoto wa kike Mungu akinijalia nimuite jina la mama yake Antonia. Mjina mbayaaaa ila for 30 millions siwezi kukataaa. Niakubali fasta fasta. Akanipa namba yake. Akachukua yangu. He had this class oozing over him, the way he talked, he sat, saa aliovaa, kiatu, nguo. Afu kidogo mtu mzima 40s hivi amazing. Alinitegaaa. Isingekuwa mtumbooo huo, ningechangamkia fursa.
Akawa ananipa updates, safari lini, ashameza, ameenda airport, kila kitu. Hili jina la carleone nalijua ni la muvi ya God Father, hawa drug dealers wa bongo wote wana obssesion na MAFIA movies. Kama Siza anajiita the Don, huyu nae Carleone. Watajijua wenyeweeee.
Mtoto kweli nilimuita Antonia. Japo bibi aliumia sanaa, sanaaa, mjukuu kupewa jina la kikafiriii. Carleone akawa anakuja hospital kuniona, mama ananiuliza kila saa huyu ndo mwenye mimba? Nikamjibu tu ndiooo. Manake ningemjibu nini. Bibi mbishi yuleeee, siku aka mtight kwenye corridor, samahani Baba yangu kidogo nataka kuzungumza na wewe! Carleone akasema sawa mama unasemaje? Mama sasa "Baba mimi nina malalamiko, sijajua wenzangu uzungu uzungu wenu unaendaje ila mimi Muislamu, Leila Muislam, mimi ndo mama yake mzazi, nimemzaa kwa tumbo langu, sasa baba hivi unavokuja hospital unanisalimia juu juu, unakoseaaaa. Sisi wa Africa, kwanza umemtia mimba, ukawa huonekani, mimba nimelea mwenyewe ile, sahivi unakuja unajifanya hunioni, baba mi sipendi hivoooo. Kama umeshindwa kufata taratibu za kutoa posa kumuoaaa, basi hospital usijeeee."Khaaaaaa! Bibi nuksi kweliii. Carleone akamjibu tu samahani mama kama nakukwaza. Leila kakwambia mi ndo baba mtoto? Bibi alastuka "Kwani sie wewe? Leila muongo muongo mda mwingine" Alivoona tahayari na jinsi alivokunyaa akahisi atapata pressure. Akamwambia "Ndio mimi, nitaleta watu wajitambulishe kwenu. Na nitamuoa Leila kwa heshima kabisaa. Nipe mda kidogoo niweke mambo sawa. Si mnajua nyie Waislamu kumuoa mwanamke ana mimba ni dhambi? Ni sawa nakuwa nimewaoa mama na mwanae. Nipe mda. Bibi akafurahi, asante baba, usinifikirie vibaya kuuliza unue imenibidiiii, sio kwa nia mbaya lakini sijui nini. Wakaagana pale.
Akaja kuniambai Leila, mwenzio nimembana korodani leo! Nikastukaa mwenzangu yupi? Huyu mzungu mweusi Kalion. Nikashika kichwa. Umefanyaje? Aaaah nimemuuliza anakuoa lini? Adabu agani anakuja hospital kibabe. Nikachoka mwili na roho. Nikauliza kasemaje? Kasema nimpe mda tu. Nikamuuliza umefurahiiiii? Akasema ndio nitaacha kufurahi. Ujue wewe ndo umewafungia wadogo zako kuolewa, ukiolewa wewe na wale wote wataolewa. Nimefurahi sanaa. Ningekuwa kafiriii ningekunywa biaaa. Mxiuuuuuuu! Bibi Antonia hanaaa.
Nikaanza kumtumia sms Carleone, i am so sorry for everything, imenibidi kudanganya cause ya situation nzima, i am sorry i had to drag him in all this issue. I can be more sorry. Akasema usijali, i understand. Nikajua tu na uzungu uzungu wake yule ndo nishampotezaaa. Si mnajua wazungu weusi wanavojitia wana principle kuliko wazungu wenyewe. Kwanza kifunga unga tu, hata asinizingue. Nishajua nimempotezaaa.
Jioni hakuja, nikajua baaas. Kwanza maisha yanaliwa tigo yaniwie mwepesi hivo nina mimba ya miezi 6 nipate bwana hivi hivi, maisha mnayajua mnayasikia? Nika bull shit tu. Nikimuangalia mwanangu napata farajaaaa. Hajui ubaya wa binadamu maskini.
