Hakumjibu pastor wala nini? Akaendelea na mambo yake mengine ikiwemo kuchat na Raul! Usiku ukapita huo. Kesho kazini akaingia kama kawaida ready to slay! Pendo akamuita Violla, kuwa ameona uwezo wake, na angependa washirikiane katika kazi zao. With them together nothing is impossible. Violla akaitikia moyoni akajua tu no together! Hapa kazi tu, utaisoma namba. Ila siasa za ofisni unacheka huku moyo mweusiiii.
Akawa anakuna kichwa race afanye tukio gani lizidi kumuweka kwenye ramani. Hapati muafaka, anakuna tu kichwa, holaaaa. Akakaona ngoma nzito. Ila ile tamaa ya kuji out perform, akaendlea kukuna kichwa. Akaona kama tukio hamna basi kampuni yao iandae tukio. Ndio! Akadreft proposal akaifoward mbele, event ya beach party ya watoto yatima. Vituo sita, wanamziki wakubwa kumi, zawadi za kutoshaaaa, burudani ya kutoshaaaa. Budget yake usipimeeeee.
Kikaa kikaowe can pull this off, for half the budget! Kikosi kazi kikaingia kazini, wakapiga mpungaa, wakagawana mapema kabisaaaa. Siku ya siku akawa hana hata stress. Akajua mambo yatakuwa byeeee! Wote wakawepo kikosi kazi na kama kawaida wame mu exclude Pendo na boss wont share their glory with anybody.
Saa 8, hakuna mtu, saa 10 holaaaaa! Mvua ikashukaaa ya balaaaa. Kuwapigia vituo wakaanza kutoa sababu za ajabu ajabu kuwa hawatoweza kufika. Wasanii wakaburudisha wateja kwenye beach si wamelipwa chao? Show must go on! Wakaimbia beach tupu pale, hakukuwa hata na maana ya kutupia picha. Waandishi ikabidi achikue mshiko wake aliopiga awazibe mdomo, wasipost picha wala kuandikaaa.
Jumapili akashinda na maleria kali sanaaaaa. Jtatu hakwendaaa, jnee hakwendaaa. Jtano akatinga ofisini, akaambiwa Lau karesign jumatatu ile ile. Akajua tu oficially her career is over. Ashakiwa unreliable katika kazi. Basi Pendo mnafiki akaandaa event week inayofata akamuweka front Sessy. Kina Side hawamuangalii usoni. Akahisi tu kuna namna.
Akamfata Lau kwake akamuuliza what happened? Akaambiwa Pendo alipanda dau, akawatoa kishkaji wahujumuuu. Sasa alishikwa akili na Sessy. Sema jtatu alivoingia akaona anarudia kazi yake ya kuwa invicinle tena it is not how he wants to spend the rest of his life. Akajutia ujana wake aliopoteza pale, scared doing nothing, hajiamini, anapelekwa pelekwa. Akaona kuna maisha mengine so kaacha kazi apige tu dili zake zingine.
Akamuuliza Sessy kapata nini? Akasema alivosikia kaahidiwa na Pendo idara mpya ya PR yeye ndo atahead. Sasa coz umri umeenda, shule hanaaa, familia inambana hakuwa na choice ya kuwaza mara 2. She had to do something for herself! Hivo yani. Too bad it costed her, her career.
Wiki 2 nyingi Pendo akatangazwa new head of PR, Side akachukua nafasi ya Pendo, Sessy akabakia pale pale. Siku alivotangazwa Pendo akamfata Violla, kumwambia if it is meant to be it will be. God is good. Violla akamwambia hongeraaa. Pendo yuko jiandae kuwa in my new team, and by now najua umejifunza not to tryanything funny. Violla akamwambia tu, sorry i played dirty. Pendo akatia "Appology accepted" Mda wa kutoka Violla akatuma resignation.
Akawa anashinda nyumbani, kula kulala na kuchat na Raul! She became more vicious than ever. Anamuona kila mtu mbayaaa. Akiwa na Raul anakuwa kama yupo yupo tu, just going along. Raul anajitahidi kuwa understandingna nini! Anakuwa mbunifu wa sehemu mpya, na nini ila Violla walaaaa hayupoooo.
Dada yake akamtafutia interview ya kazi, kufika kule hana mood kabisaaa na maishaaa. Anaulizwa kwanini tukuchukie wewe? Anajibu kwasababu nataka kufanya kazi tu, haijalishi wapi, shilingi ngapi, maslahi, nataka kufanya kazi moja kwa zotee katika hii kampuni yenu mpaka siku nitakapo kufa. Siendi likizo, siendi popotem sitoomba chochote. Wakaanaliana.
Hajafika nyumbanikapigiwa simu kazi kapata akaanze. Kesho kafika pale kasign mkataba bila kuusoma. Akawa anaenda kazini kama golf. Yupo kama hayupooo. Hapo kazini kupya boss wake akawa mkarimuu, anambeba sio kidogo. If you want to talk kibaoooo.
Dada yake akamwambia basi zaa, utapata tena hamu ya kuishi mdogo wangu. Mbona Raul mtu mzuri tu., zaeni tu muishi wote! Moyoni akajiona tu ana settle ila hajapata life partner. Na umri unakimbia, watu wanamwambia ngoja Raul aoe ndo uishi peke yako uone rahaaa.
Basi ikawa kama wanaishi wote, akitoka kazini anaenda kwa Raul. Hivo akahamia kidogo kidoho. Baadae akaja kujua ile laptop inafungiwa sababu ndo creative zake zote zipo humo. Alivoacha ambition ya kazi, Raul akawa haifichi tena ile laptop. So anaona kabisaa project zake.
Jaribu mimba, jaribu hakuna kituuu.Ikawa sasa kapanic, ikabidi aende hospital, akaambiwa hana tatizo lolote amuombe Mungu tu. Ndo akamkumbuka yule Pastor. Akaipiga ile namba, ikapokelwa, akajitambulisha mimi flani, maelezo kibao akaambiwa namba yako ninayo. Njoo ofisini tuongeeee. Wakapanga siku ya kuonana
Yule shoga mwenye wifi gubu akampigia kuwa aliondoka kwake, akamfukuza na dada wa kazi, kakaa kwao wiki 2, mwanamume hamfati wal nini. Kupeleleza mwanaume hana dada wala HG, Anafanya kazi zote ,wenyeweee, wanae kawazoesha wakitoka shule chuka kwa friji wanapasha tu. Wanaangalia katuni. Akija usiku ana deki na kufua nguo za wanae na kupikaaa. Tobaaaaa! Kadata afanyaje. Violla akamwambia rudi
Safari hii usipishane ubavu na wifi yako. Mpe ushindi wa mezanii. Usiwazee sanaaaa. Akikuchokoa muache tu ashinde. Akitaka kitu,wambie sawaaa. Mnavo shibdana ndo anapenda. Akamwambia sawa.
Alipoenda kwa pastor, alamwambia tu, i see another woman in your relationship. Tobaaaaa!
ITAENDELEA KESHO SAA 5 ASUBUHI