Weekend Story! DESPERATE!

Mariana.

I knew not marrying was an issue to many women but i never suspected it will be an issue to Anna, my young sister. She was always so lively, so bubbly, so full of life, i swear i believed she could conquer the world. She was always the smart one, and i was the beautiful one with peanut brains. She will always get the best grades and all, but i loved her all the same because she was my little sister that i grew up with.

Haya mambo ya kukosa mume yalianza kumuingiaaa, i could see she was struggling, she was tring to stay relevant and look happy, she could have fooled them all but not me, cause i knew her. Wished i could help her, tried to help her so many times but i just couldnt. I swear if it was all me i would have created the man she wanted just for her. But we always dont get what we want do we?

Mara kwa mara ananisifia Mariana una bahati sanaaa, Mungu anakupendaaa, amekupa Mume, familia, mwanaume anaekujaliaa sana, you have everything you ever wanted and i have nothing. Sio kwamba nakuwa mkosefu wa shukrani la hasha some how yes nimebahatika na Mungu ananipenda sanaa ila some how it is all my efforts na kufanya maamuzi magumu several times, yaani kujitoa akili kweli kweli na kujilipuaaa sema vile venye naonaga aibu sema ile ukweli ya ndani, so i just flow with their praises and enjoy them while they last. Ila ukweeee wa hii ndoa yangu nilivoipata pata naujua mimi na Mungu wangu baaaaaaaaaaaaaaaaaasssssssssss. Msijali wasomaji mie na nyie tenaaa nitwapa ubuyu wote A to Z venye nilimuingiza kingi huyu jibaba.

Not that i was unhappily married nor was i happily married either. Nilukwa kati kwa kati vile watu wanapenda kuangalia kile unachowaonesha basi wanaamini kumbe upuuzi mtupu. Kwanza mimi nimezaa watoto wa 2 wote wa kike, na kizazi nimefungaa kabisaaa sipendangi ujinga ujingaaa, but i could tell the bastard of a husband nilie nae badala ya kuona watoto anatoa Mungu, he is secretly yearning for a BOY child. Mxiuuuuuuuuuuu! Wanaume saingine. Mtoto wa pili nimechanika chanikaaa sifaiiii, nikapigwa na kisuuu juuu leba huko, balaaa tupu almanusraaa nifeeeee kabisaaa ila jitu zima bado linatamani mtoto wa kiume utdhani yule wa kike nimemkohoaaa sijamzaa nusu ya kufa. Basi tu maisha kama Mange Kimambi kweli anavoongea ukizaa K inakuwa kubwaa mpaka ufanyiwe vaginalplasty kurekebisha, basi kwa kuchanika kule namzidi mama wa 6, sina tu hela ningeeda kujitreat na hio vaginalplasty. Jamaniiii, nikasema SIZAIIIIII tenaaaa hata ikiingia bahati mbaya natoaaaa. Nikapiga vijiti vyangu vya kutoshaaa.

Jinaume likiwa na hila unaliona kabisaaa mambo yake basi tu unaaamua kunyamaza, baada ya kugoma kuzaa tena, nikalibamba na vipimo vya mimba vya mwanamke mwingine, so he was trying for the Boy na mwanamke mwingine. Palichimbikaaa nikamwambia kama mimi ni Mariana, ni mkeo umenioa kanisani na namtumikiaaa Mungu huyu alie hai, akakupa wewe uwe wangu, na yeye ndo kanipa mimi watoto wa kike wenye afya teleee, na nilishonwa nyuzi zisizo na idadi, K yangu ilichnikaa mpaka kesho siwezi kujichungulia nikulete mtoto leo unanilipa hiviii, huyo malaya wako atazaa mtoto wa kike, sababu tangu lini malaya akazaa mtoto wa kiume, lazima azae wa kike aendeleze kazi ya mama ake kutembea na wanaume za watu na ikitokea kazaa wakiume atakuwa shogaaa tena anaevaa sketi na kupaka shedooo.

