Violla akasema ngoja nimuanze huyu pastor, kuassume atanianza yeye anaweza asinianze wala nini. Akamtext Hi baby! Kupima upepo you know! Ikajibiwa tu Hi! Kavu kavu haina condom wala baby! Mmmmmmmh! Akaona kumekuchaaaa. Akaanza kujibebisha, baby nimeamka sijakukuta, i missed you. Akangoja jibu weee. Wapiii.
Kama nusu saa hivi, akakumbuka ni jumapili, akajua pastor kaondoka atakiwa anahubiri kuleee kanisani kwake. Akafikirikia hiki na hiki havikai. Akaamua ajindae avae nguo aende huko huko kanisani kwao. Akaanza kukunguta kabati nzima kutafuta nguo ya maana, ya kueleweka ya kusema shut the front door! Pants dropper! Akatoa nguo koja hivi alipewa na dada yake, kigauni very expensive, akachukua na miwani yake, na Stiletho heels ndefu.
Akatinga kanisani akakuta ibada iko katikati. Akacheki sms kama imejibiwa haijajibiwaa kabisaaa. Akwa kakaa anafatilia mahubiri ila macho kodo pande zile. Kwaya ikapita pale, mara Pastor akaanza mahubiri ya neno ndo afanye maombezi, wtau wote wamekaaa. Akanyanyuka akapita kati kati, mradi tu pastor amuoneee. Akatoka zake njeee, sio mpenzi wa neno kabisaaaa.
Kufika nje akawa anatafuta sigara kwenye mkoba wake ajipoze koo. Mara anashangaa dada samahani, akasitisha zoezi, bila samahani kaka. Bwana asifiwe! Violla ugeni wake ule akajibu tu Milele amina si ashazoea Roman. Yule kaka akatabasamu akamwambia huku tunajibu Amen. Wewe ni mgeni? Akasema ndio. Basi akawa anajiongeza yeye ni supplier wa vitu town na rafiki mkubwa wa Pastor Bryan. Ile kujifanya yeye nda pastor damu damu. Violla aka mwambia yeye yupo yupo tu mjini anahangaika na maisha. Story zikanogaaa vibaya mnooo. Akaja kumwambia jina lake anaitwa Jaochim, au simply Joe. Basi story zikaendelea Joe akamwambia Violla Pastor anampigia kelele swala la kuoa. Mmmmhhh! Violla akamuuliza mbona huyo Pastor yeye hajaoa? Au kaoa mimi mgeni. Joe akaanza kubwabwaja, Pastor hajaoa but ana mchumba!
Violla akastuka! Akawa anamchimbaaa, huyo mchumba yupo hapa hapa kanisani? Joe ana bwabwaja tu ndio yupo hapa hapa ndio, actually ni family friends wazazi wao, na baba wa binti ame invest sanaa kwenye hili kanisaaa. Ni mmoja wa wazee wa kanisaa. Huyo bnti alikuwa nje ndo karudi recently, so its not official but baba Bryan is kind of selling the idea to people. Violla akauliza tu, how long are they dating. Joe akamwambia i would say 2 years, maybe more. Violla akachoka kabisaaa. Wakabadilishana namba na Joe, then wakarudi wote kwenye maombi. Maombi yalivoisha tu hakuwa na mood kabisaaa, akajikokota zake akaondoka. Alivotoka tu nje, Joe akamkimbiliaa akawa hana hata points specific anayoiongea kutaka tu watu wamuone yupo na Violla. Mara Bryan akawa anakuja upande wao, Joe anamwambia Violla let me introduce you to our pastor, Anaita kwa nguvu Pastor Bryan, Bryan akawa kawaona but watu wanamtinga kati kati kumsalimu na kuongea nae.
Violla akatumia mwanya huo kusepa kimya kimya. Joe kustuka Violla hayupo, akawa kamfikia Pastor lakini. Wakasalimiana, Pastor swali la kwanza akamuuliza yule dada nani uliekuwa umesimama nane. Joe akamwambia Pastor, uliniambia mke anatoka kwa bwana, na siku ya 1 nikimuona tu huyo mke, nitamjua wala sitokuwa na shaka tenaaa. Leo nimemuonaaaa. Pastor kakomalia yule dada nani? Hasikizi hata ushuhuda wa muumini. Joe basi yuko exited kumwambia Pastor wake, yule dada nimemkuta hapa leo, and i knew the minute nimemuona kuwa nimeletewa na bwana. Halleluyaaah! Pastor im so happy, so exited, so feeling blessed. Pastor pray for me that girl becomes my wife. Actually nataka nitoe sadaka kubwa kabisaa to see that happens. Joe anajimiminaaa pastor hata hayupo nae kiakili.
Violla akarudi kwake akawa anajiuliza amuulize au asimuulize? Akaona akimuuliza he will cover his tracks na hatojua ishu yoote, atafanya maamuzi ya kukurupuka. The right thing ni kumchimba Joe mpaka ajue undani wa hio habari, ndo aamue atachoamua. Ila akajiona na gundu sio dogo. Huyu nae ana mwanamke mwingine khaaaaaaaa. Akawa amekaa tu kwenye kochi akili ikimzungukaa, ikaingia sms. Pastor huyooo. Sorry babe, ilibidi nikukimbie had to come to church for preparation and all. Violla alivoiona tu ile babe, akaamini maneno ya Joe, Pastor si wa kuja na gia namba 1, siku zote ni wa namba 4. Akasema ngoja ausome mchezo lakini. Akamwamndikia tu I miss you. Ikaja text from Pastor inamuuliza that guy niliekuona nae church leo, what did he tell you? Violla akaona eeennnnhhhhh mambo tayariiiii.
Akaamua kucheza fools card, akalipotezea hilo swali, akabadili topic, thought you would happy to see me in church, maana unanialika sanaaa. Decided to get used to my sheep since soon i will be Mrs Pastor. Ili kutikisa tuu. Pastor akajibu na ki emoji, akamuuliza would you leave your Roman Kingdom to be Mrs Pastor! Violla kumchimba tu akajibu Yes, anytiime any day, the Romans can kiss me good bye. Pastor anamuuliza so you wont mind duties of a pastors wife? Violla anamjibu not at all. Pastor yakamshinda akarudia swali, the guy in the church what did he tell you?
Violla akamua kumchezesha makida makida sasa. Akamwambia tu nothing special, that you are a good pastor, he is doing business, loves to worship in your church, normal blah blah blah. Why?" Akamtega . Pastor hakuwa convised cause anamjua Joe domo kaya hakai na kitu. Akamuuliza tena "nothing else at all" Violla akatabasamu akasema leo utacheza makida makida ya kutosha. Akamjibu tu "Nothing, now you get me concerned is something i should know, he should have told me about?" Kumpima imani tu pastor. Pastor akajibu hamnaaa, Joe sazingine anakuwaga muongo muongo sanaaaa." Violla akataka tu kumtia jamba jamba akamwambia "Actually he did tell me something to be honest" Pastor hapo hapo akajibu What?. Violla akaipotezea ili amshindishe tu tumbo joto huko. Zikaingia sms za What kama 4. Alafu ikapigwa na huyo huyo Pastor 2 missed calls. Akazipotezea zote.
Ikapigwa ya tatu na Pastor akaipokea, what did he tell you, kapanic kabisaaa, Violla akamwambia that you are pressurizing him to marry, look for a wife, and he would like to go to dinner with me. Akamsikia kabisaa pastor anashusha pumzi. Akasema tu Okay! Violla akamuuliza Okay nini sasa? Pastor hakujibu tenaaa. Akajitafakari akaona ampigie Raul for ushauri, you know.
Akamwendea hewani Raul, Raul akapokea, Violla leo umenikumbuka itakuwa una shida kubwa sanaa. Pastor hajambo? Violla akasema sijamuona toka umfanyie vitimbi unadhani. Raul akamwambia acha kunizingua ulilala nae usiku kucha, tena usinikumbushe. Nilirudi ujue, kuja kukuomba msamaha namuona Pastor anaingia akafunga na geti. Nusra nusra almanusura ile kunusuru niwaite global publishers wangoje akitoka wamu ekotikeeeeeeeeee. Basi tu nikajikaza kiume kwenda kwangu kulala. Ila kimeniuma sio siri wewe kumchagua him over me. And the sad part is he is a hypocrite, you will find out, better me the devil you know, that him the angel you dont know.
Violla akamwambia wala utabiri wako haupo mbali, he has a fiancee afu haniambiii, bora hata wewe baby mama, nimeruka mikojo nimetua kwenye nnya na miguu miwili. Raul yupo, i knew it. Come back to papa! Hahahaaaaa! Violla akamwambia shida yake ni jinsi gani ataujua ukweli.
Raul akwambia yani mission destroy Pastor hapa haishindikani, iko namna nzuri sanaa ya kuujua ukweli wote. Akawa kamuelezea na Violla akaubali yeye na Raul ni Mr and Mrs Smith. Pastor hachomoki hata kidogo kwenye hilo mission. Pastor akaja kumwambia he regrets what happened to them both, it was a mistake, he is dedicated to serving God. Kilimuuuma maan alijua tu coz ya huyo bi dada mwingine. Akawa kazini kazi haziendi kabisaaa, anaona plan la Raul halitimiii.
Joe akawa anamuita for lunch, dinner anachomoa. Siku isio na jina Joe akamualika kwenye birthday yake, akamwambia Pastor atakuwepo na yule demu atakuwepo pia. Violla kukomoa tu nae akaenda na Raul kwenye hio party. Yule dada alikuwepo mwanzoni ila pastor hakuwepo, so Violla akatumia hio chance kumzoea yule shosti. Afu akaja kumjua ni mtu poa sanaa, sema tu they have interests in the same man. Basi bi dada anaitwa Florida, cause she was born in Florida, very sweet, anamwambia i have a fiancee ni pastor. Violla yuko Waoooohhhh! Anamsifia Bryan mpaka basi. Violla yuko actually i was looking for a pastor, i am currently under demonic attacks, serious spiritual issues, can you please introduce me to your Bf, for help. I am dying here! Demons are killing me day by day, im dying! Akaanza kujiliza. Basi Florida yupo, haina shidaaa kabisaaa, jumanne hamna watu wengi, tutaenda wote ofisini kwake nitakupeleka, Mungu ni mwema, hutokufa, utaishi, kuwa na imani. Basi Violla ndo akapata moyo wa uongo.
Baadae Florida anamuuliza Joe anakuita V, what is your full name, Violla akamwambia V stands for Vanessa. Basi Florida akawahi kuondoka kwenye hio party. Alivoondoka mda mchache akaja Pastor. Huku kwa Joe, V kamtambulisha Raul kama kaka yake. Basi Joe anampa Raul heshima zote za kaka mkwe ikiwemo kumfatia bia mara kwa mara kwenye friji. Joe anajinyenyekeza hana nia mbaya na dada yake, ana malengo mema tu, na angeomba support ya Raul kufanikisha azma yake ya kumuoa Violla, Raul anamwambia huyu dada angu sikufichi mvivuu ni balaaa, kupika hajui, afu mtu wa bata sanaaa, atakusumbua shemeji. Nashukuru kwa bia ila umekuwa mkarimu na mwema sanaa kwangu na dada angu ndo maana nimekwambia ukweli. Joe akawa anashangaa but hakati tamaa, anamtaka dada mtu hivo hivo. Raul yupo kma unangangania poa ila unajitia shoti tu pale. Akaendelea kupewa huduma za kifalme.
Alivokuja tu Pastor, Raul akamuwahi, Bwana asifiwe! Pastor akashtuka kumkuta akajibu tu Amen! Unafanya nini hapa? Raul akamuoneshea V! Pastor akatikisa tu kichwa. Raul hakumkawiza akaanza kumzeveza you broke her heart you know? But luckly i am here to mend it. Pastor anazuga i dont know what you are talking about. Raul anamvuruga zaidi, anyway shamba lilishakushinda nalilima mwenzio sahivi huoni linavongara, cut me some slack basi. Pastor akamuangalia V, akakaa kimya kwa mda then akamuuliza hili shamba how long umeanza tena kulilima. Weee! Raul ndo alivokuwa anataka, yupo dont feel bad, i dont wanna make you jelous or anything but i would say soon after you left, sonner actually." Pastor akabinua mdomo kwa frustrations. Raul anazidi kumvuruga, just a piece of advice, girls like that wont last long in church, she is a devil no matter how hard you convince yourself, Lucky for you hell wants its devil back, all you have to do is let her go, where she belongs. Pastor akakaa tu kimyaaa. Raul akaendelea kubwabwaja pale mpaka Pastor akamkimbia na kuondoka kwenye hio party bila kumsalimia V.
Raul akamwambia V uju pastor alikuwa hapa kaondoka sasa hivi. V yupo wapiiii? Raul anamwambia keshaondokaaa mdaa. V kwa kumjua Raul, alijua tu hawezi kumshutua pastor alivokuwepo. Usiku wakayeya home, kila mtu kwake. Kufika tu, pastor kampigia afu kitambo kweli alikuwa hajapiga. Akapokea Bwana asifiwe! Pastor akajibu Amen! Usingepokea ningejua umelala na Raul! Bahati yako. V akamuuliza kwani nikilala na Raul kuna ubayaa? Last time i checked i was the mistake. Bryan anakoma yes i said so, so what? kila tukipishana kauli kidogo unarudi kwa Raul is that the life you have chosen? V akamuuliza kwa hio wewe ndo mwenye msimamo, maana kati yao Pastor ndo haelweki kama bunduki, mbele chuma, nyuma mbao. Mara they close, mara kama hamjui. Inamboaaa V. Akamchana live. Basi pastor yupo atleast mimi i know what i want, hata kama kuna issue btn us i still know what i want that is you, ila wewe hujielewi. V akamuuliza tu una uhakika you know what you want? Pastor akaja juu anamaanisha nini? V akamwambia they will see about that.
V alivoona hawaelewani lugha akakata simu, moyoni anasema dawa yako iko jikoni inachemka. Akatuma sms kuchimba mkwara kwa hio unanikatia simuuuu? Si ndio? V akawaza tu usikatiwe simu wewe nani bwana. Akajipumzisha kwanza kesho kazini, na jumenne keshokutwa tu. Jumanne kufika, akavaa zake akapendeza akampigia Florida, wakakubaliana waende kwa pastor, waongozane.
Pastor anacheki dirishani anawaona wanakuja wote wameshikana mikono Florida na Violla, akasema tu fack! I should have known it Vanessa ndo Violla taht girl is something else. Hapa nasevuje hapaa maana you cant tell what the V girl will do next. Kichwa ikaanza kumchemka. Violla anawaza tu Pastor atavoadhirika na shock, na atakavo kuwa mdogo wakimvamia wote ofisini, she cant wait to see his expression. Itakuwa ni pants dropper hio expression yake. Yaaani, yaaani, yaaaani akawa hapati picha, akawa anasema ngoja tufike itajulikana uko uko. Leo aibu zake mwenyeweeeeee. Wakafika ofisini wakagonga
ITENDELEA KESHO SAA 7.