Arriana
Life with Freddy was a roller coaster, maana kila siku mission impossible jipyaa yaani balaaaa. Likitoka balaa hili linaingia balaaa hiii. Pressure to get married ndo inaongezeakaa hatariii. Hadi Z alishalipiwa mahari tayari bado mimi tu jamani Mungu nimekukosea nini. Tina Mkinga alishinda kesi akapewa 50% ya mali za Kapima, akazi invest kwnye maduka yake, maana waligawana mpaka maduka. Akaachana nae kabisaa ikawa salamu inagomba.
Not everybody has a happy ending, Kapima akamuingiza ndani yule baby Mama, miezi mi 6 wakashindwana. Tina alisema hakuna mwanamke atakaeweza kukaa na Kapima na ule utemi wake. Yeye aliweza na tangu hapo sababu alilelewa kijijini mwanamke sio kitu. Ila Kapima anamjua yeye ni mkorofiiii hakuna mfano na mnyanyasaji asie na kipimo. Miezi 6 baby mama kaikimbia nyumba mwenyweee, kafungasha kaondokaaaa.
Tina alisema niliwaambiaje, na tangu hapo kajitahidi mbayaaaa Kapima sio mtu. Siku hizi ana BF na yeye heheeee, wanenda nae China. Kaka nae kashindwana na mkewe, nae Mkinga kama yeye. Ila yeye Tina kasema ndoa basi ile moja ilimtesa sanaa na ilimtoshaaa, sahivi ana mali zake kisa cha kuja kugawana na mtu kizembe nini, wapendane mbali mbali.
Kapima baada ya baby mama kuondoka kimya kimya akaingiza mwanamke bar maid si barmaid yani haelewekiii, wale wa uswahilini walioshindikana kabisaaa, ndo mke kamuweka ndani. Yule nae kaka siku mwezi sijuia, nae kashindwa, kaiba kila kitu katimukaaa. Watu wakaanza kujiuliza Kapima anawafanya nini wanawake mbona wakai au ana michezo michafuuu mbona haelewekiii mtu mzima inakuwajeee. Ndo akagiza mke kijijini ashazaa watoto 2 sijui akaachika, maana aliomba chonde chonde wasimletee mdogo, wamletee mkubwa mwenzie. Huyo ndo akakaa sasa.
Z mwenzangu alipata bahati mkaka katoka US huko alikuwa kazamia, sasa umri umeenda karudi bongo anatafuta mke, sio mchumba, sio baby anatafuta mke wa kuoa aende nae huko marekani. Z akapewa mchongo huo na shoga ake kuna kaka Diaspora green card nje nje kama vipi kubali ndoa uende. Akatae ndoa kwa raha gani aliokuwa nayo kwa mfano? Akawa hana budi kuikubali ndoa fasta fastaaa. Namuuliza shoga angu mnapendanaaa hata kupendana? Umemchunguza na kumchunguza asije kuwa shoga ukaja kujua too late. Akanihakikishia kamchunguza sanaa, na wanapendana sanaaa.
Basi anajishaua hatari, trust me mda wako ukifika you wont even have to try hard, mambo yanaenda yenyeweeee bila shaka lolote. Unauona kabisaa uwepo wa Mungu na mkono wake unauonaaa. Ukitamani kitu moyoni mwako kinakua. He is everything i wished in a man and more. Trust me mda mwingine mpaka naogopa asije kufa kabla ya harusi maana ni kama ndoto." Trust Zai the drama queen kwa kuongeza chumvi.
On the mean time mi bado niko kwenye scrumble and partition ya kuwa main chick wa Freddy imagine. For these 2 years mambo yamebadilika hatariii ila kwangu kama yamenasaaa. Everybody is getting married mi hata stablle relationship sinaaa. Namsindikiza Zai kufanya shopping ya harusi basi ananiambia achana Freddy anakupotezea mda, it will never happen, tafuta mtu low key utoke nae. Watu walikuwa wameolewa wameachika na wataolewa tena wewe hata Freddy kuku acknowledge tu kwamba huyu ndo mchumba wangu, au mwanamke wangu hakunaaa. Mambo ya kufichwaaa tu. Utashangaa naolewa mtu mwingine hivi hivi and when that happens you will die of heart attack.