Nilipigwaaaa siku hio msisikie, sikuwahi kupigwa ila siku hio nilipigwa haswaa haswaa, na kwa ile prophecy ya kishetani niliomtamkia i went over board a little, sikwenda kusema kokote kama kanipiga nikawa najikanga na chumvi maji moto basi. Aliondoka baadae akaanza kurudi baada ya kujisalimisha kwa mchungaji nyamaaafffffff. Yule mwanamke alizaa mtoto wa kike kweli, tangu lini wahenga wakakoseaga? Maskini ikawa bahati mbaya, hakukaa hata siku 3. You best the son of beach was guilty beyond measures. Sijui alihisi nina mkono kwenye lile swala, sijui ila mimi walaaaa, basi tu haikuwa riziki.

They never got back together, he got his shit straight akabadilika kabisaaaa kabisaaa na kujirekebisha kama sio yeye anajifanya mtu wa familia na mapendo mengiiii, Mxiuuuuuuuuuuuuuu. Namtizama tuuuu, aibu zake mwenyewe. Yani ndoa ni safari ndefuuu isikie tu kwa wenzio. Nikagutuka niko na Anna pale, na kama kavurugwa flani nikawa naongea nae.

Namchagiza sasa Anna mbona unachagua sanaaaa mdogo wangu, wanaume wote tu chupi mbovu, ni kutafuta yenye tobo dogo dogo ujistiri nayo safari iendeleeee. Yule chotara ulisema kibamia kazi haiwezi na yule mwanasheria ukasema mbayaaaa sanaaa kama shemeji yako heheeeeeeeeee, na shemeji yako kaharibu watoto, mitoto ya kike kufanana na baba yao ndo nini sasa, na wahaya walivo weusi wabaya, badala wachukue mishepu ya bibi zao bukoba huko wanangaa sharubu tu.

Mdogo wangu usitake kuchambaa sanaa mwisho ujichubue, lower your standards jiokotee scrapper yako hivo hivo mnaenda mdogo mdogo. Wenzio hivo hivo tumefosi kingi, kwani kuna kupendana Romeo and Julliet, hamna lolote mi sikufichi shemeji yako muhaya nimeanza kumpenda humu humu ndani, unafikiri.

Nilivokutana nae nilikuwa na shida ya field tukatambulishwa akanitafutia field, nimefika pale booss wake akajichanganya nikawa namlia pesa zake kama sio mimi, tukikutana mambo, poa, kwani vepeeee. Boss nimemchunaaa yule field ikaisha nikaenda chuo. Muhaya anakuja chuo anasalimia tu sio kivileee. Alieharibu shoga etu Zai kaniona na muhaya ndo kuniambia Muhaya ana mawe kinomaaa. Haaaaaaaa! Sijui kamjulia wapi, mi nikamwambia mbona wizarani hana cheo, akasema anacheza dili za hatari balaaa. Kama huamini muombe laki 5 mwambie huna ada. Mmmmmmmmmmmmhhhhhhh! Nikaliweka kiporo.

Huku na huku kanitongoza nikamuomba laki 5 mzima mzima, tena kipindi hiko nipo na K, hata hatujaachana, akanipaaa, aaaah, nikawa naikoga mihela, na ile kampani yetu kwa matanuziiii, K tupa kuleeeeee nataka ujinga mieeee. Sasa muhaya mwingi tatizo lake, ana ma GF longtime walisoma wote sijui wanafanya kazi wote, nikasema hawanijui. Nikabeba mimba, wenyewe K zao si wanazibania, mi nikajilipuaaaa, Kitu na box, nikagemuaaa Game over!

Nyoooooooooooooooooo, iwe rahisi hivo nakunya mpaka kigoma, nimebeba mimba, katoa mahari, afu basi. Nimezaa haongelei harusi kabisaaaaaaaaa. Kama alilogwa. Nikaanza kampeni dume, nanunaaaaa, sichekiii, siongeiiiii. Akikohoa ndoa, akienda kukojoa ndoa, akiwa anakula ndoa, swala ndo hilo hilo tu. Mwisho akawachoka aaksema basi sawaaa nakuoa kwa harusiiii. Heheheeeeeeeeeee! Mjini hapaaaa.