Asubuhi yakaja maua, nikajua Vicky, Vicky nae mzungu mzungu. Sikusoma ki note. Akaja babu siku hio, kumuona mjukuu. Bibi anamwambia kuna Mzungu mweusi anaitwa Kalioni. Babu yuko Kalioni takoniii au yeye ndo haelewiii. Nikamwambia Dad, anaitwa Carleone. Babu yuko mtajua wenyewe na makalio yenu. Babu akachukua ki note kwenye maua. Akaona C a r l eone. Aaah Kaleoneee. Nikashtukaa kujua maua yametoka kwa Carleone. Babu akaondoka.
Nikasoma kile ki note. Kimeandikwa japo nimesafiri, ila i think of you every day. Mmmmmh! Nikawaza ulimwengu unanilipa fidia nini kwa kupigwa na Siza? Unajua Ulimwengu ukikufanyia jambo baya sanaaa, unakulipa jambo zuriii sanaa baadae. Ndo umeniletea Carleone.
Siku tunatoka Carleone alikuja kituchukua. Na Vicky alikuwepo. Akamuona Carleone mara ya kwanza. Sikumwambia Carleone ana paki unga. Nishaamua sahivi nakomaa na huyu huyu carleone. Tutaishije atajua, yeye si mwanaume, atajua kwa kupaki huo huo unga tutaishi. Isitoshe nimeshazaaa sahivi, siwezi tena kudangaaa. Kama shimo diameter zitakuwa zinasoma za kutoshaaa sichekani na vicky. Na naijua stress ya kudanga au ku date una mtoto. Nikaona hapa hapa kwa Carleone nishaona ananipenda kidogo ill make hio hio kidogo i work. Hata kama tutakula nyasi mradi heshima iwepo basi, isitoshe nina mtoto hana baba, nachoringa kitu ganj.
Hata kama tutakuwa hatuna hela nyingi, mwanangu ana baba, afu Carleone mtu mzima 40s huko nimemuuliza an mke hanaa, sitaki mambo mengi. Kabla sijazaa nataka mwanaume mwenye hela, kazi nzuri, masters, majumba, gari za maana. Baada ya kuzaa nataka tu mwanaume awepo wa kusaidiana kulea yule mtoyo basi. Hahaaaaaa! How priorities change over night.
Kwanza kaja na bonge ya gariiiiii. BMW X6. Tukapanda, mama ananipa doleeeee, umepatia mwanangu. Huku huku kunafaaa. Vicky nae anani text hapa shogareee sio pa kuachiaaa shoga angu. Namwambia gari ya boss wake. Mi namjua huyuuu. Ftee P hana lolote. Akashangaa Vicky. Yupo basi mi mnikutanishe na boss wake nichuneeee mahelaaa. Hahaaaa.
Kufika nyumbani namkuta dada, mama kamleta, ananiambia ushapona miezi mi 3 sasa, mi narudi kwangu. Nikamshukuru. Maana huko kwake hakai, kazi ya ukungwi imenogaa. Anaenda mpaka Dubai, Us, Uk kufundaaa. Utamtakaa. Na mimi ndo uzazi nipumzike kufundaaa kwanza.
Carleone anakuja kila siku, we were dating kabisaaa, sema ndo kumpa mambo nilishindwaa, nampaje wakati nanukia mtoto siku nzima. Bora mtoto angekuwa wake, toto la mtu mwengineeee. Nikawa nashindwaaa. Uzazi sio mchezooo. Nikasema sizai tena ngoooo. Huyo mwanaume nitakae mzalia sijui anipe nini sijuiiii. Ila i am no longer going to go with this process again. Huyu mmoja ananitosha.
Isingekuwa huyu mtoto Carleone nishamtekaaa siku nyingiii. Mtoto gharamaaaa. Kutokana na kuzaa kabla ya wakati na complications zingine sikunyonyeshaaa. Maziwa yalikuwa hayatokii hayatokiii. Gharama zikawa kubwaaa sanaa, hospital tumekaa miezi mi 3 hela inatokaaa tu. Biashara ikayumbaaa si nikawa sifatiliii, sikufata mzigoo, uliopo ukaishaaa. Hela bank kutoa kutoa toka niachwe na mkinga zikabakia za ku back up mtaji tu. Nazo ndo zilizotusaidia hospital. Nikauza gari zote 2. Bado nikawa nimenasaa. Niko ndani naleaa. Na ukoo mzima wanamtegemea leila. Pusher kumuomba pesa siwezi.
Nikabakiwa na shamba la miti tu beka 10 la mkinga imefikia kuvunwa. Ambayo nikapanga mtoto akikua kua naenda kuuza mbao, napata mtaji wa backup, naanza upya biashara. Sasa hapa kati mtoto anakuaje. Nyumba moja wanakaa wazazi siweiz kuiza. Ya pili ya mwanangu siwezi pia kuiuza na kiinua mgongo cha usichana wangu. Ikafika mahali hali ngumuuu. Kodi nadaiawa, hela za maziwa sinaaaa. Nilijiapiza nikizaa, shopping Dubai, mwanangu atavaaa mpaka kufuru. Wapi, maisha yananifi**** tu mwanzo mwengaaa.
Nikashindwa uzalendo. Nikamuandikia pusher sms. Samahani kwa hii sms. Najua umekuwa mwema sanaa kwangu, ila nimekwamaa nimekwamaa. Naomba ukija uje na maziwa ya mtoto. Mmmmh! Nikafuta Mtoto maana sio toto lake. Nikaandika uje na maziwa ya Antonia sina hata 100. Ukiweza na pampers na wipes nitshukuru. Samahani kwa kukusumbua. Nikatuma. Haikujibiwa.
Nikawa nawaza nilivochezea hela mimi. Nikasema Siza huko jela wakule tigooo sanaa, rectum yote ibaki wazi. Sio kwa kuniharibia maisha hivi. Nikawazaaa nikaamu niende kwa Mnyalu kumpigia magotiii, najua mnyaluu hata asiponisamehe atanipa 50,000 ya kula. Nikaoga kabisaa, nikamuandaa na mtoto, nikafika nje, nikakumbuka sina gari tena. Naendaje sasa na yule mtoto. Afu mtoto mwenyewe delicate sanaa. Kazaliwa kwa tabu sana. Nikawaza niende kesho mwenyewe.
Nishamkopa vicky mpaka basi. Naona aibu kumkopa tena. Dada ananiambia mtoto analia maziwa yake yameishaaa. Nikampigia Fupi. Nikajielezaa. Fupi akanitumia 300,000 nikahemaaa. Nikanunua ,aziwa kopo 5 na pampers. Nikampigia Dr. Huyu Dogo hajafika kunywa uji huyu miezi mi 4. Vicky anasema badooo.
Jioni nikawahi kulala maana usiku kukesha. Pusher alikuja akaleta mavitu kibaooo. Ma carton ya maziwa, mi pampers, wipes, nguoo, mpaka bembeaaa, toys, shopping ya maana hatariiii. Nikafurahiiii. Sikuaminiiii. Nikatuma sms ya kumshukuru. Sasa mchana fupi alaja mchana kujitengenezea mazingira ya uchi, si katoa lki zale 3. Akakuta ma carton, dogo msafiiii nguo mpyaaa nimevisha, akajua sijachoka hivo alivotege,ea. Angejuaaaaa. Ila hakupendaaa.
Nikamuuliza Vicky mtu akizaa siku ngapi hatoi uchi. Lengo nataka nimpe karleone uchi, maana nishaona bila uchi kuhusika malezi yangekuwa magumu. Sio baba yangu mzazi yule. Aleee toto sio lake bure bure tu. Ila akinila mama mtu sio kesi sanaaa. Vicky akasema skku 40 tu. Nikaona kumbe mi mzimaa kabisaa niko fiti kurudi kazini.
Nikamtumia text, asante for the shopping, tunashukuru na Antoniaaaa. Leo tunaomba uje dinner kwetu. Nikamwambia Vicky naomba Antonia na dada waje kwako usiku tu huu wa leo. Najua wewe Dr. Utamuangalia Antonia vizuriii. Mama Antonia anatafuta kodi leo. Najisemesha sijui nitambemenda antoniaaa sijuiii. Si anyonyiii yule. Vicky anasema kubemenda hakupo ni just malnutrition . Hahaaaaa! Kutaziba huko chiniiii. Welcome to Single mothers world.