Aliosema ya mbolea sio kidogo tena ya chumvi chumvi. Ila it is just that i had made a decision Freddy is the love of my life. Nilikuwa nampenda hatariiiiii. Sijawahi kumpenda mwanaume kama hivi. Inafika mahali sielewi cha kufanya ndugu wasomajiii. If i was to love someone basi Freddy nilikuwa nampenda, i always doubted forever after zingine zote ila ya Freddy i could feel it kabisaa that is the one, and only forever after destined for me.
Niliendelea tu kuamini kuwa if i tried harder, and harder vitakuwa tu, nisife moyo, Mungu wangu si Mungu mdogo, si Mungu wa wasiwasi, Freddy was powerfull but my God was more powerful. Shoga zangu wengi waliolewa ila kuolewa Z iliniumiza cause she was rubbing on my face any chance she got. Na hivi tuli hustle woteee. Na lichomfurahia au kumonea wivu she got the man of his dreams, wanaendana kabisaaa na kuelewana their chemistry was to die for. You could see love in their eyes. Wengine waliolewa na wanaume wa wasiwasi , ndoa za mashaka mashaka, unakuta mtu hampendi mtu because he asked anakubali umri ushaenda, mambo ya wasiwasi mtupu na low key nikawaza na mimi mda si mda nitaunga Trella.
And Freddy wasnt making it any easier for me, atleast angeniambia au kunifanyia action Anna SIKUTAKIII, ningeumiaaa ningeponaaa, wapi the minute nikisema baas, sasa airtel yatoshaaa he comes back even harder making me love him even more jiulize all for what? To break my heart once again. Nilichokaaa mwenzenuuuu. Nikianza kuwasimulia heart break nilizo suffer mtanionea hurumaaa.
Ile ya tablet ilipita salama, hakupiga simu wala kutuma sms, ndo ikawa salama yake il kama alimrudia yule dada siwezi kujua kwa kweli maana it is Freddy the monster we are talking about. Kesho yake kazini akaja anajichekesha na furaha hatariii. Akanilaghai nikaenda kwake tukalala wote tenaaa.
Wiki hio tulifanya kama mara 3, hasemi kitu chochote, baadae nikamuuliza are we dating? Am i your woman. Maana ndugu wasomaji niliona naliwa tuuuu kimyaa kimyaaa. Nafujika hatariiii. Ulaji wa Uncle Freddy sio ule wa kula mbakishie baba, anafuja fuja hatari, anapiga pedali mwanaume yule mpaka unakuna kichwaaa. Nimemuuliza hilo swali kuangalia maslahi ya uchi wangu yanakuwaje sasa. Akanijubu "I dont like to put labels in my relationships. Will it means to you much more kama nikikupa tittle? Is me being there for you not enough untill uwe na tittle?" Jamaniiii, nikajikalia tu kimyaaaa nikasema leo mwisho kama atauona huu uchi sio mimi. Alijua nimechukiaaa.
Nachomsifu akijua amekuuzi anajua kuku compensate, mpaka utaacha kununaaa nakwambia tenaaaa, atakufanya ujisikie wewe ndo special kwake hamna mfano. Baada ya kuona kanijibu kunya hivo kunipooza akaniambia twende Zanzibar for the weekend. Nilitaka nisiende ila mapepo ya Zai ndo yamenikumba mwenzenu ndugu wasomaji mnifanyie maombi, nasema kabisaa nitasema No, ila najikuta Nasema Yes.
Zanzibar utamjua sasa, he was there for me, larger than the tittle ya demu wake. Kazima simu zoote kwa siku 2, ananiambia i am loosing millions by minutes just to be there for you baby. I am all yours unichoke mwenyewe tu. Tell me. Tunaongea masaa hamsiniii, hatushiwi maongeziii. Hapo ndo kuliwa kwa mwendo kasii na hivi hizo millions zimepotea basi anataka kuzifidia.
Life could never be more perfect, moonlight under the beach, the man i love all there for me, nikasema Duniani kuna Paradiso. I bet with all my heart and soul that is all i wanted for me in this life and the next. Niwe tu na Freddy afu awe mume wangu tuishi kwa upendo kama siku hizo 2. Wanasema "If you really want something with all your heart, without any doubt the powers of universe have a way to make it happen and come true. Nikasema mama universe finally kanihurumiaaa.
Tumerdui Dar, yale yale ya siku zote. Mariane ananipa moyo, wewe hadi hapo ushamla ngombe mzima kasoro mkia, unakosa tu uvumilivu, Freddy harudii mwanamke wewe ume date nae miezi sasa, huoni kama ushashindaaa sema unakosaaa uvumilivuu na kutaka mambo yaende haraka haraka, hapo ndo unapo haribu.