Ila ningetaka fairy tale mbona ingekuwa bado shoga aangu, mkpaka sijui anipendee, atake mwenyewe thubutuuuuuuuuuuu. Mambo mjini ni kufosi kingi, na wewe kujishusha ndo hutakiiii, hutakiii mdogo wangu sasa sijui tunafanyaje hili swala lako. Labda uendelee kuomba Mungu, manake sasa tufanyajeee.

I have officially stopped praying for a husband. Mmmmmmmmmmmhhhhhhh! Nikashangaaa, Anna atakuwa keshakata tamaa ya maisha kabisaaa, aiseeeeeeeeeee. Daaaaaaaaah. Kama dada mkubwa itabidi tu nifanye makarateka nitafutie mtu, maybe match making au blind date, kwanza watu kibao hawajao, wadogo zake nani yuleee, na flora na Josma, watu bado wapo, maybe i should just hook her up na vijana wenzie. Nikimwambia atagomaa hapendi vya kunyonga huyoo ashazoea vya kuchinjaaa, nitamfanyia kama coincidence kumbe kuna mkono wangu dada kubwa.

Atapata tu mtu mbonaaa, wale kina bonge Halima, mwajuma malaya, Tatu mcharuko wote wamepata waume wa maana tu hutoamini itakuwa mdogo wangu Anna, sitaki kuamini wala kukubali. Hapa niweke tu effort tuone itakwendaje.

ITAENDELEA KESHO JIONI.
 
Hehe. Kidhungu icho wana JF wataishia page ya 9!
Umenikumbusha enzi zangu! Asije Arinna akapata Fibroids zikamla uzazi akaishia kuwa chizi.com!

Let the Church say Àaaaaaaamen!

Ma mchungaji nimempenda, yupo kama Money Penny. Hihi hihi hihi hihi hey! (IN MISS ELIOT'S VOICE)

lara 1 wapaishe muda ivo ivo na mie namalizia pande langu nikusome na wewe!
Plz, usiquote uzi mrefu hivyo, unatusumbua watumia simu.
 
Zaina

Jamani kuna uchumba sugu ila huu wangu na shemela wenu Nestroy au Troy anavopenda kujiita unazidi wa AY na demu wake. 5 damn years i am waiting for the ring. Kila mwaka mpya najipa moyo, this is my year, this is my year hukuna kituuu kabisaaa. Mpaka mda mwingine nawaza sijui nijibebeshe mimba kama Mariana, naona nitajichuuza tu, if i am not good enough for him i am not good enough.

Mimi nakopwaaa kila kukicha, napigwa free lepumbu, simuombi hela hata miaaa yake siijui, simtegemei chochote, na bado na mtreat sanaaa, yani ma care ndo usiongeee, najiongezaa mpaka nakomaaa, mwanaume yule nimekutana nae kituko kitukoooo, hata kumtambulisha mbele za watu naona aibuuu, nikasema sio kesi, nimezama bank kumnunulia nguo za kimjini mjini sio kama za kina Dimond kata K na harmonise ma Sharobaro hataaa nguo decent tu hizi za mujini sneakers, pens, joggers, sweatpants cadet hivo vitu vya ukweliiii, akifika mahali watu wanatoa mijichoo wanaanza kujitongozeshaaa.

Mwanaume wa mkoa huyu hakuwa na ustaarabu hata chembe, yani codes za mjini alikuwa hazijui, mi nimempa codes zote ustaarabu ule unatakiwa mjini jinsi ya kula, kunywa, kuongea yaani sijisifii nimempeleka next level. Mademu waliomkataaga walijiuliza kwanini walimkataa, walilogwa nini na hawakupata majibu yanayo nyooka, i am telling you.

Ila fadhila mfadhili mbuzi utamnywaa mchuziiiiiiiii binadamu wana mauzi. Haongelei kabisaa swala la ndoaaa hataaa. Kuna mda tukakubaliana tuishi wote, nimeenda siku kwanza kanilaaaa usiku kuchaaa, nikavumilia, siku ya 2 mwendo huo huo, wiki nizma mechi non stop, mwezi, nikaona chiu wangu utachakaa mwenzanguuu mume wangu ajae akute depreciation of the highset order, akhaaa nikarudi kwangu.