Usiku kaja Carleone, ikumbukwe mimi ni Leila yule yule, sio mpenzi wa kupika sijui, jiko, walaaa. Dinner ni drinks tu niliandaa na snacks. Akaja basi tunaongeaa tu, tunaongeaaa. Nikawaza hapa Mama Antonia ndo unadaiwa kodi, Antonia anataka kula, anataka kuvaa, anataka kuishi pazuri, umefilisika umebakiza uchi tu, usipojasiria uchi imekula kwenu. Nikahisi shuzi limenibana. Nikaenda chooni kujamba.
Uzazi umenibadilisha kabisaaa. Kwanza nasita wakati zamani ndo profession yangu. Pili nimezeeka, na kukondeana kwa stress, sina uhakika na mvuto. Dawa ni kuzima taa tu usiku kucha. Nitajikaza, nitamfata pale. We were friends, we just talk, tunaheshimiana, sasa hizo heshima ndo zikawa zinataka kuniua mimi njaa. Nikasema leo najikaza. Kwanza nguo navulia huku huku. Nikifika pale nam time nazima taaa kabla hajaona mwili ulivokongoroka. Nikishazima taa napata confidence.
Nikakumbuka Leila mimi Leila haswaaa, chozi likanitoka. Nimefikia hatua ya kupiga mahesabu ya kuzima taa, nitoe papuchi kwa maslahi madogoo kwa mtu mdogoo kama Pusha. Ingekuwa enzi zangu ningekuwa nisha deal na boss wao kitambo. I am reduced to nothing, absolutely nothing, nahangaika na The Help, sio The bosses. Life is really a bitch. Nikavua nguo, nikabakia na chupi na sidiria. Nikaenda tena kwa kukimbiaa, kuiwahi ile switch ya taaaa.
Alishangaa yule kaka, aliona mambo ya ajabu sanaa. Mtu mzima kama mimi 30 yrs naikimbiza switch Mmmmh! Kupatwa kwa Leila mama Antonia. Nikiwaza ukizaa K inakuwa kubwa, nachokaa kabisaaa. Mara anile aone K yangu kubwa si balaa hivooo. Mbona maisha yaninyanyasa hivo lakini. Yana nilia Tigo kavu kavu bila Ky hata mate jamani. Nikajikuta nimezima ile taa, nimekalia tu nime stuck nawaza mara Kkubwa, mara maishaaa, i was just stuck
Yule mtu mzimaa, akajiongeza huyu mpaka nguo kavua mwenyewe, anataka nimpe mambo, Kama mjuavyo Carleone mzungu wa roho, anauliza are you sre this is what you want? Moyoni nawaza maisha yanavonipenya wewe baba what i want in hata umuhimu baas. We nile unilipie kodi baasi sina hata mengi. Huku najitutumua kuliza, Dont you want this? Kumtegaa tu. Hapo mikono ishaanza kutamba. Hapo ndo nilipokuwa napataka mimi.
Si nipo kazini jamani. Nikataka kuonesha mbwe mbwe nikakumbuka huyu mtu mzimaa, hataki madoido sanaa, mambo kiutu uzima zaidiiii. Basi mtu mzima mwenzie ndo mimi. Mambo taratibuuuu. Afu huyu baba mwenzenu nilikuwa nishampendaaa. Maana hakuna alichofanya extra ordinary ila roho yanguuuu kwatuuu. Sijui wema wema wake, roho yangu ishampa kibali. Hata akinigusa tu hivi kama napigwa na radiiii. Hahahaaa! Ama kweli pesa kiboko ya wanawake.
Nikamwambia twende chumbani, kiutu uzima zaidiiii. Si mnajua tena umri miaka 40 na anaikimbiza 50 sarakasi za kwenye makochi awaachie kina Siza. Nilitegema sababu mtu mzima show itakua ya kizembee so sikujipanga sanaaa, kilichonikuta ndugu msomajii, kama sio ibia ibia za maneno ya kungwi ma wili ma 3 nilikuwa najiaibisha.
Nilisahau with age comes experience. Mtu hafanyi vitu kwa kubahatisha na mazoea, ana experience. Anafanya kitu anachokijuaaa. Afu kistaarabuuu. Sio mechi ngumi, sarakasi. Anafanya hizi hizi za kawaida ila yeye si experienced anakuwa strategic, Hata akinyonya chuchu anajua jinsi ya kuinyonya sio vijana mbwembwe nyingiii hamna lolote.
Akaiona ile cheni, nikasikia sitaki uvae huu uchafuuu tenaa. Nikasema sawaaa. Aliikata kwanza akaitupa kule. Mmmh! Nawaza baba wewe Gold hio, urithi wangu wa ujanani. Mambo slow but sure. Nili ji enjoy kwa kweli, japo lilikuwa pambano la kikazi. Ikafika mahali nikasahau kama pale nipo kazini nikajikuta nasikiliizia utamu, badlaa nimpe mtu mzima utamu achomoe hela za kodi ya watu. Tukalala mpa asubuhi wote. Usiku akaniuliza dada na mtoto wako wapi? Nikamwambia wameenda kwa bibi mara moja.
Asubuhi na uvivu wangu wote niliamka kupika chai, akanywa akaniaga anaenda kwenye mambo yake. Kila akija ana ile gari, nikajua kahamishwa Packer kafanywa dereva. Basi nilioga saa zima, kutoa janaba, mama tena. Dada akarudi. Nikamshika mtoto hajalia wala nini. Nikasema wahenga na nyie kututia jamba jamba kmanina zenu, au nikawaza huenda anajua mama ake nakomaa nipate kodi ananione imani tu.
Akatuma sms anataka na leo aje tena. Vicky si atanichokaa. Nikamwambia njoo. Nikaamua mtoto mwenyewe wa zinaa, atalelewa kwenye zinaa hio hio nifanyaje sasa. Tutalala hivo hivo akibemendeka magome ya mwembe yapo nitamuogeshea. Nikazungumza na dada, kiutu uzima tu, hali ngumu sahivi mdogo wangu, atakuwa Carleone anakuja kulala hapo atusaidie maisha. Umuheshimu kama baba mwenye nyumba. Dada akasema sawa dada.
Usiku kaja, kapata msosi, kaingia master bedroom. Hapo nishamuogesha ANtonia uski saa moja ile. Nimemshindilia maziwa, najua kuamka hapo saa 7 usiku. Kama kawaida mchezo nikatoa tenaa bila ugomvi, na mwanangu kalala kwenye kitanda chake hapo pembeni. Naomba tu asije kulia kati kati ya mchezo maana itabidi tu niinuke nimpe maziwa yake. Ndo nikajua i was so so mean to single mothers all these years, hutles za kule kama ndo hizi acha mama aitwe mama. Hakulia. Nikamaliza kutumikaaa na mtu mzima, nikaoga zangu, nikasema nisinzie. Kulala moja kwa zote. Kustuka saa 2. Mtu mzima kashaondokaaa. Kumuangalia Antonia kalala, kabadilishwa pampers, chupa tupu kwenye kimashine, imebakia kidogoooo. Aaaaaah! Mama huyu, aibbuuuu. Anaelemewa.
Akaja Ijumaa tena, nishampanga dada wewe ukiamka asubuhi iweke hii barua ya kudaiwa kodi mezani, juu weka funguo yake ya gari. Jifanye katika usafishaji tu, ila hakikisha aniona hii barua. Dada akasema sawa dada. Mi nimelala jmosi hio nawaza sijui kafanikisha. Nikaja kumuuliza vipi aliisoma? Dada akaniambia kaisoma. Kaipiga na picha kwenye simu yake. Huuuuuu! Sijatumika bure.
Akawa anakuja chakula analeta, na matunzo ya mtoto analeta, ila ndo natumika hatariiii. Akija anataka mchezooo, na siku hizi zikiisha siku 2 hajaja sio yeye. Jioni akaja akasem akuna barua nimeoinaaa, nikamwambia ndio kama ulivoona mwisho wa mwezi ujao, mi sijui tunafanyaje. Akaniambia usijalii, nitasimamia show nzimaaa. Nikaanza kujikoshaa, i know you are not making much katika hio kazi yako, sipendi kuwa mzigooo, soon ill be going out mtoto kakua huyu tutasaidiana, nivumilie tu kwa sasa.