Siku ambayo sitoisahau ilikuwa harusi ya Z kama kesho kutwa, akaniambi twende tukalipie hotel Bagamoyo ya honeymoon, mi nikakubali, na Freddy aliniambia anaenda Arusha kama juzi. Tumefika hotelini tunaenda kuoneshwa vymba vilivyo. Tunafika vymbani Freddy huyu hapa anatoka na mwanamke mwingine. Mi na Zai tukapigwa na mshtukooo. Unafikiri yeye alistukaaa? Walaaaa, au sijui alijihami Anna is not what you think au kufanya effort yoyote ya kujali hisia zangu, mnyonge mnyongeni haki yake mpeniii, walaaa. Akatupita kavu kavuuuuu haina hata salamuuuu, kama hajatuonaaa. Niligeuka kumungaliaaaa, nikaishiwa nguvu nikaaa chini nikanyoosha Na miguu. Nilikaa pale chini nusu saa nahisi tu kufa kufa, kufa kwenyewe sifi, haki nawaambia niliwaza sijui tu ninywe sumu nife sijui nifanyaje. Zai akanipa moyo na nini.
Nikarudi nikaenda kumwambia Da Maria akasema masikiniii Anna, mi mwenyewe na matatizo makubwaaa, ila yako yamezidiii. Basi kaa, hapa na kwenye mkazi wake usiendee tena, kaa hapa nitamwambia shemeji yako wa pembeni akutafutie kazi bank mdogo wangu. Wala usiende kwenye kazi yake, achana nae. Wana roho mbaya sanaa K wote sio watu. Mwenyewe nataka nimuache K na mimali yake akae nayo.
Nikastukaaa! Umuache K kwani vipi? Akaniambai we are living a lie, ana mwanamke mwingine tena nimejua juzi tu, tena kashampa na mimba, na mimi nina mimba ila sijui ya nani kama K au mwarabu boss wangu. Nikapata nafuu kwanza na matatizo ya Freddy, nimsadie dada yangu. Nikamuuliza sasa Dada Maria tunafanyaje unatoa? Akasema "Sitoiiii! damu yangu hii naanzaje kumuua mtoto kwa makosa yangu. nazaa akiwa mwarabu atajijua, akiwa mweusi kama baba yake wa kihaya atajijua. Nataka nimuage K, nikapange nyumba utuuzima huu kabla sijazaa, namwambia kabisaa nina mimba sijui ya nani, ikiwa yako nitakujulisha ikiwa sio yako, utalea hao wa kwako huyu baba yake atajua la kufanya." Mmmmmh nikaona mazitooo. Nikamuuliza Mwarabu anasemaje? Akadai "Mwarabu yuko pamoja na mimi, kasema yeye yuko tayari kwa ndoa, hata kesho nikikubali kuslim, ataleta mahari, atanioa kwa ndoa mke wa pili, anatakaasanaa, anataka leo kesho, niwe mkewe, hata mtoto akiwa sio wake atamlea na hawa wa 2, ila mi ndo sitaki napumzika kwanza ndoa hiziii unatoka hii unaingia hiii sio vizuri. Nataka nikae mwenyewe nizae au ndo nitajua naendelea na nani kati yao au wote napiga vibutiii." Nikachokaaa.
Nimekaa kwa Da Maria wiki nzima, siajenda kazini, akinipigia simu sipokei, nikatuma resignation notice yangu ya 24 hrs nikawa nipo nipo tu, kazi sina, ila nina hela zangu nili save save nikasema nianze biashara za kusafiri nipate kipato niendeshe maisha. Zai nilimuomba atafute msimamizi mwingine wa sendoff akagoma, akakomaa mimi ndo msimamizi. Basi nikasimamia hivo hivo natia huzuniiii, sura imejaa masikitikooo, najizuia kuliaaaa kila mda. Na Freddy alikuja kwenye send off. K alikuja ila Marriane alishamwambia A to Z alikuwa hana rahaaa. Hamuwezi amini K alimuomba abakie hata akizaa mtoto mwarabu haina shida as long as K kakubali hamna atakaeongea chochote. Marriane akamwambia naondoka. Basi akamwambia asipange kama alivotaka akampa nyumba akae na akakubali wagawane mali, maana Marriane alimwambia hatochukua chochote zaidi ya talaka tu.
Kwenye sendoff ya Zai, mimi na K ndo tuliokuwa na huzuni kupita watu woteee ukumbiniii. Kuna mda i swear nilimuona anafuta chozi,maana sendoff afu uwe una go through break up inaumizaaa sanaaaa. Ila mimi ndo nilitisha, kwanza nilikuwa nimekonda ghflaa, nguo imepwaya, makeup imegomaa kabisaa usoni, Z alikuwa tu muelewa. Nikasimama zangu pale mbele kama mkiwa juu ya anga. Sina la kufanya, Nilisikitisha sanaaa.
Sherehe imeisha nikaamua kwenda kwangu maana kwa K mambo yalikuwa sio shwari, and the divorce was wearing him down, tofauti walivotegemea, he wasnt that muchoo, tough guy anymore. Mke anaumaaaaa, kuliko christapen. And K was like a father to me, sasa anvoachana na Maria, it was like baba na mama yangu wanaachana, na Lorraine mdogo haelewi mi naelewa, ndo wakazidi kuniongezea masikitiko juu ya masikitiko. K kanilea sanaa, kanisomesha, sasa nikawa sitaki aone niko upande wa Marriane. Nikaamua kurudi kwangu nikajiuguze kibingwa.
Nimerudi vumbii limejaa, kuchafuuu hatari, hata nguvu ya kusafisha siku nayo, nikatandua tu shuka na kuweka lingine nikajitupaaa. Nipo kama sipo. Zai was gone, nimebakia mwenyewe mjini. Sina bwana, sina nini, back to square 1. Nikiwa nawaza nikaliaa, mpaka usingizi ukanijiaaa. Nakuja kushtukaa mtu ananibusuuu. Freddy, si ana funguo nilimpaga enzi za mambo hot hot. Nilimsukuma kwa nguvu na teke la tumbo sitakagi ujingaa. Yaani kirahisi rahisi tu the way hizi siku 5 i went to hell and i came back, sio kirahisi hivo. Hajakubali wala nini, nae anapambana hadi akaniover power.
Nikajikuta tu nalia kwa uchunguu mkubwa sanaa, kilio mpaka kwikwi. Ingekuwa mtu mwingine anaejielewa kile kilio nilichokuwa nalia angeona aibu akaondoka zake au angeomba msamaha hata kwa matendo yake alio nitendea, badala yale huyu Firauni mjukuu wa Filajunaa, ndo kwanza akaendelea kunibusuu. As if kilio changu kina mturn on balaa, sijui ndo kinampanikishaaa sijui, ila navozidi kulia stimuu zake zinazidi.
Nilimtimulia mbali na magongoo alishika adabu zake zikamshikaaa natamani hata ndo ningewaambia ndo kilichotokeaaa, ila wapiiii, alikula mzigoo hivo hivo naliaaa, mpaka kilio kikaisha, mwili ukarudisha chemistry na kuonesha ushirikiano. Honestly na mimi nilichangia kupokea hukumu mbaya Freddy, cause some how i had mixed feelings juu ya kila kitu. Kwanza hated him for what he did to me, at the same time i was glad he came back to me, maana kilichonisikitisha sanaa siku 5 ni ule woga wa kuwazaa what if it is final fainla final and we were over for good. So pale mwenzenu nilikuwa nali mengiii, nalia kwa huzuni na furahaaa humo humo ndani shalo tinatina.
Na mshenzi yule vile alijua kesi yake ilivokuwa mbaya sanaaa, akamua kutoa maujuzi ya kabatini huko, yale special edition na kuyatumia vitani kujiombea msamahaa wa kibabe. Tulifanya siku hio usiku kucha, mpaka tunamaliza kufanya maradhi yangu yalikuwa yashaponaaa, wanavosema maumivu ya moyo hayapoi kwa ganziiii, ynapoa kwa dudu tu heheeeeeeeeeee. Tukiwa tumelala nilikuwa nimechokaa hatariiii, sikia tu kwa wenziooo mechi kali nikawaza nimuulize kuhusu lile tukio au nisimuulize? Nikaona he was gonna lie to me anyway, why bother, he is back with me, and i was happy, i loved him, he loved me.
Siku hio akanitamkia I love you. Basi nikahisi ndo ana nivisha peteee. Mbona watu watanikomaaa mjini hapaaaaaaaa. Usiku kucha ananiambia I love you so much, please nielewe, hata nikiwa sieleweki nielewe, nipende hata nikiwa sipendeki wewe nipende tu hivo hivo. I know it is hard to love me. Maneno mia matamuuu matamuuu. Asubuhi hajaenda kazini kashinda pale pale, ofisi ikiwa yako raha sana unaweza kuchukua off hata siku 2 unajipigia tu demu, atakae kuuliza nani? Hamnaaaa.