Mwenzenu wife material ndugu zake wakiwa na shida nampiga tough, akikwama namkwamua, actuall i make more money than him, and i am always there for him, 100% sina bwana wala kibuzi cha pembeni useme nauza mechi au vipi walaaa. As years go by we are growing apart and more apart zamani we could talk usiku kucha siku hizi maneno yameishaaa, hatuna cha kuongeaaa. Maybe cause nina grudge rohoni mwangu kwanini halitaki kunioa?

Nikaamua kuvaa kwenda kwa Mariana, najua she can be a beach na anajishauaje na hio 1 million dollar wedding utadhani Brad Pit na Angelina Jollie, muhaya mwenyewe Mbayaaaa sijui hata nisemaje the dude is ugly as hell, sema ndo ana upendo and she controls him like a remote. Ila overall Mariana ni mtu mwema sanaa, ukiacha mashauzi yake ukiweza kuyahimili ni mtu social, anajuana na watu sanaaa, na kila siku hakosi shughuli pale kwake.

And i like Anna, she is sweet na the fact she is single it makes me feel better about my situation na Troy. Nikamtumia sms Troy, njoo kwa Mariana kuna barbecue, we are expected to be together you know. Akajibu tangulia nitakukuta huko. Kufika kama kawaida Mariana mtu wa watu haina mfanooo, kuko nyomiii nyominooo. Wanawake jikoni wanaume barazani.

"Jamani Z how sweet umekujaaaa, nakupendajeeee mdogo wa mie, shemela leo haji?" Nikajikausha anakuja amepitia kwa mama mke hapo ila takuja. Wakaangaliana. Mariana hakopeshi "Jamani Troy inabidi tumuandalie keki ya SHEMEJI OA labda itasaidia uchumba gani huo miaka mi 5 looooh!" Hahahaaaaaaaaa! Wakacheka wote, si mambo ya kuchekesha lakini. Halima bonge akadakia "Labda uzae umri unaenda huo, shauri yako. Wanaume wa kubembeleza hawaaaa shoga angu. Mi si mnajua namfugaaa yule bwana na wala sijifichi wala sidanganyi, kajaa pale barazani utamuona kashika funguo ya gari langu kujitia mpanaaaa kama kibao cha chapati mwanaume suruali ila anafikishaaaa Heheeeeeeee Halooooooooo" Tukacheka wote Alma nae jamani hanaga akili. " Sio kuwaambieni ananifikisha mjichetue kupitisha TBS mumjaribu kama yaliyomo yamo, nawaambieni kabisaa FREE P.UMBU itawahusu kama mnaweza shauri yenu ingieni kichwa kicha, wengine kufuga mabwana tuna masters kwenye sekta hizo, wizara za mambo ya nje kibaooo, kuendesha wizara ya mambo ya ndani haitubaniii, mtanitakaaa mimi ndo Halima, toto la kizaramo bibi kasema mafiga ma 3 mie hata 10 twend kazi." Tukabakia tu tunacheka na masikitiko.

Mariana akamchokoza Tina, " We mwenzetu unatumia utaalamu gani maana umemuweka kiganjani, samasoti tu?" Tina akacheka kwanzaaa " Shoga zangu mmeona gari langu jipya lakiniii? Haaaaaaaaa! Mi ndo Tina Mkinga originalee, Makete Mojaaaa sibahatishii, mwenzenu samasoti siziweziiii, Halima kanifunzaa kachoka kasusa, sijui mambo yenu ya mjini romanceee sijui nini mie wa shamba bwana nawaachia nyinyi. Mie namroga mwanzo mwishoooooooo. Yaani akinisumbua tu nambadilishia mtaalamu. Akifanya kwiki kesho niko kwenye bus naenda kumbadilishia mtaalamu. Wanaume hawa bila midawa hawaendi hawasogeiiiii, mimi sipendi kweli mambo ya ushirikina ila imenibidi, we mi nimezaa watoto wa 3, tumbo lote michiriziiiii, miaka 40 na kitu ananiambia Tina kuna mtu nimekutana nae, nampenda sanaa, nyoko nyoko nyoko. Nimepigia simu mama, kaniambia we njoo Makete, hatosema fyoko wala fyokole. Mi kila siku nakwambia Tina wanaume bila dawa hawaendiii. Unatembea na miguu kwanini asikupe gari, we unaenda nae kisiasa, utazeeka na mwendo kasi. Njoo Makete tufanye yetu.