Akasema you wont be going, never, we kazi yako ndo hii kukaa nyumbani kulea, soon watoto watakuwa wengi, utakuwa busy usijali. Khaaaaaaaaaaa! Huyu vipiii. Nikamwambia mimi i dodnt what you are making ila i assume not much, siwezi kukaa hivi hivi, like i said i will be going out, i always have been taking care of myself, thanks for taking care of us, ila look at the bigger picture. Akadakia ushasema you dont know how much i am making so dont assume. Kama nilivosema you will never be going out to work, hustle, maybe ku enjoy, your work ni hii ya kulea, na watoto wataongezeka. Zamani ulikuwa una hustle cause you didnt have a man, ulikuwa na vibwanaaa, vivulanaaa vinakufuja fujaaa, havijui samani ya mwanamke. Now you a have a man, me, utapata kila kitu, kila kitu unachotakaaa, all you need to do is love me with all your heart. Nikabakia Khaaaaaaaaaa! Moyoni. Kodi naitakaaa, kujibu natakaaaa. Nikamuepusha shetani sikujibuuu.
Akalipa kodi ya miezi mi 3, akasema tutahama hapa soon. Ikumbukwe sina hata 100 japo kupelekwa sipendi what choice did i have, ndugu msomaji what choice. Sikuuliza hata tunaamia wapi. SIkutakaaa ningezidi kupasukaaa tu. Akasema ofisni kuna party inabidi twende wote. Akanipa hela kabisaa, usuke, ununue nguo nzuriii, decent, upendeze, tunaenda wote. Mmmmmmhhhhh! Nikaenda saloon na bajaji, kusukaaa. Najua walisema sanaa, Leila anapanda bajaji hata ki Vitz hanaaaa.
Sikutaka kununua nguo bongo manake hamkawii kufanana, nikaend atu kupima size kwenye maduka, nikaagiza mtu yupo nje anitumie na ndege ya kesho yake. We kuja kuivaaa, nilitokaa nyokooo. Na kiatu nikanunua hapa hapa. Na ile nywele hapo bado haijabanwaaaa. Nikikumbuka nimeambiwa mimi wa kuzaa hovyo na kulea woatoto nasikitika tu huyu bwana hatutodumu kwa mambo madogo sanaaa. Ngoja nipate hela ndo atanijuaaa.
Siku yenyewe kaniambia jiandae mapemaa saa 2 sherehe inaanza. Best yangu anaoa. Sasa jivute ifike saa 2 haupo tayari nakuacha. Mpaka saa moja na nusu niko saluni mwenzenu. Akapiga simu. Akasema usinitanie naleta nguo na viatu huko huko saluni. Mi nilikuwa saluni sitaki wamuone wasijue nime downgrade mtu mzimaaa niko naye afu huvyoo tu, we umri ule bado ana paki ungaa, bora Siza pundaa. Mi sipendi mambo madogo mwenzenuuu. Ila ndo ahsaamua. Kupaki X6 wote wakapagawa. Akaleta nguo na viatu. Nikaoga na kuvaa, wakanipaka na make up.
Leilaa kama hujazaaaa, Leila umezidi kunogaaa, Leilaaa. Na mtu mzima hajaniona nikiwa nimevaa nguo nguo hizi za kawaida, ananionaga na dera tu. Hapo nimepiga minooooooooooo, kiminoooooo cha hatariii. Naonesha guuuu. Kuniona waoooh, nikampa mabusu pale najua tunaenda tukapaki botic. Vipi baba? Kachukue nguo nyengine, hilo vazi halifai. The hair and shoes okay, dress too short. Nyooooooo! Nikagomaaaa! Kma safari ifeee. kupangiana mpaka mavazi. Mxiuuuuu.
Akasema Leila mi si nakulipia kodi, nakulisha, nakulelea mwanao, unashindwa kuniheshimu kubadilisha tu nguo? We mwanamke una kiburiii kibaya. Mi mtu mzima siwezi kwenda na wewe sehemu uko wazi wazi hivi, watu hawatoniheshimuuu. Jitahidi kuelewa sahivi uko na mimi mtu mzimaa, sio vivulana vinavokutembeza uchi uchi. Nakaona kelele zimezidi nikaingia huko Botic, nachukua nguo hata siangaliii, nishatibukaaaa. Mdada ananiuliza nguo gani? Najibu yoyote mbayaaaa iliopo, linda duka iliokaa dukani miezi 17, nipe hio hio. Kumbe kashuka yuko nyuma yangu ananisikia. Hata nilivojua kasikia sikujali, nishachokaaa mie.
Akachagua yeye nguo. Nikaenda kuvaaa tu baasi tu yani sababu sina economic power, nalelewa na mwanangu kama alivosema. Hata sijajiangalia, nimetoka hivo hivo. Yupo waooh, waooh, this is more like it blah blah blah! Nishatangulia kwenye gari akalipia ile nguo. Kuja anasema take a photo, nimevutaaaa domo hatariii. Akawa anacheka tu. Kwenye gari ananimbia cheki Dp yangu. Nikakuta kaweka ile picha domo limevutwaaa hatari. Moyoni nikasonyaa tu, like anybody cares Dp ya Drugs packer mzee amewekwa nani.
Ikaingia sms, " Leila kmanyokooo mbona upo DP ya God Ftaher! The Don Himself! Tajiri la unga lenye net work yake Khaaaaaaaaaa! Sikuweziii we malaya na kuzaa kote huko bado unakula vichwa vya maana na kupanda ngazi! shoga usinune cheka mpaka jino la mwisho" Nikaona mashikolo mageniii kama simuelewi, God Father namfugaaa kwangu, kalipa kodi miezi mi 3 anataka tuhamie shamba, God Father huyo kigegooooo. Kwanza namba siijui ukute huyu huyu mtu mzima hovyo ananichota tu akili. Nikasunyaaa tu.
Mtu mzima ovyo akaniuliza Leila umenisonyaaa? Nikasema sio wewe bwana si umesikia kuna sms imeingia huku, ndo naisonyaaa. Akasimamisha gari pembeni. Naomba nione hio sms. Tobaaaaa! Nikasema sikupiii. Ila nakusimulia. Kuna mtu ananijua back in the days sasa anafikiri mimi Leila yule yule wa zamani, ndo nimesonya cause i am changed. Akadakia naomba sms niione. Daaaaaah! Kufugwa ni utumwa. Nikatamani nibamize simu nje, ila kwa hali ya maisha ilivo sasa nitatumia kitochi. Nikampa kishingo upande.
Akaisoma, akauliza kwa hio umesonyaaa cause umejua mimi sio God Father, unanisonyaa kwa dharau kubwa Leila. Kama alikuwepo kwenye nafsi yangu angeona napigia vigele gele maelezo yake Aleleleeeeeeeee. Nikaingiwa imani kweli pamoja na kuwa mtu mzima ovyo, he is nice to me and my daughter, he has been nothing but nice to us ever since we met. Nikaweka kibri pembeni, nikaanza kujikosha.
No, nimesonyaaa cause watu wanaangalia mambo tofauti na mimi. Wao wana focus kwenye ma God Father sijui ma boss, to me, hata kama wewe ni packer tu, una pack pack madawa, kwangu na Antonia, wewe ndo God Father wetu, unatujaliii, unajali tuna sehemu ya kukaaa, unajali Antonia anapata mahitaji yake, unajali tunakulaaa. I will never exchange you for any God Father in the world. Wewe ndo God Father wetu mimi na mwanangu. Na nilicho sonya ni kuwa people focus on the wrong big things always na ku over look important things. Nikampa mate fasta fastaaa, one big happy family.
Hakusema kitu. Nikawa sasa mimi nilienuna mwanzo najisemesha. Hii gauni nzuri sana, Thank you for the dress. Mambo ya ajabu ajabu tu. Tukafika ukumbini. Nishajua we are no bodies. So sikuwa na mshawasha.
Kuingia kila mtu yaani kila mtu ana tuangaliaaaa sisi. Nikajua labda nimependeza sanaaa. Tukaenda kukaa high tablee. Kila nikigeuka mbona kama sisi ndo center ya attention. Mama yangu. Nikasema labda kwenye hii harusi huyu mtu mzima hovyo ndo ana kiuwezo kiuwezooo. Sikupatiliza sanaaa. Ikaja utambulishooo. Akatambulishwa Boss wangu. Nikajua kwa ma packer nako kuna vi boss. Kila mtu anaekuja lazima aje atusalimie atupe mikono. Mpaka mkono ukaanza kuuma. Nikamwambia mi nawahi nyumbani kwa mtoto we kaa, nitachukua bajaji. Akamuita Ommy mpeleke wife kwake afu nilete gari. Akasema sawa boss.
Ommy kila kitu karibu mama, tunaelekea wapi mama. Nikamwambia Ommy punguza bangi, mama mi naweza kukuzaa? Akachekaa. Nikamuuliza mtu mzima anakutisha we mtu mzima yule bado ana paki vitu anakutisha nini. Akastukaa, unataniaaa uko serious hujui? Nikamwambia sijui nini? Akasema huyu ndo God Father, ndo mwenye mizigo yake, ndo mwenye pesa yake ndefuuuuu. Usimchukulie poaaaa hata kidogooooo. Wallah la adhim dada nakwambia. Nikastukaaaa, na kutetemekaaa. Ina maana kama huyu ndo God Father, na mimi mwanamke wake that makes me God Mother. Nikadataaaaaaaaaaa! Finallly finallly niko kati kati ya mapesa ya ungaaaaa. aleleleeeeeeeeeeeeeeeeee. Nitawanyoooshaaaaa. Watanikomaaaa. Watanitambuaaaaa.
Nikamwambia Omary muongo bwan sio. Akanionesha chat za group, na kweli namba ya mtu mzima ovyo ndo imeandikwa GodFather, na woote woote wana mtetemekea boss wao. Afu Leila hapa ndo nambadilishisha pampers za toto la punda wake, na kumpa maziwa usiku kucha. Woga ukaiiingiaaaa. Nikawa mdogo safari nzima. Kuingia kwangu nikaban kufuli kila mahali. Sikujua ni bahati au mkosiii.
Nikawaza nikaona picha zima, nilivoenda kumpa yule packer wa mwanzo mchezo alimwambia boss wao, ndo akaja nae, amuoneshe mimi, siajabu walitaka kuniuaaa wale bila mimi kujua. Ndo maana aliniuliza kwanini nataka kumuua Punda wake. Na ndo maana alikataa hela. Yeuwiiiiiiiiii. Nikamuasha dada, nikamwambi twendeni tunahama susiku huu huu kuna matatizo yametokea.
Tukaenda kwa Vicky. Sikutaka kumwambia angetufukuzaa. Nikamwambia tu tumegombanaaa. Usiku saa 8 anapiga simu sipokei. Akatuma sms umeenda wapi nimekuta mmefunga kufuli kwa nje ya gate. Sikumjibu. Akapigaa tenaaa. Mara akaanza kugonga kwa Vicky.
Nikajikaza nikatoka, nikamwambia Vicky shoga angu nisiporudi piga simu polisi ila msitoke nje please. Nikaenda, anauliza mbona mmeondoka nyumbani na watoto bila taarifa, hivi una akili kweli wewe? Nikamwambia tunashukuru kwa msaada wako ila kuanzia sahivi hatokuwepo kwenye maisha yetu. Alichotusaidia Mungu atamlipia. You lied to me Carleone, and i cant trust you with my girl anymore. You lied to me all this time. Just Go.
Anakomaaa now umejua ukweli ndo unipende zaidiii, uninganinie ili unufaike. Nikamwambia No, mi nilikuwa nampenda packer huyo mwingine mimi hapana nawaachia wenzangu. Nikarudi ndani. Kumbe Vicky anasikiliza, akanidaka yule kaka ni nani Leila? Ni nani mpaka umetetemeka kiasi hiko? Ni boss wa unga Leila? Naomba utoke ndani kwangu, nakupenda shoga angu, nakupenda sanaa, ila mimi mtumishi wa serikali huwezi kukaa hapa. Mungu atawasaidia mtoke.
Nje nasikia gari imewashwa inaondoka. Nikambeba mwanangu na kumwambia dada twende zetu dada. Nje usiku wa manane. Ikapita boda boda tukapanda mshikaki. Nawaza twende kwa Mnayalu usiku huo, kwa fupi, au twende hotel, sipati majibu
ITAENDELEA.