Ananibembeleza rudi kazini, nikamwambia sirudii, i wanna do something else with my life, anauliza unataka kufanya nini, namwambia nataka niende china nikaagize nguo nije niuzee. Basi ananimbia nitakupelela my love kwa mara ya kwanza niliitwa my love mwenzenu, nayajua masoko yotee ya nguoo, tena tutaenda Istanbul fashion zao ziko hot hot, na Vietnam. It is good you are doing something you love. Moyoni nawaza angejua mtaji wenyewe ni 200 asingeshoboka hivo.
Tukawa tuko hot hot, full kupendana, siku hio nasafisha kwake nikakuta pete kabatini iko kwenye box lake, kidogo nizimie kwa furahaaa. Nikafurahiiii, nikajua FINALLY. He was gonna pop the question, i couldnt wait. Nikampigia Z, japo internationa tariffs sio mchezo akasema I am happy for you kama kweli maana Freddy simuamini amini." Namtetea he is gonna do it, Oh My God! Ill be the happiest person on earth. Basi nikachukua nikaipima kabisaa ni exact fit. Nikashinda nayo kwanza mchana kutwa ianze kuzoea vidole. Nikairudisha. Nimekaa kwake siku 3 haniambii kitu, tumbo likaanza kunicheza and it struck me huenda hio pete amenunua amuengage msichana mwingine amabe sio mimi. Nikaondoka bila kuaga.
Jumamosi akapost picha yupo kwenye mahari ya mshkaji wao, akamtag yule dada, nikamfata profile yake nimuone vizuriii, ndo nikaona ile peteee. Kumbe ndo ilikuwa ya huyu dada. Nikanyongeaa tu sasa nifanyaje. Back to square 1. Akaja siku tumeombana kiugomvi kidogo tuuu cha kupishana maneno, akanifukuza kwake. Na mimi nikaondoka. Mda huo Marriane alishajifungua mtoto mwarabu wa kiume. Asha slimu, wamemtia maji anasubiri ndoa ya 2 hio kwa mwarabu. Akasema hafanyi shereheee wala nini kashazeeka.
Sas mimi nikawa unstable Maria anaolewa mara ya 2 mi nipo tu jamani how come? Basi nakuwa na stress na kitete, namjibu Freddy kunya kunya. Alivonifukuza akani block kabisaaa. Nikawa nipo nipo tu, nikawaza huu dno mda wa kuanza ile business niliokuwa nataka kuianza. Nikafanya taratibu za safari, basi nikkutuna na Troy ubalozini. Long tiem no see, akaniambia yupo Kariakoo na Tina Mkinga. Akasema ane anaenda China karibuni tuongozanee. Nikashukuruuu. Tukawa tuna chat maana mimi na yeye ndo tumebakiaaaa single. Ananimbia bado hajapata nguvu ya kudate. Na mimi nampa moyo hivo hivo siku zinasonga.
Kulikuwa na harusi, Freddy kaja na mdada mwingine mzuriii, ni mzuriiii balaaaa, na mimi nikaenda na Troy. Sasa design kama hakutarajia kama mimi nitaenda na Troy. Ikawa kama hatujuani kabisaaa. Nikiwa chooni yule dada Akaja, nikawa busy na mambo yangu. Basi Ananiuliza "Are you Anna?" Na tonationa ya England, nikasema Freddy kapata Muingereza hongera yake. "Nikamjibu ndio" Basi ananimbia "Freddy speaks a lot about you, he will definitely kill me if he knows i am talking to you right now, but you seem a nice person, can i have your number?" Nikataka kumpa ya uongo ila nikaamua kumpa ya kwelii.
Mda wa kuondoka nikawa naondoka na Troy, Freddy uzalendo ukamshindaa akanifata Anna njoo tuongee, nikamwambia sina la kuongea na wewe, basi anafosi, Troy akamjia juu kasema hatakiii. Basi akarudi kwa demu wake, ila kama mnavojua wabongo waliozaliwa nje kama wazungu tu yeye anaona poa tu. Roho iliniumaa sanaa kumchunia Freddy vile, kwanini kani block na kanifukuza kwake.
Basi jioni yule mdada kapiga, ndo akajitambulisha I am Lilly, Fred's cousin at the aprty remember me? Nikastukaaa kumbe cousin looh! Nikashusha pumzi, basi akaniambia Freddy talks about you a lot, tells everybdoy about you, he really likes you, and you were mean to him tonight. I think you should start treating Freddy better. Na accent yake. Hahahaaa. Nikamwambia wewe hujui tu ndugu yako alivokuwa kauzu. Tukaongeaaa wakwe tenaaaa masaa ma 2.
Baada ya kukata nikagundua kwanza nimmfanyia Freddy umafia, afu kumbe hakuwa na demu, ndo nikastukaa nimejambia kwa mbelee, na hata akiniacha itakuwa si sababu yake bali ni uzembe wangu. Manake fikiria mi nimeenda na kidume kingine, badi kajikusnaya kutaka tuongee, kwa Freddy hio ni bonge ya effort afu nika mrubbish mbele za watu. Hiiiiiiiiii! Na Freddy sio mtu wa mchezo mchezo, nikagundua makosa yangu. Nikakurupuka fastaaa kwa Freddy usiku huo huo sijui saa 8. Mlinzi ananijua akanifungulia. Freddy akagoma kufungua mlango.
Namsikia yupo ndani kabisaa, nimegongaaaa nimegongaaaa. Nikakaka pale pale mlangoni Masaa ma wili kila saa mlinzi anakuja kuchungulia naondokaaa. Naona aliona boss wake kubwa la maadui sio kidogo. Saa 10, mbu wamenilaa sio utani, akafungua mlango, ingia usije kuumwa malaria. Nimeingia najikuna mwili mzima mbuuu wamenikomeshaaa. Basi kaa mbali hachekii, kama hanioniii.
Nikamsogelea, akasema sitakiii, nenda kwa Troy, wewe wa kuniaibisha mbele za watu. Nikaanza kujielezaaa masaa 2 tena. Troy anafanya business tu, tunaongozana China, naondoka Kesho jioni ndo anaenda kunionesha masoko huko China. Akajibu tu haya. Nimekaa najieleza masaa ma 3. Hamnaaa kitu holaa. Nikajiondokeaa tu. Wala hata hakunistopishaa nendaaaa. Nikawa najua sasa baaaaaaaaaaaaaaaaaas. Jioni naend airport, nimecheck in na Troy, nimekaa economy mawazo yamenishikaa sio kidogo. Safari niliona ndefu sanaaa. Tumefika China tulipanda Emirates, tumetoka Airport nikasikia Anna! Nikastukaa sauti ya Freddy kabisaa. Nikajua mawazo tu ukiyaendekezaaa yanakudhuruu unaanza kuimagine vitu. Akaja kunigusaaa. Nilistukaaaaa. Umekujaje hukuuu? Umepata wapi viza? Troy anashangaaa, hana la kusema. Akaniambia twende.
Nikamuaga Troy juu juu tu sasa nifanyaje the love of my life yuko pale mbele yanguuuu. He followed me to China. Nikamfata, akaniambia mi ninayo visa ya mwaka unlimited entry. Weeeeeeeeeee! Ni rahaje jamani. Basi all of the sudden China was Pink full of love. Ukikaa na Freddy huishii maisha ya kubahatisha kujibana bana Xhuxanlo sijui hotel mbuzi unajiachiaa 5 star.
Mchana anipeleka masoko, anamlipa mchinambebabji wa mizigo, ananisaidia kuchaguaa, jamanii si utasema mume ndo huyuuu. Hela zikisha tunatumia za kwake anasema utanirudishia ndo nisha hongwa hivo. Baada ya mzigo kutosha tukaenda viwandani anaenda kutoa oda yeye sasa za mizigo yake. Basi ana jali, mnafanya hustles mchana, usiku game. Mizigo yangu akaweka kwenye container zake. Basi kuliwa nchi za watu raha sanaa msisikie. Kwa zile siku 15 tulizo kaa kule mambo yalikuwa bam bam. Freddy anajua kupenda wewe hamna mafanooo. Anajaliii, afu yuko humble, mtu ane oda containers kukusindikiza kwa wamachinga uchukue pc 50 sijui ngapi, sio rahis tena anafanya kwa moyo kabisaaa. I was so inlove with me. Tuka hangout na Troy pia siku moja huko huko China. Anaingia club za downtown Ghuanzhou zile za wachina wenye hela balaa. Na mimi niko pembeni yake, Mrs wa msimu, life can be sweet.
Nikawa naomba Mungu siku hizo 15 zisiishe.
ITAENDELEA KESHO SAA 4 USIKU.