Mama kamleta mtaalamu toka Mbamba bay, bibi kigagula mwanga mwanga kweliii, bibi hata hasikii vizuri. Akaniambia umechelewa, nyi mnajitia umjini mwingi, wenzenu wa nje wanakuja huku leo kesho, nyie hamji mnategemea nini. Ashamtekaa tayari ila namrudishaaa. Kanifanyia dawa pale siku 5. Doooh! Akaniuliza familia yao hawakusumbui, nikasema siku hizi siwasomi wanafurahia mimi kuachika, hasa mama anachoga sanaaa. Bibi akasema sio kesi nitakupa mambo watatulia wote. Wale wepesi tu.

Nimerudi bado anakomaa nataka kuongea na wewe, nataka kuongea na wewe, kuongea huko anataka aniambie talaka. Nikawa namzungusha huku nishamuanzishia midawa, Saaingine naambiwa mpe kijiko kimoja akinitibu naweka hata vi 4 potelea poteee, mxiuuuuuuuuuu. Nikawaalika familia nzimaa, ningewaambia mimi wasingekuja, si hawanipendii, kuwakomoa nikawatumia meseji na simu ya mume ndugu zangu naomba mje kuna jambo nataka kumtamkia mke wangu mbele zenu. Msijibu hiss sms ila mje jumamosi ijayo. Nika idelete. Wkaja wote wanajua sasa naachika rasmiii, nyooooooooo.

Wamekuja nimeendaa chakula na dada, nikamtuma dada dukani, nikawatilia dawa woteeee, kwenye chakula cha familia nikatia dawa muleeeeeee, chezea mimi nyie" Mmmmmmmmmmhhh! Tukawa wote tunamuangali kwa jicho la mashakaa, ila kusikiza tunataka. Tukamuliza eeehhh ikawaje?

"Nikawalishaaaaaaa kama kawaida, wakala wote, na tangu hapo sisikii fyokoo wala fyokolee, na Mume nimezibitiiii, hatikisikiii, gari hio kanikabidhiiii, mshahara anakabidhi na salary slip sipendagi ujingaaa. heheeeeeeee! Z hujaamua tu, twende makete mdogo wangu mbona huyo Tloy sijui nani ndani ya mwezi inafungwa harusi na tunasahau kabisaaa. Asiesaidika ni Anna maana hata wa kumoga hana masikini hahhaaaaaaaaaaaaa" Tukacheka wote kwa masikitiko mpaka Anna akacheka ila najua lilimuuma sana moyoni.

Watu wakawa wanatoa toa macho tu chezea Mkinga weyeee. It was appealing offer ndani ya mwezi struggles za miaka mi 5 kuishaa, sema Devil never wins atakusaida siku 2 au 3 afu basiii. Nikaamua tu its not worth it, ila kama simfai akiwa na akili zake nitamfaa nini akiwa ametekwa ufahamu. I am woman of principles, A man should want you for himself, he should show efforts, hapo ndo nikakumbuka Mariana was one lucky beach.

Mume anampenda jamaniii, yaani sijui nisemaje. Kuna siku tulikuwa mimi yeye na Troy tunakula makange, yalivoletwa tu mezani akapata guilty akamwambia wa jikoni embu bandika kuku 2 hapo hivi hivi afu funga, Tukajua anaongeza and we were like kuku 2 tenaa na tuko wa 3 tu, nikajisemea maybe company is comming labda kuna watu wake wanakuja huwezi jua. Zilipokuwa tayari kampigia simu boda boda wake akaja kufata anampa maelekezo peleka nyumbani kwa mke wangu, mwambie isio na pili pili ni for the girls, yenye pilipili ni for her na dada na wanaume wengine humo ndani. Mi nitachelewa. Mwambie mumeo alikuwa anakula makange roho jinsi anavokupenda akakuagizia mkewe unipambe pambe si unajua mi pale nimefika bei kwa shemeji yako. Nisifie hatari. Akamlipa. Nikasema kweli mwenzetu kapataaaa.

