Akawa kamuomba directions za huko kwake. Ikawa kafika sasa kwa pastor. Akafunguliwa geti na wa kiume wa pastor. Akaingia sebuleni. Akawa kakaa kwanza. Pastor kaja na nguo za mazoezi basi body ndo liko on display madai katoka kupasha. Violla akaanza kumuelezea tu, ilibidi nimuulize baada ya kuniambia you see another woman woman. And yes there is a woman, tena wana mtoto. Sikuwa nimejua coz she is abroad, Pastor what have i done wrong? What have i done to deserve this? I am such a nice person, why do i have to face all this? Machozi yanamtokaa ya uchungu.
Pastor anamwambia ni mambo tu ya kawaida ya kibinadamu, hutakiwi kuwaza saaaana. Sometimes Mungu kakupangia makubwa zaidi ya hayoooo. Violla akamuuliza Pastor in the spiritual world what do you see about my future? Is there a part that i will be really happy? Maybe happily married with kids? Au kama hamna la maana wewe niambie tu ukweli usinifiche niishi kwa kujiachia. Pastor anamuelezea sasa siwezi nikaona your future like that, mpaka nioneshwe na Mungu or nifunge na kuomba mpaka nipate kibali cha kuona ya mbeleni, it is not that simple. Honestly i know nothing of your future.
Violla anangangania basi pastor kama vipi naomba ufanye hayo maombi ya siku hizo 7 au mwezi ila upate kunisaidia kujua future yangu imekaaje, what do the heavens have to say about it? I really need to know. Basi Pastor akamwambia sawa mimi nitakuombea haina shida. Ila ni muhimu sanaa, sanaaaa uwe unakuja kanisani Jpili. Violla akaona vile ameomba aombewe maombi mazito akijitia kibri kutoenda kanisani kwao atakuwa haombewi. Akasema tu sawa nitakuwa nakuja. Pastor anamuuliza promise this Sunday? Violla yuko promise wakati anajua kabisaa haendi kokote.
Akaaga pale akaondoka zake, kurudi nyumbani kwanza kujipumzishaaa. Kufika nyumbani dada yake anamwambia una habari bonge kapata bwana mpya anataka kumuoa na wanae? Tena boss mkubwa tu! Violla akabakia kashangaaa! Eeeeeeh! Akaambiwa habari ndo hiooo, na ubonge wake, na wanae 2, kapata bwanaa anataka kumuoa kabisaaa na keshakubali kuwalea wale watoto. Ndugu wa mie mumewe ndo anakumbuka shuka kumekucha, hataki kutoa talaka, hataki kusikia nini, anampenda mkewe madai yake. Loooooh! Alivomnyanyasa dada wa watu ni balaaa.
Violla akachoka kabisaa, bonge ndoa ya 2 hio, yeye hata moja bado, na alivokuwa anamchamba wima wima siku ile ameumbukaje sasa? Balaaaa, balaaaa! Akawa kajipozisha kwanza kitandani apate kunyoosha mgongo, ikaingia sms ya Pastor, All will is well! Na vifungu kibao vya biblia. Violla akaona kupunga mawazo amchagize Pastor, akamuuliza Pastor anapenda kitabu gani katika biblia yote? Patsor akajibu anakipenda kitabu cha Matayo. Akamuulia na yeye anapenda kitabu gani? Violla akajibu Wimbo Ulio Bora. Kumchagizaa tu. Pastor akamuuliza kwanini unapenda huu Wimbo ulio bora? Violla akamjibu basi tu naupenda. Pastor akamuuliza unapenda zaidi verse ipi?
Violla akamjibu Song of Solomom 1:2 ambayo inasema "Let him kiss me with the kisses of his mouth – for your love is more delightful than wine" kumchagizaa tu. Pastor akamjibu yeye katika hiko kitabu anapenda Song of Solomon verse 3:4 ambayo ikabidi afungue biblia aisome fastaa ikawa inasema hivi "Scarcely had I passed them when I found the one my heart loves. I held him and would not let him go till I had brought him to my mother's house, to the room of the one who conceived me" Mmmmhhhhh! Akaguna Violla akaona kazidiwa nguvu kina kirefu. Basi kila akikaa anamkumbuka Pastor na lile bdoy lake. Akaona ule ni uchuu tu wala sio upendo na dawa ya uchu ni kuonja kitu, afu ukishakionja hamu inakuwa inakutoka basi.
Pastor akamwambia ile offer ya kesho jmosi bado ipo, if she is not doing anything amsindikize kwenye concert ya wasabato ambayo pastor atahudhuria. Violla akawaza na kuwazuaaa, kuwa kweli wasabato wanaimba vizuri sanaa, na wanaburudishaa mnooo, ila yeye shangingi kushinda kwenye concert siku nzima sio jambo la mchezo mjue. Ila akakumbuka uchu wake nao, ikabidi tu akubali just incase ikimuwezesha ku move forward kwenye mambo yake ya kidunia.
