Weekend story! Dare the devil and face your own ghosts!

Pastor wa gia number 4 leo anaenda kuumbuka kwa Gia namba 2 tu....
Huyu mwanamke Violla hafai ku date na mwanaume mwenye akili ndogo.
 
Ha ha ha ha ha Lara utanivunja mbavu mwenzio loooh nakupenda my Dada yaani unanitoa stress zote na hii story..ubarikiwe sana
 
Jamani Raul ni kiboko huyu kaka loooh sasa kumponda violla eti hajui kupika blah blah ha ha ha ha huyu kaka ni maumivu ka jipu la kwapa looh
 
@lara1 hii story ni nzuri sana,can't wait mwisho wake..najua pastor atarudi tu kwa v,wanapendana hawa
 
Anyway Mungu atanilipia kwa namna ingine.[/QUOTE]
Eee Mungu Baba wa Mbinguni, Mbariki Dada huyu( huyu na Kazi za Mikono yake, ili aweze kuendelea kutupa furaha Sisi wanyonge, Ambao akianza kuchajisha naweza nikashindwa kumudu gharama ya hii Furaha yangu,ambayo yeye ni kipaji chake........ameeee!!!
 
Pastor kuona wanakuja akajiambia to live to die another day, sio siku hio maana hakuwa kajipanga wala nini. Akachukua simu yake fastafasta akaiweka silence, Akampigia dada Cate, akamwambia naomba uje ofisini haraka kuna waumini utawakuta hapa waambie sipo nipo kwenye kikao cha dharuraaa, waongoze mpaka ukumbi wa mikutano waningoje hapo. Cate akawa anauliza kwanini Pastor? Pastor akaanza kufoka huu sio muda wa maswali na majibu ni mda wa kutii na kutekeleza maelekezo nayokupa. Cate akasema sawa boss.

Wakagongaaa mara ya kwanza, mara ya pili, mara 5, hakuna jibu. Florida akasema maybe hayupooo, Violla akazungusha kitasa kikafunguka, Florida akashangaa kwanini Pastor hakuitikia? Kuingia ndani kweupeee! Ofisi haina mtu. Florida akazidi kushangaa kwanini Pastor aache mlango wazi! Wakakaaa. Hawajakaa vizuri Cate huyooo, akajitambulisha yeye ni Cate, pastor kapigiwa simu ya dharuraaa, so amewahi mkutanoni na kumpa maelekezo afunge ofisi, ndo kaja kuifunga so wakamngoje chumba cha mikutano.

Violla akaona pale iko namna kuna chezooo afu halielewi, akachukua simu akaipiga akitegemea kama pastor kabana mahali simu italia huko alikobanaaa. Kimyaaaaaaaa! Kaipiga mara 3. Akasema bahati yake. Pastor akawa anaona Violla calling akatikisa kicwa na kujipongeza kwa kuiweka silent mda ule. Maana yule dada ni kiboko, unachowaza wewe yeye yupo hatua 5 mbele. Balalaaa hilo. Basi yule dada yupo twendeni kule. Violla akaweka simu juu ya meza, akaanza kujisemesha eeh hilii picha ya kongamano lilikuwa na watu wengi. Cate akamwambia dad twendeni kule. Violla akasema sawa ngoja nichukue pochi yangu. Akawa anawaza atabakije mule maana alijua kuna namna, au apandishe mashetani fake? Akawaza kuja kukemewa na kutiwa misingi ya bure hataaa. Akachukua pochi akaiona simu yake akaiacha kusudi wakatoka wote Cate akafunga mlango kwa nje.

Wameenda kama nusu hatua Violla akasema nimesahau simu yangu pale mezani? Cate akawa kachoka akampa funguo akaichukue. Akasema hapo ndo anapopataka. Pastor akawa katoka chooni, kakaaa kwanza mezani anatafakari tukio zimaaa, mara anasikia mtu anaingiza ufunguo, akawaza Cate? Akaona achungulie akakuta Violla . Akakimbilia chooni alikojibanza mwanzo. Violla akaingia akaa kwanza. Afu akamwambia Bryan toka huko chooni bwana, najua upo chooni. Bryan akasema atakuwa ana blaff, akachuna!

Violla akamwambia bwana najua upo chooni, simu yako umeisahau hapa mezani wakati tulivotoka haikuwepo, hii round 2 najua hukujipanga maana nilivotolewa humu ukajua ume save. Hahahaaaaaaaaa! Bryana akaweka mikono kujipiga kichwa sio kwa kusahau simu kule. Violla akasema nasoma sms zako huku, kama kidume bana huko nisome sms zote na nikikuta namba ya mdada nampigia bila kujali nani wala nani na kuwaambia mimi mkeo. Bryan akatoka chooni kwa aibu, akwa anacheka tuuuu. Sio kwa kubambwa kule, na Violla akawa anacheka, anampa uso wa ushindi. Bryan yupo usingesahau simu ningekuwa nimesave. Violla akamwambia what makes you think nilisahau? Niliiacha kusudi ili nirudi, nikawaza ningebaki mda ule lazima ungekuwa umelock choo, so nisingekubamba, ndo maana sikujaribu kukifungua mara ya kwanza kukupoteza maboya tu kuwa i buy the meeting story.

Nilijua upo coz gari yako ipo parking niliona wakati naingia, afu kama ungekuwa na mkutano wa dharura hapa either ungekuwa chumba cha mikutano au humu, sababu Cate alisema twende chumba cha mikutano nikajua tu lazima uko humu ndani, nikaacha simu ili nikiirudia nikukute kwa kukushtukiza. Hahahaaaaa! Busted! Bryana ikabidi tu atabasamu. Violla anazidi kumchamba wima wima, i thought you had more balls, to face us man to women, after all we just a bunch of women, but you resorting to hiding in the toilet, to save your a.ss is so sissy and girly. Hahahahaaaaaaaa! Who would have imagined you the almighty pastor is this balls less! Hiding like a little girl, scared piece of shit, i bet if your dad was here you have ran to dady sissy! Bryan akaingilia, enough, yes i am scared, yes i hid in the toilet, yes i am a coward, and yes that was girly of me, i get it you dont have to tell me. So lets get down to business. What do you want now you have in the corner you want. A glorified apology of the century? You want me to go on my knees and beg for for your forgiveness? You gonna black mail me to do do what you want or else you will tell Florida, or cause a scene? You gonna bully me now? What is it you do tough girl? What?

Violla akacheka kwanza, akamwambia tu, i was just gonna say goodbye! I wish you all the best. Akachukua mkoba wake na simu yake akachimba. Akataka kuondoka kimya kimya ila akagongana na Florida njiani. Ooooooh! Here you are nimekutafuta sijakuona. Violla akazuga tu aah iwas kind of lost. Basi Florida anamshawishi wamngoje pastor, V ashavurugwa zake akamwambia tu, kuna mahali natakiwa but nitakuja another day. Florida akawa anamuonea huruma, anamwambia kuna birthday ya mdogo wangu Alhamisi ijayo make sure you come. Violla akamwambia nitajitahidi dear.

Violla akaondoka zake, akaenda ofisini. Roho ikawa inatamaniii ampigie Raul, anavomjua Raul atampeleka kona kona amabazo itabidi aeleze vyote hata ambavo hajapanga kueleza. Kila mda anashika simu afu anacha. Akachoka nafsi yake mwili na roho. Akamkumbuka yule kaka anaemtongozaga hapo ofisini. Akajiambia how better to forget someone by getting someone else. Akamfata kwenye ofisi yake, akamuuliza tu, still interested in that dinner? Yule kaka akabutwaa, akajibu tu Yes! Yes! Violla akamwambia 2 night then. Akasema absolutely. Baada ya Violla kuondoka akakumbuka hana balance ya hio dinner, ana 100,000 tu Mpesa kumalizia huo mwezi. Afu ashamkubali mtoto Violla, kwa watu kama yeye kila siku sio Jmosi ujue aseme asiende leo waende siku ingine, akampigia mchizi wake Hamis amkopeshe 200,000. Ammy akamwambia jioni saa 12 uhakika, asiwaze. Akawa karelax kabisaaa anamtegemea Ammy.

Violla kazi haziendi, akaamua anede kwa shoga wake anaeleta nguo za UK, aangalie tu na kununua chochote kitachoingia mwilini kupunguza stress. Akamkuta anavuta kimsokoto. Basi anakivuta kwa bashasha ana enjoy na anaonekana relaxed. Akamtolea masanduku akaendela kuvuta tu kitu chake kwa raha kabisaa. Yule dada akamuona Violla anautolea macho ule msokoto, ikabidi tu amualike, maana na yeye alikuwa anavibania vipisi vyake, ila anyway maana alionekana wazi kavurugwa. Akamkaribisha tu "Unatumia haya mambo?" V akawaza fasta akasema kuna mwanzo wa kila kitu. Akakurupuka "Ndio natumia, thanks for asking thought you were never going to ask, ndo mambo yangu hayooo." Yule dada akatoa kikaratasi juu ya kabati akasema ayaaa hizi zimeisha too bad, sikujua nika restock, anyway kama mzoefu nina kitu nilikitoa UK, cha Jamaica mojaaa, nilitumia kimoja kilinibabatiza vibaya mnoooo. Sijajajribu tena labda nikupe ujaribu. Violla yupo nipe mkubwa, mimi ndo mambo yangu hayaaa. Akamgea kimsokoto kidogo sanaaa. Akamuwashia. Violla cause anatumia sigara akaona kawaida tu, akakivuta kwa pupa choote kikaishaaa. Yule dada akamwambia nimekukubali kamandaaa, wewe mamba yao. Looooh! Kikawa stimu hazijampanda sasa. Akaona ulikuwa upotevu wa pumzi tu. Dada akamshari asidrive, kikianza kukolea ni balaaa. Violla akalipa akashika usukani moja.

Njiani akaanza kuona magari saba saba! Akafunga breki, akapaki pembeni. Anaona dunia inazungukaaaa! Akachukua simu ampigia Dada ayake, namba anziona kubwaaa! Akajitahidi akampigia. Dada yake akaja na boda boda akamuendesha mpaka kwao. Kufika anasikia kiu kali, akaende kunywa maji kwenye dispencer anaona kikombe hakimtoshi. Akalala pale kwenye dispencer akafungulia maji yanaingia tu mdomoni. Kanywa lile dude kama robo nzima! Bado ndo kwanza stimu zinachanganya. Akaenda kukaa kwenye shower na nguo zake akafungulia maji ya baridi kama lisaa zima. Kidogooo akili zikaanza kumkaa sawa. Akaendela dozi ya maji baridi, kunywa na kujimwagiaa, saa 11 akaona kidogooo ana nafuu, ila hali yake kama mgonjwa wa homa.

Akakuta Pastor 10 missed calls, akampuuzia akampigia yule mchizi wa ofisini Tito, wanamuita T. Akamuuliza mtoko wapi? T akajichanganya chagua mwenyewe. Violla akachagua Zhonghaaa. T akasema poa, poa. T akamcheki Ammy hio 200,000 ni aje arif? Ammy anazingua zingua afu saa 12 hio. T akaamua aende kibishi na laki itamtosha kwanza Zhonghaa sio sehemu ya maana kihivooo, wachina hawanaga bei. Kufika akamkuta Violla. Ikaletwa MENU. Kuicheki hivi anaona 80,000 120,000, 300,000 chupi ikambanaaa. Cheapest meals ni 35,000 26,000. Balaa hilo. Akaaanza kuiona ile 100,000 ndogo sanaa. Ila akajikaza kiume na kumtext Ammy amrushie hio pesa asilete masihara.

V akafika kwanza akaagiza wisky ya kichina. Akamuita yule mchina akawa anabonga nae kichina, bwana nimevuta bangi imenizidi naomba unifanyie portion ya kutoa hii Bangi mwilini. Mchina akasema iko portion ya kutoa sumu ila ni 120,000. T hakusikia vizuri ila akajua tu iko namna. Maana akaona wanachukua majani wanaenda nayo jikoni wanakuja kumuuliza Violla kama ingradients hana allergy nazo. Akasema hanaaa. Yeye akaagiza maji, sasa mdude aliogiza Violla akauona unakuja, umeandikwa kichina tupu afu uko kenye kichupa kidogooo, inakuja ki glass kidogooo. Mmmmmmh! Akawaza lile dude kama sio 300,000 sijuiiii. Akachuna kwanza. Wakaleta hio portion ikiwa kwenye kichungu inachemka, wakamuwekea akainamisha pua Violla ule moshi ukamuingia wote. Akajiuliza hii ndo shisha ya kichina au? Ila akaona pale maji marefu.

Akaenda chooni, njiani akamuita muudumu na kumuuliza ule mdude anaokunywa yule dada bei gani kwanza? Muhudu yuko hauna hata bei kaka ule mbonaa, usiogope ni 88,000 tu kwa kile kichupa, na mtu walau anywe 2 ndo apate stimu inayotakiwa. Mmmmmmmhhhh! T akaona maji marefu, huku Ammy hamjibu bora tu atumie sanaa kujiondoa. Akaenda chooni karudi kawaza anamtoka vipi Violla. Akamwambia mshakaji wake ampigie, akapokea kwa bashasha, haloooo, eeeeehhhh, imekuwajeeee, sawaaaaa huyo mpaka kwenye gari lake, motooooo. Akamuacha Violla pale. Violla kumpigia baada ya kuona haji, akajua tu bill imemkimbiza. Akaona sio kesi akamuita Raul!

Raul kuja ikawa full shangweee! MENU imeletwa, Raul yupo nishauri wewe mchina ninywe nini? Mchina yuko ya bei gani labda? Raul yupo bei sio issue, nishauri ninywe kitu gani cha uchinaniii ambacho sitajutia, nataka niwe mteja wa kudumu, huyu dada hapa tapeli, mtu hajawahi kwenda china anajua kichina chote, anajua mpaka wine. Wewe nishauri, nisipolewa silipi, nikilewa sana silipi, chungu silipi. Mchina akacheka. Akamshauri dude la 100,000. Akasema letaaa. Na chakula usitulishe nyoka na kono kono. Mchina akamwambia kula oxtail soup inaongeza nguvu za mzee. Raul akasema niletee hio nina kazi nzito leo 120,000 ingine. Ikawa sasa mwendo wa kugida maji, kampa kampa kampa tenaaa. Wakaona haina stimu changanya whisky za kichinaaa. Kikawakaaaaaa, ikafika mahali anajifinya Violla kucheki tu kama hajafa na kufika jehanamu au haoti ndoto.

Wameenda wameenda ikafika saa kanasaaaaaaa. Hawezi kujitikisa kabisaaaa. Akasema mama ndo nakufa mimi hivi kimoyo moyo. Akaona giza. Akazima kwenye meza. Raul akaitisha bili, ikaja 780,000 akawauliza mnapokea $$$ wakasema ndio kwa rate mbaya lakini, akawalipa $$$ akajibebea mzoga wake akaishia.

Violla anastuka yupo kwa Raul, afu kavaa chupi tu. Akachoka mwili na roho.

ITAENDELEA SAA 4 USIKU.
 
Khaa, Lara, hii kali, umeuaaa. 'Anajifinya kuona kama hajakufa' LOL
Yani hii story kadiri muda inavoenda ndivo inapozidi kuwa tamu zaidi.
Leta mambo, saa nne hiyoo...
 
Hahahhaha! Namhurumia sana huyo Tito hiyo mvua ya matusi atayokula huko ofisini kesho yake...Yaani sipati picha....Una laki unatoka na demu? Hata Uswazi siku hizi laki haitoshi!
 
Hahahhaha! Namhurumia sana huyo Tito hiyo mvua ya matusi atayokula huko ofisini kesho yake...Yaani sipati picha....Una laki unatoka na demu? Hata Uswazi siku hizi laki haitoshi!

Hahahaaaaa! Mishahara yenyewe 500,000 kutoka ukachoma 100,000 nzima ujue sio rahisi. Mi ndo maana namshukuru Mungu kila siku nimezaliwa mwanamke, sipati picha ningezaliwa mwanaume ingekuwajeee. Ningeteseka sanaaaa.
 
Khaa, Lara, hii kali, umeuaaa. 'Anajifinya kuona kama hajakufa' LOL
Yani hii story kadiri muda inavoenda ndivo inapozidi kuwa tamu zaidi.
Leta mambo, saa nne hiyoo...

Hii kwa sisi watu wa bata ni kawaida, unakuta umekunywa vitu majina huyajui, umevuta shishah, bangi, umewakaaaa haswaaaaa. Sasa unajifinya kujua kama uko hai na huoti. Mnake mda mwengine unaweza lala usiku ukawa unaota bata refuuuuu, afu badae unastuka kumbe ilikuwa ndoto. Hahahaaaaa!
 
Ooh ok!!but mbna kwa simu haizingui wala nini?mi natumia simu pia au kuandika kwa simu unaona untek tym ndefu kutype??
 
Back
Top Bottom