Asione mtu anauza kitu, anamwambia mpelekee ofisini atavochukua uje uchukue hela huku. Basi anachagua anavotakaaaa. Weekend lazima ashinde nyumbani, akitoka ana familia yake yote . Hajibani muhaya yuleee aaaaah. Shule wanae wanazosoma sasa, utafurahiiii. Japo ni serial cheaterrr! Alafu sasa Muhaya sio panzi leo yuko na mwanamke huyu, leo yule, akipata mwanamke anakaa hapo jumla jumlaaa. Sahivi ana kidada kibosi cha bank. Kama kumbi kumbi. Mariane hajui ila Anna anajua kama shemeji yake mwingi. Na hamwambii dada mtu sijui kwanini.

Nikaamua kumtikisia Maria kidogo, " Da Maria wewe unatumia nini kwa shemela kumtulizaa na kukupa life unalotakaaaa" Nikamtegaaa tu kiunafiki." Mimi mwenzenu nabahati, Muhaya ananipenda sanaaa, sanaaa, from inside tu ndo maana inakuwa rahisi, ila kabila lake nawajua vizuriii kama wanakuwaga na mambo mengiii, so naenda nae kikomandooo. Kwanza nahakikisha namfilisi anabaki hana hata miaa, akienda kumla mtu mjue kabisaa kapigwa FREE P.UMBU tu hamna la maana lolote atalomfanyia hela hanaaa. Yaani nikinusa helaaa atayoipata naipangia mradi wa maendeleo ya familia na investments. Hi large lifestyle nayoishi ni kumfilisi atulize kidudu hiko. Shule za ghali, namtia jamba jamba akifikiria kuzaa huko nje chupi imbane ndani huku jahazi linazama je huko nje si atakufa kabisaa. Namfanyisha endless investments nahakikisha hana idel money kubwa ya maana yoyote maana nyaku nyaku wakinusa hela wanaeza hata pindua serikali yangu. Sasa kamamtu anataka kukaa Free P umbu akae, aone ananikomoa mimi au kipapa chake. Na haya maisha mda mwingine nafanya kusudi tu kujishebedua wake wanzangu kama wapo wanijue heheheeeeeeeeeee!" "Haloooooooooo! " Tukadakiaaaaaaaaa wote kwa mbwembwe.

Ikaingia text ya Troy. "Sijui nikwambiaje i was hoping to tell you inperson ila nimekutana na mtu mwingine, she is preggo for me naenda kutoa mahari karibuni, its better usikie kwangu mwenyewe" Mmmmmmmmmmmmh! Nikamuita Anna, na kumuomba anisndikize. Sasa pale story zimenoga akawa anasua sua. Nikamuonesha text. Akainuka fastaaa. Tunaondoka bila kuaga. Mariana akatubamba " Aaaaaaaaah ndo mshashiba mnakimbia kuosha vyombo rudisheni vipapa vyenu hapa, .............. na maneno kibao Ana akasema achana nae, twende zetu." Tukaishia kwa miguu hata sijui tulikuwa tunaenda wapi.

ITAENDELEA KESHO JIONI
 
My dear sis,know it please au ? i am your admirer na sitoacha,please kindly uwe unanijibu baby,hujui tu jinsi gani nafarijika na kukuzimia zaidi na zaidi baby,Lara 1 .you are such a talented writer ever.
 
Waoooo aiseee lara 1 tulikumisi saaaanaaa jukwaani karibu tena uwanjanii...
Story nzuriiii saaanaa kama kawaida yako hukoseagi kabisaaaaa
Sipati picha hiyo story ya ngosha itakuaje
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom