Weekend Story! DESPERATE!

Weekend Story! DESPERATE!

Huyu bi dada ni shidaaaa, too educative and you won't get tired of reading her stories. Thanks mkuu
 
Wanafunzi walioko likizo waingie humu wakutane na vitu vya mkinga unafikiri huko mbele watakuwaje!
 
Mkuu Samaritan huwezi amini kuna wanawake vichwa maji wanapractice kila anachoandika lara 1

Hahahaaaaa! Ficus mbona hunipendi hivoo lakini mi binadamu mwenzio, story iliopita ulisema ya kitoto sijasahau ujue, nimejikusanya kuja na ya kikubwa kuku challange tu napo bado unaniona mwanga kigagula BUT WHY? Hahahaaaaaaaaaaa!
 
Hahahaaaaa! Ficus mbona hunipendi hivoo lakini mi binadamu mwenzio, story iliopita ulisema ya kitoto sijasahau ujue, nimejikusanya kuja na ya kikubwa kuku challange tu napo bado unaniona mwanga kigagula BUT WHY? Hahahaaaaaaaaaaa!
Usijali lara 1 ni angalizo tu nimetoa.
Hii ya sasa umenikuna kidogo nakufuatilia kwa karibu ulisema saa tano usituangushe mkuu.
 
Pastor kwa hayo maombi atafel, mama mchungaji anahitaj kukunwa. Asipomkuna muhaya atamsaidia!
 
Anna

Ukaribu kati yetu na Z ukaongezeka kwa kasi ya ajabu, maybe because we were both single, or maybe becuase we never considered to be friends before or it was Karma we became really good friends. Z design alipanic sanaa mtu mmekaa 5 years anakucha for no specific reasons, ilimuuma sanaaa, kupita maelezo. Men can be murderous. Mtu hujamkosea chochote wala nini, he just decided.

Zai maskini hamuwezi amani baada ya kutumiwa ile meseji alimbembeleza wasiachane hata kama huyo dada akizaa yeye hana neno, amemsamehe mradi tu waendelee, Troy akagoma he has made up his mind anamuoa huyo dada wa uswahilini. It broke her heart akawa anafanya mambo kama kachanganyikiwa flani. Anaweza usiku kupiga simu kwa Troy akatukanwaaaa mpaka basi. Kesho anapiga tena, kama alivurugika flani.

Nikawa close nae kumpa tu ushauri na nini, just to make sure she is not alone. Mwanaume akikwambia nimekuchoka kubaliii, kaa nae mbali. Upendo ukishaishia takuwa a monster you never knew. Zaina learned the hard way. After series of abuse, mishushuo, misuto, matusi, kuvuliwa utu, ikafika mahali akakubali enough is enough mwenyewe kwa hiari yake na akamuona Troy in the side he was not showing her. Kuna siku waligongana na Troy kiwanja akashindwa kuvumilia akamfata kwa wema tu, vile moyo unaweza kukuvuruga, Kumbe Troy alikuwa na mama Kija, afu Z hakumuona alikuwa amekuja nyuma ya Troy, sasa yeye pale mda kibao akahisi Troy yuko peke yake, ile anamfata Mama Kija huyu hapa afu Zkampa mgongo Troy anamuona, wacha amshushueee Z. Nimesemaa SIKUTAKIIIIIIIIIIIIIIII, mbona huelewiiii, kwani duniani hamna wanaume wengineeee mpaka mimi tu, sitakiiiiiiiii, sitakiiii, toka toka tokaaa. Khaaaaaaaaa! Jamaniiii nyie. Hadi Mama Kijacho akaingilia kati Troy kuwa na utu, kaja tu kukusalimia, kwani salamu inagombaaa." Ndo ikawa salama ya Z. Z alidhalilika mpaka basi.

Mi nilikuwa nae sikutaka kumstopisha cause nilikuwa nimemchokaa, kila mda namwambia Troy hajawahi hata kukupenda mbishiiii, i neede her to learn the hardway. Alivojidhibitishia pasipo shaka lolote kuwa Troy is a dog she was glad they were over, and she was glad for the breakup, and everything, akafuta namba, sms, choma picha zote, delete zingine na kuwa mpya. Troy hakuamini. Wakikutana na Z anamlia cobis na kumfungia viooo kama hamjuiiii, kile kitete chochote kwishaaaa. Troy itakuwa akawa aajiuliza what hell happened overnight.

Akaja kuniuliza mimi, Ooooh Anna eti Z anatoka na nani? Nilivokuwa nimemchoka, nikamjibu "Anatoka na baba yako mzazi, mama yako yule sahivi ujue uwe unameheshimu." Akacheka tu kwa masikitiko. "Anna come on biff ni kati yangu na Z why pick sides, we were friends remember. Baba alifariki mda and you know it so quit throwing daggers, anatoka na nani?" Nikamtizamaaaa, nikamuona boya tu, nikaa kimya. Akaendelea kungangani kama deni, nikaona huyu kumkomoa nimtajie mtu ambae hatoweza kwenda kumuuliza, atabaki kuumia tu ila hatoweza kufanya ushenzi ushenzi wa kutuma sms za matusi au usumbufu wowote. Nikamwambia anatoka na Shemeji K sasa run your month and see what K will do you. Like expected his expression was PRICELESS. Akkaondoka kimya kimya. Kilimuuma kile kitu hamna mfano.

Siku ya kuanza vikao vya harusi hakumuita shemeji K, kawaita wote kasoro K. Sasa wote wanamuuliza K unaenda, K akawaambia mi hajanipigia maybe kasahau, yule mdogo wangu lazima nije. K akaenda hivo hivo na akajiteua mwenyekiti. Hahahaaaaaaaa! Basi ka Troy kakawa kanajiona excuse of a man, kakawa kadogoooo. Kanawaza K anamtomba demu wake wa zamani no wonder he is in a hurry to marry him off to a loser ili yeye ajisevie demu wake class 1, mnafiki mkubwaa, tena mzandikiii. Akawa anavumilia tuuu. Akanifata Anna roho inaniuma snaa K anavonikosea heshima, tena atakuwa alikuwa anamla tangu niko nae mi nakwambia. Inaniuma sanaa. Fine yeye ana hela ana uwezo, but man you gotta respect a dude man to man even if you hitting his girl." Nikamkumbusha "EX girl." Troy akawa tu mpole hana jeuri ya ku biff na Shemeji K. Basi mi namtia upepo "You better watch out how you treat Z, K wont be so patient with you abusing Z anymore." Troy akazidi kuvurugika. Akajua Z jeuri yake anaitoa kwa K.

Then Mariane alitualika dinner, nikaenda na Z, tukamkuta na Uncle Freddy. Ilikuwa tu familly dinner. Tukiwa tunaosha mivyombo na Z jikoni, basi Z anamsifia uncle Freddy, Anna yule Freddy umeona ile time piece aliovaaa? It costs millions. Freddy sio wa mchezo mchezo, the guy is loaded kama shemeji yako K. And he has class. Ningepata mtu kama Freddy Troy ningemuamisha mji, nyoooooo. Hahahaaaaa! Wakcheka. Nikamwambia Uncle Freddy utamuweza wewe, yule best friend wa K nae ana mambo mengi sanaaaa. Wanaume wa mjini hawa mi siwawezi kila mwanamke anamtaka uncle Freddy. Z anamsifia wewe K mbayaaa, mweusiii, muhaya yule kitu Freddy handsome wa nguvuuu, na hela anayo, nigee mie namba ya Freddy nijaribu bahati yangu." Nikashtukaaa i dodnt know why ila i started looking Freddy from a different angle. Nilishajizoesha uncle Freddy, uncle Freddy, sasa Z anavo mpitch kwangu my parception changed but hwa still THE OLD UNCLE FREDDY I KNOW. Nikamwambia namba sina but Marriane anayo, maybe umuombe. Z yupo achana na Marriane, nitamuomba mwenyewe si yupo sebuleni.

Wakarudi sebuleni, mi nikaenda kucheza the girls, wananipendaaa sanaaa, kidogo hakiwezi kusem mamdogo kinasema Odo. Basi fanya fujo hatari. Dada akaja kunipa taarifa Mama (Mariane) anasema Shoga yako kamganda uncle Freddy huko sebuleni mpaka aibu, embu toka chumbani kabla hajaja mwenywe kukutoa. Nikajua kushakuacha. Nikatoka. Shetani ana nguvu sanaa, sijui kikoko tu sijaliwa mda mrefuuu, mimi ni mgumuuu kutoka K kuliko Mange Kimambi, but i started seeing uncle Freddy in a different light sijui ni Zaina effect sijui, but come on men, tunaheshimiana na Uncle Freddy vibaya mnoo. Ill just admire him from afar. Z got his number for sure, she has a way with men, always she had a way with men.