Jmosi mapemaa, kavaa gauni lake refu mpaka chini, utamjuaa, Wakakutana na Pastor na kwenda kwenye hio concert sasa. Pastor anamsifia nguo kama hizo ndo zinampendeza ni hatariii. Anamwambia tu, ukivaa decent unapendeza sanaaa. Violla yupo haya ndo mavazi yangu kwa wingi, yale ulio niona nayo ni bahati mbaya tu. Wakafika kwenye concert wakatengana kwanza, Pastor akaenda kwa ma pastor wenzie. Violla kasikiza nyimbo 3 tu akawa kishaborekaaa Akatoka akatafuta baa ya jiranii akawa anakunywa bia zake taratibu na kusogoa na campany ya hapo bar. Mara kamapani ikawa kubwa, mambo yakaanza kuzunguka round, ikawa kampa, kampa, kampa tenaaaa. Alikunywa bia za kutoshaaa. Wanaume wanamnunulia bia kwa fujo wanajua wakimlewesha atakuwa chips funga wakajibwedee, wanashangaa wanalewa wao tu. Kumbe akinywa 4 anaenda chooni kujitapisha zote, afu akirudi anaanza upya kunywa. Saa 11 akajua concert itakuwa imeishaaa. Akanunua ndizi mbivu akarudi ukumbini. Akawakuta The voice ndo wanaimba.
Walipotoka wakakutana na pastor, Pastor akamuuliza mbona uliondoka kati kati? Akajua kumbe alikuwa alikuwa anamfatilia. Akajikausha tu, ooh nilikuwa nasikia kizungu zungu ndo nikawa nimekaa nje kupunga upepo. kamwambia mimi nilikuja nje kukutafuta sijakuona, ulienda wapi? Ikabidi sasa Violla atumie akili za reserve, alienda kutafuta panadol na chakula. Ikawa ame save.
Basi Pastor anamchokoza ule mstari umeusomaa lakini? Violla yupo nimeusomaaaa. Pastor anamuuliza umeuonaje? Violla anaona haya najibu nimeuonaaa tu, ni mzuriiii. Basi anamsistizia usiache kuja kanisani kesho, ni muhimu. Violla anamwambia usiwe na shaka mimi nakuja kanisani uhakika. Kurudi home akapasi kabisaa, akatega alarm kwa ajili ya hio ibada ya kesho. Akaingia kulala. Kuja kustuka saa 5 asubuhi, tobaaaaaaa! Akachoka mwili na roho. Kucheki simu kakuta missed call za Raul tu. Akapumuaaa kwanza.
Jioniii Pator akamwendea hewani, mbona hukuja kanisani? Akasema nimdanganye nini nilikuwa katikati kimbembe akiniuliza alihubiri nini nitamjibu nini? Akaona bora awe mkweli tu alipitiliza kulala. Basi pastor akawa disapointed kama hata ibada ya subuhi inamponyoka, je yeye ambae mara nyingi uski wa manane ndo anaomba sanaaa, maana mbingu zipo wazi. Violla akajikosha kosha pale mradi siku ipite.
Raul akawa anaendelea kumpigia simu yeye hapokei wala nini. Anaziacha tu. Kwanza hakuwa na la kumwambia, pili alimdisapoint sanaaaa. Kubwa aliloliwaza sahivi ni kupiga mechi ya kirafiki tu na pastor, hamu imuishe afu basi. Alimtamanisha sanaaa siku ile, ikawa kila mbinu anayoifikilia ya kumpata Pastor anaiona kama haina nguvu. Na alichokuwa ahataki ni kitendo cha kukosea hesabu afu pastor amblock na huo upuuzi alikuwa hautaki kabisaaa.
Wiki ikapita bili hata matukio mengi. Ikawa Pastor hajamcheki wala nini. Violla akampigia, anahitaji huduma jioni hio hio kama itawezekana. Pastor akamwambia karibu, anytime huduma nakupatia. Violla yupo basi nakuja huko. Kafika kula huduma yenyewe kuulizia kama yale majibu ya maombi yake yamefanikiwa au bado? Pastor akawa anamuelekeza tu bado kwa kweli hayajapatikana. Akafungua biblia amsomee mistari ya uvumilivu Violla akasogea kwa pastor kule, ile kuangaliana, Violla akaanza kumbusu pastor. Pastor nae akaonesha ushirikiano mzuri tu. Denda kama la dakika 3 flani amazing. Afu wakachiana Violla akazuga kuomba msamaha as if imetokea bahati mbaya, na sio intended wala lengo. Pator yupo it is okay, okay ile kukurpushwa na matukio.
Akaaga Violla na kuondoka, moyoni akajua kabisaa hesabu pale hazikwenda vizuri, pastor ni mzito kuliko alivomkadiria. Kitendo cha kupigana mpaka denda watu mko wawili na kuachiana kinaonesha pastor ana uvumilivu wa ajabu sanaaaa. Na Violla kiukweli dozi aliyomkadiria itakuwa ndogo , huenda limu underdose. Ila sasa ndo ashakosea hesabu, na kifuatacho ITV alijua pastor atambock tu au kumpotezea kiutu uzima. Hesabu ashazikosea tayari. Akajua tu ishakuwa basi tenaaaa. Uchu wake ndo umekosa tibaaaa.
ITAENDELEA KESHO SAA 5