Mda wa kuondoka Z ana gari lake ila akajifanya kalewa sanaaa hawezi kudrive Freddy ampeleke, na Mariane nae kachoka Freddy mimi anipeleke. Tukapanda wote gari ya Freddy. Sasa Kwa Z karibu ila anangangania Fredy anishushe mimi kwanza afu arudi kumshusha yeye of which ni nonsense mzunguko Freddy akagoma Z akakubali kushuka wa kwanza. Basi tukabaki tu mi na uncle Freddy. Njiani ananiuliza unafanya kazi wapi? Namwambia najitolea NIC bado hawajaniajiri, yupo njoo ufanye kazi kwenye kampuni yangu, come on sisi kama ndugu why hukuniambia you are in need of a job? Monday njoo ofisini. Nikashukuru Mungu kwa ajira.

Basi story zikaendelea, zikaendela, mpaka nikafika kwangu. Nikamshukuru kwa lif. Akauliza humkaribishi uncle wako ndani? Nikatamani nimkaribishe ndani sema nikakumbuka u bachelor huu michupi iko mpaka sebuleni, minguo mpaka mlangoni, sehemu yenyewe chumba kimoja na master, nikawa nimesawajika , nikamwambia next time. Akasema basi uje jtatu for interview.

Nikawa nimeingia zangu ndani nawaza na kuwazua. Ikaingia sms Anna nakutongoza mwezi wa 8 huu hujanikubali. Wanaume wa siku hizi wana rekodi mpaka tarehe alioanza kukutongoza. I dont like the guy honestly. I dont why au ndo kulogwa kwenyewe sijui. Juts tu nkiwa nae no butterflies in the stomach yani msisimko hakuna kabisaaa. Nikawa nawaza na kuwazua. Ikaingia tena text ya yule chotara firauni, "I still miss you" Jitu limeoaaa na kuoaa ila kusema hata miezi mi 3 ya ndoa ipite badooo, lishaanza kutengeneza mazingira ya mchepuko, hahahaaa.

Nikalala zangu, Akapiga Z simu, nikapokea vipi mbona usikuuu. Bila haya akajibu "Nampigia Freddy hapokei, usingepokea na wewe ningejua shoga angu umenizunguka mmelala wote na Freddy." Hahahaaaaa! Nikamwambia "Zai acha upuuzi nimekuja chooni kupokea simu yako Freddy kalala fofoooo. hahahaa" Tukacheka tu wote. Basi Z yupo love at foirst sight sijui nini. Hana lolote kaona Freddy ana mawe balaaa ndo kulowa chupi fasta fasta, wanawake wa sahivi sio kwa uchumi huuu. Alivoona gari ya Freddy ndo kabisaa kaona kwa Troy alikuwa anafanya ujingaaa.

Kusema nilale akapiga Mariane anagomba "Kuna mtu namba ngeni kanitumia sms kwamba K anamwanamke na wewe unajua A to Z, wewe kweli wa kunifanyia mimi hivo ndugu yako, dada yako wa tumbo mojaaa? Sitaki kuamini. Niambie huyo mwanamke ni nani na nitampata wapi? "

Mmmmmmh! Nikawaza fasta fasta niaksema huyu anahisi tu, ngoja ni buy time na kama kwli anamjua anamjua yupi sasa nisije kuharibu zaidi ukute anaeambiwa sie mi nitakae mtoa sadaka nikamjibu "Jamani dada mimi sijui chochote mbonaaa jamani, haki mi kweli nijue nisikwambie haiwezekani, labda nikufanyie upekuzi nikupe jibu"

Ikaingia sms kutoka kwa Mariane "Usikanyage kwangu hukaribishwi, usiwasogelee wanangu, namba yangu futa, usinitafute kwa lolote, kuanzia leo mimi sio dada yako wala mimi sio ndugu yako, tusijuane, tukikutana barabarani tupishane kama mbwa, hata salamu ina gomba, nakutakia maisha mema, kweli mnafiki unae ndani kwako siku zote" Khaaaaaaaaaaaaaaa! Tobaaaaaaaaaaaaaa!

ITAENDELEA SAA 1 USIKU.
 
Huu mtanange wa Anna na Z kwa Fred sijui atashinda nani!
 
Hakuna kitu knachowauma badhi ya wanaume kama kujua his ex gf ana date na man mwingine, na huo ndo upepo unaopga Troy. Atashindwa kuihandle ndoa yake!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom